Siasa kama ulivyo mchezo wowote kuna wachezaji, kuna wachezeshaji na bila
kusahau wachezeshwaji, mara nyingi wachezeshaji katika mchezo huu ndiyo
wachezaji, na wale ambao tunadhani ni wachezaji ndiyo wachezeshwaji.
Brzezinski
na timu yake nyuma ya mapazia ya vyombo vya habari ndiyo walikuwa wachezaji na
Obama mbele ya kamera za vyombo vya habari alionekana kama mchezaji lakini kwa
hakika alikuwa mchezeshwaji kama mwana sesere aliyefungwa kamba kichwani,
mikononi na miguuni na alivichezesha viungo hivyo kila kamba hizo zilipovutwa,
Brzezinkis ndiye mkono ulioshikilia kamba hizo.
Mpango wa Brzezinski kupitia kwa Obama ni kutengeneza mitandao ya kisiasa
ambayo itaweza kuiporomosha Urusi, utakumbuka mpango wake huu ulianza tangu
wakati wa Jimmy Carter ambapo yeye alikuwa ni msimamizi wa siasa za mambo ya
nje za Marekani ambapo akapelekea kuundwa kwa Taliban ambao waliifanya kazi hii
vizuri sana nyuma ya kile kilichoitwa ‘Holy War’, lakini safari hii mpango huu
hauta ilenga Urusi peke yake bali pia China nayo itaingizwa ndani ya nyumba.
Ukiitizama Urusi Brzezinki amekuwa makini akisambaza propaganda zinazo lenga kuchora
msatari wa kuto kuelewana baina ya Umoja wa Ulaya na Urusi kupitia Kosovo ambayo
mustakabali wake wa kisiasa unaonekana kuachwa katika hali ya utata kwa
makusudi ili Moscow iweze kunyoeshewa vidole kwa aina yoyote ya uwozo unaotokea
hapo.
Lakini kwanza Obama anatakiwa kuwatoa wa China nje ya Afrika. Wachina ambao
wanachukuliwa kama taifa linalo jitahidi kulisaidia bara hili kiviwanda na
kulipatia nafasi za kusimamisha uchumi wake kwa njia mbalimbali ikiwemo
mgawanyo sawa wa kimapato katika miradi mbalimbali hali hii ni kikwazo kikubwa
kwa mawakala wa fremasonry yaani International Monetary Fund na World Bank
ambao wao nia yao ni kutonyonya mpaka tone la mwisho la damu yetu.
Hata hivyo
Brzezinki ana picha kubwa zaidi juu ya hili la kuwafukuza wa China nje ya
Afrika. Kupitia kwa Kennedy Mweusi Brzezinki anampango wa kuwapora wachina kila
aina ya rasilimali wanayonunua kutoka Afrika, ikiwemo mafuta, gesi za asili,
madini na kila kile ambacho kimebakia kama makombo baada ya vile walivyo pora
wakati wa ukoloni, baada ya ukoloni na kwenye ukoloni mambo leo.
Mpango ulio
chaguliwa juu ya hili ni njia ile ile iliyopendekezwa na mababu wa fremason,
Priory of Sion kwenye kile walichokiita protocal of sion, njia hiyo ni
kuzivunja vunja nchi za ki Afrika kupitia vita vya wenyewe kwa wenyewe kitu
kitakacho wakimbiza wa China nje ya Afrika. Na hili litasimamiwa vilivyo na
kile kinachoitwa Africom ambayo imeundwa na Marekani.
Kupitia mpango wa Brzezinki Afrika itakuwa ni uwanja wa mapambano baina ya
Marekani na China, na maanisha mapambano ya kiuchumi na siasa, lakini mapambano
ya bunduki itakuwa ni baina ya wa Afrika sisi kwa sisi. Afrika itawaka moto,
mauwaji ya watu chini ya jangwa la sahara yatakuwa ya kutisha. CIA wataingilia
kati na hata kuingilia siasa za nchi za ndani za Afrika kwa uwazi kabisa nyuma
ya kile kitakachoitwa vita vya ugaidi ambavyo wakala wake ni Al-Qaeda ambao kwa
sasa kutokana na taarifa za vyombo vya habari za kimagharibi na hata vya hapa
Afrka Al-Qaeda tayari wako ndani ya nyumba, wako Afrka, Algeria na Tunisia na
kazi zao chafu zimeshaanza kuonekana, kumbuka Algeria ni moja wapo ya nchi
zinazo zalisha mafuta kwa wingi Afrika.
Utakumbuka Al-Qaedah ilikuwa ikidhaminiwa na CIA kupitia hela za dawa za
kulevyia wakati Taleban wakidhaminiwa na Brzezinki na mtandao wake wa
Trilateral Commission. Hakuna Holy War wala Jihadi; kama alivyo Kennedy Mweusi
vikundi hivyi, ni sawa na mwanasesere anayechezeshwa kwa kamba zilizoshikiliwa
na bwana wakubwa hawa. Moto umeshawaka Nigeria moja ya wazalishaji wakubwa wa
Mafuta Afrika.
(sehemu hiyo hapo juu niliandika
muda kabla moto haujawaka Afrika, lakini yametokea, moto umewaka, serikali
zimepinduliwa, wachina wamekimbia, illuminati wanabeba chao na waafrika bado
tunapigana risasi kwa faida yao)
Uingereza na Israeli kwa pamoja kwa miongo kadhaa wamekuwa wakiivunja vunja
Sudan, lakini leo picha iliyoko Darfur inatumiwa na Marekani pamoja na Uingereza
kama kisingizio cha kuitawalia nchi hiyo mambo yake nyuma ya kile wanacho
tuambia kuwa kuna uvunjaji mkubwa wa haki
za binaadam katika eneo hilo.
Kusema Sudan inakiuka haki za binaadam hakuhusiani kabisa na mpango wa
kuondo zahama hilo kama vyombo vya habari vya kimagharibi na mawakala wao
wanavyo dai lakini zadi inahusiana na mpango wa kukata 7% ya mafuta ya China
ambayo yanatoka Sudan. Habari zinasambazwa kwa kasi kuwa shughuli za kiuchumi
za China nchini Sudan zinazorotesha kwa kiasi kikubwa utaratibu wa kuondoa baa
la njaa na tatizo la mafuta duniani.[1]
Aina hii ya propaganda muda si mrefu inapokelewa na vikundi vinavyo jiita
vinasimamia haki za binaadam ambavyo ni vikundi vya watu wale wale katika sura
tofauti lakini nyuma ya ajenda ileile.
Nchi yoyote duniani ambayo kwa namna moja ama nyingine inanufaika kiuchumi
na au kiviwanda kutokana na ushirika wake na China na kwa maneno mengine China
nayo inajijenga misuli yake ya kiuchumi na viwanda kutokana na miradi yake
mbalimbali iliyomo nchini humo, nchi hiyo haiwezi kuepuka mpango huo wa
Brzezinki.
Mfano ni Burma na Venezuela ambazo historia ya maendeleo yao kiuchumi
haijakamilika bila kuitaja China. Shughuli inayo endelea Pakistan ambapo
Kennedy mweusi amekiri yuko tayari kuipiga bomu la nyuklia Pakistani endapo
itaonekana kushindwa kupambana na Taliban na Al-Qaedah, shughuli hiyo haina
lolote kwenye kile kinachosemwa vita dhidi ya ugaidi bali zaidi, ni vita vya
kuizorotesha nchi hiyo ambay muda mrefu imekuwa mshirika wa China,vurugu hizo
ni za kuwakimbiza wa China kutoka humo.
Tunaona siasa za vuta ni kuvute baina
ya Pakistani na Marekani sasa.
China itakapo tengwa na kupokonywa washiriki wake wote wa kiuchumi, na
kunyimwa uwezekano wowote wa kupata mafuta na malighafi zozote kutoka nje ya
China, hatua itakayo fuata ni kuizorotesha serikali ya China na wakati huo huo
kuipambanisha na Urusi, suala la kuizorotesha serikali hiyo tumelioa
linavyoshika kasi kupitia Tibet kwa kiongozi wao wa kiroho Dalai Lama.
Lakini kwa vile Urusi na China zote
zinafahamu kuhusu njama hizi za Brzezinki mchezo unakuwa mgumu,na hasa pale utakapo jenga
mazingira ya kuonganisha mahusiano yenye chuki ya Urisi na China dhidi ya
Marekani na washirika wake wapya. Upande mwingine wa shilingi mwana sesere huyu
atakuwa na kazi ya kuiunganisha Iran na Syria na kwa pamoja zisimame kuwapinga
wa China na wa Rusi.[2]
(Mpango huo wa kuionganisha Iran na Syria dhidi ya Urusi umekwama baada ya Assad kushindikana kutolewa madarakani, ingawa kwa upande wa Iran Kibaraka amefanikiwa hata kuwaruhusu waendelee na mradi wa nyuklia wenye manufaa kwa binadam, na kuziruhusu asset zilizokuwa zimezuiliwa na Marekani zirudi Iran, lakini bado ni pagumu sababu Muiran na Mrusi wanaujua mchezo mzima mwisho wake ni wapi)
Muandishi wa kitabu cha Barack H. Obama:The Unauthorised Biography anajaribu kutupa taswira ya mchezo
mzima kuhusu Iran na Marekani kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kisiasa
dhidi ya Urusi na China namna utakavyo kwenda, haya ndiyo maoni yake,
Iran itashawishiwa wawe rafiki na Marekani kwa ahadi ya kupewa nguvu sawa
na Marekani ndani ya Mashariki ya kati, si-m-China wala m Rusi, si m Pakistani
wala mu Egypt atakaye kuwa na sauti ila Iran mshirika wake mpya, Marekani.
Rasilimali ngapi za Iran zinazozuiliwa na Marekani kwa muda wote huo sasa
zinafikia thamani ya dola bilioni mia na zaidi, vipi unaonaje Iran akipewa na
ahadi hii ya kupata aseti zake hizo.
Unaonaje ahadi ya kutolewa kwenye listi ya
nchi zinazo dhamini ugaidi na vikundi vyake. Bila kuwasahau washirika wakubwa
wa Iran Hezbollah kuwa na wao watapata chochote. Lakini hayo ni mambo madogo
tu, unaonaje ishu ya nuklia kama alivyo fanya Bush Baba alimkabidhi Saddam
silaha nyuma ya mapazia halafu Bush mwana akaja kuzidai mbele ya hadhara,
unaonaje Iran akapewa ruhusa ya kuendeleza mradi wake huo nyuma ya mapazia.
Tunaweza
kukupatia teknolojia bora kushinda hii uliyonayo, silaha bora na mabomu ambayo
unaweza kuyarusha kokote pale duniani na yakafika Moscow, sema tu kama ndiyo
hilo unalo taka, sasa hivi tutakupatia. Ujue tu kwamba adui yako mbaya kuliko
wote hajawahi kuwa Marekani bali Urusi.
(I STILL WONDER HOW DOES THIS GUY COME TO KNOW THIS,NI KAMA ALIKUWA ANAANDIKA SCRIPT YA MOVIE YA OBAMA, SABABU KAICHEZA HIVYO HIVYO)
Si unakumbuka namna walivyo kufanya
walipo chukua baadhi ya maaeneo yako wakati wa WWII, ule ulikuwa ni uharibifu
mkubwa. Sisi hatujawahi kufanya kitu kama hicho na wala hatuta jaribu kufanya
hivyo.
Tunachotaka sisi ni kuwa marafiki
na kukusaidia kuwa na nguvu za kutosha kupambana na adui yako wa kweli,
Moscow... kama unavyo fahamu muheshimiwa rais wanachi wako wanaichukia Urusi
kuliko wanavyo ichukia Marekani na Uingereza na wakati wowote utakapo wachukia
warusi ujue unawaridhisha watu wako na sisi tutakusaidia... sema tu unataka
nini... unaonaje kuhusu manuari, tukakupatia manuari inayokwenda mpaka bandari
za kusini ya Urusi zikiwa na mizinga ya kinuklia, hapo utawazuia Urusi
wasiendelee kukuibia mafuta yako kutoka kwenye bahari ya Caspian, na kama
wakijaribu kujibu mapigo usiwe na hofu tutakuwepo kukupa sapoti.
Fikiri
mwenyewe kuhusu hili. Halafu kuna hawa wa China, kwa nini unapenda kufanya nao
biashara sana, muda si mrefu watakuweka kwenye mfuko wao wa suruali yao
kutokana na jinsi unavyo wauzia, halafu tunajua hulipendi hilo... bora ufanye
biashara na sisi hata kama ni kwa dola. Tunachotaka ni kuwa ufahamu kwamba sisi
ni wakweli vibaya mno. [3]
Jamaa huyu hayuko mbali sana na ukweli kwa sababu ni mchezo huu huu
aliufanya Brzezinki kwa wa Afighanistan kupitia mujaheedina ambao ni zao la
mpango wake, akawa pambanisha na Urusi na kilichobakia hapo ni historia,
alifanya hivyo kupitia kwa Jimmy Carter, leo mchezo uleule wa mtu yule yule
utafanyika kupitia kwa Obama. Halafu wa Syria nao watafatwa, watashikwa kama
walivyo shikwa kwenye Gulf War ya mwaka 1991. Lengo si kuwapambanisha wa Iran
na Syria bali kuwa unganisha dhidi ya China na Urusi.
Viongozi wote wa nchi za viwanda kama vile wanachama wa G8, vibaraka wao
wanao patikana katika ngazi tofauti za uongozi kwenye nchi mbalimbali duniani,
vikundi vya waasi na vikundi vya kigaidi, wote kwa pamoja wanashirikiana juu ya
kufanikisha ajenda yao ya kishetani, wanafanya kazi kama watu tofauti wenye
mitazamo na maono yanayo pingana kwenye majukwaa ya kisiasa, lakini juu kabisa
kileleni wanaongoza na ajenda moja, ajenda ya New World Order. Ambalo
walimwengu tunaweza kujiuliza ni; wachache wangapi katika viongozi wetu hawako
kwenye mfuko wa Illuminati?
Mkono wa Illuminat umekuwa mrefu kiasi cha kuweza
kuichagulia nchi yoyote duniani kiongozi na kuwapangia sera za kiutawala.
Haijalishi kama angeshinda McCain badala ya Obama jibu lingekuwa lile lile
kwani anaye tawala si Obama bali asasi za siri, mashirika na makampuni makubwa nyuma ya mapazia. Kama unataka
kujifanya kuwa wewe ni mchezaji badala ya mchezeshwaji unaondolewa kwenye
systeam, kama wakina Kennedy, Ali Bhuto wa Pakistan, Aldo Moro wa Italy na
wengine wengi.
Fahamu kuwa kila vita vikubwa vinavyotokea, vilivyotokea, mapinduzi ya
kisiasa, anguko la kiuchumi, magonjwa ambayo hayahusiani chochote na maumbile
asilia kama vile Ukimwi, Ebola, Swine Flu na mengine yatakayo kuja, ni kazi
iliyo pangwa vizuri na kuetekelezwa na watu wale wale ambao wako mstari wa
mbele kujifanya wanataka kufanya tofauti na hivyo.
Unajua ni kwa nini unavutika na makala za namna hii?
Unavutika nazo kwa sababu unatafuta jibu la swali ambalo unadhania hakuna
aliyetayari kukupatia jibu lake. Huna maelezo yakutosha juu ya unacho taka
ispokuwa unahisi kipo. Unahisi kuna kitu ambacho hakipo sawa hapa duniani. Kama ugonjwa hisia hizo
zinakunyima utulivu. Hisia hizo ndizo zinazo kufanya uvutike na makala za namna
hii, kuna kitu ambacho hakiko sawa.
Kila mahala, kila kona nguvu hizi za muungano usio mtakatifu zimetapakaa.
Hata sasa mahali ulipo zipo. Unaziona unapo tizama kupitia dirishani,
ukitembea, ukiwasha luninga yako. Unazihisi nguvu hizo za kimasonia unapokwenda
kazini, unapokwenda kwenye nyumba ya ibada, na hata unapolipa kodi yako kwa
serikali ambao mara zote ni vibaraka na wanaseserere wa big brother, nguvu hizo ni dunia iliyo vutwa mbele ya macho yako na kuyapofua
kiasi cha kutoona ukweli.
Kutoona ukweli? Ukweli ni upi?
Ukweli ni kuwa wewe ni mtumwa wa ulimwengu wa kimasonia. Kama walivyo
watu wengine, umezaliwa kwenye gereza hili lenye uzio usio onekana, harakati za
kila siku za kile kinachoitwa kutafuta maisha zimeyapofua macho yako usione
minyororo na kuta nene zinazokufunga kifikra, kimaumbile na kiroho, u mtumwa
wewe. Bahati mbaya hakuna wa kukuonesha nguvu hizo za kishetani zimejikita
kiasi gani, unapaswa uwone mwenyewe, ni nacho jaribu kufanya ni kukuonesha njia
ya kwenda kujikomboa na kuwa huru, na kuonesha mlango na wewe ndiye unayepaswa
kupita kwenye mlango huo.
Jiandae na posti ya 'MALKIA' atakaye mrithi 'MFLAME' Obama ... tchao
Asante Baba
ReplyDelete