Mungu anapo wateuwa mitume wanakuwa wanatoka katika mkondo wa damu maalum,
anakuwa chini ya uangalizi wa Muumba wake kuanzia maisha ya wazee wake, maisha yake
akiwa tomboni, utoto wake, ujana wake mpaka anapo kabiziwa jukumu hilo zito na
tukufu kwa ajili ya kuwaongoza watu wake.
Hivyo mitume wote wa Mungu Mmoja ni
ndugu kwa vile wote wanatoka katika mtiririko wa damu moja.
Illuminati nao kwa
maelfu ya miaka wamekuwa wakitumia utaratibu kama huu kuhakikisha wanamuweka
mtu mwenye damu yao katika nafasi ya juu ya uongozi, mtu ambaye pande zake zote
za maisha yake wamezimulika na zimekuwa kwenye uangalizi wao kwa muda flani, mfano
mzuri ni Barack Obama.
Tumeona kwa ufupi sana namna gani pande zake zote za
maisha yake zilivyokuwa zimezungukwa na CIA, kuanzia kwa babu na bibi mpaka
kuja kwa mama na baba, lakini si huko tu, mtu yoyote ambaye aliyaathiri maisha
yake utotoni na ukubwani kwa muda flani eitha kwenye elimu, mwalimu
aliyemfundisha, chuo alicho somea kazi yake ya kwanza, watu alio fanya nao
kazi, aina ya shirika alilofanyia kazi na mengina katika hali flani utakuta
yalikuwa na mahusiano na CIA.
Vita vya mwisho baina ya mwanga na kiza vitapiganwa katika misingi ya damu,
itakuwa ni vita baina ya damu tukufu ya mitume na damu chafu ya kishetani.
Ndiyo maana kiongozi wa vita hivi kutoka upande wenye nuru atakuwa ni mtu
anayeitwa Al Mahadi, mtu ambaye anayo nasaba ya moja kwa moja na vizazi vya
mitume kupitia mtume wa mwisho Muhammad (Rehma na Amani Ziwe Juu Yake) Al
Mahadi atasaidiana na mtume Issa (Rehma na Amani Ziwe Juu Yake) au kwa jina
jingine Yesu. Al Mahadi huyu si yule anayetajwa kwenye dini ya Ushia.
Kwa upande wa kiza vita hivi
vitaongozwa na Dajjal maarufu kama Mpinga Kristo, Yesu ndiye atakaye muuwa Mpinga Kristo ndani ya Jerusalem katika
mahala panapoitwa Baabu Lud. Kisha baada ya hapo Yesu akishirikiana na ndugu
yake Al Mahadi watasimamisha ufalme wa Mungu Mmoja katika jiji la Jerusalem,
jiji ambalo Mpinga Kristo na watu wake watataka kulifanya kuwa ndiyo makao makuu
ya New World Order kama tunavyoona harakati hizo zinavyo shika moto siku hadi
siku.
Hilo halito fanikiwa, kitimbii chao hichi kitashindwa vibaya na dini ya
Mungu Mmoja itasimamishwa kutokea hapo Jerusalem na kuondoa dhulama katika uso
wote wa dunia. Hili pia litathibitisha kuwa Jerusalem siyo jiji la wafalme kama
wanavyo dai Illuminati bali jiji la Mitume wa Mungu Mmoja.
Obama alipochapisha nsha yake inayohusu hamu na mpango wake kama kiongozi
mtarajiwa wa Marekani alitumia jarida la Foreign Affair, jarida hili
linachapishwa na asasi ya siri inayo julikana kama Counil on Foreign Relation,
Obama pia ni freemason wa daraja la 32 katika hekalu la Prince Hall Freemason
ambalo ni maalum kwa watu weusi[1].
Kijana huyu ni mtiifu
kwenye muungano huu usio mtakatifu, mpaka kufikia daraja ya 32 na hatimaye
kuruhusiwa kuikanyaga White House hapana shaka ameonesha kuwa anaweza kuibeba
ajenda kutoka pale freemason mwenzake George W Bush alipoiachia mpaka pale
ratiba ya ajenda itakapo muelekeza kuifikisha, hivyo sahau “changes” na tegemea
hadithi ile ile uliyoipata kwa Bush na huenda mbaya zaidi itategemea ajenda
inataka nini.
Mpakwa mafuta huyu wa nyumba ya Freemason amekuja na hadithi ya changes na
hope, naam, tumaini, kuna matumaini tutaraji matumaini na mabadiliko. Maana ya
tumaini peke yake imetegemea wakati ujao achilia mbali neno mabadiliko. Kwa
maneno mengine tuko kwenye hali mbaya na kijana huyu ambaye safari hii
nimeshuhudia dunia nzima ikimfanyia kampeni kama kiongozi wa dunia amekuja
kutuambia tuendelee kuvumilia shida hizi walau kidogo kwani hapo mbele, hapo
mbele kuna matumaini, upo na mimi mpaka hapo, kwa hiyo kama wanavyo ambiwa wale
wenye Ukimwi waishi kwa matumaini ndivyo sasa tunambiwa sote tuwe na matumaini,
tutumainie jambo, sawa?
Kwa maneno mengine tusubiri wakati ujao mambo yatakuwa mazuri, hii ndiyo
maana hasa ya tumaini, haizungumzii wakati uliopo bali wakati unao kuja. Dunia
nzima ilikuwa na bado iko kwenye matatizo, madhila, mashaka na uharibifu
mkubwa, dunia nzima ilikuwa inahisia za tunataka mabadiliko sasa, msimamo ambao
si mzuri kwa ajenda hivyo kampeni za tumaini zimekuja kufanya hayo mabadiliko,
hali bado ni mbaya maradufu lakini walimwengu wanasema tumpe muda kijana, tuna mtumainia
ataleta mabadiliko, hisia za mabadiliko sasa zimekufa na badala yake ni hisia
za matumaini. Hakuna kilicho badilika lakini tuna tumaini hivi ndivyo mteule
anavyo fanya kazi.
Watu wana tumaini la nini? Tumaini la mabadiliko, Bill Clinton na wengine
pia wameshaitumia mbinu hii inayoitwa changes. Babylon Brotherhood wanajua kuwa
watu hawaikubali hali waliyo nayo, na wanataka mabadiliko kwa hivyo njia
nyepesi ni kuwaletea mabadiliko, kwa hiyo wanakuja na mavazi yale yale unayo
taka wavae, na sura ile ile unayoipenda, lakini...
Je bwana Changes amepata kutuambia ana maanisha nini anapo zungumzia,
tumaini, mabadiliko, na kuamini? Tumaini la nini, mabadiliko yepi, na tuamini
nini? Mbinu hapa ni kumuacha mfuasi mwenyewe aamue ni mabadiliko na au ni
tumaini gani analo taka na Obama anakuwa ndiyo jibu la matakwa yake. Tunacheza
na akili za watu hapa, hatuwapi kile wanachotaka lakini tunawarubuni mpaka
wanaona wamepata wanachotaka na wametukomoa, lakini kinyume chake ndiyo sahihi.
Kwa hiyo Obama ana simama mbele ya
watu hao kama ndiye kila kitu wanachotaka kuamini, kutumainia na badiliko. Vile
ambavyo wapiga kura walivyo kuwa wanataka ndivyo Obama alivyo kuwa, chochote
unachotaka kibadilike, chochote unacho kitumainia, chochote unacho kiamini
kielekeze kwa Obama na hapo utamuona mtu aliye tayari kukuleta hayo, yeye ni
kila kitu, yeye ni chochote unacho taka kiwe. Kwa hiyo Obama hakuwa na haja ya
kupambanua alikuwa akimaanisha nini anapo sema changes, hope na belive.
Hii ndiyo maana Obama
alifananishwa na Messiah, Abraham Lincoln, John Kennedy na au Kennedy Mweusi na
wakati mwingine alifananishwa na Buddha, vyovyote unavyotaka awe ndivyo
anavyokuwa, chochote unacho kitaka mtizame yeye, na utapata tumaini la
kukipata.
Waambie watu kile wanachotaka kusikia, na nyamaza kimya juu ya
kile wasichotaka kukusikia, utawateka vizuri sana, kwa mtu anaye onekana
kuwa ni tofauti na Bush ndicho walimwengu walichokuwa wanataka. Lakini kuwa
ambia peke yake haitoshi ila namna gani unawaambia, hii ndiyo inayoleta
tofauti. Vipi unafanya unachokifanya hapa ndipo ilipo lala hatma ya mchezo
mzima.
Akisimama kwenye jukwaa ni Obama, na anapo zungumza na kutabasamu ni Obama
yule ambaye dunia ilikuwa ikimtumainia, lakini watu fulani nyuma ya mapazia
wamemuandaa mteule wao na kumpa mafunzo ya namna gani ya kuzungumza na kuteka
fikra za uma.
Mazungumzo yake hayatoki moyoni bali kwenye ubao maalum ambao
watazamaji hauwoni, aina hii ya teknolojia katika kuzungumza inajulikana kama
autocue. Mafunzo maalum ya kudanganya macho ya uma kwa ‘kumaanisha kile
unachosema’ ni kama mchezo wa kuigiza, Blair alifunzwa kutumia mbinu hii, na
aliitumia vyema kama alivyo fanya Clinton,
Bush ndiye aliyeshindwa kuitumia njia hii ipasavyo ndiyo maana ilibidi
kufanyika kazi ya ziada, ili kumfikisha White House. Kumbuka Bush hakushinda
uchaguzi ule ila mpinzani wake ndiye aliyeshinda, na alipokuwa White House
ilimbidi kutumia nguvu za kivita kutekeleza matakwa ya ajenda.
Wale waliotolea macho kampeni hizi, wakazitazama kwa jicho na fikra huru
tangu kipindi cha Obama anapambana na Hillary mpaka Obama anasimama na John
McCain watakubalina nami kuwa wakati huu ajenda ilikuwa inamuhitaji Obama, ni
kwa sababu gani ajenda inamuhitaji mtu mweusi ndani ya white house ni swali
litakalojibiwa na yeye mwenyewe katika kipindi cha utawala wake, hivyo
kilichokuwa kikubwa kinafanyika ni kurubuni mtazamo na wawazo ya walimwengu
hususani ya wapiga kura wa Marekani kumkubali kijana huyu mweusi.
Kazi hii ilikuwa ni nyepesi sana kwa sababu moja kuu, watu hawako huru,
watu wamefungwa minyororo isiyo onekana, mawazo, mitazamo, maoni na maono ya
watu wa vyombo vya habari, watu maarufu, na wale wenye ushawishi wa aina
mbalimbali katika jamii ndiyo yaliyofanywa kuwa ni maono, mitazamo na misimamo
ya walimwengu wote, kiuhakika opofu huo ndiyo uliwezesha kuchaguliwa kwa Obama
na si hitajio la Wamarekani wala tumaini la walimwengu kama inavyonekana bali
ni hitajio la Babilon Brotherhood na ndiye tumaini lao.
Wakati Obama na Hillary wanapambana niliona kasoro nyingi za makusudi
katika kampeni za Hillary. Mwana mama huyo mwenye nafasi kubwa ndani ya mtandao
wa Babilon hakuonesha ushindani wa dhati na wala hakuonesha juhudi zake za
makusudi za kuwa anataka kuingia Ikulu, kwa wale waliofuatilia kampeni zake
muda wote alionekana ameridhika na vile anavyoendesha mambo yake pamoja na
kwamba mbinu zake zilikuwa hazimletei ushindi.
Wakati kila nukta moja Obama
aliyoipata kushawishi ulimwengu alitumia ipasavyo. Clinton hakuonekana kujutia
kushindwa kwa mbinu na sera zake bali zaidi alionekana kama mtu
anayejifurahisha kwenye majukwaa ya kampeni wakati Obama muda wote alionesha
uso na moyo wa kazi.
Baada ya Obama kumshinda Hillary mambo yalizidi kuwa wazi zaidi kuwa ajenda
inamuhitaji mtu mweusi. Kwa wale watumiaji wa internet na hasa wasomaji wa
e-mail kwenye mtandao wa Yahoo na Hotmail kulikuwa na kampeni za kumpigia debe
Obama. Kampeni hizo ziliendeshwa kupitia tangazo maarufu la Green Card ambalo
mara nyingi utalipata unapofungua email zako kwenye hizo tovuti mbili.
Utakumbuka kipindi flani ambapo Marekani ilikuwa ikiandamwa na jinamizi la
eitha au la wabadilishe katiba ya nchi hiyo ili iweze kumruhusu mzaliwa kutoka
Austria na mcheza filamu maarufu Arnold Schwarznegger kugombea urais wa nchi
hiyo, kipindi hicho kwenye tangazo la Greencard walikuwa wakiweka picha mbili
tu, picha ya raisi aliyemaliza muda wake na picha ya Schwarznegger na
wakikuambia yupi ni rais wa marekani kati ya hawa wawili?
Katika kampeni za safari hii
walianza na picha za Hillary, halafu baadae zikaja za Obama zote zikiuliza ni
yupi rais wa Marekani, hawajapata kuweka ya John McCain na wala ya mgombea
mwenza wake.
Wakati Obama akijizatiti na kuunga sera za chama chake, McCain kwa makusudi
alikuja na sera mbovu zinazopingana na sera za chama chake na pia zinazopingana
na sera za rais aliyekuwepo madarakani ambaye naye anatoka kwenye chama chake,
kwa hiyo wakati Obama anasonga mbele na sera zilizoandaliwa vizuri McCain
alikuwa na kazi ya kutatua migogoro ya kisera.
Kituko kingine ni mgombea mwenza
wa McCain ambaye kwanza kubalina na mimi kuwa McCain hakupewa mwana mama huyo
kwa bahati mbaya bali kwa makusudi mazima, wakati McCain anapingana na sera za
Bush mgombea mwenza Sarah Palin alikuwa akipingana na sera za McCain, kama ni
chombo basi kilikuwa kimeshapoteza dira yake hakifahamu ni wapi kinaelekea,
narudia hayakufanywa haya kwa bahati mbaya. Sarah alizidi kuwachanganya na
kuwakatisha tama wafuasi wa chama chake pale alipoanza kujitangazia kuwa yeye
atashinda katika uchaguzi wa awamu nyinginena si huu anaofanyia kampeni, haya
kuwa maneno ya kuwaambia wa fuasi wako, kwa maana nyingine ni kuwa uchaguzi huu
yeye na McCain wameshashindwa, alisema maneno haya wiki kadhaa hata kabla ya
kura kuanza kupigwa, kwa mtu yoyote mwenye akili hawezi akawapa kura watu ambao
tayari wameshaonesha kuwa hawako tayari kufanya kazi wanayoiomba.
Wakati
Republic wakiwa katika makanganyiko huo kwa Democrat kila siku mpya iliashiria
ushindi kwao.
Wakati wa kile walichokiita US Presidential Debate McCain alizidi kuonekana
kituko kwa kutengeneza mazingira ambayo Obama aliyatumia kujitangaza vyema,
wakati Obama anazipambanua sera zake McCain alifanya kazi ndogo sana kuhusu
hilo bali zaidi aliuliza maswali ambayo yalihitaji ufafanuzi zaidi kutoka kwenye
sera za Obama ambapo kijana huyo mweusi akazidi kuzichanganua sera zake kwa
watazamaji.
Baada ya mjadala huo waendeshaji wa mjadala huo kupitia televisheni
ya VOA bwana Jim Malone mwandishi wa habari yeye alimponda McCain waziwazi na
wakati huo huo akimpamba Obama, bwana Barry Wood ambaye anasimamia habari za
kiuchumi katika kituo hicho cha televisheni na yeye aliungana na Obama, hivyo
maoni ya watu hawa wawili yanakuwa maoni ya mamilinioni ya watazamaji na hivyo
ndivyo Obama alivyoikanyaga White House.
Kwa picha halisi Kennedy Mweusi ni kibaraka wa matajiri wakubwa wanaomiliki
Wall Street na benki nyingine kubwa ndani ya Marekani na kimataifa,
anawakilisha kazi za asasi nyingine za siri kama Trilateral Commission,
Bilderberger Group, Council on Foreign Relations, Skull and Bones Society na
Ford Foundation. Mama yake Obama ambaye amepata kufanya kazi katika mashirika
mbalimbali yakiwemo World Bank,US Agency for international development na Ford
Foundation amemuachia Obama uongozi wa biashara za familia ambazo nazo
zinamuelekeo ule ule wa Ford Foundation na ambapo mashirikia hayo daima
yamekuwa yakipata dira na muongozo wake kutoka kwa Ford Foundation na alipo
toka hapo akaingia kwenye asasi ya siri mama wa Umoja wa mataifa Trilateral
Commission.
Matakwa na baraka nyingi kutoka kwa asasi za siri kama, the Trilateral
Commission, the Bilderberger group, the Ford Foundation, Skull and Bones, the
Chicago School, the Council on
Foreign Relations, na kutoka kwenye vitengo vingine vinavyoshikilia sehemu
muhimu ya utawala wa Marekani wakiwemo vinara wa Wall Street ndicho kilicho
mfanya Obama kuonekana ni Kenndedy mweusi mbele ya mwanamama mweupe Senator
Clinton. Obama si tumaini la wa Marekani na au walimwengu kama wanavyo sema
watu wengine bali ni tumaini la Babylon Brotherhood.
Kasi ya Obama aliyo kuja nayo haina tofauti na ile ya Hitler wa
Ujerumani, Wajerumani walikuwa katika hali ngumu kiuchumi na kijamii, wakiwa
katika hali mbaya kama ile akatokeza mtu aliyeitwa Hitler ambaye kwa sera zake
alionekana kama Messiah kama ambavyo anavyo onekana Obama. Alingia katika
madaraka kwa namna ambayo Obama kaingia nayo White House, sisemi Obama ni
Hitler wa Marekani ila nakuonesha namna gani mbinu moja ianavyotumiwa zaidi ya
mara moja na mabilioni hawana hata wazo la kung’amua hilo. Hitler naye aliahidi
mabadiliko (changes), matumaini (hope) na kuamini juu ya kitu fulani (belive),
watu waliibuka na kumuunga mkono Hitlar wakiwa na tumaini. Walichokipata ni
serikali ya kifashisti.
No comments:
Post a Comment