Kuna somo la mahesabu katika Quran, ningependa nalo hili tulitupie macho
kidogo.
Mahesabu ndiyo lugha ya sayansi, na mahesabu ndiyo lugha moja
inayowezwa kuzungumzwa kote ulimwenguni, na ndiyo lugha ambayo haiwezi
kuathiriwa na muda.
Hata hivyo leo tunaufahamu ulimwengu na maajabu yake kwa
kutumia kanuni mbalimbali za kimahesabu. Galileo ambaye ameyapa mahesabu haki
yake katika tafiti zake, alisema kwamba, mahesabu ndiyo lugha ambayo MUNGU
MMOJA ameitumia katika kuutengeneza ulimwengu.
Wanafalsafa kama Pythagoras,
alikuwa akidhania kuwa, kanuni ya msingi ya ulimwengu imewekwa katika tarakimu,
na wakuhusisha tarakimu na mambo ya kimaajabu na mazingaombwe. Na ni hivi
karibuni tu, madai ya kisayansi yamethibitishwa kwa kutumia tarakimu au kwa
uwazi zaidi kwa kutumia kanuni za kimahesabu.
Kutoka kwenye ugunduzi wa balbu
wa Edson mpaka kwenye magari yaendayo kwa kasi, kutoka kwenye nadharia ya time relativity kutoka kwa Einstein,
mpaka nadharia ya gravitationtoka kwa
Newton, zote hizi asili yake ni deni walilokopa kutoka kwenye lugha ya
ulimwengu, lugha ya kimahesabu.
Quran nayo kitabu cha MUNGU MMOJA, hakikuacha
kuelezea umuhimu wa lugha hii katika usawa na uyakinifu wa ulimwengu ndani ya
mahesabu.
“Na kuisoma Qur’an. Na mwenye kuongoka, basi ameongoka kwa faida ya nafsi
yake; na aliye potea - basi sema: Hakika mimi ni miongoni mwa waonyaji.”
“Na sema: Alhamdu Lillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Yeye
atakuonyesheni Ishara zake, na mtazijua. Na Mola wako Mlezi si mwenye
kughafilika na myatendayo.”(Quran 27:92-93)
Aya tuliyoisoma hapo juu, inaelezea kwamba, katika nyakati zijazo MUNGU
MMOJA, atazionesha alama zake kwa watu, ili watu wale wenye akili, wenye
kufikiri watambue juu ya kuwepo kwa MUNGU MMOJA, na wamuabudu kwa namna ile tu,
anayoitaka yeye, kwa namna ile tu aliyo watuma mitume wake wafundishe, na siyo
vinginevyo.
Hili peke yake linatuthibitishia kuwa Muhammad yeye siyo mwandishi
wa kitabu hichi, kwani ni namna gani angeweza kuandika vitu ambavyo baada ya
milenia moja ndiyo viweze kujulikana? Hata kama angekuwa na maarifa na akili
kiasi gani, Muhammad asingeweza hata kwa kujaribu kutabiri kwamba ataonesha
miujiza siku zijazo, siku na miaka itakayo fuata baada ya kuondoka kwake. Yeye ni binadam kama binadam wengine, maono, fikra, mitazamo na mipango yake lazima yaathiriwe na nyakati kama ilivyo kwa binadamu mwingine, ni MUNGU MMOJA tu ndiye hawezi kuathiriwa na nyakati, sababu nyakati ni moja kati ya viumbe vyake, naye haathiriwi na viumbe vyake, naye ndiye mwenye nguvu, uwezo, mamlaka na maamuzi ya yasiyo athiriwa na nyakati kama ahadi aliyoitoa kwenye aya niliyo inukuu hapo juu.
Na
vipi aweze kutabiri vitu vya baadaye ambavyo kuthibiti kwa vitu hivyo, hata
kidogo kusingeweza kumnufaisha yeye kwa chochote, au kumpunguzia dhiki kutoka
kwa maadui zake, au kuwanyamazisha maadui zake, kwa vile utimilifu wa utabiri
huo ni kwa wakati ujao, ambo si yeye wala maadui zake watakao kuwepo
kuthibitisha ukweli wa maneno yake.
Mbali na hayo ulimwengu wa Kiislamu
wenyewe, haukuwa ukifahamu vingi katika hii miujiza ya Quran mpaka hivi
karibuni tu. Hivyo wakati mtume Muhammad Rehma na Amani ziwe juu yake
alipokuwapo katika zama zake, maisha yake, na yale aliyo yafanya na hii Quran
vyote vilikuwa ni miujiza kwa umma wake, baada ya kuondoka, harufu na ladha ya
miujiza hakuondoka na yeye, zama hadi zama, kwa nyakati tofauti nuru ya Quran
imekuwa ikiendelea kuwamulikia watu, kwa nuru ya kweli, kwenye matukio,
maumbile, tabia na sifa za ulimwengu na vile vilivyomo na ikielekeza ni nani
mfanyaji wa kazi hii, kwa lugha nyepesi sana, lakini iliyo ngumu mno kuiigiza.
Quran ni muujiza na kama wanavyo sema, time
will tell.
Tumeona kuwa Quran yenyewe imetoa changamoto kwa wale ambao wanaoipinga na
kuikana, kwamba ikiwa wanadai kuwa hii ni kazi ya Muhammadi, yaani ni maneno
yake, basi waandike japo sura kumi tu mfano wake na wailete kwa umma tuione.
Lakini Quran ikapunguza makali ya changamoto, ikawataka wafanye basi japo sura
moja tu, lakini hakuna aliyefanya, ikawaambia tena basi changanyikeni na majini
musaidiane katika hili, na ikawathibitishia kuwa hata wakichanganyika juu ya
hili hawato weza, na kweli mpaka leo binadamu wanashirikiana na majini kwenye
mambo mbalimbali, lakini kwenye hili la kutengeneza japo sura moja tu, bado
hawajaweza.
Hii changamoto peke yake inatosha kukifanya kitabu hiki kuwa ni
muujiza. Kama ni maneno yake Muhammad ni wapi alipata hiyo nguvu na ujasiri wa
kuipa changamoto dunia nzima, kwa zama zote, kwa watu wote na majini na
mwishowe washindwe changamoto hiyo? Mbona hakuna aliyekuja na walau hiyo sura
moja na sasa ni zaidi ya miaka 1400 tangu hiyo Quran ilipo sema hivyo.
Swali la kujiuliza kwa nini Quran, kitabu chenye sura 114, kilicho letwa
kwa watu karne ya saba na mchunga mbuzi asiye fahamu kusoma wala kuandika, kiwe
ni fumbo kwa ulimwengu na watu wa zama zote mpaka majini? Kina nini maalum
kitabu hichi?
Kitu cha kwanza kabisa kwenye Quran ni mahesabu. Kila sura kwenye kitabu
hichi imepangwa na kufungamanisha kimahesabu kwa namba maalum, na maneno yaliyo
tumika nayo mpangilio na idadi yake umefungamanisha kimahesabu, kiasi kwamba
ukiondoa neno moja au ukalizidisha au ukaondoa sura nzima, itakuwa ni sawa na
kujaribu kutatua tatizo la kimahesabu kwa fomula isiyo kuwa yake. Kila aina ya
hesabu inayo fomula/kanuni yake ya kuweza kuitatua, unapoingiza hesabu kwenye
kanuni isiyo yake, hesabu hiyo inakataliwa na kanuni husika.
Hivyo unapo toa
herufi moja au kuizidisha kwenye kitabu hichi, moja kwa moja unauvuruga mfumo
wote ulio tumika kuandikia kitabu hicho, mpangilio mzima unaporomoka na mkononi
utajikuta unacho kitabu kingine, lakini siyo Quran. Katika lugha ya kigeni
tunasema Quran imekuwa coded, ili
uweze kupunguza au kuongeza chochote, kwanza uivunje code yake iliyo tumika, kitu ambacho kitapelekea kuivuruga Quran
yote.
Hivyo unaweza kuongeza kitu au kupunguza kwenye kitabu hiki, lakini lazima
ujue hicho utakachokiongeza au kukipunguza utabaki nacho wewe mwenyewe, na
utakuwa unaidanganya nafsi yako na hao, walio kubali kurubunika, lakini Quran
yenyewe itabakia vile, vile kwa vile utakuwa hujaweza kuivunja ile code yake. Utaweza kuandika msahafu wako
kama walivyo fanya baadhi ya watu, utaweza kuongeza baadhi ya sura kama walivyo
fanya baadhi ya watu, lakini vyote hivyo vitakapo zamishwa kwenye Quran
vitakataliwa na Quran yenyewe.
Yaani haihitaji watu, waumini au Waislam waseme
kuwa hayo hayakuwepo yameongezwa, aihitaji hilo. Hata kama watu wote watakuja
na Quran ya kughushi na kusema ndiyo ya ukweli, na majini wote wakaikubali,
bado Quran yenyewe, itaikataa hiyo Quran ya kughushi kwa nafsi yake. Yaani Quran
inajilinda yenyewe kwa kutumia code
iliyo tumika kukiandika kitabu hichi, unapaswa kuivunja hiyo code, kabla ya kuivunja hiyo Quran,
unapaswa kuivunja hiyo code, kabla ya
kuighushi hiyo Quran, inakupasa ughushi hiyo code yake, na hicho ni kichekesho sababu hakuna code ya kughushi, na kwa code hiyo Quran inajilinda yenyewe hata
kama dunia nzima, ikija na kitabu kingine na kusema ndiyo Quran.
Hivyo kughushi hii Quran kuko kwa namna mbili, eidha waandike kitabu
kingine mbali kabisa na Quran, kisha wakiite Quran au waongeze na kupunguza
chochote katika Quran.
Njia zote mbili ni ngumu na haziwezekani. Kuandika kitabu kingine mbali na
kisha ukiite ni Quran, mwandishi atahitajiwa kati ya mengi asiwe mwenye
kuathiriwa na kitu tunacho kiita muda, yaani wakati uliopita, wakati uliopo na
wakati ujao visiwe na athari hiyo ya kinyakati kwa mwandishi, sifa ambayo
tunajua hakuna kiumbe chochote chenye ujuzi huo, si majini wala binadamu.
Hivyo
basi hiyo kazi haitoweza kuhimili changamoto za muda kwa vile mwandishi wake, eidha
hana ujuzi wa kutosha kwenye kile kinacho itwa wakati ujao, au uliopita au
uliopo. Msomaji makini anaweza kuona ni aina gani nyingine ya ugumu ambao
unawafanya mpaka leo washindwe kuja na walau sura moja tu. Njia ya pili ya
kughushi ambayo ni kuongeza au kupunguza chochote kwenye Quran, inakumbana na
kikwazo kimoja kikubwa sana, nacho ni code
ya Quran.
Jinsi kilivyo kitabu hichi ni kuwa kila sura sehemu ilipo inafungamana
kimahesabu na sura nyingine eidha iliyo mbele au nyuma yake, kila neno nalo
linafungamana na neno jingine kama hilo na kila herufi inafungamana na herufi
nyingine zilizomo humo, na vyote hivyo vinafungamana na code ya Quran ambayo ni nambari 19. Hii inamaanisha nini basi?
Ni kwamba, endapo utaichomoa au
kuiongeza herufi, neno, sura moja, itakubidi ubadilishe kila herufi au neno au
sura ili hicho ulichokiweka au kukitoa kiweze kuingia kwenye code ya Quran. Kwa vile kila herufi,
neno, sura inafungamana na nyingine, utakapoigusa moja, ni kwamba code haitakuwa sawa mpaka uiguse kila
herufi katika Quran, hivyo ukigusa moja, nyingine iliyo fungamana nayo
inadondoka, na hiyo iliyo dondoka itakuwa imefungamana na nyingine ambayo hata
haukuwa na mpango wa kuigusa nayo itadondoka, na nyingine na nyingine, mwisho
wa siku utajikuta inakubidi uiandike Quran yote upya, kwa vile lengo lako ni
kutaka ikae ndani ya code nambari 19,
nahofia utakacho kiandika kitakuwa hakisomeki, lakini kama utamaliza kukiandika
kwani kunayo uwezekano mkubwa ukawa mwendawazimu, kwa sababu kila herufi, neno,
sura unayoigusa inafyetuka, na inapo fyetuka inaifyatua nyingine na iliyo
fyatuliwa nayo inaifyatua nyingine, na nyingine na nyingine, je ni muda gani
utakuchukua kuzipanga hizi ili zikae kwenye code
nambari 19 kabla haujawa mwendawazimu?
Wale wanao dai kuwa hii Quran tuliyo nayo imepunguzwa basi, waitizame kauli
yao upya ama la, wailete hiyo sura wanao dai kuwa wanayo, au huo msahafu walio
nao na kisha utumbukizwe kwenye code hii ya Quran na tuone ni majibu gani
yatapatikana. Na ikiwa hawawezi kufanya hivyo, basi na tuache kibri, na tuache
kumzushia MUNGU MMOJA na Mtume wake Rehma na Amani zimshukie, na tuogope adhabu
zake kwani adhabu yake ni kali na wameandaliwa makafiri.
Katika Quran neno ‘siku’ kwa Kiarabu (yewm) limetumika mara 365. Idadi hiyo
si kwamba tu inathibitisha idadi ya masiku katika kalenda, lakini pia inaonesha
mahusiano baina ya kinyota baina ya dunia yetu na jua. Pale dunia yetu inapo
maliza kulizunguka jua, inakuwa imefanya hivyo mara 365, yaani zimepita siku
365 tangu dunia ilipo anza kufanya hivyo kwenye nukta yake ya kwanza. Hivyo
utaona neno ‘siku’ limetajwa mara 365, sawa na idadi ya siku ambazo dunia yetu
inazitumia kulizunguka jua.
Neno
|
Idadi ambayo neno hilo
limetumika ndani ya Quran
|
Siku
|
365
|
Idadi ya siku ambazo Dunia inatumia kulizunguka jua
|
365
|
Quran hiyo, hiyo pia imetumia
neno siku lakini kwa upande wa wingi, yaani masiku, katika lugha ya Kiarabu
(eyyam,yewmeyn). Neno ‘masiku’ kwenye Quran limetumika mara 30. Nambari hii au
idadi hii inawakilisha masiku 30 ya mwezi. Kwenye kalenda ya Jua mwezi huwa na
masiku 30 au 31, wakati kwenye kalenda ya mwezi huwa na masiku 29 au 30. Hivyo
idadi ya thelathini ni namba ya kati na kati baina ya kalenda hizi mbili.
Unaichukua mwezi masiku 29.53 tangu kuandama mara ya kwanza mpaka kupotea na
kuja kuandama tena, kama mwezi mpya, katika mahesabu kuna kitu tunacho kiita
makadirio, hivyo tunapo ikadiria 29.53 tunapata 30, kama ambavyo ilivyo kwa jua
ambapo dunia yetu hutumia siku 365.25 ambayo tukiikadiria, tunapata 365.
Neno
|
Idadi ambayo neno hilo
limetumika ndani ya Quran
|
Masiku
|
30
|
Idadi ya Masiku katika mwezi
|
30
|
Neno ‘mwezi’ (Qamar) pamoja na
yale yanayo husiana na satelaiti hii, yametumika mara 27 kwenye Quran. Idadi
hii ya 27 ni sawa na idadi ya masiku ambayo ‘mwezi’ kama satelaiti inayo
yatumia kukamilisha mzunguko wake. Hapa ni kabla hauja onekana tena, yaani ndani
ya siku 27, mwezi huwa umeshamaliza mzunguko wake, lakini mpaka tuje kuona kwa
jicho itahitajika siku moja au mbili zaidi, hivyo basi, hapa Quran inazivuta
fikra zetu kwenye masiku yale tu ambayo mwezi unakamilisha mzunguko wake kabla
huja andama tena na kuwa mwezi mpya, nayo ni masiku 27. Hivyo hapa neno mwezi
kama satelaiti limefungamana kimahesabu kwa idadi ya siku zake inazo zitumia
kukamilisha mzunguko wake, hivyo huwezi kuliongeza, wala kulipunguza neno hili
kama ambavyo huwezi kupunguza wala kuongeza neno siku au masiku kama tulivyo
ona hapo juu, kwani nayo yamefungamana kimahesabu kwa idadi maalum.
Neno
|
Idadi ambayo neno hilo
limetumika ndani ya Quran
|
Mwezi kama satelaiti
|
27
|
Muda ambao mwezi unatumia kukamilisha mzunguko wakekabla haujaonekana
tena kwa macho.
|
27
|
Mzunguko wa dunia kulizunguka jua
ni siku 365, wakati mizunguko 12 ya mwezi kulizunguka jua ni miezi 12. Quran
inasema kunayo miezi 12 kwenye mwaka, Quran 9:36. Kwa upande mwingine Quran
imetumia neno ‘mwezi’ (shehr) mara 12 tu, kudhihirisha kuwa kunayo miezi 12
kwenye mwaka.
Neno
|
Idadi ambayo neno hilo
limetumika ndani ya Quran
|
Mwezi
|
12
|
Idadi ya miezi au idadi ya miezi inayo patikana kwa kulizunguka jua kwa
mwaka.
|
12
|
Neno ‘bahari’ (al-bahr)
limetumika mara 32 kwenye Quran, neno hili ‘al-bahr’ linatumika pia kumaanisha
mito na maziwa. Na neno ‘aridhi’ (al-berr) limetumika mara 12 kwenye Quran. Uso
wa dunia ni kilometa za mraba milioni 510. Inakadiriwa kuwa takribani kilometa
za mraba milioni 360 ni mito, maziwa, bahari na kadhalika, halafu takribani
kilometa za mraba milioni 15 ni barafu. Kama tukizitoa hizo kilometa za mraba
milioni 15, aridhi itabakiwa na kilometa za mraba milioni 135. Tutakapo tafuta
uwiano baina ya haya maneno mawili ‘aridhi’ na ‘bahari’ kwenye Quran ni 12/32 =
0.375. Na uwiano baina ya nchi kavu na sehemu za maji kwenye uso wetu wa dunia
ni milioni 135/360 kilometa za mraba ambayo ni sawa na 0.375. Hapa maneno haya
mawili yamefungamanishwa na mazingira halisi ya ulimwengu.
Neno
|
Idadi ambayo neno hilo
limetumika ndani ya Quran
|
Uwiano wa maneno hayo
kama yalivyo tumika kwenye Quran
|
Aridhi
|
12
|
12/23 = 0.375
|
Bahari
|
23
|
|
Neno
|
Idadi ya kilometa za
mraba kwa maeneo hayo mawili katika uso wa dunia
|
Uwiano baina ya maeneo
hayo mawili kwenye uso wa dunia
|
Aridhi ukitoa maeneo yenye barafu
|
Kilometa za mraba milioni 135
|
135/360 = 0.375
|
Bahari
|
Kilometa za mraba milioni 360
|
|
Hivyo utaona Quran, namna ilivyo fungamanisha, hapa tunaona maneno mawili
tu yahusiayo bahari na nchi kavu yalivyo fungamanisha na mazingira halisi ya
dunia, hivyo utakapo iondoa sura ambayo imetaja moja katika maneno hayo, moja
kwa moja utaharibu uwiano huo, au ukazidisha kitu ambacho ndani yake yatakuwepo
maneno hayo, moja kwa moja uwiano huo utatoweka., na kwa kupitia mazingira
halisi, kitabu chako hicho kitaonekana ni kile cha kughushi.
Sura ya 18, ambamo ndani yake
kumeelezewa hadithi ya watu wa pangoni, hadithi ambayo Muhammad (s.a.w) alipo
kuja kwa watu kuwapa ujumbe wa MUNGU MMOJA, katika moja ya majaribu waliyo mpa
ni kutaka Muhammad awaelezee hadithi ya watu wa pangoni.
Hadithi hii ilikuwa
ikiwahusu vijana ambao walimuamini mtume
Issa, (Yesu) Rehma na Amani ziwe juu yake, lakini baada ya Issa (Yesu)
Rehma na Amani ziwe juu yake, kupaishwa mbinguni na utawala wa Roma kuanza
kuwanyanyasa wafuasi walio mfuata mtume Issa (Yesu) Rehma na Amani ziwe juu
yake, ili waweze kuachana na dini yao na mafundisho ya MUNGU MMOJA, Vijana hawa
katika kutafuta hifadhi walikimbilia katika pango kujinusuru na walipo kuwa
huko pangoni MOLA wao akawajaalia kulala, na walilala kwa miaka 309. Vijana
hawa walipo amka kutoka kwenye usingizi wao, hawakujua ni muda gani walilala,
walidhani wamelala siku moja au sehemu ya siku.
Iliwabidi kumtuma mmoja wao
mjini kwenda kuwatafutia chochote wale kutokana na njaa waliyo kuwa wakisikia,
aliyetumwa alipofika mjini alikuta mji umebadilika, dini ambayo mwanzo ilikuwa
imepingwa na kuwafanya wao wakimbie waliikuta ndiyo dini ya serikali, lakini
waliikuta dini hii tayari imeshabadilishwa vibaya sana, upagani umeingizwa
ndani ya dini hiyo, sarafu yao nayo ilikuwa yakale mno, maneno aliyo kuwa
akiyatamka, nguo alizo kuwa amevaa, ni vitu vya karne tatu nyuma na muongo
mmoja kasoro mwaka mmoja, walikuwa kama kioja, lakini pia walikuwa ni watu wa
ajabu, muda taarifa zilitapakaa kila kona ya mji…
Hapana shaka hii ilikuwa ni
hadithi ya kuvutia mno, basi Waarabu kupitia kwa wafuasi wa Ukristo na Uyahudi,
walikuwa wakiambiwa vitu vya kumjaribu navyo Muhammad, Rehma na Amani ziwe juu
yake, wakitegemea atashindwa kujibu vitu hivyo ili waweze kumpinga, ndipo
wakataka kujua hadithi ya watu wa pangoni toka kwa Muhammad.
Si kwamba Mtume
Rehma na Amani ziwe juu yake aliwaelezea hadithi yenyewe, lakini pia aliwaambia
kuhusiana na vile ambavyo walikuwa wakitofautiana juu ya hadithi hiyo, lakini
zaidi aliwapa na somo linalo patikana kwenye hadithi hiyo, tizama tafsiri ya
Quran kutoka kwa Yusuph Ali, hapana shaka amekieleza vyema kisa hichi.
Kwenye Quran kisa hichi kilipo
tajwa, MUNGU MMOJA, hakutaja moja kwa moja miaka 309, bali, alisema miaka mia
tatu jumlisha na tisa. Nambari zote zilizo tajwa kwenye Quran, jumla ya nambari
hizo ni kigawanyo cha nambari 19, ambayo ndiyo code ya Quran. Hivyo basi endapo Quran ingesema moja kwa moja 309,
jumla ya nambari hizo zisingeweza kugawanyika kwa 19.
Hadithi ya vijana hawa 7,
maarufu kwa ulimwengu wa Kikristo kama Seven
Sleepers, imeanzwa kutajwa kwenye aya ya 9 mpaka aya ya 25. Aya zote hizo
ni kuhusu vijana hawa saba, na aya ya 25 ikasema vijana hawa wamekaa kwenye
pango kwa miaka 300+9. Kuanzia vijana hawa walipoanza harakati za kuinusuru
imani yao, mpaka walipo ingia pangoni, Quran imetumia maneno 308 na neno la 309
ni neno la 300+9.
Ni muda gani vijana hawa
walikaa pangoni
|
309
|
Ni maneno mangapi
yametumika kuanzia mwanzo wa aya inayo waelezea vijana hawa mpaka muda walio
kaa pangoni
|
309
|
Ingawa sura hii, NAMTAFUTA MUNGU,
ni moja ya sura muhimu sana kwenye Posti hiz, sura zilizo tangulia ni kama
utangulizi wa kuitambulisha hii sura, nisingependa kuifanya ndefu kiasi cha
kumchosha msomaji wangu, ningeshauri kwa ufafanuzi mpana, maarifa na elimu
zaidi juu ya Quran, msomaji avipitie vitabu nitakavyo vitaja na ambavyo kwa
njia moja ama nyingine, nimevitumia kwenye kazi hii, vitabu hivyo kwa sababu
moja kwa moja vina zungumzia somo hilo kwa kina, hapana shaka vitawakilisha
kazi yenye tija na matokeo mazuri kwa msomaji anaye taka kuufahamu ukweli, si
dhani hata kidogo mpaka hapa ulipofika kwenye kukisoma kitabu hichi ni kwa
ajili ya starehe, hapana, kuna ambacho unacho kitafuta, na kitabu hichi ni
utangulizi tu wa kile unacho taka kukifahamu, basi pitia vitabu hivi na vingine
ili uweze kuwa huru, na sehemu kubwa ya vitabu, makala, majarida yaliyo tumika
humu yanapatikana bure kwenye wavuti, ni jukumu lako kuvitafuta.
Kwa ajili ya
undani kuhusu Quran tafadhali pitia kazi za Harun Yahya, tafsiri ya Quran ya
Yusuph Ali na ile ya Ibn Katheer, The Bible, The Quran and The Science cha Dr.
Maurice Bucaille na The Quran Unchallengeable Miracle cha Caner Taslaman,
kuvitaja kwa uchache.
Ulimwengu umeumbwa kwa kufuata
taratibu na kanuni maalum, na viumbe vyote tunavyo vifahamu na vile tusivyo
vifahamu navyo, vimeumbwa kwa malengo, taratibu na kanuni mahususi. Uhai wa
ulimwengu huu na vyote vilivyomo umeegemea kwenye kanuni hizo, kitendo hicho
cha ulimwengu na vyote vilivyomo kuwemo ndani ya kanuni hizo, kuziheshimu na
kuzifuata vilivyo, ndicho kinacho itwa kujisalimisha, ulimwengu wote na vyote
vilivyomo umejisalimisha katika sharia na kanuni hizo takatifu za maumbile,
yaani ulimwengu wote ni Islam, umejisalimisha.
Hali kadhalika mwanadamu naye,
anawajibika juu ya kanuni na sharia hizo, tofauti na viumbe wengine, binadamu
na majini wao wanayo hiari, ya kuzifuata au kutozifuata sharia hizo, lakini
vyovyote watakavyo amua kutokana na uhuru walio pewa, malipo yake watayakuta
mbele ya MOLA wao.
Hivyo kwa mwanadamu, kukubali kuwa yeye ameumbwa, na
amewekewa sharia na mipaka, ambamo anatakiwa kuishi kwa kufuata kanuni hizo, na
anawajibika juu ya vitendo vyake, hilo ndilo lengo kuu la Uislamu kuanzia kwa
mtume Adam (a.s) mpaka mtume wa mwisho Muhammad (s.a.w)
Hivyo mwanadamu anayo HATMA ya
kuwepo hapa, malengo mahususi. Binadamu analo jukumu zito zaidi kwa yeye kuwepo
hapa, jukumu ambalo litaamua, hatma ya maisha yatakayo fuata baada ya haya.
Kama tulivyo ona tabia ya roho ni tofauti sana na mwili wenyewe, imekuwa
ikikitafuta kile ambacho mwili haukielewi, hatma yake.
Tumeona na kujiuliza kwa
nini mtu maarufu leo duniani mwenye utajiri unao tosha kulisha vizazi na vizazi
kwa karne na karne, kwa nini afe na kuuacha nyuma huo utajiri, ikiwa hatma yake
mwanadamu ni hapa duniani?
Hebu tutizame maisha yetu
wenyewe, ndoto zetu za utotoni, za ujana, mipango yetu, ni nini kimebakia
katika hayo? Tumekuja duniani hali ya kuwa ni madhalili na baada ya hapo tukawa
tegemezi juu ya mazingira yetu.
Haijalishi tumezaliwa kwenye jumba la kifalme
au kwenye kibanda, migombani au hospitalini, tukiwa na maarifa kidogo au hatuna
kabisa, tukiwa na mwonekano ‘mzuri’ au ‘mbaya’, ukiwa nacho au huna, ni kiasi
gani uwezo wa maumbile yetu unaweza kusimama dhidi ya mazingira yetu, ambayo
roho zetu unayakana? Zaidi tunavyo yafahamu mazingira yetu, ndivyo tunavyo zidi
kuyaogopa, ndivyo tunavyo zidi kuzikimbia ndoto zetu.
Tunapo tambua kuwa tupo hapa
duniani si kwasababu ya nasibu, wala
hatuishi hapa na kuendelea kwa sababu ya natural
selection, na yote yanayo tokea si kwasababu ya survive for the fittest, lakini kwa sababu na malengo mahususi
ambayo hatma yake imelala kwenye dunia nyingine.
Tunapo tambua kuwa hatma yetu
ni juu ya namna tutakayo ishi hapa, na hatuwezi kuishi kama tutakavyo, bali kwa
kufuata kanuni, taratibu na sharia za kimaumbile alizo ziweka MUUMBA mwenyewe,
kanuni ambazo katufunza kupitia mitume wake mbalimbali, hapo tunautambua Uislamu,
hapo tunautambua, ujumbe mmoja, toka kwa Mungu Mmoja, kwa watu wote wa zama
zote, na tunapoufuata, basi tunakuwa Waislam, yaani wale waliojisalimisha, kwenye sharia na kanuni hizo za maumbile zilizo wekwa na
MUNGU MMOJA.
No comments:
Post a Comment