“Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilimu, wameshuhudia kuwa hakika
hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu ila Yeye
Mwenye nguvu na Mwenye hikima.”
“Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa
Kitabu hawakuhitilafiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio
kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi
Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.” (Quran 3:18-19)
Leo nataka tuzungumzie mada moja tata kidogo, pana lakini iliyofanywa ndogo na akili zetu ... nataka tumtafute Mungu
Je ni kweli kuna ‘Mungu’ yaani
yule mbaye aliyeumba vyote tuvionavyo na tusivyo viona, tunavyo fahamu na
tusivyo fahamu. Au ni ‘ulevi’ wa imani za kidini unao tufanye tuamini kuwa
Mungu yupo.
Ni kweli kuna haja ya kuwa na ‘Mungu’ katika maisha yetu ya kila
siku au ni ufinyu wa fikra za kibubusa zinazo tufanya tuamini kuwa hatuwezi
kuishi bila ‘Mungu.’ Je huyo ‘Mungu’ alitokea wapi, asili yake ni ipi? Je anao
wazazi, watoto je? Haya ni mengine mengi ni moja ya maswali mazito yanayo
izunguka nadharia au imani ya kuwepo kwa ‘Mungu.’
Maswali haya yamebeba uzito
mkubwa sana katika fikra za viumbe huru hawa wawili, binadamu na majini.
Lakini ugumu wa majibu katika
maswali haya na uhakika wa majibu hayo unakwazwa na nyenzo duni za ‘mtafiti’ wa
maswali hayo na pili ‘mtafiti’ mwenyewe hajitambui kuwa yeye ni nani, ni nini
hasa makusudio ya yeye kuwepo kwenye eneo hili linalo itwa dunia.
Hivyo ikiwa
‘mtafiti mwenyewe atashindwa kujitambua, kutambua asili yake, imekuwaje akawepo
hapa ni wazi pia hatoweza kutambua nini hasa makusudio ya kuumbwa kwake na
zaidi hata asili ya kila kinacho mzunguka na aliyeviweka hapo hatoweza
kumtambua.
Hivyo utaona hata majibu ya maswali magumu juu ya kuwepo kwa MUNGU
hayatokuwa na mashiko bali dhana na nadharia ambazo zitakubaliwa katika kipindi
fulani cha historia na kukatiliwa katika kipindi kitakacho fuata.
Kwakuwa ‘mtafiti’ huyu ameanguka
katika hatua za awali na zilizo za msingi katika ‘utafiti’ wake, majibu yake ya
mwisho katika suala analo lifanyia utafiti yatakuwa na msururu wa makosa ya
msingi na udhaifu mkubwa katika kujibu dhana nzima ya kuwepo au kutokuwepo kwa
Mungu.
SEARCH FOR THE GOD?
Binadamu na Majini kama mashine au viumbe ambao mpaka sasa kwa mnasaba
wa post hii hatujafahamu asili yao ni wapi, basi hawawezi hata kidogo kujibu
swali la kwa nini wapo hapa. Mathalani mashine yoyote ile haiwezi kujiamulia
sababu ya kutengenezwa kwake, bali ni yule aliye itengeneza ndiye anaye fahamu
ni nini makusudio ya kutengeneza mashine hiyo.
Halikadhalika majini na wanaadam
mpaka watakapo weza kufahamu ni ipi asili yao, hawatoweza kujibu swali la ni
yapi madhumuni ya wao kuwepo hapo na hivyohivyo hawato weza kujibu swali la ni
nani aliye nyuma ya vyote wanavyo viona na wasivyo viona.
MASHINE ITAWEZA KUMTAMBUA MTENGENEZAJI WAKE?
Lakini kupatikana kwa ‘mtafiti’
mwenyewe katika mazingira haya inatosha kumfanya ‘mtafiti’ akiri kuwepo kwa
nguvu inayo simamia maisha ya ‘mtafiti’ ambaye endapo ataikana nguvu hiyo basi
moja kwa moja atafanya kosa la kimsingi kabisa kwa kuipatia nguvu hiyo jina
jingine au kumpatia mwingine asiye stahiki nguvu hizo.
Historia kwa zama zote
imethibitisha kuwepo kwa kosa hilo. Hivyo swali la msingi juu ya kuwepo kwa
MUNGU haliwezi kujibiwa na kuthibitishwa na yeyote isipokuwa MUNGU mwenyewe.
Kama ambavyo mashine haiwezi kujibu swali la ni nini kazi yake ndivyo ilivyo
kwa binadamu na majini hawawezi wao binafsi kwa kutumia uduni wa ufahamu wao,na
uduni wa zana atakazo zitengeneza kutokana na ufahamu huo kuweza kujibu swali
tete na lililo na msingi wa mustakabali wa maisha yake na vyote vinavyo
mzunguka juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa MUNGU.
Charles Darwin, mwana materilist ni miongoni mwa walio fanya
kosa hilo katika nadharia yake ya ‘evolution.’
Kwa vile Darwin alikataa juu ya kuwepo kwa yule ambaye anaweza kufanyiza uhai
katika ulimwengu wote, mazingira ya ulimwengu yakawa ni magumu kuachwa bila
kutafutiwa ‘yule’ ambaye anaweza kuwa ndiyo sababu ya ulimwengu kutokea.
Hivyo
Darwin ‘uwazi’ au nafasi hiyo akaijaza kwa kutumia, ‘uwezekano wa kinasibu’ au
kibahati ndiyo uliyo weza kuleta maisha katika ulimwengu na vyote vinavyo
tuzunguka.
Lakini kibaya zaidi ni kuwa nadharia hii ya Darwin haikuweza hata
mahala pamoja katika sayansi ya utafiti kuthibitisha ukweli wake.
MTAZAMO WA UMMA JUU YA NADHARIA YA EVOLUTION
Kutokana na nadhari ya bwana
Darwin ni kuwa vitu kadhaa visivyo na uhai vilikuja pamoja kwa nasibu na
kutengeneza ‘seli hai’ ya kwanza.
Kosa la kwanza kabisa kwenye hili ni Darwin
kuacha kuelezea kitu kimoja ambacho ni kidogo mno, lakini chenye maana kubwa mno
kwenye darasa zima la uumbaji nacho ni asili ya vitu hivyo vilivyo jikusanya
kwa nasibu na kutengeneza seli hai ya kwanza.
Kwenye ulimwengu wa Darwin ni
kama vitu ‘visivyo hai’ vilisha kuwepo kabla, lakini asili ya hivyo ‘vitu
visivyo hai’ ni wapi? Kiuhakika kabisa madai haya ya Darwin yalikuwa na makosa
ya msingi kabisa kwenye ulimwengu wa tafiti za kisayansi. Kisha Darwin
akaendelea na makosa yake ‘kibubusa’ kama ifuatavyo;
NADHARIA YA EVOLUTION KATIKA PICHA
Seli hai hiyo moja iliyo
patikana kwa nasibu, ikageuka kwa nasibu tena na kuwa kiumbe hai cha kwanza
kama mnyoo, kisha kosa likaendelea tena kuwa mnyoo huyo mmoja kwa nasibu tena
akageuka na kuwa kiumbe hai kingine, na kingine, na kingine mpaka dunia yetu
hii ikajaa viumbe wote unao waona ukiwemo wewe mwenyewe unayesoma posti hii.
BUT HIMSELF HE LOOK LIKE MONKEY PERHAPS WHY HE CAME WITH THE THEORY
Ingawa nadharia hii ni kichekesho, haikuweza kuoneka hivyo kipindi ambacho
inaanzishwa, na kupewa ushirikiano na wale ambao wanaitwa ni ‘wanasayansi’
ingawa nadharia hiyo haijafuata sharia yoyote ya kisayansi kukazidi kuipa nguvu
na kuisambaza kote duniani.
NDIYO WATOTO WETU WASIFUNDISHWE UDARUWIN NA EVOLUTION.
Ikafundishwa kwenye mitaala mbalimbali, kibubusa
au hata kwa makusudi. Mpaka leo bado nadharia hii inafundishwa pamoja yakuwa
nuru kali ya sayansi ya leo inathibitisha makosa ya msingi ya nadharia hii,
lakini watu fulani wenye ajenda ya ‘kumfuta’ au ‘kuzima’ nuru ya muhusika
katika sanaa hiyo ya uumbaji wanaendelea kwa uduni na udhalili wa mbinu zao kuipigia
debe nadharia hii na kuendelea kuifundisha.
KAZI INAENDELEA YA KUPOTOSHA VIZAZI NA VIZAZI
Kama walivyo materilist, Freemasons nao wanamkana Mungu, ingawa materialisim wao wanakana kabisa dhana
ya uumbaji, Freemasons wao wanaikubali lakini hawampi Mungu Mmoja sifa hiyo
bali miungu wengine wanao wakubali wao, akiwemo shetani.
MMOJA WA MIUNGU YA KIFREEMASON ANAYEFAHAMIKA KAMA JAHBULON
Hivyo nadhari hii ya
Darwin ilikubaliwa kote kwa materilist na Freemasons, ingawa kila mmoja aliikubali
kwa sababu tofauti na mwingine. Materilist wao waliikubali na bado wako na
nadharia hii ya Darwin kwa vile ndiyo njia nyepesi ya kukidhi mahitaji yao ya
kuonesha kuwa hakuna Muumba, kwa wao nadharia ya Darwin inakubalika si kibubusa
tu, bali kisayansi.
FREEMASON NA EVOLUTION NI TOTO YA DUGU BOJA.
Kwa Freemasons kwa vile wao wana lengo la kuwaongoza
walimwengu wote kwenye shimo la kiza, kukataa kuwepo kwa Muumba ni njia nyepesi
kwao katika kuwasaidia kuwapotosha walimwengu na lengo lao mahususi la kuumbwa
na kuwapatia malengo mengine kama tulivyoona, hivyo nadharia hii Freemasons
wanaikubali si kwasababu wanakataa uumbaji, lakini kwa vile wanamkataa Muumbaji
mwenyewe.
NADHARIA YA UUMBAJI KWA FREEMASON IMEEGEMEA KWA WAUNGU WA KIPAGANI.
Hivyo nguvu kubwa ya fedha, wanasayansi, wanahistoria, watafiti na utafiti
vilitumika katika ‘kuibariki’ nadharia hii ya evolution. Mazingira yasiyo
halisi yakatengenezwa, masalio yasiyo halisi nayo ‘yakavumbuliwa,’ na yote
yakija na hadithi nzuri za kuipa nguvu, kuipamba na kuikamilisha nadharia hii
ya evolution.
Lakini yote waliyo kuwa wakiyafanya kwa ajili ya kuuhadaa ulimwengu
na walimwengu yalianguka patupu, kama wasemavyo waungwana; njia ya muongo ni fupi.
Hakuna nyanja yeyote ya sayansi inayo
husiana na suala zima la viumbe na uhai iliyo weza kuthibitisha madai ya
Darwin, siyo microbiology, wala biomathematics, wala cell biology, wala
biochemistry, wala genetics, au anatomy, au physiology, au anthropology na wala
hata paleontology, isipokuwa nyanja zote hizo zimefanikiwa kuweka mezani
ushahidi usio na shaka na usio hesabika kwa wingi ambao unaivunja vunja nadhari
ya evolution.
Lakini huo haukuwa mwisho wa
‘tafiti’ hizo au nadharia hiyo, kwa vile the
end justifying the means, kuitupilia mbali nadharia hii inaonekana ni
gharama mno kwa Freemasons na wana materilist, kuitupa nadharia hii
kutahalalisha kufunguliwa kwa makufuli mazito na minyororo mizito ya kifikra
waliyo fungwa walimwengu tangu kuja kwa nadharia hii, mabuku rejea ya chomwe,
kazi mbalimbali za ‘kitafiti’ na urongo zichomwe, ‘wanahistoria,’ na
‘wanasayansi’ wapoteze kazi na fedha, msumari wa mwisho ugongwe kwenye jeneza
la wanamaterilist na kifo cha wanamasonia kitangazwe.
hakuna ambaye kajiandaa
kwa hili, hivyo kwa gharama yeyote ile nadharia ya Darwin lazima iendelee
kupewa hadhi ya kisayansi na sifa zisizo zake, utafiti uzidi ‘kutengenezwa,’ na
‘kuvumbuliwa’ ili kunusuru uso wa sayansi ya leo.
Masalio halisi ya historia katika udongo (fossil) yamekuwa ndiyo kikwazo
kikubwa kwa nadharia hii ya Darwin. Masalio hayo yanathibitisha kuwa maisha ya
viumbe wote duani hayakupitia mabadiliko yanayo elezewa na Darwin. Utafiti
wenye mashiko unakubali kuwa viumbe hai wako vilevile kama walivyo kuwa
mamilioni ya miaka kabla ya leo, yaani hawakupitia kitu kinacho itwa
‘evolution.’
AINA HII YA MASALIO NI KIKWAZO KWENYE NADHARIA HII YA DARWIN, SABABU HAYA NI MASALIO YA ZAIDI YA MIAKA MILIONI MIAMOJA NA ... HAYAONESHI KIUMBE HICHI KUPITIA MABADILIKO YEYOTE YALE.
Masalio ya historia katika udongo ni kama maandishi yasiyo futika. Masalio
hayo ni sehemu ya kiumbe kilicho pata kuwepo eneo hilo. Kutokana katika kona
mbalimbali za dunia, masalio hayo yame patikana na kuweza kueleza ni kiumbe
chanamna gani kilichopata kuwepo eneo hilo.
Masalio hayo yanathibitisha kuwa
viumbe walipatikana wakiwa wako kamili, wala hakuna masalio yanayo onesha
kiumbe kikibadilika kutoka kiumbe fulani kwenda kingine. Hii ni kuthibitisha
kuwa uhai kwenye ulimwengu huu umeumbwa kutoka kusiko na chochote. Lakini pia
masalio ambayo tunakutana nayo kwenye mabuku rejea, majarida, makala na vyombo
vingine vya habari; ambayo yanaonesha kuwa uhai umetokea kwa nasibu, na viumbe
wamekuwa wakibadilika hatua kwa hatua si masalio ya kweli bali ni yakutengeneza
na kughushi.
MIAKA MILIONI MIA MOJA, YUPO VILE VILE KAMA HAWA TUNAO WAONA SASA.
Kwenye masalio hayo kutoka kwenye kona mbalimbali za dunia na yaliyo kusanywa
kwa muda mrefu yameendelea kuthibitisha kuwa, samaki tunaye mwona leo ndiye
samaki aliyekuwepo mamilioni ya miaka kabla, wadudu wa leo ndiyo wadudu wa
mamilioni ya miaka kabla, hali kadhalika kwa ndege, reptilia na wewe mwenyewe,
hakuna aliye badilika kutoka umbile la kiumbe fulani na kuelekea kwenye umbile lingine
lililo bora zaidi, bali vyote vimekuwa na maumbile yake kamilifu tangu enzi na
enzi.
MIAKA MILIONI 300, LAKINI MPAKA LEO ANAONEKANA VILEVILE, HAKUNA MABADILIKO
Kiumbe hai kinapo kufa tishu laini ambazo zinapatikana kwenye misuli ya
kiumbe hicho na viungo vingine havichukui muda kuanza kuoza. Katika mazingira
ya baridi kali au sehemu ambazo barafu inapatikana ikiwa imegandamana, tishu
hizo zinakuwa haziozi, hivyo kiumbe hupatikana akiwa mkamilifu. Sehemu zilizo
ngumu kwa kiumbe husika ndizo zinazo stahimili muda mrefu sana na kuweza
kutengeneza masalio yake. Kwenye mimea mara nyingi huwa ni sehemu ngumu ya mmea
kama vile shina lake na hata wakati mwingine majani yake kutegemeana na
mazingira ya eneo husika.
Darwin anasema kuwa uwezo wa sokwe kuweza kuigiza tabia za binadamu inatosha
kabisa kusema sokwe ameweza kubadilika na kufikia binadamu wa leo. Sokwe anapo
fundishwa kufanya vitu mbalimbali vinavyo fanywa na binadamu, huvifanya vizuri
vitu hivyo, anawezwa kufundishwa kutofautisha rangi na maumbo ya vitu
mbalimbali, lakini dai hili ni duni mno kulinasibisha na kulifanya ndiyo moja
ya misingi ya dai la kubadilika kwa viumbe hasa sokwe kutoka hatua hiyo na kuwa
binadamu; kwa sababu kuna viumbe wengine wengi ambao wana utambuzi na ufanisi
mkubwa katika vitu mbalimbali wanavyo weza kufundishwa, kama vile mbwa, paka,
farasi, ndege na wengineo. Lakini kwa nini kubadilika na kuwa binadamu kiumbe
aliye huru kutokee kwa sokwe peke yake na siyo hao viumbe wengine, au kwa nini
evolution imruhusu sokwe na manyani kuwa binadamu na iwazuie hao wengine.
Mathalani ndege aina ya kasuku anapo fundishwa, anaweza kutofautisha kati
ya umbo la duara na mraba, rangi nyekundu na bluu, na anaweza kupanga vitu
katika uwiano ulio sawasawa, lakini zaidi Kasuku anaweza kuongea kwa kuigiza
sauti ya binadamu, kitu ambacho sokwe hawezi kufanya; kutokana na nadharia ya kibubusa
hapana shaka kasuku alikuwa na nafasi kubwa kabisa ya kuwa binadamu kuliko
sokwe[1], lakini Darwin mwenyewe
kasha mchagua sokwe wake.
Wanakaa kwenye meza makubwa ya duara, wamevaa miwani zao, wanataja mabuku
makubwa ya rejea, wanataja maneno ya Kilatini, kwa kujua au bila kujua na
kukuambia sokwe amevuka daraja na kuwa binadamu, lakini nyani alikuwa, bado
yuko, na ataendelea kuwa nyani na hivyo ndivyo ilivyo kwa viumbe wengine wote.
Huu ni ukweli wa msingi kabisa ambao tafiti zinazo fuata sharia ya sayansi ya
utafiti zinavyo tueleza, hivyo ndivyo tunavyo ona kwenye maisha yetu ya kila
siku, na hivyo ndivyo ile sauti yetu ya ndani kabisa inavyo sema, kwamba nyuma
yetu yupo ambaye ameyafanya haya na wala hayajatokea kibubusa kama Freemasons
nyuma ya ajenda zao wanavyo tueleza.
HOW CAN DARWIN EQUATION FIT HERE???
Inakadiriwa kupatikana kuwepo kwa aina 6,000 za sokwe kote duniani katika
zama zote za historia, na wengi kati ya aina hizo za sokwe wamekwisha futika.
Leo hii kuna aina 120 tu za sokwe walio bakia. Rasilimali kubwa ya wana
evolution ipo kwenye aina hizi 6,000 za sokwe walio pata kuishi kwenye mgongo wa
aridhi.
Wanatengeneza mazingira ya mabadiliko ambayo wanadai binamu alipitia mpaka
kufikia binadamu kamili kwa kupanga mafuvu ya sokwe walio toweka pamoja na ya binadamu
na kisha kuyatolea maelezo yao yakibubusa. Kwa njia hii hata msomi aliye shikwa
akili anaingia ‘line.’ Lakini hata
hivyo wakati umefika wa kuchora mstari mwekundu kwenye mbinu hizo, wapo
watafiti huru na wasomi ambao, maslahi ya uma yanakuja kwanza na tafiti hizi
zinatuthibitishia kuwa yote hayo yanayo fanywa na wana evolution si kingine
bali kughushi kukubwa mno.
Ikiwa nadharia yao ni ya kweli kwa nini basi
wanaghushi, masalio, maelezo na hata mazingira lakini zaidi mpaka hongo za aina
kwa aina zinatolewa ili makosa ya msingi kwenye nadharia hiyo yafumbiwe macho.
Kwa nini?
FUVU LA PILTDOWN MAN
Piltdown man, masalio haya yanasemwa yaligunduliwa mwaka 1912 na Charles
Dawson, wakasema masalio hayo yana muda wa miaka 500,000, nayo yalichukuliwa
kama ushahidi tosha wa maendeleo katika mabadiliko ya kutoka kwenye sokwe kuwa binadamu.
PAMOJA NA KUGUNDUA UGHUSHI HUO LAKINI BADO WANAENDELEA KUTUFUNDISHA KUWA EVOLUTION ILITOKEA.
Lakini miaka arobaini baadaye na baada ya ‘masalio’ hayo kupatikana wanasayansi
wakaamua kuyachunguza tena na wakakuta kuna ughushi wa hali ya juu mno.
Fuvu la
Piltdown Man liligundulika kuwa ni fuvu la binadamu hasa aliye ishi miaka 500
iliyo pita. Mfupa wa taya la chini ni taya la sokwe aliyekufa karibuni, meno
yake yalibadilishwa na kuongezwa ili yaweze kufanana na binadamu, Kisha mifupa
yote ikapakwa potassium dichromate ili iweze kuwa na mwonekano wa kale.[2]
THEY CAN LIE AT WHATEVER COST AND TIME, JUST
TO MAKE SURE YOU REMAINS IN CHAIN AND FOOL.
Mwaka 1922, Henry Fairfield Osborn, mkurugenzi wa American Museum of Natural
History, alitangaza kuwa amefanikiwa kupata jino la gego la zama za Pliocene.,
KWA KUTUMIA JINO HILO MOJA UKWELI FAMILIA NZIMA IKAJENGWA, HII NDIYO SAYANSI YETU.
Jino hilo lilikuwa na sifa za sokwe na binadamu na likasemwa kuwa linatokana na
‘Nebraska Man’ eneo ambalo jino hilo ‘liligunduliwa.’
Kwa kutumia jino hilo
moja mifupa ya ‘Nebraska Man’ ilipatikana na mtu kamili akatengenezwa, na hata
familia nzima ya Nebraska Man ikapatikana.
HOW FAR CAN THEY GO TO MAKE US BELIEVE IN THEIR THEORY ...?
Lakini mwaka 1927, mifupa mingine
inayo husiana na jino hilo ilipatikana, na ushahidi huo mpya ukathibitisha kuwa
jino hilo la gego siyo la sokwe wala binadamu bali ni la nguruwe pori anaye
patikana Marekani anayefahamika kama Prosthennops.[3]
YES, HALIKUWA JINO LA BINADAM, BALI LA NGURUWE, LAKINI CHA AJABU JINA LA NGURUWE LILIWEZA KUUNDA MIFUPA SI YA BINADAM MMOJA, BALI WA FAMILIA YAKE YOTE. MAAJABU YA DARWIN HAYO NA EVOLUTION YAKE.
Mwaka 1932 kiroja kingine kilipatika India, ‘masalio’ ya kile kilicho itwa Ramapithecus yaligundulika. Masalio hayo
yalidai kuthibitisha ule mstari ambao sokwe alibadilika na kuwa binadamu, tukio
ambalo wana evolution wanadai kutokea miaka milioni 14 iliyo pita. ‘Masalio’
haya ya Ramapithecus yalitumika kwa
miaka 50 kama ushahidi wa msingi kabisa kuthibitisha nukta hiyo ya mabadiliko
kutoka sokwe kwenda binadamu.
Lakini tafiti zilipo kuja kuchukua nafasi yake,
tafiti za kweli ilibainika kuwa meno ya Ramapithecus
yanazo sifa zilezile walizo nazo sokwe. Mwaka 1982 Aprili, jarida la Sayansi
likiwa na makala ya “Humans lose an early ancestor” lilitangaza kuwa Ramapithecus ni sokwe wa aina ya
orangutan ambao wamesha futika.[4]
Tunaweza kwenda zaidi na zaidi katika kuonesha mapungufu kwenye ‘masalio’
ya Darwin na evolution yake, hata hivyo kuna kazi mbalimbali zilizo fanywa
kwenye hili somo, ningeshauri kwa wakati wako binafsi uzipitie mwenyewe
uliuweze kuona, na mmoja kati ya wasomi na watafiti walio weza kufanikisha hili
ni Harun Yahya, unaweza kutembelea wavuti wake na utajionea kazi hizo kwa kina kirefu,
na ikiwa hutaweza kutosheka na hilo kunayo mabuku rejea aliyo yataja kwenye
kazi hizo, majarida ya kisayansi na vyanzo vingine, basi unaweza kuvipitia ili
kuweza kujikinaisha mwenyewe.. Utamu wa
ngoma ni uingie ucheze.
Kama ulivyo kwisha kuona hakuna utafiti wa kisayansi, ila ule wa kughushi
unao thibitisha juu ya nadharia hii ya evolutiona na hadithi za Darwin. Wapo
wanasayansi ambao wanaamini nadharia hii eidha kibubusa au wanayo ajenda
tofauti na nadharia hiyo, na haswa tunakuwa na shaka kama kweli ni kibubusa
hasa pale wanapo amua kughushi tafiti zao ili kuwapotosha walimwengu, swali la
msingi ni kwa nini basi wanaghushi?
Wakati Darwin alipo amua kuivalisha nadharia yake nguo, au kuelezea
mazingira yaliyo pelekea kupatikana kwa evolution, Darwin alikuja na ‘survive for the fittest.’ Yaani
aliyekuwa na nguvu ndiye aliyeishi, aliyeweza kuhimili misukosuko mbalimbali
ndiye aliyeweza kubadilika kutokana na mazingira hayo na kuhama kutoka kiumbe
kimoja kwenda kingine.
Hivyo maendeleo ya viumbe hao yalitegemeana na uwezo wa
kiumbe husika kupambana na mazingira yake. Mwenye nguvu ndiye aliyeshinda.
Mdhaifu alifutika kabisa. Hivi ndivyo Darwin anavyo beba nadharia yake.
Darwin anadai kuwa mpambano huo wa kuishi haupo tu kwenye mazingira bali
ndani kabisa kwenye moyo wa viumbe wote, ‘survive for the fittest’ ni moyo wa
shughuli za viumbe wote, ni dira na mwelekeo kwa viumbe hao, ndiyo kitu pekee
kinacho chochea maendeleo kwa viumbe hao zama hadi zama. Kwenye kitabu chake
kilicho kwenda kwa jina la The Origin of
Species, "The Origin of Species by Means of Natural Selection or the
Preservation of Favoured Races in the Struggle for Life", anaelezea
kwamba ‘fight for survival,’ si
kwamba inapatikana kwa hayawani tu lakini pia kwa makundi ya rangi mbalimbali
ya binadamu. Hivyo watu wa rangi fulani ni bora juu ya watu wa rangi nyingine
kutokana na uwezo wao wa kuhimili mpambano wa ‘fight for survival.’
NADHARIA HII INAFUNDISHA KWAMBA MATAIFA YAMENDELEA HATUA MBALIMBALI ZA EVOLUTION, ISPOKUWA KWA WATU WEUSI NA BARA LAO, WAO BADO WAKO KWENYE KUNDI LA SOKWE, YAANI KUWA MWEUPE NDIYO KUWA BINADAM MKAMILIFU.
Darwin akasema kuwa watu wa rangi nyeupe, (Wazungu) ndiyo kundi ambalo
linaonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kupambana kushinda kwenye ‘fight for survival,’ wakati watu kutoka
bara la Afrika na Asia wakiwa wameachwa nyuma katika mpambano huo na hivyo
kuashiria kuwa muda si muda watu weusi na watu wa Asia watafutika kabisa
kutokana na kushindwa kwao na watu weupe hasa kutoka bara la Ulaya ndiyo
watakao bakia, au survive.
NOT ME SAID THAT! ITS DARWINISIM
Utaona kuwa nadharia ya Darwin ilizaa ugonjwa mwingine mbaya sana, ugonjwa
wa ubaguzi wa rangi, kwani watu wa bara la Ulaya kutokana na nadharia hii ni
kuwa wao tayari wamesha fanikiwa na kuendelea katika hali ya ubinadamu kamili,
wakati watu wa Afrika na Asia wao wameachwa nyuma na wapo kwenye hatari ya
kufutika kama walivyo futika viumbe wengine.
Hivyo mtu yeyote asiyekuwa mweupe
wa Ulaya yeye bado yupo kwenye hatua ya mabadiliko ya kuelekea kwenye ubinadamu
kamili, wakati mtu mweupe wa Ulaya tayari yeye ni binadamu mkamilifu. Uwazi huu
baina ya hawa binadamu wawili wa Darwin utapelekea binadamu wa Asia na Afrika
kufutika kabisa kwani mwenzao wa Ulaya tayari keshakamilika na tayari anafahamu
mbinu na njia za ‘fight for survival,’
zaidi kuwashinda wenzake na hivyo yeye pamoja na masokwe wengine wote
watatoweka.
Mwana anthropologist wa India Lalita Vidyarthi anaelezea ni namna gani
nadharia ya Darwini ilivyo leta ubaguzi wa rangi kwenye fani ya sayansi ya
jamii;
“Nadharia yake (Darwin) ya survive of the fittest ilikaribishwa na
kukumbatiwa na wana sayansi ya jamii wa kipindi hicho, na waliamini kuwa binadamu
amefanikiwa katika hatua mbalimbali za evolution, mafanikio ambayo yana onekana
kwa watu weupe wa Ulaya (Wazungu). Katika nusu ya pili ya karne ya kumi na tisa
ubaguzi wa rangi ulikubaliwa kama ukweli wa msingi na sehemu kubwa ya
wanasayansi wa Ulaya”[5]
BLACK MAN CONSIDERED TO A PROPERTY OF WHOMEVER MAY HOLD ON 'IT' FIRST AND HE CAN SALE 'IT' TO WHOMEVER HE WANT TO WHATEVER PRICE HE WANT AND ME MAY USE 'IT' IN WHATEVER MANNER HE DESIRE. AND IF THE MASTER CHOSE TO KILL 'IT' NO PROBLEM IT IS YOUR PROPERTY, SO DO AS YOU PLEASE.
Kwenye sayansi ya leo nadharia ya Darwin si kwamba imeshindwa kuthibitisha
madai yake, lakini zaidi ni kwamba imepitwa na wakati, mbele ya uso wa kweli wa
masalio ya kihistoria nadharia hiyo inayeyuka kabisa. Hivyo madai ya msingi ya
nadharia hiyo ambayo ni kukataa kuwepo kwa Muumba nayo yanakuwa yameruka
patupu.
Hayana ushahidi wowote ule. Hadaa na uongo wa aina kwa aina unatumika
kuibeba nadharia hii, eidha kwa kughushi hayo yanayo itwa masalio ya kihistoria au
kwa kupika taarifa mpya ambazo zinaonekana zitaibeba nadharia hiyo lakini bado,
penye ukweli uwongo hujitenga, na penye nuru kiza hutoweka, kila wanalo kuja
nalo bado linakuwa na soni kwenye uso wa sayansi ya leo, soni ya kushindwa na
kudhalilishwa kwa kila ‘uvumbuzi’ wanao kuja nao.
Hakuna kote duniani, kokote kule, ambako yame patikana masalio yanayo
thibitisha kuwa viumbe uhai wa wanyama, wadudu au mimea umepitia katika hatua
mbalimbali za mabadiliko mpaka ukakamilika na kuwa kamilifu. Bali masalio hayo
yanaelezea hadithi tofauti na ile ya Darwin, kuwa mdudu alikuwa ni mdudu
mamilioni ya miaka nyuma na bado ni mdudu leo, mende alikuwa ni mende zama hizo
na ni mende leo, samaki alikuwa ni samaki mamilioni ya miaka huko nyuma na bado
ni samaki leo, n.k.
Hivyo viumbe wote walitokea wakiwa na ukamilifu na kila kile ambacho
tunacho waona navyo leo ndivyo walivyo kuwa navyo mamilioni ya miaka nyuma, huu
ni ushahidi ambao umeandikwa chini, kwenye matabaka mbalimbali ya aridhi kote
duniani kutoka kwenye masalio ya viumbe, wanyama, wadudu, ndege, samaki n.k.;
lakini endapo unao mtazamo tofauti au umeweza kunaswa kwenye nadharia ya kibubusa
ya Darwin, tuletee ushahidi wako na uweke hadharani kila mtu aone ili tuweze
kukubaliana na hayo unayo tuambia, lakini usipige kelele kwa maneno matupu
yasiyo na ushahidi.
Bado tunamtafuta Muumba, katika yote tunayo yapitia kwenye ulimwengu wa sasa na yanayo tokea kote ulimwenguni, na tunayo yasoma kwenye mfulululizo wa posti hizi na yale ambayo tunadhani yanaweza kutokea endapo uma utaendelea kulala kwenye
usingizi wake wa pono, swali moja la msingi ambalo msomaji hatosita kujiuliza
ni ‘Je Mungu Yupo?’ au nililishwa ulevi wa kidini niweze kutawalika vyema, na
kama yupo iko wapi nafasi yake juu ya haya yote yanayo jitokeza kwenye uso wa
dunia leo hii?
Kujibu maswali hayo hatuna budi kwanza kumtafuta huyo ‘Mungu,’
na kwenye hilo tumeanzia kwa Darwin mwenyewe ambaye yeye si kwamba tu alimkataa
Muumba lakini kitendo cha nadharia hii kukubalika kufundishwa kwenye mitaala
mbalimbali kote duniani ni kusema kuwa ‘kiserikali’ Muumba hayupo na hivyo
ndivyo serikali mbalimbali duniani zimewafundisha wananchi wake kumkataa
Muumba.
Hivyo utaona nadharia hii kwa gharama zozote zile wananchi
wanalazimishwa kukubali kuwa uhai kwenye uso wa dunia ulitokea kwa nasibu na
hakuna yeyote anaye paswa kujinasibisha na chanzo cha uhai kwenye ulimwengu.
Serikali haina dini, lakini si sawa kusema hivyo kwa sababu neno dini kati ya
tafsiri zake nyingi ni ‘mfumo wa maisha’ hivyo serikali kama serikali haiwezi kujiongoza
bila kuwa na ‘mfumo’ wake au ‘utaratibu’ wake wa kiutendaji ambao nao utakuwa
na mipaka yake ambao ndiyo ‘dini’ ya serikali.
Hivyo serikali inapo sema haina dini haimaanishi kuwa haina mfumo, inayo,
na msahafu wa mfumo huo au dini hiyo, au biblia ya mfumo huo ni katiba ya nchi.
Dini ambayo serikali haina ni dini ya kukubali kuwa kuna Muumba. Ingawa
utashangazwa kuwa pamoja na kwamba serikali haziko tayari kufuata muongozo wa
huyo Muumba kwa vile kivitendo na kinadharia zinamkataa na kukataa kazi zake na
kuwalazimisha wananchi wake kumkataa kwa kuwafundisha nadharia ya Darwin kama
ukweli wa msingi juu ya chanzo cha uhai kwenye ulimwengu huu, serikali bado
zinamuomba Muumba katika shughuli zao za kila siku, nami najiuliza ni Muumba
yupi ambaye zina mwomba na Muumba yupi ambaye zinamkataa?
Leo hii hata ukikutana na profesa wa historia, au daktari, mwandishi,
mwanasayansi ambaye anakubaliana na nadharia hii ya Darwin kuna vitu kadhaa ambavyo
atakueleza kuthibitisha uhalali wa madai yake, tutavitizama vitu hivyo na
makosa yake ya msingi kabla ya kuachana na nadharia hii na kutafuta ukweli
mwingine wa msingi juu ya kuwepo kwa Muumba wa ulimwen
HOW CAN CHANCE STAND THAT?
Moja: Magwiji kwenye nadharia hii wanasema kuwa
ushahidi wa kisayansi umethibitisha kuwa uhai umekuja kwa nasibu kutokana na
mgongano wa kinasibu wa kikemikali. Ukweli ni kuwa hakuna ushahidi wowote wa
kisayansi au utafiti wowote ule au majaribio yoyote yale kwenye sayansi ya
miamba, mimea au tawi lolote kwenye sayansi ya historia linalo thibitisha madai
hayo, na zaidi ya yote hata kinadharia tu, nadharia hiyo imethibitika
haiwezekani.
Pili: Wanadhani
kuwa masalio ya historia yamethibitisha kuwa uhai wa viumbe kwenye dunia hii
ulianza hivyo, na kwamba umekuwa ukipitia mabadiliko mbalimbali. Huu ni uwongo
hakuna masalio yoyote yale, kokote pale yaliyo kuja kupatikana na
yakathibitisha hivyo, isipokuwa yote ni masalio ya kughushi yanayo kubaliana na
uwongo wao huo. Masalio yote yanathibitisha kuwa viumbe wote wamekutikana wakiwa
ni wakamilifu wa maumbile yao tangu awali na kuwa hawajapitia hatua yoyote ile
katika zama zozote zile.
Tatu: Masalio ya ndege wa Archaeopteryx, ambaye
alihesabiwa kama ushindi mkubwa kwenye nadharia hii kwamba ndege huyo hapo
kabla alikuwa ni reptiliani. Lakini imegundulika kuwa Archaeopteryx alikuwa ni
ndege kamili mwenye uwezo wa kuruka, na hakuna reptiliani mbaye ameweza kupatikana
kuwa yeye ndiye asili wa ndege huyo. Times
do tell the tales.
Nne: Katika mchakato wa kuwathibitishia
walimwengu juu ya ukweli wa nadharia ya evolution, kulipatikana kile kilicho
itwa ‘horse series,’ ambapo wana evolution walichukua ‘masalio’ ya farasi walio
ishi katika zama tofauti sehemu tofauti duniani na kuyapanga, hasa kufuatana na
maumbile yao. Kutoka dogo kwenda kubwa, kuthibitisha kuwa kiumbe hicho
kimepitia mabadiliko ya evolution katika zama mbalimbali mpaka alivyo leo. Hili
lilichukuliwa na wana evolution kama ushahidi wao wa msingi sana juu ya
nadharia yao kuwa ni ya ukweli. Lakini imekuja kuthibitika kuwa farasi hao
hawana mahusiano yoyote baina ya mmoja na mwingine, kwamba farasi aliyetangulia
katika ‘series’ hiyo si kweli wa nyuma yake ndiye baba au babu yake bali katika
mpangilio wao huo wa kuangalia maumbile, walifanya kosa kwani aliyedhaniwa
kutangulia ndiye alikuwa wa mwisho na wajamii tofauti kabisa ya farasi tofauti
na ile waliyo mpanganayo.
Tano: Wana evolution walimchukulia kipepeo
aina ya moth katika wakati wa mapinduzi ya viwanda England kama moja ya
ushahidi wao mkubwa wa kipepeo huyo kupita njia ya mabadiliko inayo tambuliwa
na Darwin kama evolution. Walicho kuwa wakidhani ni kwamba kipepeo huyo ameweza
kubadilika rangi yake na kuwa yenye kukolea zaidi kutoka kwenye ile iliyo
fifia. Lakini kama zilivyo shahidi zao nyingine, hii nayo ilikumbwa na vikwazo,
kwamba moth hakubadilika rangi bali wakati wa mapinduzi hayo ya viwanda
kulikuwa na moth wa aina mbili, mmoja ni yule aliyekuwa na rangi iliyo kolewa,
wakati mwingine ni yule ambaye alikuwa na rangi iliyofifia, moth wenye rangi
iliyofifia walianza kutoweka na wakati huohuo wale wenye rangi iliyo kolea
wakiongezeka kwa kasi kubwa. Hivyo dhana kuwa walibadilisha rangi yao kwa
kutumia kile kinacho itwa na wana evolution kama ‘naturalselection’ hakikutokea kabisa, na utafiti wao ulikuwa ni
wakughushi kama walivyo zoea, na hivyo ushahidi wao mwingine ukaanguka patupu.
YANI CHOCHOTE WAKIONA KINAYO NAFASI YA KUPIGIA DEBE UWONGO WAO, BASI WANAKURUPUKA NACHO.
Sita: Wanasema kuna mafuvu ambayo ni ‘masalio’
ya historia yanayo thibitisha kuwa mwanzo binadamu alikuwa ni sokwe na kuna
ambayo yanaonesha namna alivyo piga hatua moja mpaka nyingine kutoka sokwe
mpaka binadamu kamili. Lakini kama tulivyo ona hakuna aina hiyo ya masalio hata
kidogo popote pale ulimwenguni, na yale wanayo yaita ni ‘masalio’ si chochote
bali ni ya kughushi. Hivyo hawana ushahidi wa kushikika zaidi ya maneno marefu,
marefu ya Kilatini kutoka kwa wataalamu wao.
URONGO MWINGI, LAKINI SASA TUMEJUA NI TAARIFA ZA KUPIKWA.
Saba: Wanasema wanaevolution kuwa binadamu
anapo kuwa kwenye tumbo la uzazi au yai anapitia hatua za mabadiliko ya
ki-evolution kama wanavyo pitia viumbe wengine. Wamefikia kusema binadamu
katika hatua zake za awali akiwa tumboni alikuwa na matezi kama yale ya samaki,
ambayo kutona na mabadiliko ya evolution yamekuja kutoweka. Mwana baiolojia wa
evolution Ernst Haeckel alipo kuja na hoja hiyo mwanzoni aliibadilisha hata
michoro yake na kwa makusudi kabisa ili kuthibitisha madai yake hayo, lakini baadaye
hata wanasayansi wenzake wa evolution walikiri kuwa namna yake ya kughushi
ilikuwa hata si yakisayansi. Kwa maneno mengine ni kweli wanaghushi, lakini
huyu mwenzao hakughushi kisayansi.
UHUNI MTUPU, WANACHORA VIMICHORO VYAO, SABABU WATU HAWANA MUDA WA KUTAFITI AU NYENZO BASI WANAJUA WATU HATUTAGUNDUA UHUNI WAO.
Nane: Wanasema wana evolution kuwa binadamu na
viumbe wengine wanavyo viungo ambavyo vimetoweka kutokana na kwamba waliacha
kuvitumia viungo hivyo kwasababu mbalimbali za mabadiliko ya ‘natural
selection,’ wako wanao amini kuwa binadamu pia alikuwa na mkia lakini umetoweka
kutokana na kwamba hautumii. Kulipa nguvu dai lao hilo wana evolution
wanaipinga DNA, kwani kama tunavyo jua maumbile ya kiumbe chochote kile, tabia,
shughuli, sifa n.k. vyote vimeandikwa kwenye DNA yake. Dai hili nalo ni sawa na
msemo usemao ‘mfa maji haachi kutapatapa,’ viungo vyote walivyo navyo viumbe
wote akiwemo binadamu vinafanya kazi, hakuna kiungo kulicho patikana kuwa
kimeacha kufanya kazi kwa sababu ya mabadiliko ya kimazingira, ni kama aliye
viweka hapo anajua ni kwasababu gani viko hapo na havijatokea kwa nasibu au kwa
utaratibu wa ‘natural selection’ na hapa tupo kwenye juhudi ya kumtafuta huyo
mbunifu aliye anzisha haya yote kwani mjomba wetu Darwin tunaona hana jipya
zaidi ya kufoji ili kutupotesha kwenye ukweli wa msingi juu ya kuwepo kwa
mbunifu mwenyewe.
Hizi ni kati ya zile tu ambazo ukikutana na waumini wa evolution utakuta
wamejikita huko kama ushahidi wao wa kuthibitisha ukweli wa madai yao ya
kutokea kwa evolution. Sababu ambazo kama tulivyo ona hazina mashiko yeyote
kwenye jicho la sayansi ya leo na kwenye fikra za watu huru.
Watu wengi hudhani kuwa nadharia hii ya eveolution
muasisi wake ni Darwin, lakini kama nilivyo kwisha kutaja huko mwanzo, nadharia
hii ni kazi ya wanafalsafa wa materilist ambao waliona kwao nadharia hii inayo tija
kwa mipango yao, nao kwao siyo kwamba inayo ukweli au kanuni za msingi za
kisayansi lakini kwa vile juhudi ni kumkataa Muumba na hata kuikataa roho, kwa
wanamaterilist nadharia hii kwao inabaki kama ukweli wa msingi pamoja na kuwa
kila tofali lake moja limejengwa kwa kanuni za uwongo na kughushi na bila
kanuni za sayansi ya utafiti.
Kama utamkataa Muumba kwenye kazi ambazo zinathibitisha zenyewe, au
zinasimama zenyewe kama ushahidi wa kazi za Muumba, hapana shaka kazi hizo
lazima uzitafutie mbadala, na kwa Darwin na materilist wenzake ‘mbadala’ huo
umekuwa ni ‘survive for the fittest,’
kama kanuni ya msingi ya maendeleo ya uhai kwenye sayari hii na nukta ya msingi
ya kuendelea kuwepo kwa uhai na viumbe katika uso wa dunia. Hivyo mwanadamu
ametokea kwa nasibu na ameendelea kuwepo achilia mbali kutoweka kwa viumbe
wengine na kuyashinda majanga mbalimbali kutokana na kanuni hii ya ‘survive for
the fittest.’ Hivyo mwanadamu ni ‘lijinyama’ lisilo na maadili wala muongozo
wowote kwani kuwepo kwake hapa hakutegemei yeyote wala chochote zaidi ya uwezo
wake wa ‘survive for the fittest, matokeo ya nadharia hii kumfuta Muumba kwenye
kazi anazozifanya na kazi hizo kuzipatia jina jingine au kumpatia mwingine
mbali na Muumba mwenyewe, moja kwa moja kuna mwondolea binadamu msingi wa
utashi wake kwamba hawajibiki kwa lolote analo fanya liwe baya au zuri kama wanavyo
sema wamasonia kuwa ‘the end justfy the
means’ na ‘the end’ yenyewe ni
ku-survive for the fittest’
haijalishi ni lipi kiumbe huyu atafanya kulifikia lengo hilo la ku-survive hatowajibika kwa yeyote kwa vile
yeye mwenyewe katokea kwa nasibu na siyo kazi ya yeyote katika kutokea kwake,
na kuendelea kuwepo kwake hakutegemeani na yeyote bali uwezo wake wa kuwashinda
walio wadhaifu kwa namna yeyote ile ili aweze ku-survive.
MTOTO HUYU ANATAMBAA KUELEKEA KUNAKO KAMBI YA CHAKULA YA UN, AMBAYO KUTOKA HAPO NI UMBALI WA KILOMETA MOJA, NDEGE ANAMSUBIRIA MTOTO HUYU ASHIWE NA NGUVU KABISA AANZE KUMLA, BINADAM MWINGINE ALISIMAMA AKAPIGA PICHA HII NA KUONDOKA, HAKUMSAIDIA MTOTO HUYU KWENYE UBAYA UNAOMSUBIRI MGONGONI KWAKWE SABABU ALIHOFIA ATAPATA MARADHI YA KUAMBUKIZA, HIVYO ALIONDOKA NA HAKUNA ALIYEJUA NINI ILIKUWA HATMA YA MTOTO HUYU. HAPO NDIPO TULIPOFIKA, LAKINI MATANI NA MATANI YA VYAKULA YANAMWAGA KILA MWAKA KOTE DUNIANI, LAKINI BAJETI YA ULINZI YA MAREKANI YA MWAKA MMOJA INATOSHA KUONDOA UMASIKINI WOTE DUNIANI, NA HAKUNA ATAKAYE KUFA KWA NJAA, BAJETI YA KUANDAA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA INAWEZA KUONDOA NJAA KWA KIASI KIKUBWA KWA NCHI MASIKINI.
BUT WHO IS CARE?
IS SURVIVAL FOR THE FITTEST.
Matoke ya mafunzo hayo ni uharibifu usiyo kuwa na macho, unyama ushenzi na
ufedhuli ambao hauwezi kufikirika achilia mbali kutamkika. Nguvu ya utashi na
akili huru ya kutafakari na kutambua mambo itakuwa imefunikwa na matakwa ya
nafsi ya mwanadamu, Matakwa ambayo hayatoweza kuwa na kikomo ya nafsi iliyo
haribika, hakuna sheria wala mipaka ambayo nafsi hiyo itaweza kuitambua, siyo
sheria za nchi wala za Muumba. Nafsi hiyo imefisidika kupita kikomo kwa vile
kanuni inayo iyongoza imemnyang’anya jukumu lake kama kiumbe kilicho umbwa na
kujiita kiumbe kilicho jiumba. Hii ndiyo hasa maana ya kutokea kwa nasibu,
kwamba hujaumbwa bali umejiumba, na ukiwa umejiumba ni nani atakaye kuwa na
mamlaka na wewe, inamaana wewe ndiyo muumba mwenyewe. Kila kinacho kuzunguka
kimejiumba chenyewe tofauti yako wewe na viumbe wengine siyo utashi wa akili
huru, bali uwezo wako wa ku-survive for
the fittest. Kwa msingi huu haijalishi nini utakacho kifanya, hakuna wakuuliza.
Haya ndiyo maradhi ya makubwa ya jamii yetu ya leo. Lakini baya zaidi ni
kuwa wapo ambao bado hatuja kubaliana na nadharia hii ya Darwin na wenzake
hivyo tuko kwenye juhudi ya kumtafuta Muumba; hivyo basi Freemasons na wenzao
wametangaza vita dhidi yetu, vita hiyo ipo katika sehemu mbili, kutumaliza
kabisa sisi na sehemu ya pili kuvibadilisha vizazi vyetu kukubaliana na nadharia
hii. Kama tutakavyoona katika posti zitakazo fuata kuwa hivi sasa kuna
vita vikubwa dhidi ya afya yako na wewe mwenyewe binafsi na kuna vita dhidi ya
familia yako katika mbinu njia na namna mbalimbali.
Zingine unazitambua na
zingine huzitambui kabisa. Suala la watoto kupigania haki zao, kinamama
kupigania haki zao, hizi ni moja ya mbinu zao,jamii hizi mbili yaani kina mama
na watoto tunajua fika kuwa wanazo haki zao za msingi na zinazo tambulika na
kuheshimika katika kila jamii, lakini kwa kutumia jina hilohilo kama vile ni
watu ambao mafunzo mengine hasa ya kidini na kijamii zingine yamewanyima haki
zao, ili kuingiza ‘haki’ ambazo unajua wakipewa haki hizo moja kwa moja
itapelekea katika kufanikisha mpango wako wa kumfuta Muumba katika maisha yao
na kuwafanya ni wanyama wanao -survive
for the fittest- basi wewe moja kwa moja hukuja kuwapa haki zao bali
kuwanyang’anya haki yao ya msingi kabisa ambayo ni haki ya uhuru, haki ya
kutokuwa mnyama bali kuwa kiongozi ambaye atathibitisha kuwa kazi zinazo
fanywa na Muumba hazifanywi kwa bahati mbaya au kimchezo mchezo bali kwa
sababu, msingi na madhumuni maalum.
Kwa wao hakuna ‘nyeupe’ wala ‘nyeusi’ wanasema hivyo wakimaanisha yaani
hakuna jema wala baya. Hivyo hata ikibidi kuuwa watu bilioni tano kama wanavyo
tekeleza mpango huu kwa njia mbalimbali hilo kwao halionekani kama ni kitu,
‘kibaya’ bali njia ya wao ku-survive.
Mamilioni ya watoto wanakatishwa uhai wao kwa njia ya utoaji mimba, mamilioni
wengine wanaachwa kwa makusudi wafe kwa njaa, mamilioni wengine wanauwawa kwa
kuchomwa sindano yenye magonjwa mbalimbali, mamilioni wengine wanapatiwa chanjo
ambazo baadaye zitazalisha madhara ya kukatisha uhai wa watu hao, mamilioni
wanakufa kwa vita wanavyo vidhamini wao, haya yote hayana tafsiri ya ‘ubaya,’
‘uovu,’ ‘unyama,’ na mengineyo ambayo ungeyaita kwao hakuna ‘nyeusi,’ wala
‘nyeupe,’ kwao kuna matokeo tu, na matokeo yenyewe ni ku-survive, ni njia gani
utatumia uweze ku-survive, haijalishi; na kwa nini ijalishe chochote ikiwa kwao
hakuna Muumba?
Kitabu cha mwanauchumi wa Uingereza Thomas Malthus alicho kiita An Essay on the Principle of Population,
kinatajwa kuwa ndiyo chachu ya kazi ya Darwin, mwanauchumi huyo kutokana na
mahesabu yake aliona kuwa kasi ya ongezeko la watu duniani inakuwa mno, kwa
sababu kwa materialisim kila mtu ni mungu mwanauchumi huyo akijivisha viatu
visivyo vyake aliona hilo ni tatizo kwa kasi ya watu kuongezeka kuwa kubwa na
akapendekeza vitu kadhaa vifanyike ili kupunguza kasi hiyo ya ukuaji wa watu
duniani. Machafuko, majanga, vita, njaa na magonjwa ndizo nyenzo aliziona kuwa
zingefaa katika kukamilisha zoezi la kupunguza kasi ya ukuaji na idadi ya watu
kwenye sayari hii kwa ujumla. Kuna watu ambao wanapaswa kufa ili wengine
waishi, si unawajua ni akina nani wakwenda na akina nani wa kubaki, ambao
wamesha survive for the fittest yaaniWazungu
wa Ulaya hao wanayo haki ya kuishi, watu wa Asia, Afrika, Amerika ya kusini na
wakazi wa asili wa Amerika ya Kaskazini, Australia, hao bado wanajivuta vuta,
wanapaswa kufa.
Hii ni survive for the
fittest hivyo machafuko, vurugu, vita, magonjwa, ukame na mengine hapa ni
nyumbani kwao, sababu hizi ni zana ambazo lazima ziendelee kutumika ilimradi
anayetakiwa kufa bado tupo hai, bado tunazaliana.
Wakati naanza kupata pata
akili nilikuwa nikijiuliza kwa nini vita haviishi, ni kweli hakuna namna ambayo
vita hivi, njaa na magonjwa kwenye bara letu vinaweza kutoweka na dunia kuwa
sehemu ya amani, sikuwa na elewa kuwa kikwazo ni nini, kumbe hata mimi
niliyekuwa nikijiuliza swali hili sina haki ya kuishi, kumbe nimekuja kwa
bahati mbaya sikutakiwa kabisa niwepo, sasa ndiyo naelewa kwa nini waasi
wanaweza kupewa silaha nzitonzito lakini hawana hata ndala, nguo zao chakavu na
wamedhoofu kiafya. Kumbe sisi tunapaswa kuendelea kuuwana ili weupe waishi.[6]
HII SIYO NADHARIA, BALI NDICHO WANACHO KIFANYA HASWA USIKU NA MCHANA.
Kwenye nusu ya kwanza ya karne ya kumi na tisa kote Ulaya, viongozi na
wakubwa wengine walikuwa wakikutana kuangalia ni namna gani wataweza kupambana
na tatizo jipya wanalo liona, nalo ni ongezeko la watu duniani. Njia gani
zitumike ili kuweza kufuata muongozo wa Malthus katika kupongeza idadi ya watu,
hasa masikini, si kwa kuwaondolea umasikini wao, bali kuwaua au kuwatengenezea
mazingira ya vifo vyao, na kuwafunga vizazi vyao. Ikafahamika kuwa ili
kuwamaliza watu masikini lazima nchi za Ulaya zihakikishe kuwa badala ya
kuwasisitizia watu masikini katika masuala ya usafi, wawahimize wawe na tabia
ya uchafu, ambayo itapelekea kuwepo kwa maradhi aina kwa aina. Miji yao ifanywe
kuwa na mitaa yenye njia nyembamba, tuwajaze watu wengi kwenye nyumba ndogo,
miji ijengwe karibu na mabwawa machafu, tuwalazimishe watu wakaishi kwenye
mazingira magumu, maeneo ambayo hayafai watu kuishi.[7]
Mbadala huo ukitumika wale madhaifu ambao wameshashindwa kwenye vita hivi
vya survive for the fittest
watatokomea, na idadi ya ukuaji ya watu itapungua na kuwa kwa idadi ile tunayo
taka. Darwin naye akaibeba muongozo huu wa Malthus na kuanisha kuwa unapatika
kwa kila kiumbe, akawataka watu wamkane Muumba wao na akawatengenezea njia ya
mapambano baina ya madhaifu na wale wanao jiona kuwa ni fittest.
Nadharia hii ya
Darwin ikamzaa mtoto aliyeitwa ‘ubaguzi’ kwenye karne ya 19 ambaye naye kwenye
karne ya ishirini akamzaa mjukuu wa Darwin kupitia ‘ubaguzi’ aliyeitwa ‘fashisti.’
Adolf Hitler kwenye kitabu chake cha Mei Kampf, anakubali kuwa ni maono ya
Darwin ndiyo yaliyo muongoza mpaka kufikia hatua ya kupambana vita vya kibaguzi
kati yake na ‘rangi’ nyingine zote zilizo salia.
Abiria mwingine aliyekata tiketi ya first
class kwenye ndege ya Darwin ni mkomunisti. Abiria huyu ndege hii anaipenda
sana. Mahusiano baina ya ‘abiria’ huyu anayeitwa komunisti na ‘ndege’ inayo
itwa Darwin ni kuwa wazazi wa abiria huyu Marx na Engels wote walikuwa ni
washangiliaji wa ‘huduma’ zinazo tolewa na ‘ndege’ ya Darwin. Marx na Engels
wamezisoma kazi za Darwin ikiwemo the Origin
of Species na walipendezwa sana na kazi hiyo hasa kwenye upande wao wa ki-materialism. Kwenye kitabu chake alicho
kiita The Dialectics of Nature,
Engels ambacho amekiandika kwa kufuata maoni ya Darwin, amejaribu kuongezea
‘utamu’ kwenye nadharia ya evolution kwenye sura aliyoiita ‘The Part Played by Labour in the Transition
from Ape to Man,’ wakomunisti wa Urusi ambao walifuata nyayo za Marx na
Engels, kama vile Plekhanov, Lenin, Trotsky na Stalin wote wanakubaliana na
nadharia ya evolution ya Darwin. Mao ambao alisimamisha ukomunisti China na
kuuwa mamilioni ya Wachina kufanikisha lengo hilo alisema;
“Ujamaa wa China umejengwa
chini ya misingi ya nadharia ya Darwin ya evolution.”.[8]
Kwenye kitabu alicho kiita China and Charles Darwin, mwanahistoria
wa Harvard University, Janes Reeve Pusey ameelezea kwa kina madhara ya Darwin
kwenye ukomunisti wa Mao nchini China.[9]
Mahusiano baiana ya nadharia zote mbili, ukomunisti na evolution hayana upenyo,
kwa vile evolution inaipa nafasi ukomunisti kutekeleza ajenda, sera, mipango na
maono yake kupitia tafsiri ya evolution. Ukomunisti umeuwa takribani watu
milioni 120 katika harakati zake za kujipenyeza kwenye maisha ya ulimwengu huu,
lakini halionekani hilo ni ovu kwa vile wana-survive for the fittest.
Darwin na nadharia yake inayo tumiwa kama msingi wa kukataa kuwepo kwa
Muumba, mpaka leo haijaweza kuthibitisha madai yake hayo, zaidi ni matatizo
makubwa katika karne hii na zilizo pita katika nyanja mbalimbali za maisha yetu
ya kila siku, vurugu, umwagaji wa damu, umasikini, mauwaji na mengine na
mengine na mengine ambayo kwenye dunia ya leo yana onekana kuwa ni mambo ya
kawaida kutokana na ‘baraka’ za Darwin kupitia nadhari ya evolution kwenye
misingi ya survive for the fittest.
Tulikuwa tunamtafuta Muumba wa ulimwengu, lakini cha kwanza tulicho
kiangalia ni sayansi ya leo iliyo jengwa kwenye misingi ya Darwin ambayo
inafanya kila inalo weza nyuma ya watu fulani, kuthibitisha kuwa hakuna Muumba,
hata hivyo tumekutana na mapungufu ya kutosha juu ya madai yao hayo, na zaidi
ya yote tumeona kuwa nadharia hiyo imejengwa katika misingi ya maelezo ya
uwongo na ushahidi wa kughushi. Watu makini wenye mipango makini katika kufikia
jambo lao, katu hawawezi wakajenga misingi, kuweka maelekeo na njia ya kufikia
malengo hayo kwa kutumia maelezo ya uwongo na takwimu za kughushi, na hakuna
jambo lenye uzito na majibu elfu moja yenye kuridhisha kwetu sisi wanadamu kama
kutambua asili yetu ni wapi, na ramani ya Darwin inatupeleka kwenye shimo la
nyoka na nge na katu haitaweza kujibu maswali yetu magumu juu ya nini madhumuni
yetu ya kuwepo hapa, ikiwa imeshindwa kuthibitisha asili yetu ni nini ni wazi
haiwezi kutuhakikishia hatma yetu ya maisha ni ipi, hivyo marafiki, maadui, wapendwa,
ndugu, wasomi, vijana wenzangu, wanavyuo, wahadhiri, wanafunzi na kila binadamu
kokote alipo hatuna budi kuachana na nadharia ya Darwin katika kila nyanja ya
maisha yetu tuliyo ruhusu nadharia hii ikaingia na hasa kwenye suala la muhimu
na zito kuliko yote, suala la kumtafuta Muumba wa ulimwengu huu.
Nadhari ya Charles Darwin na kokote alikoitoa imeshindwa kututhibitishia
ikiwa ni kweli hakuna Muumba, na sisi tunamtafuta Muumba, na ukweli ndiyo utakao tuweka huru na
Darwin siyo mkweli.
TUKUTANE HAPA HAPA NEXT TIME, BADO TUKO KWENYE SAFARI YA KUMTAFUTA MUNGU ... WAPI TUTAINGIA TUTAJUA HAPA HAPA....
Atlas of Creation na Harun Yahya
Salaam brother Salim,
ReplyDeleteNichukue fursa hii kukupongeza sana kwa moyo wako na jitihada zako kutuletea elimu hizi za hali ya juu sisi ndugu zako (waislam) na wengineo pia (wasio amini)
Binafsi nimepata faida sana kupitia blog yako, na pengine labda nimezidi kupata faraja kuwa kile nilichokuwa nakiamini (na kuendelea kukiamini) mpaka leo hii kumbe kuna ndugu yangu mwengine (wewe) yungali katika upande wangu.
Mara zote nimekuwa nikiwaza mengi kuanzia dunia na mambo ya aakher na kila mara nimekuwa nikitamani walau apatikane mtu japo mmoja nitakayeweza ku-share nae haya mengi niliyonayo akilini mwangu.
Naamini ni Mungu ameniongoza (alhamdulillah) kupata fursa ya kuifikia blog yako na kuhakiki niwazacho na nikiaminicho juu ya mambo lukuki yanayoendelea katika ulimwengu huu ambayo binafsi nayaangalia katika jicho hasi (-) sana tangu nilipoanza kupata akili na kujitambua.
Dunia imekuwa nyeusi na inayotisha mno (kwa wenye akili na uelewa kama Mimi, wewe na wengineo wachache) 'nitaendelea'....
Makala zako hakika ni za thamani ya hali ya juu kaka. Niendelee kukupongeza kwa kazi hii ngumu na ya kujitolea kutuelimisha. Naamini elimu kama hizi no ngumu kuzipata mahali kokote hasa kwa sisi tulio katika 'dunia ya tatu' na ambao tulishaathiriwa na mambo ya kidunia.
ReplyDeleteTumekuwa wagumu kuamini kuwa tunapotea, ama tulishapotea na hatimaye hata pale ambapo anatokea mtu mwenye ufahamu/ujuzi kama wewe na kujaribu kutufahamisha nyeusi ni ipi na nyeupe ni ipi... basi mtu huyo ataonekana kutuko, kikwazo au aso-maana kwao na labda kuishia kuchekwa pia kisa hujaandika habari za kileo zinazoendana na matakwa yao. Huku ndiko kupotea kaka.
Nina mengi sana ya kuzungumza kabla ya kuanza kuchangia nilonayo kwenye mada zako. Inshaallah nitaendelea kufuatilia mfululizo wa kila makala yako na kuielewa vizuri. Ila kwanza wacha tu nikupongeze kwa hiki ulichoamua kukifanya na inshaallah Mungu atakulipa. Mimi nitakuwa balozi wako mzuri kufikisha haya kwa wengine.
Asante sana kaka Salim. Una akili sana wewe!
Salim msangi kwanza napenda kukupa pongezi maana mimi mwenyewe nilikuwa najiuliza hivi kama kweli nilifundishwa darasani kuwa Binadamu katokana na nyani mbona mpaka leo nyani wanazaliana na hawabadiliki kutoka stage moja kwenda nyingine!!!!!? Na kibaya zaidi wapo wanao wafuga nyani sasa mbona abadiliki japokuwa karahisishiwa kuservive??? Hakika ALLAH ndio kila kitu maana kwa neno "kuwa" uwa linakuwa vile atakavyo.
ReplyDelete