Leo kwenye safari yetu tunatizama, 'new age' ambayo ni dini lakini pia ni sayansi au ni mtazamo wa ulimwengu na binaadam ambao unakubalika na wanasayansi wengi ... ni sayansi kwa maana mtazamo wake unaathiriwa na Darwin, lakini pia unahusisha nyanja mbalimbali za sayansi ... na waumini wake wanaegemea kwenye sayansi kuthibitisha misimamo ya dini hii ...
Hatuja kata tamaa bado tunamtafuta Muumba wa haki, tuachane na Darwin,
ingawa nitarudi tena kwake wakati nitakapo kuwa nahangaika kutafuta asili ya
binadamu hasa ni wapi lakini kwanza tutizame wana New Age wanatusaidiaje katika kumtafuta Muumba.
Ninapo zungumzia ‘NewAge’ msisitizo wangu upo kwenye majibu mazito au
mepesi yanayo tolewa na watu wa sasa kutokana na msukumo na ushawishi wa
maendeleo ya sayansi kwa ujumla, lakini hasa sayansi ya anga na sayansi ya
saikolojia.
Sayansi ya nafsi au saikolojia ilikuwepo tangu na tangu, lakini
zaidi katika zama zetu hizi kumekuwa na taarifa nyingi zaidi, maandishi mengi
zaidi, makala nyingi zaidi na wataalamu wengi zaidi kuhusiana na elimu hii, halikadhalika
kwenye sayansi ya anga.
Sayansi hizi mbili zimekuwa na msukumo mkubwa katika
kulielezea suala tete na kujibu maswali magumu juu ya kuwepo kwa MUUMBA. Lakini
pia katika sayansi hizi mbili na hasa ile ya anga tutakuta kwa kiasi kikubwa
imekopa mawazo, mitizamo na maono kutoka kwa mjomba wetu, mjomba Darwin.
Ingawa Sayansi inathibitisha juu ya kuwepo kwa MUUMBA kwa namna mbalimbali,
na baadhi ya wanasayansi wakibadili misimamo yao na hata kuanza kufuata
mafundisho ya baadhi ya dini, kama kukubali kwao juu ya kuwepo kwa MUUMBA,
lakini bado sayansi hiyo kwa namna mbalimbali inatumika kama silaha ya kumkataa
MUUMBA, na baadhi ya wanasayansi wakisimama kama uthibitisho kuwa hakuna
MUUMBA.
Sayansi ya leo na watafiti wake wanatumia zaidi majukwaa ya sinema na
tamthilia na vitabu vya hadithi za kufikirika kama darasa la kuwaelekeza
walimwengu kuwa ni namna gani ulimwengu umetokea kwa nasibu na wakati mwingine
ukiwaonesha walimwengu muumba mwingine wanao mfahamu wao wanasayansi na
wakifanya juhudi kuwashawishi walimwengu kupitia vyombo mbalimbali vya habari,
makala na majarida kumkubali mungu wao.
HOOLYWOOD WANAPENDA NADHARIA YA WAUNGU KUTOKA SAYARI YA MBALI
Ingawa si rasmi sana lakini katika nchi nyingi za Ulaya na zile zinazoitwa
za ‘dunia ya kwanza’ kwa muda mrefu kumekuwa na ‘tetesi’ kuwa aliens au viumbe
kutoka sayari nyingine ndiyo miungu wa ulimwengu huu. Dai hili limekuwa
likiletwa kwenye akili za watu na hasa vizazi vya sasa kwa kupitia kazi za
filamu, tamthilia, majarida na vitabu. Kazi zenye gharama za mabilioni ya dola
zinatengenezwa kutoka kwenye katuni mpaka tamthilia zenye maudhi na fikra
pandikizi kuwa muumba wa ulimwengu huu ni Aliens.
Mkufunzi kwenye masuala ya Mashariki ya Kati na Biblia bwana Zacharia
Sitchin alikuja na vitabu kadhaa akielezea kuwa ‘Anunnaki’ walio tajwa kwenye
masalio ya kale ya wa Sumeri, kama watu walio kuja kutoka mbinguni na kutua
duniani.
Sitchin akawalinganisha Anunnaki na ‘Nephılım’ walio tajwa kwenye
agano la kale kama walio kuja duniani kutoka mbinguni. Baada ya miaka mingi ya
utafiti na kutafsiri kazi hizo za kale na lugha yake kuja kwenye lugha ya watu
wa sasa Sitchin akahitimisha kuwa dhana ya ‘Anunnaki’ kutoka kwenye kumbukumbu
na masalio ya historia ya kale ya wasumeri na ile dhana ya ‘Nephilim’ kutoka
kwenye agano lake kuwa zote zinaelezea kitu kimoja, au zote msingi wake ni
mmoja.
Dhana hiyo au msingi wa dhana hiyo ni kuwa hapo zamani sana, zama za
kale kabisa kabla binadamu hajafika kwenye uso wa dunia, jamii ya viumbe fulani
kutoka sayari au ulimwengu mwingine walifika kwenye sayari hii ya tatu kutoka
kwenye jua na kutokana na maendeleo yao ya sayansi waliweza kuanzisha uhai
katika sayari hii, hasa uhai wa kiumbe kinacho itwa mwanadamu.
Dhana hii ndiyo
inayo tiririka kwenye mishipa ya uhai wa asasi zote za siri za Illuminati
wakiwemo Freemasons. Kama nilivyo tangulia kusema Freemasons hawamkatai MUUMBA,
bali haki hiyo wanawapatia viumbe wengine.
Dhana ya Sitchin na wenzake si kwamba uhai umetokea kibubusa, hapana, uhai
umetengenezwa, au uhai umeumbwa, lakini ni nani huyo aliye umba uhai? Hapa
ndipo tunapo chora mstari wa mgawanyiko baina ya waumini wa MUNGU MMOJA na
wafuasi wa ndani kutoka kwenye asasi mbalimbali za siri na zile za kishetani.
WAUNGU KUTOKA SAYARI YA MBALI
Darwin tulisha mkataa mapema kwa vile yeye anadai uhai umeibuka kibubusa madai
ambayo ameshindwa kuyathibitisha. Lakini sisi tulio bakia baada ya kumkana
Darwin tulidhani kuwa tunaimba wimbo mmoja na wenzetu ambao nao wanadai kuwa
uhai, umefanyizwa na haukuja kinasibu, lakini tumeona wao wanayo muumba wao
tofauti na yule tunaye mfahamu.
HOOLYWOOD WAKIWA KAZINI
Lakini swali ambalo ningependa sote tujiulize ni kuwa; ni nani huyo
aliyeiumba sayari hii ya tatu kutoka kwenye jua ambayo viumbe hao waliikuta ipo
tayari na wao wakafanyiza uhai?
Kutoka kwa wana New Age ambao wanaamini kuwa
Aliens ndiyo mungu muumba wa ulimwengu, hakuna uthibitisho au maelezo yeyote
kwa njia ya maandishi au matamshi waliyo yatoa kwenye hadhara kujibu swali hilo
hapo juu, kuwa ni nani aliyeumba dunia. Ukiwabana wana New Age kuhsiana na uumbaji maelezo na vielelezo vyao vinaangukia kwenye mikono ya Darwin. Hivyo weka akilini mwako hilo kuwa
asubuhi kabisa ya nadharia hii ya Aliens tunakutana na kizingiti, na swali
lisilo weza kujibika.
UFO, AINA YA CHOMBO KINACHO TAJWA KUTUMIWA NA MIUNGU HAYO.
Tukiegemea kwenye kazi ya ‘mtume’ huyu wa NewAge bwana Sitchin na wenzake
kama Alan F. Alford, R. A. Boulay, Neil Freer, Dr. Arthur David Horn, Dr. Joe
Lewels, C. L. Turnage, Lloyd Pye, Laurence Gardner, na William Bramley wanasema
hivi;
Takribani miaka 450,000, kundi la viumbe wenye maumbile yanayo karibiana
sawa na haya ya binadamu wa leo lakini wao wakiwa ni bora zaidi kimaumbile,
walifika kwenye dunia hii wakitumia vyombo maalum vya usafiri wa angani.
‘Mitume’ hawa wanatuambia kuwa viumbe hao walitoka kwenye sayari ambayo ukubwa
wake ni mara tatu kulinganisha na dunia yetu. Sayari waliyo tokea wasumeri
waliita Nibiru ambayo inasemekana kuwa watu wa kale waliifahamu na kuichora
sayari hiyo.
NIBIRU KWENYE SOLAR SYSTEAM
Wasumeri kupitia kwa ‘mitume’ hawa wanasema kuwa sayari hiyo ni ya 12
kwenye mfumo wetu wa jua wa ‘Milkway’ lakini wanasayansi wa sasa bado
hawajaweza kuing’amua sayari hiyo au kuinasa kwenye mitambo yao kwa vile
inasafiri kupitia kwenye orbiti iliyo na umbo kama la yai na hupita karibu na
dunia yetu kila baada ya miaka 3,600. Viumbe hao walifika hapa duniani wakati
sayari ya Nibiru ilipo kuwa karibu sana na ile ya dunia, nao walitua juu ya
maji.
MICHORO UNAO ELEZEA SAYARI YA NIBIRU
Viumbe hao walihitaji kuweka kambi sehemu ambayo wangeweza kupata maji,
hali ya hewa nzuri na mali ghafi zingine za kuwawezesha kuishi na kuendelea na
safari yao, sehemu hiyo haikuwa nyingine bali kwenye aridhi yenye rutuba ya
Mesopotamia, leo inafahamika kama Iraq.
Lingine ambalo tunaweza kuliona hapa ni kuwa viumbe hawa kutoka sayari ya
mbali nao walikuwa ni wahitaji wa malighafi zilizomo hapa duniani kwa ajili ya
wao kuweza kuendelea kuishi. Swali ni je MUUMBA anaweza kuwa muhitaji wa alivyo
viumba?
MICHORO YA KALE INAYO ELEZEA KUHUSU WAGENI HAO
Muumba anaweza kutegemea mazingira fulani tu ndiyo afanikishe jambo
lake kama wao walivyo tegemea sayari yao ikurubiane na dunia yetu ndiyo watue
kwenye maji? Majibu ya maswali yote haya ni hapana, MUUMBA yupo huru na juu ya
vile alivyo viumba na wala haitaji chochote kutoka kwa viumbe wake na
ameepukana na mapungufu yote hayo. Hivyo tena hapa tunaingia na walakini
mwingine juu ya mungu huyu wa New Age.
MAFUVU HAYA SI YALE YA SOKWE WA DARWIN, UHAKIKA WAKE KWAMBA SI YA KUGHUSHI BINAFSI SIJAUPATA, LAKINI SI AINA YA HISTORIA INAYOFUNDISHWA KWENYE MITAALA YETU YOTE KOTE DUNIANI, SWALI KWANINI HAYAFUNDISHWI AU HAPASEMWI CHOCHOTE KUHUSIANA NAYO, SIJUI, LAKINI KUNAYO NADHARIA NYINGI NYUMA YA MAFUVU HAYA, NA MOJA WAPO NI MAFUVU YA BINADAM WALIO ZALIWA BAINA YA BINADAM NA WAGENI KUTOKA SAYARI YA MBALI.
Wageni hao wakaanza kuitawala dunia wakiongozwa na mfalme Anu, au El au An
kutegemeana na tafsiri na mapokezi. Watawala hawa wapya walihitaji madini
katika sayari hii kwenda kuitumia kwenye sayari yao, na walihitaji nguvu kazi
ya kuweza kuwasaidia kuchimba malighafi hizo. Ndipo ‘miungu’ hao walipo amua
kumuumba binadamu ambaye ataweza kufanya kazi hizo, katika lugha ya Kisumeria
binadamu huyo alitajwa kama LU.LU jina ambalo kutokana na ‘tafsiri’ za ‘mitume’
hao Kiyahudi lilitamkwa kama Adama, yaani lenye maana ya kilichotengenezwa kwa
udongo.
Lakini miungu hao si kwamba ndiyo walianzisha maisha ya binadamu, bali
kutokea kwenye nadharia ya Darwin tayari alikuwepo kiumbe ambacho bado hajawa
binadamu kamili, na miungu hao wakamchukua kiumbe huyo na kuchanganya DNA yake
na ile ya miungu na kumtengeneza Adama ambaye atafanya kazi za machimbo Afrika.
Hivyo basi kwanadharia hii, Aliens hawawezi kuwa ndiyo MUNGU kwa vile wao wenyewe walikuja
na kuikuta dunia ipo tayari, lakini pili walikuwa ni wahitaji wa hichi walicho
kikuta hapa kwa maana nyingine wanayo mapungufu ya kuweza kutengeneza malighafi
hizo. Tatu ni uzoefu wao wa kuweza kuwa na maarifa makubwa kwenye ‘baiolojia’
na ‘DNA’ na kwa kuunganisha seli hai za
binadamu ambaye alikuwa bado hajakamilika, bado alikuwa ana-evolve- kuelekea kwenye ubinadamu
kamili, kutokana na nadharia ya Darwin na kuchanganya na ile seli hai au ‘DNA’
ya Anunnaki na kumpata binamu mwenye sifa za kuweza kufanya kazi wanazo zitaka.
Lakini mpaka leo utaratibu wa kisayansi wa kunakili DNA ya kiumbe kimoja na
kuchangana na ile ya kiumbe kingine haujaleta tija yeyote na wala haujaweza
kutoa kiumbe tofauti na vile ambavyo DNA zao zimechanganywa na zaidi, madhara
na mapungufu kwa viumbe hao imekuwa ni kubwa zaidi. Lakini hata hivyo hadithi ya
‘mitume’ hawa wa New Age kuhusishwa na ile ya mjomba Darwin ambayo kama tulivyo
iona haina mashiko yoyote kunatufanya moja kwa moja kuona nadharia hii ya New
Age inayo fundishwa kwenye kumbi za filamu haina jipya zaidi ya mwendelezo wa
kazi za mjomba Darwin.
MOJA YA VITABU VINAVYO ELEZEA MISINGI YA NEW AGE, KUNAYO NA FILAM YAKE PIA, NA MSURURU WA VITABU SASA VINAVYO KWENDA NA MAUDHUI HAYO HAYO.
Mbali na ‘mitume’ hawa wa New Age kuwapa Anunnaki sifa ya uumbaji, hakuna
kitabu chochote kinacho daiwa au kuthibitishwa kuwa kimeandikwa na Anunnaki
kinacho thibitisha dai hilo, au ambacho Anunnaki wenyewe wanadai kuwa
wamehusika na kazi ya uumbaji.
Tukiacha Aliens ambayo nayo misingi yake ni ile yakumkataa MUUMBA, lakini
ikiwa haijitoshelezi na yenye mapungufu yanayo zusha maswali katika kila mstari
wake mmoja wa maandishi; tunayo New Age Movement, ambayo hasa ndiyo wamejaribu
kuipika iwe mfano wa dini kwa watu wote.
New Age Movement tofauti na
zilivyo dini zingine haina kitabu chochote,haina kiongozi wa kiroho, haina
makao makuu,haina muongozo rasmi, haina imani rasmi. New Age Movement ni uhuru
wa kiroho unahusisha mahusiano baina ya wanachama na waumini ambao muungano
wao, au mahusiano yao yanajengwa na wao kuwa na aina moja, mtizamo mmoja,
ufahamu mmoja au uelewa mmoja kama msingi na muongozo kwenye kitu wanacho
fahamu.
Si lazima waumini wakubaliane katika kila jambo, likiwemo moja tu la
kuwaunganisha hilo linatosha.
New Age Movement ni juhudi za
watu mbalimbali kote duniani za kutafuta utulivu wa roho, akili, na mwili nje
ya mfumo wa dini zenye kuamini juu ya kuwepo kwa MUUMBA. Katika New Age
Movement muumini anaweza kuendelea kujiita ni Mwislamu, Mkristo au Myahudi kwa
jina na kwa maneno lakini kivitendo si mfuasi wa dini hizo, kivitendo anakana
juu ya kuwepo kwa MUUMBA.
KWAO DINI ZOTE ZINATAKIWA ZIUNGANE NA KUWA MOJA.
Katika New Age Movement MUUMBA, anahusishwa na nafsi
ya mtu binafsi, kuwa MUUMBA ni kuweza kujitambua wewe mwenyewe na kufikia daraja
la juu sana katika uwezo na ufahamu wa kajitambua wewe binafsi. Mafunzo yao
yanafundisha kuwa wewe ni sehemu ya nguvu kubwa na muhimu iliyo anzisha
ulimwengu huu, wewe na nguvu hiyo ni kitu kimoja, unachotakiwa kufanya ni
kuitambua nguvu hiyo, ukiitambua nguvu hiyo, utajitambua wewe, na ukijitambua
wewe, utamtambua MUUMBA, na wewe na MUUMBA ni kitu kimoja, na hicho ndicho
unacho takiwa kukitambua, kuwa wewe ni MUUMBA, wewe ni MUNGU.
New Age Movement
wanaamini kuwa kila mmoja wetu ni mungu isipokuwa watu hawafahamu, kwa vile
bado hawajajitambua.
Kwa nchi za Ulaya New Age Movement ni moja kati ya dini zinazo kuwa kwa
kasi mno. Hii ni kwasababu dini yenye mizizi mirefu ndani ya Ulaya, yaani
Ukristo umeshindwa kwa kiasi kikubwa kukidhi mahitaji ya kiroho, na kiakili kwa
waumini wake ambao sasa wameamua kutafuta mbadala wa hitajio hilo la kiroho na
kiakili.
Imani ya kwanza na iliyo ya msingi kwa New Age Movement ni kwamba, Kila
kitu unachokiona ni mungu, kila kitu unacho kiona, ukiwemo wewe mwenyewe ni
sehemu ya kitu kimoja ambacho kimesababisha kuwepo kwa uhai kwenye ulimwengu
huu. Kwa kutojitambua kwetu ndiyo sababu tumejiweka katika hali ya chini kama
‘kiumbe’ lakini sisi ni miungu ambao bado hatuja jitambua.
MUNGU kwa NEW Age
Movement haina tafsiri ambayo sisi tunaitumia katika dini zetu kama vile kwenye
Uislamu ambapo MUNGU ni MMOJA TU, HANA MSHIRIKA, HAJA ZAA WALA HAJAZALIWA, WALA
HAKUNA MFANO KWAKWE YEYE KITU CHOCHOTE.
Kwa New Age Movement tafsiri ya MUNGU
ni tofauti na hiyo ya Uislamu, New Age Movement wanatambua jina MUNGU kwenye
misingi hii; Ni nguvu iliyo leta uhai, siyo nguvu ya kimaumbile bali ya kiroho,
ambayo ipo ndani ya kila kitu, kila mtu, kila ‘kiumbe’ndani ya kila nyota,
sayari na galaxy. Mungu ni kila kitu unacho kiona, na kila kitu ni Mungu, huu
ndiyo ufahamu, ukweli wapekee na ulio wa msingi kwenye imani ya New Age
Movement.
Msingi wa pili wa imani ya New Age Movement ni kuwa hakuna wa kuabudiwa.
Kutokana na kuwa kwenye imani hii kila kitu na kila chenye uhai ni Mungu, basi
hakuna wa kumuabudu mwenzake, bali kilichopo kila anaye jitambua au atakaye
jitambua kuwa yeye ni ‘mungu’ basi afanye vile ambavyo ufahamu wake wa hali ya
juu unavyo muongoza, au afuate maelekezo ya juu kabisa kutoka kwa, ‘mwalimu,’
mkufunzi ambaye anaamini hivyo.
Msingi wa tatu wa imani hii ni kuwa , Ulimwengu, uhai, na vitu vyote vya
asili havikuumbwa na Mungu, bali vyenyewe ndiyo miungu. Kwamba ulimwengu na
uhai vimetokea kwenye ‘nguvu ya uumbaji’ iliyo ndani ya ulimwengu, ndani ya
kila kitu na kila kiumbe.
Msingi wa nne ni kuhusiana na maisha baada ya kifo. New Age Movement
wanaamini kuwa hakuna kifo, kuna wanao sema kuwa roho inahama na kwenda kwenye
kitu au kiumbe kingine, kuna wanao sema kuwa roho inapumzika kidogo kabla ya
kuamua kuwa ni mwili gani tena iuchukue na kuendelea na maisha. Hakuna pepo
wala moto wala siku ya mwisho, hizo ni imani za kibubusa walizo nazo watu
kutokana na ufinyu na ufahamu wa nini hasa maana ya mungu.
Msingi wa tano ni kuwa hakuna shetani, hakuna uovu. Kinacho itwa wema au
matendo mema ni nguvu ya uungu watu waliyo nayo ambayo hawaifahamu na
‘kimakosa’ wanadhani wameamrishwa kufanya hivyo na mafundisho fulani, lakini
kumbe hiyo ni asili yao wao kama miungu kufanya mambo mazuri bila kutegemea
malipo ya pepo au moto, kwanza hivyo vitu havipo, na wanacho kifanya kama wema
ni nguvu ya uungu waliyo nayo. Na wanacho kifanya kama ubaya ni kutokana na
kushindwakajitambua kuwa nafasi yao ipo kwenye duara la uungu.
Msingi wa Sita, uokovu kama unavyo tafsiriwa kwenye mafunzo ya dini ya Ukristo;
hakuna kwenye New Age Movement. Tafsiri ya uokovu kwao inakuja hivi;Mtu
anapofikia hatua ya kuitambua nguvu za ‘maumbile’ zilizo sababisha kuwepo kwa
uhai kwenye ulimwengu huu, na akatambua kuwa yeye ni sehemu ya nguvu hizo, basi
mtu huyo anakuwa ameupata uokovu.
Zipo njia mbalimbali zinazo tumika kwa mtu
kuweza kufikia hali hiyo ambazo zinahusisha na ‘kucheza’ au kuubadilisha hali
ya ufahamu wa ubongo kwa kutumia vitu kama vile hyponosis, meditation,aina
fulani ya muziki, aina fulani ya dawa,lakini pia hali hiyo inaweza kufikia kwa
kutumia aina mbalimbali ya ‘vifaa’ vya kiroho kama vile aina ya madini ya
Crystals,aina maalum ya karata, uchawi, kupokea taarifa maalum kutoka kwa
viumbe wasio kuwa binadamu maarufu kama channeling.
Wanaamini kuwa uokovu kwa watu wote utafikiwa pale ambapo sehemu kubwa ya watu
watatambua kuwa wao wote ni wa moja, wao na mungu ni wamoja, ni kitu kimoja,
hali hiyo ndiyo itakayo leta New World Order, kwa vile ulimwengu mzima
utatambua kuwa binadamu wote ni wa moja, ustaarabu wao ni mmoja, na kutakuwa na
serikali moja ya dunia kuhakikisha kuwa kuna furaha na amani.
Msingi wa Saba, mateso ambayo binadamu inayashuhudia kote duniani ni matokeo ya uchu,
ulafi, chuki, ujinga wa kutofahamu nafasi yetu hapa duniani kama miungu. Pia
wakati mwingine wanaamini kuwa mateso yanatokea kwa sababu maalum kama vile
kusaidia ukuaji wa kiroho na kujifunza somo maalum la maisha haya na mateso
yanayo tokea yanaweza kutafsiriwa kama ni aina ya somo ambalo tunalipitia kama
waungu.
Msingi wa Nane, utoaji mimba si suala linalo katazwa, kwa vile hakuna mafunzo rasmi
yanayo ainisha hilo, na hata hivyo New Age Movement ni wapiganiaji wa kubwa wa
haki za wanawake ikiwemo hii ya kuwaruhusu kutoa mimba. Utaona haki hii ya
utoaji mimba inawiyana sawia na mipango na mbinu za kupunguza idadi ya watu
duniani, mbinu inayotumiwa sana na maadui zetu.
Misingi hiyo nane niliyo itaja ya New Age Movement siyo rasmi, kwa vile
dini hii haina kitabu maalum kama muongozo wake, lakini hizo nane ni za msingi
na utazikuta katika kila muongozo na mwalimu wa New Age Movement. Unaweza
usizipate katika mpangilio nilio ueleza, zinaweza zikaongezeka au kupunguzwa
lakini utazikuta zimesimamia katika mazingira na nadharia hizo kuwa sisi
binadamu na kila kinacho tuzunguka ni miungu.
Ingawa jina lake ni ‘New Age’ Movement, mafunzo yake siyo ‘New’ katika
historia ya mwanadamu katika kumkana MUUMBA. Nadharia ya ‘umoja’ (oneness)
imeelezwa vyema katika kitabu cha kimila cha Kiyahudi ambacho ni lini hasa
kimeandikwa mpaka leo hakijulikani, lakini kilicho wazi kwenye kitabu hicho ni
kwanza si kazi ya Wayahudi, bali ni ‘urithi’ walioupata wakati wanatoka
Babyloni, ni kazi ya mashetani Wababyloni ambao Wayahudi walipokea kwa njia ya
mdomo.
Kutoka karne ya kumi na nane mpaka karne ya ishirini, ulimwengu umeshuhudia
kufufuliwa kwa kazi za kale mno na waandishi mbalimbali zilizo beba maudhui ya
New Age Movement. Alikuwepo Paracelsus kwenye zama za kati ambaye kazi zake
zilibeba maudhui ya ki-hermatik. Ingawa mafunzo ya hermetic yanatajwa kama ni
falsafa ya Ulaya, mapokeo au mafunzo au dini ya Ulaya lakini kiuhakika kabisa
asili yake ni mashariki ya kati, nayo ni mafunzo yenye asili ya uchawi na inayo
husiana na miungu wa kale wa Egyptna elimu ya kishetani iliyo pokelewa Babylon na Waisraeli wakati wakiwa utumwani hapo.
MOJA YA MISINGI NA MAFUNZO YA KIHERMATIC, 'AS ABOVE SO BELOW'
Karne ya kumi na nane ilimshuhudia Emanuel Swedenborg, huyu alikuwa ni
mwana sayansi, mwana falsafa na theolojia wa Kisweden. Mwenyewe alijiita
kupitia kwenye kazi yake aliyo ichapisha mwenyewe kama ni mtumishi wa bwana
Yesu Kristo, kazi hiyo ilikwenda kwa jina la True Christian Religion.
Lakini
zaidi alifahamika kwa kazi yake maarufu iliyo kwenda kwa jina la Heaven and
Hell. Alipo fikisha mika 53 aliingia kwenye maisha ya kiroho rasmi na hapo
akaanza kuona ndoto na maono yanayo muongoza na anayo poswa kuyatumia kuiongoza
jamii. Anasema alipokea maono kutoka kwa bwana yanayo mwelekeza kuandika upya
kuhusiana na maisha ya mbinguni kwa ajili ya kuujenga upya Ukristo.
Kutokana na
imani ya ‘kanisa jipya’ au imani ya Wakristo ambao wanafuata mafunzo ya New Age
Movement, ni kuwa Emanuel Swedenborg,
amefunguliwa macho ya kiroho ambayo yana muwezesha kuanzia kipindi hicho na
kuendelea, kuweza kutembelea, peponi, motoni, kukutana na malaika, mashetani na
viumbe wengine wa kiroho na kwamba siku ya hukumu ya mwisho imeshatokea mwaka
1757, katika maelezo yake ni kuwa hilo limetokea katika ulimwengu wa roho na yeye akishuhudia.
Aina hii ya mafunzo iliporuhusiwa kuingia kwenye milango ya kanisa ikawa ni chumbuko la mafunzo ya New Age ndani ya makanisa. Maajabu na mazingambwe kufanywa ni sehemu ya ibada. Mstari baina ya uchawi, ushirikina na ibada umekuwa mwembamba kiasi wakati mwingine unashindwa kutofautisha kipi ni kipi.
Kutoka karne ya kumi na tisa mpaka ile ya ishirini, mizizi na mbegu za New
Age Movement ilizidi kuota kupitia kwa watu kama Godfrey Higgins,Eliphas Levi,
Helena Blavatsky, na George Gurdjieff . Kazi ya mwana mama Alice Bailey na
asasi ya Theosophical Society zilipulizia roho ya uhai kwenye dini hii ‘mpya.’
Kwa jina ni New Age Movement, lakini kimafunzo ni moja kati ya dini za kale
za kipagani. Ndani ya New Age Movement kuna mafunzo ya yanahusiana na imani ya Mungu mmoja, miungu
zaidi ya mmoja, imani za kale za kishetani, imani ya inayo nadi kuwa dunia nayo
ni mungu mama, sayansi, elimu ya nyota, elimu ya mazingira, saikolojia na
fizikia. Wakati mwingine mafunzo yake yana beba jumbe au yanaathiriwa na
mafunzo ya dini za Mungu mmoja na zile za kishetani. Utakuta huko kuna baadhi
ya mafunzo ya Kiislam, Kikristo, Kiyahudi, Kibuddha, Taoism, Usufi, upagani
mambo leo,mafunzo na nadhari za kimagharibi, ilimradi ni vurugu na mchanganyiko
wa kila namna.
MALENGO NI KUZIUNGANISHA DINI ZOTE KUWA MOJA. KUMEKUWA NA JUHUDI ZISIZO RASMI ZA KUONGANISHA MITAALA YA KIDINI SHULE ZOTE KUTOKA MSINGI MPAKA VYUO, MAMBO HAYO YANAKWENDA KIMYA KIMYA
Hapa kwetu baadhi ya watu hawa walipata kuhojiwa na Redio ya Clouds kwenye
kipindi chao maarufu cha ‘Leo Tena,’ mwanzo walijinadi kuwa wao ni Freemasons,
lakini katika maelezo yao hawakuthibitisha ni namna gani wao ni Freemasons,
maelezo yao yalikuwa ni ya kujikanganya, mmoja akafahamika kuwa ni mshirikina
au mganga wa kienyeji, wakati mwenzake akijaribu kujitutumua kuwa ni Freemasons
lakini maelezo yake yakimtaja kama mwana ‘New Age Movement.’
Alijitahidi kadiri
alivyo weza kuonesha mfanano na uwiano baina ya dini kubwa duniani, maelezo
yake yalikuwa yakilenga kuziunganisha dini mbalimbali duniani na hasa hizi dini
kubwa, kitu ambacho ndiyo roho ya New Age Movement.
Lakini pia New Age Movement moto wake unakolezwa na kile kinacho fahamika
kama ‘Age of Aquarius’ ambacho tutakutana nacho kwenye post zingine
nikizungumzia mambo yanayo randana na haya..
Binadamu wa leo amesimama kwenye kona, kwenye daraja linalo elekea kwenye
zama mpya, maarufu kama Age of Aquarius.
Tunapo likaribia geti la zama hizo mpya, matumaini mapya, mipango,
ndoto, mitazamo, nadharia, imani na mwelekeo mpya nao inafunguka. Hali hii ya
‘New Age; sauti yake ilianza kupazwa tangu miaka ya 1960 kupitia vyombo
mbalimbali vya habari, majarida na aina nyingine za mawasiliano, lakini bado si
watu wote wanafahamu nini hasa maana ya ‘New Age.’
Wimbi la nchi za Magharibi kwenye miaka 1960 kuhusiana na New Age
kuliwafanya watu wengi kuamini kuwa tumeingia kwenye New Age. Kuna wanao dai
kuwa tumeingia kwenye zama za Aquarius tangu mwaka 1781, wapo wanao dai
hatutaingia mpaka miaka 50- 100 ijayo, na mengine na mengine. Lakini ni vigumu
sana kusema ikiwa tayari tumeshaingia au la katika zama hizo au ni lini
kiuhakika tutaingia, kwa vile tukio zima linategemeana na safari ya kutoka
‘nyumba’ moja ya Zoadic kwenda nyingine, na kwa vile ukubwa wa nyumba moja na
nyingine ni tofauti na nafasi baina ya nyumba hizo hali kadhalika, inakuwa ni
vigumu mno hasa ikichukuliwa kuwa kwenye hesabu zetu mzunguko huo umewekwa kwa
kipindi maalum, bila kuzingatia tofauti ya umbali na ukubwa baina ya vikundi
hivyo vya nyota.
Kwenye miaka hiyo ya 60 mpaka 70, idadi kubwa ya wasomi wasio makini,
waliwashawishi wanafunzi pamoja na watu wengi kuondoka katika nchi zao za
kimagharibi kuelekea nchi za mashariki, hasa India, kwa ajili ya kutafuta
‘hekima, elimu,ukweli, ufunuo , nuru na karma
njema.
Ni wachache kati yao ndiyo walio elewa kuwa, wanaifuata njia ileile,
iliyopitwa na mwana mama miaka mia kabla, mwana mama huyo kupitia safari kama
hiyo akaweka misingi ya ‘NewAge Movement’, ambayo leo hii tunaiona duniani
kote, kama ni inayo fufuka.
WAKINA MAMA VINARA WA NEW AGE, SI BURU VUGUVUGU HILI LINALISIMAMIA KWA NGUVU ZOTE HAKI ZA AKINA MAMA.
Mwanamke huyo hakuwa mwingine ila ni Helena P. Blavatsky, ambaye
anafahamika kama mtume wa dini hii ya New Age. Mwaka 1875 mwana mama huyu
alianzisha asasi iliyo fahamika kama Theosophical Society.
Mwana mama huyu alifundisha upagani, udugu wa kidunia, na muungano wa dini
zote duniani, isipokuwa dini za Mungu mmoja, hizo alisema haziwezi zikaungana
na kile alicho kiita ukombozi kwa mwanadamu.
Alimlaumu na kumkashifu Mungu
mmoja, kuwa hakuwa akitenda haki, na alisema huyo alikuwa ni Mungu tu wa wana
wa Israeli na siyo zaidi ya hapo, anasema kuwa vitabu vitakatifu vimekosewa,
kwani ni shetani ambaye ndiye aliyekuwa Mungu mzuri na wa haki.
Alisema kuwa alikuwa na uwezo wa kuwasiliana na viumbe wenye roho tu, kama
vile majini na malaika. Vitabu vyake kama vile ‘Isis Unveiled’ na ‘Secret
Doctrine’ aliweza kuvinadika kupitia taarifa ambazo zilikuja kutoka kusiko
julikana na kumiminika kichwani mwake naye akaanza kuyaandika, wakati mwingine hutokea mkono huanza kuandika
wenyewe bila mamlaka yako, na wakati huo unakuwa upo kwenye hyponetic au kwa
hapa kwetu tunaweza kusema umepandisha shetani, njia hizi pia hufahamika kama
channeled.
Kwenye kitabu chake alicho kiita ‘The Secret Doctrine’ Blavatsky ameandika
hivi;
“Lucifer anawakilisha uhai, mawazo, maendeleo, ustaarabu .”
Kwenye kitabu chake, 'The Secret Doctrine' Blavatsky ameandika,
“Haki na
uhuru kwa Lucifer ni alama kuu, ni Nyoka, ni Mwokozi na ni Lucifer ndiyo Mungu
wa sayari yetu na Mungu wa pekee,”
halafu akaendelea kuandika,
“Na bikira wa
Virgo (kikundi cha nyota ya virgo) ambaye amekuja kuwa Mama wa Mungu na Mama wa
Shetani kwa wakati mmoja, kwani ni mama mwenye Baraka siku zote, lakini kwenye
historia uhalisia, Lucifer au Luciferius ndiyo jina. Lucifer ndiye mtakatifu na
nuru ya mbinguni, ni roho mtakatifu na shetani kwa wakati mmoja.”
Blavatsky alipo kufa mwaka 1891, Annie Besant, mwanamama mwanajeshi,
masonia na mwanachama wa asasi ya Fabian Socialist Society ya England alichukua
nafasi ya Blavatsky. Mwana mama huyu alikuwa ni rafiki wa George Bernard Shaw,
H.G Wells na viongozi wengine wa asasi hii ya Fabian, hivyo alikuwa kwenye
nafasi nzuri mno ya kupenyeza mawazo ya mwenzake aliye mtaangulia kwa watu
muhimu mno. Unakumbuka nembo ya asasi hii ni Mbwa Mwitu aliye vishwa ngozi ya
kondoo.
Alishiriki katika maandamano mbalimbali kwenye kupaza sauti yake isikike
juu ya kile anacho kitaka walimwengu wakifahamu, aliandika vitabu mbalimbali
kuongezea nguvu kwenye kazi zilizo tangulia za Blavatsky.
Baada yake huyu akaja mwanamama mwingine aliyekwenda kwa jina la Alice Bailey.
Utamkumbuka mwana mama huyu nimemtaja kwenye posti zinazo zungumzia ndoa za
jinsia moja, namna alivyo weka mapendokezo ya kufikia lengo la wanaume kuowana
wao kwa wao na wanawake wao kwa wao, leo tena tunakutana naye kwenye New Age
Movement, na dini hii haipingani na mambo ya kishoga, kama tulivyoona kwenye
dini hii hakuna jema wala ovu.
Bailey naye akishirikiana na mume wake Foster
Bailey, ambaye alikuwa ni mwana masonia wa daraja la 32, wakiwa wameshikilia
jukumu la asasi ya Theosophical,
walifanikiwa kuweka misingi imara juu ya kile ambacho leo tunakiita ‘New Age
Movement.’ Katika hili waziwazi waliweka hadharani mguso wao wa kiushetani, na
wakatengeneza kampuni ya uchapishaji iliyo kwenda kwa jina la Lucifer
Publishing Company na jarida waliloita jina la Lucifer. Kwa vile dunia ya
kipindi hicho ilikuwa ‘bado’ haijawa tayari na maono hayo ya kishetani na kuona
kwamba wangeonekana ni kichekesho, walibadilisha jina la kampuni hiyo na kuita
‘Lucis Publishing Company’ lakini mguso wa kiushetani bado uko palepale, kwani
walicho fanya ni kufupisha jina la bwana mkubwa wao, kutoka ‘Lucifer’ kuja
kwenye ‘Lucis.’
Mwaka 1922 wakaanisha ‘Lucis Trust’ ambayo mpaka leo bado ipo na inafanya
kazi kwa mwavuli unao zibeba asasi zingine zilizo za kishetani au zenye maono
na malengo ya New World Order ikiwemo dini mpya kwa watu wote, ambayo wafuasi
wake kwa sasa ni ‘wana NewAge.’ Baadhi ya mashirika na asasi zilizo chini au
zinazo dhaminiwa na ‘Lucis Trust’ ni United Nations, Arcane School, World
Goodwill, Triangles, Lucis Publishing, Lucis Productions, Lucis Trust Libraries
na New Group of World Servers.
Alice Bailey naye alipokea ‘ufunuo’ wake kupitia kwa Djwhal Khul ambaye
kupitia kwake aliandika vitabu ishirini. Lengo kuu ni kutengeneza kile kinacho
fahamika kama ‘Harmonic Convergence,’ pia unafahamika kama muungano wa kiroho,
au nukta ya mageuzi ambayo itafikiwa au kutokea pale ambapo mataifa yataweka
kando kasoro na tofauti zao, katika sura mpya itakayo fahamika kama ‘New World
Order’ na muungano mpya wa kidunia, wakati ambao serikali ya dunia, na dini
moja ya dunia itapatikana, zama mpya au zama za Aqurius zitakuwa zimeanza.
Ni
kutoka hapo tu. Ndipo mmoja anaye ngojewa atakapo tokea, kama ni Yesu, Mahdi,
Krishna, Maitrayaa au yoyote yule katika dini au mafundisho yoyote yale anaye
tajwa kuwa atarudi, basi wakati huo ndipo atakapo onekana, kama nilivyo kwisha
tangulia kueleza katika posti zilizo pita, maadui zetu wanayo hiyo teknolojia
ya kufanya watu hao waonekane kuwa ‘wamerudi,’ lakini zaidi watu hao hawato
waita watu katika mafundisho ya dini waliopata kuifundisha hapo kabla, lakini
watawaita watu katika ‘muungano wa kidunia,’ ‘katika dini mpya ya muungano wa
kidunia,’ katika dini ya wana NewAgers’.
Kama kawaida viongozi wako wa kidini watakuwa mstari wa mbele kuwaunga mkono
jamaa hawa na kukushawishi wewe muumini
wao kwa vifungu vilevile kutoka kwenye kitabu chako kitakatifu uwaunge
mkono ‘wateule’ hawa wa kale lakini wakiwa na dini mpya kabisa.
Kwenye kazi zake Bailey ameweka wazi kabisa kuwa, patakuwepo na dini mpya;
“Mafunzo ya kiroho yamehama kutoka kwenye imani za zamani na kuja kwenye
nuru mpya ya kiroho ambayo itaiangaza na kutapakaa duniani kote kama dini mpya
kwa dunia yote. … Uyahudi ni wakale mno, na zaidi umejitenga na hauna ujumbe wa
kweli wa kiroho na kiakili kushinda ule unao tolewa na imani mpya … imani ya
Kikristo nao imeshatekeleza malengo yake. Waanzilishi wake wanatafuta kuleta
agano jingine jipya ambalo litawamulika
watu kila kona. (Uislamu nao hauna lolote zaidi ya vurugu tunazo ziona)”
Mwandishi wa kazi moja matata, bwana David Livingstone, alipoandika
‘Terrorism and Illuminati’ kwenye utafiti wa kazi hiyo alifichua kuwa Lucis
Trust inafanya kazi zake kupitia wana bodi wateule wa kimataifa kama vile, John
D. Rockefeller, Norman Cousins, Robert S. McNamara, Thomas Watson, Jr. wa IBM
na kinara wa New World Order na Freemasons wa daraja la 33 na mwenye mikono
iliyo jaa damu za walimwengu bwana Henry Kissinger.
Oganaizesheni hii ya Bailey
pia inafanya kazi kwa mashirikiano na asasi zingine ambazo nazo ni washiriki na
wachezaji wazuri wa nyimbo za New World Order kama vile; CFR, Bilderberger
group na Trilateral Commission.
Aprili 25, mwaka 1982, mamilioni ya watu kote duniani, walisoma vichwa vya
habari vya magazeti mbalimbali, kote duniani, vikisema, ‘KRISTO SASA YUPO
HAPA.’ Habari hizo zilikuwa na maudhui kwamba, katika historia ya ukuaji na
maendeleo ya mwanaadamu, kiumbe huyu mwana wa Adam amekuwa akiongozwa na watu
wenye nuru, viongozi wa hekima, viongozi wa daraja la juu kiroho, ambao
viongozi hao nao wanaongozwa na mwalimu wa dunia, ambaye anafahamika kama Lord
Maitreya.
Taarifa hiyo ilidai kuwa kwa wakati huo ‘Kristo’ alikuwa anaishi duniani, na ndani ya
miezi miwili tu, atajidhihirisha kwa kila mtu amuone. Wakati huohuo Mwingereza
Mkristo anaye fuata ‘agano’ jingine jipya, au mfuasi wa ‘Ukristo wa kisasa’ na
mfuasi wa imani ya Theosophical, bwana Benjamin Crème, alianza kuizunguka dunia
na akitangaza kuwa yeye anazungumza kwa niaba ya ‘Kristo.’
Katika mahojiano yake na mazungumzo yake mbele ya hadhara, alielezea kuwa,
si kwamba anasimama badala ya Yesu Kristo, bali ni kwa niaba ya ‘Mwalimu wa
Hekima,’ ambaye kutoka kwake Yesu Kristo, Buddha, Krishna, Muhammad na wengine
ni wanafunzi wake. Kwa maneno mengine Crema alikuwa anatuambia kuwa na yeye
sasa ameingia kwenye orodha hiyo ya kina Muhammad, Yesu Kristo, Krishana na
wengine, kwani na yeye sasa Crème anazungumza na ‘Mwalimu’ yuleyule aliye
wafundisha wakina Yesu na wenzake, yaani Crème ni mtume, mtume wa ‘New World
Religion.’ Haswa ndivyo alivyo kuwa na ndivyo alivyo mpaka hivi sasa.
Kampeni hii ya kimasoni ya Crème, iliyo fanywa nyuma ya jina la Ukristo,
ilidhaminiwa na oganaizesheni ya New Age Religion inayo fahamika kama Tara
Center, kutoka makao yake makuu ya London, Los Angeles na New York. Lakini
mwalimu huyu wa Crème au Lord Maitreya hakuweza kujitokeza kama ilivyo elezwa,
nadhani wimbi hili la New Age na dini yao lingekuwa limejitundika kitanzi chake
yenyewe, ingekuwa limejichimbia kaburi lake, propaganda na vipindi vyao
mbalimbali kote kwenye redio na luninga vingeanguka patupu.
Lakini haikuwa
hivyo, uwezo wa binadamu kuchanganua mambo umekwisha kabisa, uwezo wa kufikiri
umefunikwa na kiza cha majibu mepesi ya wanasiasa na vipindi vya luninga, Crème
bado anatambulika kama mtume wa New Age, na mtandao mpana wa New Age unaingia
na kupenya kwenye kila kona ya dunia, kupitia mitandao ya kitaifa na kimataifa,
kupitia vikundi vya wanaharakati mbalimbali, watizame kwa makini wale wanao
jiita ni ‘ma-activist’ au ‘wanaharakati’ tizama vifungu vya ‘biblia’ yao,
tizama msukumo ulio nyuma ya kazi zao, utaona vidoti vinavyo chora picha ya New
Age, picha ya New Age Religion, picha ya Crème.
Mitume hao wa New Age utawakuta katika kila taasisi za kitaifa na zisizo za
kitaifa, mmoja mmoja au kikundi na hata makundi, wanaojijua na wasiojijua,
miongozo yake utaikuta kwenye mikutano ya Umoja wa mataifa, kumbuka moja ya
wafadhili wa kazi za Umoja wa Mataifa ni Lucis Trust. Utaikuta miongozo hiyo
kwenye sera za mashirika yenye nguvu na ushawishi kwenye dunia ya leo kama
vile; Club of Rome, Aspen Institute, Council on Foreign Relations, World
Federalists, World Bank, na mengine na mengine.
Wafuasi wa dini hii mpya utawakuta kwenye sura mbalimbali kama vile,
wanajimu wanao amini juu ya nguvu za nyota na kuvipa viumbe hivyo sifa zisizo
zake, utawakuta kwenye vikundi vinavyo dai kupigania haki za wanawake, haki za
watoto, haki za binadamu, haki za mashoga. Utawakuta kwenye wanaharakati wa
mazingira, utawakuta kwenye wafuasi wa Kabbala, utawakuta kwenye viongozi wa
kidini na wafuasi wa dini kuu tatu kama vile Uislamu, Ukristo na Uyahudi lakini
wakipaza sauti vifungu katika baadhi ya mafundisho kwenye vitabu vyao
vibadilishwe ili kuendana na ‘hali’ ya sasa.
Utawakuta kwenye duara la
wanasayansi, wana diplomasia, viongozi wa taasisi mbalimbali duniani, viongozi
wa nchi, utawakuta kwenye maduara ya watu maarufu na matajiri wa dunia hii leo.
Hawana chochote zaidi ya biashara. Lakini wao kuwa wafanya biashara siyo shida,
shida ipo kwenye madai yao na ushuhuda wao.
Hapa kwetu Tanzania tunao wengi, na
kila leo wanaibuka, lakini tabia na sifa zao zimevaa vazi la wana-newagers. Mfano msafi kabisa kwenye aina
hii ya dini na mitume wake ni Babu wa Loliondo. Sina haja ya kuandika hapa ni
nini kilitokea yalishaandikwa na kusemwa na bado familia zilizo athirika na
kitimbi cha Babu wa Loliondo, zimelipa gharama kubwa ikiwemo uhai kwa wapendwa
wanafamilia wenzao, kutokana na madhara ya New Age Movement.
Si maanishi kuwa
Babu wa Loliondo ametumwa na akina Creme moja kwa moja, hapana, namaanisha kile
alichosema na alichokifanya kwa watu waliomsikia na kumuamini na kumfuata
kinayo sifa, sura na tabia za akina New Age Movement.
Leo hii tunao mitume na manabii mbalimbali, ambao wanadai kupokea maono
kutoka kwa MUUMBA mwenyewe, lakini kila tunapo watizama mitume hawa wa leo,
kila tunapo sikiliza maneno yao, nafsi zetu zinakiri kuwa kuna shida katika
shuhuda zao, katika kazi zao, katika maneno yao na alama zao, lakini kwa vile
dunia ya leo imezama kwenye kuutengeneza mwili kuliko roho, kasoro hizo
tunazifunika, ile tupate kile jicho letu ilicho tupatia, moyo wetu ulicho
tamani bila kuwa na wasiwasi wowote juu ya matendo yetu.
Hayo ni madhara yanayo tokana na mafundisho ya Darwin kwa walimwengu.
Ingawa Darwin alikataa juu ya kuwepo kwa roho, wakati New Age wao wakisisitiza
kuwa roho ipo, na hiyo ni moja ya misingi yao mikubwa kwenye dini hii; lakini
wengi wa wafuasi wa dini hii utawaona waapo kwenye kwa ajili ya kupata manufaa
ya kiwiliwili kuliko roho.
Hiyo ndiyo athari ya mafunzo ya Darwin, kwamba watu wamesahau kuwa wanayo
asili mbili, asili ya roho na asili ya mwili, watu wamebaki na asili moja tu na
ndiyo inayofanyiwa kazi usiku na mchana, asili ya mwili. Hii ni kwasababu tangu
tupo chekechea mpaka tunastaafu ajira, tunacho fundishwa, tunachokiona, tunacho
aminishwa ni juu ya ulimwengu wa kivutu zaidi, ulimwengu wa materialisim.
Sasa
ulimwengu huu wa materialisim unaboresha mwili na kuiacha roho imedhoofu, sasa
watu wanarudi nyuma kutafuta ‘peace of mind’ ambayo wameikosa kwenye
‘materialisim’ na hapo wanakutana na new age movement ambayo inatoa ahadi ya
kutatua matatizo ya leo ya ulimwengu kwa ujumla au kwa mtu mmoja mmoja, pao kwa
hapo. Ndiyo utaona watu wanajazana kwenye aina hii ya mafunzo na dini bila
kujali imani yake ni dini ipi, na sababu athari ya Darwin imekuwa kubwa sana
kwenye maisha yetu ya kila siku, hata tukienda huko hatufati ‘peace of mind’
tunafuata sabuni ya roho, tunafuata pesa ambazo manabi wa dini hii wanahubiri
kuwa watakupatia kwa wepesi, ili ukajitatulie shida zako kwenye ulimwengu wa
kivitu zaidi kuliko roho.
Tunamtafuta Mungu, Muumba wa ulimwengu wote, Muumba wa tunavyo vijua na
tusivyo vijua. Tulianzia na Sayansi yetu ya leo ya karne ya 21. Sayansi hii
kwenye suala la uumbaji imejikita zaidi kwenye nadharia ya Darwin kama ndiyo
msingi wa ukweli juu ya uumbaji, katika posti iliyo tangulia tumeichambua
nadharia hii na kweli tumekutana na mapungufu ya kutosha na kiufupi tumeiyona
haiwezi kutusaidia katika safari yetu hii yenye maana kubwa kuliko. Safari ya
kujitambua na kutambua asili yetu.
Hata hivyo kwenye karne 21 sayansi yetu ikachukua njia nyingine isiyo rasmi
kwa kasi zaidi. Njia hiyo ni uwezekano wa kuwepo viumbe wengine ambao huenda
wakawa ndiyo waungu wenyewe, njia hii mpya imefuatana na ile ya kale kidogo
lakini yenye jina jipya, New Age Movement, njia hii nayo tumeitazam kwa uchache
lakini kama tulivyona katika misingi na taratibu zake ni kama muendelezo wa
kazi za kina Darwin.
New Age inatuambia haina haja ya kumtafuta Mungu, kwani sisi wenyewe ndiyo
waungu. Lakini tunapo itazama kwa undani tunaona kuwa madai hayo nayo hayana
majibu sahihi juu ya kile tunacho kitafuta.
Kama sisi ni waungu, mbona ....? Kama sisi ni waungu mbona ...? Kama sisi
ni waungu mbona ..,?
Maswali tutakayo jiuliza yanaweza kujaza majalada na majalada, mabuku na
mavitabu makubwa makubwa na hayoto kuwa na majibu sahihi.
Hivyo kiukweli kabisa New Age imeshindwa kutuambia asili yetu ni wapi,
imeshindwa kutuambia sisi ni akina nani. Ilichoweza kufanya ni kutuongezea dozi
kwenye nadhari ya Darwin ambayo nayo ilisha shindwa kabisa. Hivyo hii nayo tuna
achana nayo.
Bado tunaendelea kumtafuta Mungu na kwakuanzia tumetaka kufahamu sisi ni
akina nani, ambapo tukiweza kujua asili yetu, tutaweza kumjua hata huyo
aliyenyuma ya sisi kuwepo hapa ...
Next post tutaendelea kuitafuta
asili yetu, lakini safari hii tukitazama dunia zote mbili, dunia ya roho na
dunia ya mwili
till next time ...
So ngoja nisema hivi mwenyezi mungu tuongezee imani tuwe na imani na uwepo wako
ReplyDelete