Uwongo ndiyo uti wa mgongo na moyo wa agenda hii ya Ushoga.
Daktari analizungumzia hili la kinasaba cha ushoga.
Leo tunatizama uongo wa kusema ‘USHOGA NI MAUMBILE YA ASILI’ au ‘USHOGA UPO
KWENYE VINASABA ‘DNA’ ZA BINADAM.
Huo ni urongo kama tutakavyo ona.
Kusema kauli hizo, ni kwa makusudi mazima ya kupunguza msuguano na makali
ya nguvu kinzani dhidi ya ushoga. Kwamba hali ya ushoga mtu anazaliwa nayo, na
kwamba ni maumbile ya kiulimwengu ambayo inabidi wengine tuyakubali na
tusiwapinge wala kuwaoneshea vidole.
Hii ndiyo kazi ya sayansi na wanasayansi wa kutengenezwa, kwamba wamegundua
kunayo kinasaba katika maumbile ya binadam aynayo mfanya kuwa shoga.
Lakini ukweli wa msingi ni kwamba, mtu hazaliwi ‘shoga’ lakini anachagua kuwa
shoga katika mwenendo wa maisha yake. Hivyo ushoga mtu hazaliwi nao, bali ni
tabia nayo amua kuifuata mtu baadae katika maisha yake kama zilivyo tabia
zingine. Mtu hazaliwa na ‘kinasaba’ cha wizi au uzinifu lakini mtu anachagua
kufanya matendo hayo katika mwennendo wa maisha yake, na akitaka pia anaweza
kuyaacha na kuwa sawa na wanajamii wengine.
Kama yalivyo matendo mengine maovu, ushoga nao ni mojawapo ambayo ni
kinyume na sheria za kimaumbile zilizo wekwa na Muumba Mwenyewe. Kutengeneza
mbadala mwingine dhidi ya ukweli huu, ili matendo yao machafu yafanyike bila
yeyote kuguna ni moja ya njia ya kupunguza haya na aibu kwa mashoga ambao wengi
wao wanajidhiki na kuteseka na msongo wa mawazo unao sababishwa na mkanganyiko
baina ya nafsi na akili zao.
Kwamba ITS OK TO BE GAY! Lakini ndani kabisa
kwenye nafsi zao, wanapokuwa wenyewe, na kuzitazama nafsi zao, na kuzihoji
akili zao juu hili, hakuna wanachopata zaidi ya aibu, haya, soni, mashaka,
vinavyo pelekea kupata msongo wa mawazo, na mwisho kabisa kukiri katika nafsi
zao kuwa wanacho kifanya kinapingana na sheria za kimaumbile.
Lakini ndiyo wameshageuzwa kuwa mashine ya kuitengeneza jamii kukubaliana
na uozo huo, watafanyaje? Inabidi wameze japo ni chungu, mwisho wa yote
wanaishia kuteseka wao na kila aina ya dhila unalo lijua, watatumia dawa za
kulevyia kupindukia, ulevyi kupindukia, kila aina ya uchafu wa kupindukia na
mwisho wa siku wanaacha, ‘socide note.’
Wakufunzi wa agenda hii wanatumia msamiati kama vile, ‘we are born that
way’, kauli hii inawapa matumaini mashoga waweze kupambana na nafsi zao wenyewe
ambazo zinakiri kuwa ‘they ate not born that way’, lakini pia inawapa
wanasodoma ‘confidence’ ya kutembea kifua mbele na kujitangaza kwa uma kuwa wao ni wanasodoma na gomora.
Hawataki kusikia kabisa kwamba usodoma na gomora ni ugonjwa na unatibika.
Kukubali kwamba ushoga ni ugonjwa na unatibika ni kukubali kwamba ushoga si
maumbile ya asili na wala hakuna kinasaba cha ushoga. Hivyo hilo linapingwa vikali
na usishangae ukafunguliwa mashtaka ya kuwabagua na kuwanyanyapa mashoga chini
ya vifungu vya haki za binadam.
Katika mazingira ambayo watu wa jinsia moja, mathalani wanaume wametengwa,
kama magerezani, mashuleni, jeshini na kwengineko, baadhi ya wanaume watafanya
vitendo vya ushoga kwa makusudi kama njia ya kuonesha, ubabe, nguvu, kiburi,
utawala wa mabavu dhidi ya mfanyiwa. Lakini wote mfanyiwa na mfanyaji baadae
katika maisha yao wataoa na watapata watoto.
Utaona ni maamuzi ya mtu kuchagua kupita njia hiyo. Mashoga wanapiga kelele
kama kuna uchaguzi, basi uchaguzi wa wao kuwa mashoga haujafanywa na wao, bali
ni mpango wa Mungu. (Mola Tusamehe) Hivyo wanaukataa ukweli kwa kumrushia
lawama Muumba kwamba ndiye aliye wachagulia kuwa hivyo. Lakini kwenye masuala
mengine ni uchaguzi wao, kasoro hili, utaona ubinafsi walio nao, mazuri ya
kwao, mabaya, ya Mungu.
Utawaona mashoga wanatembea kwa mshikamano, wakiwa uchi au nusu uchi,
kuelezea uhalali wao wa kuwa mashoga. Lakini hili huwezi kuliona kwa watu ambao
si mashoga kwamba wanatembea kwa mshikamano kuelezea jinsia yao, au
kuwalazimisha watu kuifuata na kuikubali, hii ni kwasababu kile kinacho elezewa
na mashoga kuwa ni chao, si chao bali wamekiokota walipo kiokota na wanataka
kukihalalisha kwa kila namna na kwa kila jinsi kwa wengine ili waishi kwa
amani, lakini, mwizi ni mwizi tu, anaporudi ndani kwake na kuhesabu marundo ya
fedha alizopora, anakiri kwa nafsi yake kwamba si zake bali kapora, na ilivyo kwa mashoga, mwisho wa siku wanapokuwa wenyewe, bila kamera mbele yao,
bila kipaza sauti karibu yao, bila mashoga wenzao pembeni yao, wanakiri, hili si
langu, na huyu si mimi!!!!
Haijalishi ni ukelele mkubwa kiasi gani unao pazwa, au ni nguvu kiasi gani
inayotumika kulifanya jambo la ushoga ni jambo la kawaida, ukweli utabaki kuwa
ukweli siku zote, bahari ya maandishi ya kughushi, na propaganda zinazofika
kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro haviwezi kubadilisha ukweli huo. Kwamba
Ushoga siyo ‘life Sytle’ bali ni ugonjwa wa akili na unatibika kwa anayetaka
kufanya hivyo.
Siku zote ugonjwa haubebi chochote ispokuwa magonjwa, na
ukiachwa utaendelea kualika magonjwa mengine yaje kushiriki karamu. Ugonjwa wa
ushoga nao uko hivyo hivyo, tafiti huru na zilizo kawaida kabisa zinaonesha
hili.
·
Kiwango kikubwa cha msongo wa mawazo, woga na wasiwasi kwa ujumla wake,
utumiaji wa dawa za kulevyia wa kupindukia na mfano wake, yameripotiwa kwa
kiasi kikubwa kwa mashoga, tena vijana.
·
Kiwango kikubwa cha wasiwasi, mabadiliko ya mara kwa mara ya tabia,
matumizi makubwa ya huduma za afya, hasa afya ya akili (saikolojia) nalo
limeripotiwa kwa kiasi kikubwa kwa mashoga kuanzi miaka 15 mpaka 54.
·
Ushoga wenyewe umekuwa ni ugonjwa dhidi ya utamaduni wa sehemu husika na
kumekuwa na vita baina ya jamii ya mashoga na wale wasio kuwa mashoga.
·
Ugonjwa wa ushoga umepelekea mpaka kwa nchi na viongozi wa kidini
kulazimishwa kubadilisha katiba au vitabu na mafundisho ya dini zao ili waweze
kuwapa mashoga haki sawa na raia au waumini wengine.
·
Mashoga wanabadilisha sheria za kuasili, ili waweze kuasili watoto, na
baadhi ya nchi wamesha ruhusiwa kufanya haya. Wanapora watoto wa wengine na
kuwafanya wa kwao. Hawataki kuwa na watoto lakini wanataka kuwa baba na ‘mama’
wa watoto wa watu wengine. Ajabu sana.
·
Watoto wadogo wa kiume wamekuwa waathirika wakubwa wa vitenfo hivyi vya
kishoga, kutoka kwa makasisi, viongozi wa kidini wanao tumainiwa, walimu na
viongozi wengine katika nyadhifa mbalimbali, watoto wetu wa kiume si salama
kwenye macho ya wagonjwa hawa.
Watu wa haki za binadam, wanaharakati wa haki sawa na zile za mashoga,
wamefanya kazi hii chafu kwa nguvu na kila hila na mbinu waliyoijua kumimina
propaganda za kila aina kwa jamii ili wailaghai na kuwarubuni kukubali uozo huu
kwenye maisha yao ya kila siku, hali wanajua kabisa ushoga ni uchafu, uozo,
ugonjwa na moja ya mbinu chafu za shetani za kumshusha binadam katika hadhi ya
chini kushinda mnyama.
Kusema ushoga unayo kinasaba ni propaganda za kuzishika akili za watu kama
walivyo zishika kwa kutuambia kuwa ukimwi umeletwa na sokwe. Hawana ushahidi
wowote wa hicho kinacho itwa sayansi kuthibitisha madai yao hayo ya kinasaba
cha ushoga, kama ambavyo ni zaidi ya miaka 30 sasa na hawajaweza kuthibitisha
japo kwenye karatasi moja la A4 kuwa ukimwi umeletwa na sokwe.
Yote wanayo taka kuyafanya ni kuona dunia nzima imezingirwa na kiza cha
maovu, ufedhuli, ushetani na kila baya unalo weza kulifikiria ili dola ya kiza,
dola ya shetani, dola ya Al Masih Dajjal/Mpinga Kristo isimame pasina kizuizi.
Nadharia kwamba ushoga una kinasaba cha DNA kwa muhusika na kwamba ni kitu
ambacho muhusika hawezi kukibadili sababu ndivyo maumbile yake yalivyo, na sawa
yeye kuwa hivyo, na ni makosa makubwa kumnyooshea vidole na kumlaumu, watu
wenye nadharia hii wanatukuza vitendo vya Sodoma na Gomora na kumnyooshea
kidole yule ambaye anasema tofauti.
Lakini ukweli ni kuwa shoga anatengenezwa, au anajitengeneza, lakini mtu
hazaliwi shoga. Mtu anafanya uchaguzi wa kuwa shoga kama ambavyo mlevi anavyo
chagua aina ya kilevi anachotaka, lakini haimaanishi kuwa kazaliwa mlevi.
Wazazi / walezi wanayo nafasi kubwa ya kuamua mtoto awe nani baadae.
Familia ambayo inasema ni sawa mtoto kuwa vyovyote atakavyo, inafanya kosa
kubwa la kusimika misingi ambayo baadae itakuwa chanzo cha mtoto huyo kuwa ni
adui kwa jamii.
Mtoto anaye lelewa na mashoga wawili unadhani hatma yake itakuwaje?
Unadhani mtazamo wake utakuwaje juu ya suala hilo?
Kwanini basi kama ushoga ni kitu unazaliwa nacho kufanyike kmapeni kubwa ya
gharama kubwa, hata nchi itishiwe kunyima misaada kwa sababu tu inawanyima
mashoga ‘haki’ zao.
Kwanini waandamane barabarani uchi? Kwanini waendee umbali wote huo ni kitu
gani wancho jaribu kusisitiza? Kwamba wako Ok? Au wanajifariji kwamba wanaweza
kukubalika kwa njia hiyo? Mbona basi kesi za wao kujiua zimekuwa nyingi
kushinda watu wa kawaida?
Mtanange wa mada hii bado unaendelea, tukutane tena hapa, kutizama namna ushoga unavyo fundishwa kwa watoto ... Yes watoto wanaanza kufundishwa siyo ngono tu, lakini ushoga pia ... anafundishwa wapi? anafundishwa na na nani? Nani analipa gharama za elimu hiyo ? ..
Dont miss, I will tell You here here....
Endelea kututoa gizanikaka
ReplyDeleteEnter your comment...dah, kaka endelea kutufumbua macho
ReplyDelete