Saturday, December 7, 2013

NYEUPE NA NYEUSI NDANI YA FREEMASON

LEO WAPENDWA NINGEPENDA TUTIZAME SAKAFU NDANI YA HALL LA KIMASONIA, NIMEPENDA KULIZUNGUMZIA HILI KWA VILE SAKAFU HIYO HAIPO KWA BAHATI MBAYA NDANI YA MAHEKALU YA KIMASONIA, NA UTAZIKUTA KATIKA KILA KONA YA HEKALU LA KIMASONIA KOKOTE DUNIANI, LAKINI MBAYA ZAIDI, ALAMA ZENYE KUFANANA NA NAKSHI ZA SAKAFU HIYO TUMEKUWATUKIKUTANA NAZO NA KUZITUMIA KWA NAMNA MBALIMBALI BILA KUJIULIZA ZIPO HAPO KWA MAANA NA SABABU GANI, SASA LEO TUTAANGALIA MAANA HALISI YA SAKAFU HIZI .....

KARIBU TUWE SOTE


Mwanachama wa kimasoni kwenye chekered floor. Katikati utaiona ile nyota, yenye ncha iliyo elekea juu. Wakati mwingine huweka ile yenye ncha iliyo elekea chini kutegemea na mahitaji na ibada husika.


SAKAFU YA VIBOKSI VYEUPE NA VYEUSI
        Karibu alama na nembo zote za freemasonry ni kwa ajili ya kuleta uharibifu kwa watu, katika mahekalu yote ya kimasoni utaona sakafu yenye rangi nyeupe na nyeusi, mfano wa chombo cha kuchezea drafti, wanasema rangi hizo mbili zinamaanisha mahusiano kati ya uovu na wema, na au nguvu mbili kinzani chanya na hasi.
        Mfano wa hizi rangi mbili utaziona pia kwenye kile kinacho fahamika kama ‘Yin na Yang,’ Nazo hizo mbili zinawakilisha nguvu mbili tofauti, au viwili tofauti vyenye kukinzana. Yin ana Yan zinachukuliwa kama, hasi na chanya. Yin inawakilisha umilele, kiza, kike, kushoto n.k. Yang ni kinyume, na inawakilisha historia, mwanga, kiume, kulia n.k. Yang ni kiume, chanya na inawakilishwa na jua. Yin ni kike, hasi na inawakilishwa na mwezi. Utaikuta nembo hizi kwenye dunia ya Mashariki zimejikita kwenye dini kama vile za Confucianism, Buddhim, na Taoism. Wakati kwenye dunia ya Magharibi utazikuta nembo hizi kwenye uchawi, mambo ya nyota, mazingaombwe na imani. Albert Pike anasema kuwa sakafu yenye rangi nyeupe na nyeusi, inawakilisha ubaya na wema kutokana na kanuni za wa Egypt na watu wa Persia. Ni ulingo wa mapambano baina ya malaika Michael na Shetani ...nuru na kiza, mchana na usiku ...
        Aina hii ya sakafu yenye rangi mbili maarufu kama Checkerd floor inasemekana asili yake hasa ni Egypt, ilitumika kuwakilisha makutano baina ya ‘nuru’ na ‘kiza,’ au makutano ya nguvu hasi na chanya. Freemason wanamsimika mwanachama wao juu ya chekered floor, na ibada kadhaa wazifanya juu ya sakafu ya aina hizi. Kiibada za kishetani sakafu ya aina hii inawakilisha dunia mbili tofauti, dunia yetu na dunia ya mashetani. Binadamu na majini tunaishi kwenye dimensional mbili tofauti, majini wanapo ingia kwenye dimensional yetu, yaani kwenye huu ulimwengu wetu wa three dimensional (3D) ndipo tunapo weza kuwaona wakiwa na sura za viumbe na vitu vilivyomo kwenye ulimwengu wa 3D, kwenye nukta ambayo hiyo dunia yao inapokutana na yetu, ndipo panapo patikana chekered floor, yaani kifaa cha kuzikutanisha dunia mbili.


MFANO HALISI WA HEKALU LA KIMASONIA, NA HIYO NDIYO SAKAFU YAKE NA KILA UNACHO KIONA HUMO HAKIJAWEKWA KWA BAHATI MBAYA, KINAYO MAANA YAKE HALISI NA ILIYO KAMILI.


        Kwenye filamu ya Matrix, Neo alipotaka kukutana na Mepheus, kwanza ilimbidi apite kwenye sakafu yenye chekerd floor, hii ikimaanisha kuwa Neo, amekatiza kutoka dimensional moja kwenda nyingine. Hivyo mahala ambapo nguvu mbili za hasi na chanya, au kiza na nuru zinapo kutana ndipo, sehemu mahususi kwa washirika wa mashetani kufanyiza makafara. Hivyo Chekered floor ni chombo cha usafiri ambacho kinamtoa muhusika kutoka kwenye dimensional moja kwenda nyingine.




Mwanamuziki Rihanah, kwenye vidio hii, amefanyia wimbo wake kwenye Checkered floor, usidhani hili limefanyika kwa bahati mbaya, nyimbo na vidio zao zinasimamiwa vilivyo kuhakikisha kinacho takiwa kuwemo kinapatikana, na kisicho takiwa kinatolewa. Lengo ni kutunywesha hizi nembo zao katika fikra na mitazamo yetu bila sisi kuzifahamu maana yake, na hata kama ni mbaya sisi tusijue ubaya wake ila tuzikubali.





 Wakati ulipo fika wa Briney Spear kutimuliwa, au kuondolewa kwenye zana zinazo tumiwa na Illuminanti dhidi ya Umma, na  Christina Agulera kuingizwa kwenye nafasi yake, zoezi hili la kumsimika lilifanyika hadharani kwa njia ya onesho lililorushwa moja kwa moja na luninga (Live) Mtizame Madonna msimikaji mwenyewe kavalia nyeusi, anayeingizwa na anaye tolewa wote wamevali a nyeupe, kwenye sakafu lilipo fanyikia onesho hilo, ilikuwa ni ya Chekerd floor, Madonna alishuka ngazi 13 za piramidi kuwafuata wadada hawa wawili, hadharani alimpatia Britney Goodby Kiss, na Crsitna Initiation Kiss, na kutoka hapo maisha ya Brtiney kwenye vyombo vya habari na kila kona yalifutika, na endapo yalionekana basi yaliwekwa kwenye mguso wa hasi, wakati kwa mwenzake aliyeingizwa mpaka leo bado anazidi kupaa. Lakini hakuna aliyefahamu kuwa onyesho hilo lilikuwa na ajenda mbali kabisa na burudani.

No comments:

Post a Comment