LEO WAPENDWA NINGEPENDA TUTIZAME
SAKAFU NDANI YA HALL LA KIMASONIA, NIMEPENDA KULIZUNGUMZIA HILI KWA VILE SAKAFU
HIYO HAIPO KWA BAHATI MBAYA NDANI YA MAHEKALU YA KIMASONIA, NA UTAZIKUTA KATIKA
KILA KONA YA HEKALU LA KIMASONIA KOKOTE DUNIANI, LAKINI MBAYA ZAIDI, ALAMA
ZENYE KUFANANA NA NAKSHI ZA SAKAFU HIYO TUMEKUWATUKIKUTANA NAZO NA KUZITUMIA
KWA NAMNA MBALIMBALI BILA KUJIULIZA ZIPO HAPO KWA MAANA NA SABABU GANI, SASA
LEO TUTAANGALIA MAANA HALISI YA SAKAFU HIZI .....
KARIBU TUWE SOTE
Mwanachama
wa kimasoni kwenye chekered floor. Katikati utaiona ile nyota, yenye ncha iliyo
elekea juu. Wakati mwingine huweka ile yenye ncha iliyo elekea chini kutegemea
na mahitaji na ibada husika.
SAKAFU YA VIBOKSI VYEUPE NA VYEUSI
Karibu alama na nembo zote za freemasonry ni kwa ajili ya kuleta uharibifu kwa
watu, katika mahekalu yote ya kimasoni utaona sakafu yenye rangi nyeupe na nyeusi,
mfano wa chombo cha kuchezea drafti, wanasema rangi hizo mbili zinamaanisha
mahusiano kati ya uovu na wema, na au nguvu mbili kinzani chanya na hasi.
Mfano wa hizi rangi mbili utaziona pia kwenye kile kinacho fahamika kama ‘Yin
na Yang,’ Nazo hizo mbili zinawakilisha nguvu mbili tofauti, au viwili tofauti
vyenye kukinzana. Yin ana Yan zinachukuliwa kama, hasi na chanya. Yin
inawakilisha umilele, kiza, kike, kushoto n.k. Yang ni kinyume, na inawakilisha
historia, mwanga, kiume, kulia n.k. Yang ni kiume, chanya na inawakilishwa na
jua. Yin ni kike, hasi na inawakilishwa na mwezi. Utaikuta nembo hizi kwenye
dunia ya Mashariki zimejikita kwenye dini kama vile za Confucianism, Buddhim,
na Taoism. Wakati kwenye dunia ya Magharibi utazikuta nembo hizi kwenye uchawi,
mambo ya nyota, mazingaombwe na imani. Albert Pike anasema kuwa sakafu yenye
rangi nyeupe na nyeusi, inawakilisha ubaya na wema kutokana na kanuni za wa
Egypt na watu wa Persia. Ni ulingo wa mapambano baina ya malaika Michael na
Shetani ...nuru na kiza, mchana na usiku ...
Aina hii ya sakafu yenye rangi mbili maarufu kama Checkerd floor inasemekana
asili yake hasa ni Egypt, ilitumika kuwakilisha makutano baina ya ‘nuru’ na
‘kiza,’ au makutano ya nguvu hasi na chanya. Freemason wanamsimika mwanachama
wao juu ya chekered floor, na ibada kadhaa wazifanya juu ya sakafu ya aina
hizi. Kiibada za kishetani sakafu ya aina hii inawakilisha dunia mbili tofauti,
dunia yetu na dunia ya mashetani. Binadamu na majini tunaishi kwenye
dimensional mbili tofauti, majini wanapo ingia kwenye dimensional yetu, yaani
kwenye huu ulimwengu wetu wa three dimensional (3D) ndipo tunapo weza kuwaona
wakiwa na sura za viumbe na vitu vilivyomo kwenye ulimwengu wa 3D, kwenye nukta
ambayo hiyo dunia yao inapokutana na yetu, ndipo panapo patikana chekered
floor, yaani kifaa cha kuzikutanisha dunia mbili.
MFANO
HALISI WA HEKALU LA KIMASONIA, NA HIYO NDIYO SAKAFU YAKE NA KILA UNACHO KIONA
HUMO HAKIJAWEKWA KWA BAHATI MBAYA, KINAYO MAANA YAKE HALISI NA ILIYO KAMILI.
Kwenye filamu ya Matrix, Neo alipotaka kukutana na Mepheus, kwanza ilimbidi
apite kwenye sakafu yenye chekerd floor, hii ikimaanisha kuwa Neo, amekatiza
kutoka dimensional moja kwenda nyingine. Hivyo mahala ambapo nguvu mbili za
hasi na chanya, au kiza na nuru zinapo kutana ndipo, sehemu mahususi kwa
washirika wa mashetani kufanyiza makafara. Hivyo Chekered floor ni chombo cha
usafiri ambacho kinamtoa muhusika kutoka kwenye dimensional moja kwenda
nyingine.
Mwanamuziki Rihanah, kwenye vidio
hii, amefanyia wimbo wake kwenye Checkered floor, usidhani hili limefanyika kwa
bahati mbaya, nyimbo na vidio zao zinasimamiwa vilivyo kuhakikisha kinacho
takiwa kuwemo kinapatikana, na kisicho takiwa kinatolewa. Lengo ni kutunywesha
hizi nembo zao katika fikra na mitazamo yetu bila sisi kuzifahamu maana yake,
na hata kama ni mbaya sisi tusijue ubaya wake ila tuzikubali.
Wakati ulipo fika wa Briney Spear kutimuliwa, au
kuondolewa kwenye zana zinazo tumiwa na Illuminanti dhidi ya Umma, na
Christina Agulera kuingizwa kwenye nafasi yake, zoezi hili la kumsimika
lilifanyika hadharani kwa njia ya onesho lililorushwa moja kwa moja na luninga
(Live) Mtizame Madonna msimikaji mwenyewe kavalia nyeusi, anayeingizwa na anaye
tolewa wote wamevali a nyeupe, kwenye sakafu lilipo fanyikia onesho hilo,
ilikuwa ni ya Chekerd floor, Madonna alishuka ngazi 13 za piramidi kuwafuata
wadada hawa wawili, hadharani alimpatia Britney Goodby Kiss, na Crsitna
Initiation Kiss, na kutoka hapo maisha ya Brtiney kwenye vyombo vya habari na
kila kona yalifutika, na endapo yalionekana basi yaliwekwa kwenye mguso wa
hasi, wakati kwa mwenzake aliyeingizwa mpaka leo bado anazidi kupaa. Lakini
hakuna aliyefahamu kuwa onyesho hilo lilikuwa na ajenda mbali kabisa na
burudani.
No comments:
Post a Comment