LEOTUTAZUNGUMZIA ALAMA NEMBO ZA
KIMASONIA, NA LEO TUTATIZAMA KWA UNDANI NAMBARI TISA (9), KISHA KUMI NA MOJA
(11), HALAFU MWENGE …
Kwa freemasonry lugha yao ipo
mahususi kwenye maumbo na alama mbalimbali lakini pia bila kusahau nambari,
umuhimu wa nambari kwa freemasonry na asasi nyingine za siri unakuja pale
ambapo elimu ya kale kabisa ilihifadhiwa katika nambari na kwa watu hawa
hisabati limekuwa ni somo muhimu mno,
“Elimu ya
kwanza duniani imekuja Kwa alama mbalimbali, hekima za watu wa Chaldean,
Phoenician, Egypty, Kaanani, wanafalsafa kama akina Zoroaster, Sanchoniathon,
Pherecydes, Syrus, Pythagoras, Socrates na Plato, vyote vya zamani vilivyokuja
katika mikono yetu, vimekuja kwa njia ya alama”
Nembo/Alama ni muhimu sana kwa
wamasonia na freemason wanajifunza maana mpya ya kila nembo, nambari kila
wapandapo daraja moja (degree), hivyo nembo moja au nambari inaweza kuwa na
maana zaidi ya moja na maana tofauti kwa masonia wa daraja tofauti, ni wale
freemasons walio katika daraja ya juu tuu ndiyo wanao jua maana halisi ya nembo
hizo na wengine hawajui kwani hao hawastahiki chochote ila kupotezwa.
Katizame ile Filamu ya Davinci
Code, Jina la Filam hii linatokana na jina Leonard da Vinci mtu huyu ambaye
huenda tukaja kuisoma hadithi yake huko mbele. Filamu iliyozua utata kwenye
Kanisa na kuzusha mkanganyiko, Freemason wenyewe ndiyo waliotengeneza Filam hii
na ina mengi kuelezea kuhusu freemason hasa kwa watu wanao wajua freemason
lakini kwa mtu wa kawaida anaweza kuona ni sinema ya kawaida yenye lengo ya
kulipaka matope Kanisa mbali na vitu kadhaa vilivyoelezea filamu hii pia
inaelezea jinsi gani nembo/ alama zilivyo na umuhimu kwa Freemason katafute
uitizame kama hujapata kuitizama.
Katika hili leo ningependa
kuitizama nambari hizi mbili, 9 na 11 maarufu kama ‘NINE, ELEVEN’ ingawa
sitazungumzia tukio muhimu katika historia yetu la minara miwili kule
Washington D.C. mpaka baadae kidogo.
Tuanze na nambari tisa (9)
Kutoka kwenye kitabu kilicho itwa A lexicon of
Freemasonry, kilichoandikwa na Freemason mkubwa na maarufu, Albert G
Mackey, MD, anasema,
“ ... kutoka kwa wafuasi wa Pyhagoras
ni kuwa namba tisa (9) inayo uwezo na nguvu ya kujizalisha yenyewe kwa
kuizidisha, ichukulie nambari hii mfano wa kitu chenye au kisicho na uhai,
ingawa umbile lake litakuwa ni lenye kubadilika, lakini kitu hicho hakitofutika
kamwe (sababu kinayo uwezo wa kujizalisha chenyewe.) Pia nambari hii inayo
maana aya ndani zaidi kwenye umbo la duara, ambalo kimahesabu umbile hili lina nyuzi
za digrii 360 ambayo ni sawa na kuchukua 3+6+0= 9 ..”
Maana yake ni nini hasa, hii
inatueleza kuwa freemasonry wanapo itzama nambari tisa (9) kwa ni kama
wanakitazama kitu ambacho hakiwezi kufutika, kumalizika, kufa au kuondolewa,
kitu ambacho daima kinajizalisha chenyewe. Hivyo kwa freemasonry nambari tisa
(9) ni alama ya umilele.
Apron hiyo hapo juu ya kimasonia
huvaliwa na mwana masonia mbaye ameingia daraja la tisa (9), hufungwa kiunoni,
mwanachama huyo hujulikana kama Memphis-Misraim, utaona kwenye Apron hiyo
kumechorwa ibada mahususi ya kimasonia, ‘ibada ya kuchinja mtu’
Tunapo ichambua Aproni hiyo
inayovaliwa na mfuasi wa kimasonia laiyefikia daraja la tisa (9), tunakutana na
hayo yafutayo,
Kwanza mkono ambao umeshika kisu ni
mkono wa kulia, ambao nao kwa freemasonry mkono wa kulia ni ‘mkono wa utii,’
‘mkono wa uaminifu,’ na pia ndiyo mkono unao tumika kuchukulia kiapo.
Jambia ambalo limeshikwa na mkono huo
kikawaida hushikwa na mtu maalum anayefahamika kama ‘Grand Sword Bear’ na
jambia lenyewe huitwa ‘Sword of the State’.
Kichwa nacho kwenye Aproni hiyo kinayo
maana yake mahususi, kichwa hicho kinamaanisha ‘utawala ambao upo’ yaani
utawala ambao siyo ule wa kimasonia, kwa vile siku zote vita vyao freemasonry
ni dhidi ya watu na serikali zao.
Kichwa kinapo katwa kama inavyo
oneshwa kwenye aproni hiyo, hushikiliwa kichwa hicho na kuacha damu itiririke
bila kizuizi na hapo ikimaanisha ‘maisha mapya’ au ‘utawala mpya’ au NEW WORLD
ORDER’ inakuja kuchukua nafasi ya kiuatawala.
Unakumbuka kile kilicho tokea Mei
29, 2004, raia mmoja wa Marekani na ambaye anayo asili ya ‘Uyahudi’ bwana
Nick Berg, alikamatwa na kuchinjwa ‘live’ na watu wanao jiita nia
‘magaidi.’ Vidio ya kuchinjwa kwake ilirushwa kwenye kila kituo kikubwa duniani
cha Luninga,
Kila kituo cha luninga duniani
kilionesha habari hii. Kama kawaida wauwaji walijitambulisha kuwa wao ni
kikundi cha kislam, ambacho kimekerwa nay ale wanayo yafanya Wamarekani na
majeshi yao kwenye aridhi ya Iraq.
Tukio hilo lilikuwa ni la aina
yake kwenye historia ya vyombo vya habari, kwani hakuna kabla ya hapo na baada
ya tukio hilo kulipatwa kuoneshwa tukio lenye maudhui ya kuogofya na kutisha
kama hayo kwenye mtandao wa luninga kwa kiasi kikubwa kama hicho.
SWALI: KWA NINI TUKIO HILO LILIONESHWA
NA KUONESHWA KWA KIWANGO HICHO KOTE DUNIANI?
Tukio hili lilioneshwa kwa sababu,
wakati walimwengu wasiyo jua chochote wakiendelea kuaminishwa kuwa waliyo fanya
hayo ni Waislam, na ndivyo kitabu chao kinawataka wafanye hivyo, upande
mwingine wa shilingi ni kuwa, huo ulikuwa ni ujumbe kwa fremasonry wa daraja la
juu, illuminanti na wengine wote wanao shiriki katika kufanikisha NWO.
Tukio hilo lilikuwa sawasawa na
ibada ya kimasonia ambayo inaonekana kwenye Aproni ya mfuasi aliyefikia daraja
la tisa (9)
Nick Berg alikatwa kichwa chake na
kwa kutumia kisu kilicho shikwa na mkono wa kulia wa muuaji wake.
Kishwa Muuwaji akakishika kichwa
cha Nick kwa mkono wa kushoto, akakining’niza kuachia damu itiririke kama
ilivyo kwenye Aproni ya kimasonia,
SITAWEKA PICHA HIYO YA NAMNA KICHWA
CHA NICK KILIVYO NING'INIZWA BAADA YA KUTENGENISHWA NA KIWILIWILI KWA SABABU ZA
KIMSINGI KABISA. HUWEZI KUONDOA UOVU KWA KUUONESHA KIVITENDO UOVU HUO, BALI
UTAKUWA UNAUSAMBAZA ZAIDI.
Muaaji akiwa amekining’iniza
kichwa cha Nick Berg kwa mkono wake wa kushoto baada ya kukikata kwa mkono wake
wa kulia. Hii ilikuwa ni picha mbaya sana kwenye historia ya luninga.
Ujumbe waliokuwa wanapewa watu
hao, kote duniani, katika majukumu na nafasi zao ni kuwa, muda umefika kwa wao KUONESHA UTII
WA KIAPO CHAO, UAMINIFU KWENYE NCHI ZAO, KWA KUING’OA UTAWALA ULIOPO SASA KOTE
DUANIANI, MA KUWEKA MAZINGIRA YA UJIO WA NWO.
Cha kuvutia zaidi ni kuwa, miaka
miwili baada ya tukio hilo, yaani baada ya ibada hiyo ya kimasonia iliyofanywa
‘LIVE’ kwenye mitandao yote ya Luninga duniani, ambalo lilikuwa ni ujumbe
mahususi kwa wafanyakazi wote wa NWO kokote walipo kuamka na kuanza kazi ya
kuandaa mazingira ya NWO, au kwa jina lingine kama wanavyoiita wao ‘NEW
INTERNAL KINGDOM,’ ambayo wanaamini kuwa huko wataishi milele au watapata uwezo
wa kuishi milele, kama ambavyo uwezo huo unavyo wakilishwa na nambari tisa (9).
Cha kuvutia ni kuwa Mwanamasonia mmoja ambaye mpaka sasa inasemekana yupo
kwenye daraja la tatu (3) kwenye mtandao huo, daraja la wale
wanao faa kudanganywa, au maarufu kama Blue Degree, mimi
huwaita ni mauwa kwenye ukuta wa kimasonia, mwanachama huyo hakuwa mwingine bali
mwanamuziki maarufu wa Hip Hop JAY-Z.
Unajua Jay Z, alifanya nini?
Jay Z, alikuja na albamu yenye
jina la ‘KINGDOM COME’, hii inavutia sana, sababu ujumbe
ulikuwa unapatikana kwenye ibada ile ya kimasonia iliyofanywa ‘LIVE’ kote
duniani, ni kuwataka wanachama, vibaraka na wafanyakazi wa NWO, kuonesha utiifu
wa kiapo chao, uaminifu kwa kuzivuruga na kuzimaliza serikali zilizopo sasa, na
kuweka mazingira ya ujio wa ‘NEW INTERNAL KINGDOM’ halafu miaka miwili tu baada
ya tukio, mwanamasonia huyo akaja na albamu yake inayo kwenda na jina ambalo
moja kwa moja linawiana na matakwa, au amri ambayo ilitolewa na wauwaji wale wa
kimasonia miaka miwili kabla.
Kwa hiyo
nambari tisa (9) ni moja ya namba zenye nguvu sana kwa freemasonry,
halikadhalika nambari ambayo inagawanyika kwayo yaani nambari tatu (3).
Nambari
hii tisa (9) kama tulivyoona ni namba inayo ashiria hali ya ‘UMILELE’ kwa
chochote kile chenye kuhusishwa nacho, na hapa tumeona kati ya vitu ambavyo
jamaa hawa wanavihusisha na umilele ni ‘NEW INTERANAL
KINGDOM’ au ‘NEW WORLD ORDER’ ambayo
wanaifanyia kazi na ambayo waliombwa rasmi kupitia kwenye luninga kuandaa
mazingira ya KINGDOM hiyo KWA IBADA YA KIMASONIA ILIYO FANYWA
LIVE KWENYE LUNINGA, IBADA AMBAYO ILIFAHAMIKA KWA WANAMASONIA ZAIDI, TENA
MASONIA WA DARAJA LA JUU KUANZI 30 NA KUENDELEA.
TUMEONA
MMOJA WA WANACHAMA WALIYO UFANYIA KAZI UJUMBE HUO KWA NAFASI NA KAZI YAKE NI
MSANII JAY-Z ALIPOKUJA NA ALABAMU MIAKA MIWILI BAADA YA TUKIO, ALBAMU AMBAYO
KIMAJABU AJABU, IMEBEBA JINA SAWIA NA UJUMBE ULIOTOLEWA NA WAUWAJI WA NICK
‘KINGDOM COME’
JAY-Z NI
MFUASI WA DARAJA LA CHINI ASINGEWEZA KUELEWA MAANA HALISI YA IBADA ILE YA
KIMASONIA, LAKINI KIKAWIDA WATU KAMA JAY-Z NA WENZAKE VILE WANAVYO VIFANYA,
KAMA WALIVYO FANYA WAUWAJI WALE HUWA NI AMRI AU MAELEKEZO KUTOKA JUU, AU KUTOKA
KWA YULE AMBAYE ANASIMAMIA SHUGHULI ZAO, AMBAO WAO WANAKUWA NA PICHA KUBWA YA
NINI KINAENDELEA.
Katika ulimwengu wa kishirikina na ulimwengu wa kimasonia
nambari kumi na moja (11) inafahamika kama nambari kuu ya kishetani, katika
kazi yetu hii ya leo, tutaitizama nambari kumi na moja na kazi yake kwenye
tukio la kupigwa kwa minara miwili ya WTC.
Nambari 11, kwenye duara la wenye kufuata elimu ya kishetani
inafahamika pia kama zawadi na urithi kutoka kwa yule anayefahamika kama ‘LIGHT
BEARER’ au ‘MBEBA NURU’, hili
ni jina kabisa lililotafsiriwa kutoka kwenye lugha ya Kiyahudi, unajua
kwenye Kiyahudi LIGHT BEARER NI NANI?
LIGHT BEARER NI LUCIFER
Lakini pia unapotizama duara la vikundi vya nyota 12, maarufu
kama Zodiac, kikundi cha 11 kwenye
duara hilo kinafahamika kama AQUARIUS, na
kipindi tulicho nacho sasa utakuwa umeshasikia na utaendelea kusikia mengi
kuhusiana na kiile kinacho fahamika kama ‘NEW AGE’ au zama mpya, hii
ni kwa vile freemasonry na wale wote wenye kufuata mila za kishetani kutoka
Babiloni wanaamini kuwa tupo kiuhakika katika zama za AQUARIUS, tupo
kwenye ZAMA MPYA, zama za kumpokea Masih,
Masih wa zama mpya, masih wa NWO.
JE UNAMJUA MASIH WA NWO?
NAJUA UTAULIZA HILO SWALI!
SI MWINGINE BALI NI DAJJAL, PIA ANAJULIKANA KAMA ANTI-CHRIST, AU
MPINGA KRISTO.
Lakini kile ambacho wengi wanashindwa kukifahamu au wanasema
kile ambacho hawakifahamu ni kuwa MASIH-DAJJAL AU ANTI-CHRIST SIYO SAWA TUNAVYO
TAFSIRI MAJINA YAKE HAYO AMBAYO YAMEKUJA KUTOKANA NA SIFA ZA MAUMBILE NA TABIA
ZAKE. KABISA, KABISA NAFASI YAKE NA SHUGHULI ANAZO TARAJIWA KUZIFANYA
HAZIMUWEKI KWENYE CHEO CHA KUMPINGA KRISTO (ISSA MWANA WA MARIAM), HAPANA NA
HII NDIYO HASA MAANA YA NAMBARI 11.
MAANA YAKE NI IPI?
MAANA YAKE NI KUWA, NAMBARI 11, INASIMAMA KAMA ALAMA YA MFANANO,
UWILI, KINZANI AU NGUVU MBILI ZENYE UWIANO ULIO SAWA LAKINI ZINAZO KWENDA NJIA
MBILI TOFAUTI, YAANI NYEUPE NA NYEUSI, MCHANA NA USIKU, KIZURI NA KIBAYA N.K.
HIVYO BASI TUNAPO SEMA TUPO KWENYE ZAMA AMBAZO ILLUMINANTI
WANAMTEGEMEA KRISTO WAO KUWA YUPO NJIANI, DAKIKA YEYOTE ATAINGIA KWENYE
ULIMWENGU WETU HUU WA 3D, ZAMA AMBAZO KWENYE DUARA LA ZOADIC ZINAWAKILISHWA NA
ALAMA YA AU KIKUNDI CHA NYOTA CHA AQUARIUS, ZAMA AMBAZO NAFASI YAKE NI NAMBARI
11, ZAMA ZA DAJJAL, HAIMAANISHI KUWA DAJJAL
NAFASI ATAKAYO KUJA KUICHUKUA NI KUMPINGA ISSA MWANA WA MARIAM, HAPANA LAKINI
ATAKUJA KUJIFANANISHA NA ISSA MWANA WA MARIAM.
Na hii utaona katika kazi ambazo Dajjal atakuja kuzifanya ni
kuwarubuni watu kuwa yeye ni Kristo, na hatofanya chochote kumpinga, ila Kristo
mwenyewe, Issa mwana wa Mariam ndiye atakaye kuja kumpinga na hatimaye kumuuwa
Dajjal. Hivyo Dajjal atakapo kuja, kama ilivyo nambari kumi na moja, atakuja
kujifananisha na Kristo. Kama ambayo maana nambari kumi na moja inavyo tumika
kumfananisha Shetani na Mungu Mmoja, na kumpa Shetani nguvu na mamlaka sawa na
yale ya Mungu Mmoja.
Katika kitabu cha Isaya tunakutana na maneno haya,
“Nawe ulisema moyoni mwako (Lucifer), nitapanda mpaka mbinguni,
nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; nami nita keti juu ya mlima
wa mkutano, katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vua
mawingu. NITAFANANA NA YEYE ALIYE JUU.” Isaya
14:13
Umemsikia Lucifre baada ya kushushwa kutoka mbinguni kile alicho
kisema, kwamba ANATAKA KUFANANA NA YEYE ALIYE JUU, tunafahamua aliye juu ni
ninani, ni MUNGU MMOJA, hivyo Lucifer anataka kujifanannisha na MUNGU MMOJA,
kama Dajjal anavyo taka kujifananisha na Masih mwana wa Mariam, na hii ndiyo
maana hasa ya nambari 11.
Hivyo basi unapo chukua nambari 9 ukaiweka pamoja na nambari 11,
kwenye ulimwengu wa kishetani unapata zaidi ya nambari zilizo pangwa. Kama
tulivyo ona nambari 9 kazi yake ni, au maana yake halisi ni kuharibu, utawala
uliuopo, mfumo uliopo kwa kukisimamia kiapo cha kimasonia, na wakati huo huo,
nambari 11, ikiwa na maana ya kusimamisha utawala mpya, utawala ambao utakuwa
sawa na utawala wa Mungu Mmoja, lakini huu ni wa kishetani.
Hivyo kuangushwa kwa
minara ile miwili, hii ilikuwa ni ujumbe kuwa tumeshaibomoa, au tumeshauvunja
utawala wa Mungu Mmoja na sasa tunasimamisha Utawala wa Lucifer, na tangu baada
ya tukio lile tumeona dunia imegeuka kuwa mbaya mara dufu, serikali moja baada
ya nyingine zinapinduliwa kutengeneza njia ya ujio wa serikali moja duniani
kote, serikali ya Illuminanti, serikali ya Dajjal.
MPENDWA MSOMAJI NISINGEPENDA UAMINI HAYA NINAYO YAANDIKA HUMU,
LAKINI NATAKA UYAELEWE ... KWA AJILI HIYO BASI HAPA CHINI NITAWEKA KWA UPANA
ZAIDI NAMBARI 11 na maana yake HALISI YA KUTUMKA KATIKA KUFANIKISHA TUKIO LA WTC...
Kilicho tokea 9/11 ilikuwa ni moja ya ibada kuu kuliko za kishetani....
moja ya ibada muhimu kuliko kutiririsha nguvu za kiza kwenye uso wa dunia....
Kwa kawaida nembo au alama fulani huwa ni mbadala au kiwakilishi
cha kitu fulani, hivyo navyo nembo za kimasonia popote zinapo kuwepo, huwepo
kama mbadala wa kile kilicho kusudiwa, mathalani katika kila hekalu la
kimasonia panakuwepo na nguzo mbili zimesimama, nguzo hizo wanasema
zinawakilisha nguzo zinazo patikana ndani ya hekalu la Mfalme Solomoni
(Freemasonry ni wazushi na waongo na wamemzushia mtume huyu wa Mungu Mmoja
kwamba alikuwa ni mchawi na mshirikina na kwamba alikuwa ni freemason).
Hivyo basi nguzo hizo mbili kwa namna mbalimbali kote duniani
zimekuwa zikisimamishwa kwa njia mbalimbali, na katika miji ya kisasa hutakosa
aina hii ya majengo ambayo huwakilishwa na majengo pacha, na minara miwili ya
WTC, ni mfano mzuri wa nguzo hizo mbili ambazo freemason wanaziitikadia. Lakini
pia kwa upande mwingine nguzo hizo mbili huhesabiwa kama tatu, na hii ni kwa
uwiano wa Piramidi tatu zinazo patika kwenye uwanda wa Gaza, Egypty. Unapo
jumlisha uwazi uliopo baina ya nguzo mbili hizo, basi huhesabiwa kama ni nguzo
tatu.
Kama tutarudi kwenye asili hasa ya nguzo hizo mbili, ambako ni
Egypty, ni kwamba Piramidi zile moja ya kazi yake kubwa ni kufungua kile
kinacho fahamika kama ‘STAR GATE’
STAR GATE, ni njia ya kuelekea kwenye uwanda mwingine wa kimaumbile,
sisi tupo kwenye uwanda wa 3D. Lakini pia ni mlango wa kuelekea kwenye kile
kinacho fahamika kama ‘Higher Counseousness’
Hivyo basi kuangushwa kwa minara ile miwili pia tunaweza kusema
ni alama ya kufunguliwa kwa Star Gate.
Jua hukamilisha mzunguko wake baada ya miaka 11, hata hivyo
mzunguko wa mwisho wa jua ulikadiriwa utatokea baina ya mwaka 1989 au 1990.
Halafu mzunguko utakao fuata utakuwa ni mwaka 2000 au 2001.
Mwaka 1990, katika bunge la Marekani, raisi wa kipindi hichi,
Bush Sr. Alitoa hotuba maarufu, hotuba ambaye iliashiria kutangazwa kwa
mchakato wa kuelekea kwenye New World Order, hutuba hiyo ilikuwa ni tarehe
9.11.1990, baadhi ya vitu alivyo sema kwenye kauli hiyo ni “... what
it takes ? It’s more than a small country, it’s a big idea, a NEW WORLD ORDER ...”
Halafu baada ya miaka 11 kamili, au baada ya jua kukamilisha
mzunguko wake, ibada kubwa ya kishetani ikafanyika kufungua milango kuelekea
kwenye NEW WORLD ORDER. Ikafanyika tarehe 9.11.2001
Unamkumbuka babu yake na Bush Jr, au Baba yake na Bush Sr,
ambaye aliandika kitabu cha kishetani alicho kiita ‘Book of Law’ wakati
alipokuwa ndani ya Piramid la Gaza, hiyo ilikuwa ni mwaka 1904 baada ya kufanya
meditation ndani ya King Chember, kwenye Piramid la Gaza, alipokea ufunuo wa kitabu
hicho, huyu ni Aleister Crowley,
Au pia alifahamika kama 666, alisema kuwa aliwasiliana akiwa
hapo na kiumbe kinacho fahamika kama Oz, kwenye kazi zake pia alitumia alama hii...
Moja ya maana inayo patikana kwenye nambari hii Ni sawa na nambari
777 na pia kuwa na mahusiano na mungu anaye fahamika kama PAN.
Aleister Crowley akachora aina hichi cha kiumbe chenye
maarifa lakini kisicho kuwa binadamu ambacho alikiri kukiona wakati akifanya
ibada zake humo.
Sasa turudi kwenye 9/11
Kabla tukio lile halijatokea, au kabla ibada ile ya kishetani
haijaanza, mjukuu wa Aleister Crowley alikuwa kwenye shule ya watoto na
alikuwa akiwasomea hadithi...
... Unafahamu ni hadithi gani Bush alikuwa akiisoma, kabla ya
kufanyika kwa ibada kuu ya kishetani, ibada ambayo itaadhimisha miaka 11 ya
mzunguko wa jua, ibada ambayo itafungua milango ya NEW WORLD
ORDER, Ibada ambayo itafungua mlango wenye nguvu za giza katika uso wa
dunia ... unajua ni hadithi gani Bush Jr, alikuwa akiisoma?
Kwa vile ushahidi upo wa kutosha kwamba si kwamba tu Bush
alifahamu juu ya tukio hilo, lakini zaidi ni kwamba yeye na utawala wake
walishiriki kikamilifu kuhakikisha hilo linatokea kama lilivyo pangwa, na zaidi
ya yote kwake yeye na familia yake, na Illuminanti wengine tukio lile lilikuwa
ni ibada maalum ya kufungua milango hiyo niliyo itaja hapo juu, Je katika
wakati muhimu kama huo unadhani Bush alikuwa akisoma hadithi gani kwa watoto wale...?
Alikuwa anasoma kitabu kinachoitwa ‘MY PET
GOAT’, Kitabu hichi kilisha pigwa marufuku kutokana na maudhui yake
ya kishetani na ibada za kishetani zinazo tajwa humo kama zawadi kwa mungu
anayefahamika kama PAN.
Utamkumbuka mungu huyu PAN ndiye
aliyempatia Aleister Crowley babu
yake na Bush ufunuo wa kuandika kitabu cha kishetani kinacho kwenda kwa jina la
‘BOOK OF LAW’, na mungu huyu huchorwa au kuoneshwa katika maumbile mbalimbali
lakini akiwa na KICHWA CHA MBUZI, hivyo
kichwa cha mbuzi pia hufahamika kama ‘GOAT OF
MEANDEZ’ na huwakilishwa na picha au mchoro wa nyota yenye
ncha TANO lakini iliyo elekezwa chini, nacho hufahamika kama ni kichwa
cha SHETANI.
Hivyo basi wakati na kabla ibada hiyo kuu ya kishetani
haijaanza, Bush Jr, alishatia ‘Tabaruk’ ya tuko hilo kwa kuanza kuwasomea
watoto hadithi za MBUZI,
ambazo ni zawadi kwa mungu PAN, kwa
maneno mengine Bush Jr, aliaanza kumtukuza mungu PAN, au
shetani mwenyewe, hadharani, mbele ya vyombo vya habari, mbele ya watoto
wadogo, mungu PAN, na kuzitaka baraka zake
kabla ya tukio lenyewe kuanza.
Huwezi kuamini, nami sitaki uamini, ILA uelewe, kwamba katika
vitabu vyote vya watoto vilivyopo kwenye uso wa dunia, Bush hakuona kitabu bora
zaidi cha kuwasomea watoto asubuhi ile, isipokuwa kitabu ambacho ni zawadi kwa
mungu PAN, mungu aliyempatia Babu yake na Bush ufunuo
wa kuandika kitabu cha kishetani.
Maneno yaliyopo kwenye kitabu hicho, ndiyo maneno ambayo darasa
zima lilikuwa likiyatamka, wakiongozwa na Bush mwenyewe wakati tukio hilo, au
wakati ibada hiyo kuu ikichukua nafasi yake. Unaweza kuona ni namna gani maadui
zetu walivyo jipanga, ni namna gani walivyo makini katika kutekeleza ibada kwa
miungu yao, tukio kubwa kabisa la kufungua milango ya kiza linafanyika, na
mungu mwenye dhamana hiyo, au shetani mwenyewe anaombwa, tena na watoto,
walimu, na kiongozi wa taifa kubwa duniani, mbele ya kamera, kuikubali na
kuipokea ibada hiyo ‘takatifu.’
BUSH, AKILIONGOZA DARASA
KUMTUKUZA PAN, MUDA MCHACHE KABLA YA 9/11
Freemasonry na wafuasi wengine wa aina hii ya ibada hupendelea
kuzigeuza alama zao kinyume nyume, au juu chini, na chini juu, hii ni desturi
ya kishetani, na Bush hakuwa amelisahau hili, pia, hasa kwenye tukio muhimu na
ibada ‘takatifu’ kama hiyo, desturi hii ya kishetani haikurukwa ... Bush
alikuwa akikisoma kitabu kile CHINI JUU, JUU CHINI.
UMEONA HAPA BUSH ANAKISOMA
KITABU JUU CHINI NA CHINI JUU, MILA NI MUHIMU SANA KWA HAWA JAMAA ...
Utakumbuka moja ya vitu ambavyo tulivitaja huko nyuma kuwa
vinawakilishwa na ile minara miwili ni NGUZO MBILI KWENYE HEKALU LA ‘SULEIMAN’
au KWENYE HEKALU LA KIMASONIA,
Minara hiyo miwili pamoja na sehemu ya kuingilia ndani ya hekalu
la ‘suleiman’ ilifahamika kama ‘THE GATE’ kwenye lugha yetu tungeita ‘MLANGO’
DUBAI YA LEO HIYO
Ila utajiuliza swali moja, mbona ni kanuni hiyo hiyo ya ujenzi
wa minara miwili mirefu utaikuta kwenye kila kona ya majengo katika miji yetu
ya kisasa?
Lakini unafahamu wanaiita jina gani, wanapo jumuisha minara hiyo
na sehemu yake ya kuingilia?
Wanaiita jina lilelile walilo kuwa wakilitaja huko Egypty kwenye
dunia ya kale, ‘THE GATE’
Kama minara ile miwili ilikuwa ni MLANGO, basi ulikuwa ni mlango
wa kwenda wapi?, Sote tunajua unapovunja mlango basi unapita au kitapita kile
kilicho kusudiwa kupita au kilicho kuwa kikizuiliwa kisipite kwenye MALANGO
huo.
Unakumbuka ni eneo gani lingine liligongwa na ndege zile?
Sehemu nyingine iliyogongwa ilikuwa ni PENTAGON.
Pentagon nayo umbo lake ni mfano wa nyota, lakini siyo nyota ya
kawaida, bali nyota inayo itikadiwa kuwa ni nyota ya KISHETANI, Nyota yenye
ncha tano, nyota ya kichwa cha mbuzi.
Ibada hii ililenga kufungua kile kinacho fahamika kama STAR
GATE, Kwa madhumuni ya kufungua chaneli za kiza katika uso wa dunia zitakazo
wawezesha ILLUMINANTI kusimamisha NEW WORLD ORDER, kwa vile kadiri kunapo
kuwepo na nguvu za kiza nyingi ndipo na nguvu za hawa jamaa zinapo zidi juu
yetu, na sote tumeshuhudia ni damu kiasi gani imemwagika na inaendelea
kumwagika baada ya tukio lile, ni uharibifu kiasi gani umefanyika na unaendelea
kufanyika kwa jina la tukio lile, ni vifo kiasi gani vimetokea na vinaendelea
kutokea kutokana na tukio lile, ni vilema wangapi wanazaliwa na wataendelea
kuzaliwa kutokana na tukio lile na ... na ... na ...
Ninacho kieleza hapa kwa mnasaba wa 9.11, ni kuwa
pale ambapo unapo taka kuwatambua maadui zetu, kuwatambua viumbe wanao
shirikiana nao, viumbe kutoka kwenye uwanda mwingine, viumbe kutoka kwenye
dimensional tofauti na hii ya kwetu, yaani unapo shughulika na majini au
mashetani. Unapo taka kuwafahamu Illuminanti au watu ambao wanayo aina fulani
ya elimu na maarifa ambayo kwa wengine hawana ...
Jamaa hawa wamechagua lugha nyingine tofauti kabisa na lugha
inayo fahamika kote ulimwenguni, lakini ni lugha ambayo ni wachache sana
wanaifahamu, lugha ambayo imevuka mipaka, mataifa na makabila, lugha ya nambari
na maumbo.
Utakuta wanafanyia kazi aina hii ya elimu ambayo utaisikia
wakiita SECRET NUMEROLOGY na SECRET GEOMETRY.
Hii inamaanisha nini basi, hii inamaanisha kuwa kila nambari,
inayo maana yake maalum iliyo pewa, kila umbo limepewa maana yake maalum, maana
ambayo inawasilishwa au inakuwa ndiyo ujumbe au mawasiliano ambayo yanapatikana
pale ambapo nambari au umbo linapo wekwa, andikwa au kuchorwa.
Hivyo basi katika maana hizo, tunakuta kuwa nambari 10, ni
ALFA na OMEGA, au Mungu, na nambari 11, ni
hatua au sehemu iliyopo juu ya Mungu, au 101 ni
juu ya Mungu.
Hivyo basi unapo toka kwenye 9 na
kurukia kwenye 11 bila kwenda
kwenye 10, ni sawa kwenye
lugha hii na kumruka Mungu, umetoka kwenye 9 na
hukwenda kwenye 10, bali umekwenda
kwenye 11, yaani umemruka Mungu na kwenda kwa yule
ambaye eidha anajifananisha na Mungu au anajinasibisha au wewe unamnasibisha
kuwa yeye yupo juu ya Mungu.
Hapa tunasema unamjaribu Mungu, unampa Mungu changamoto, ndicho
wanacho kifanya katika lugha hii. Hivyo tukio la 9.11 lililotokea
kwenye 9.11 yenyewe lilikuwa ni
jaribio kwa Mungu na kwa wale wanao muamini Mungu ... na historia inathibitisha
hii haikuwa mara ya kwanza kumjaribu Mungu ...
Ukiwa unafahamu nini maana hasa ya 9.11,
jiulize kwanini nambari ya dharura, nambari ya kutaka msaada kwa baadhi ya nchi
ni 911?
Yaani unapo taka msaada, unapokuwa kwenye wakati wa shida
usielekee kwa mwingine ila kwa yule ambaye wao wana muitikadia kuwa yupo juu ya
Mungu ...
Ukiwa na shida elekea kwa Shetani na utasaidiwa, hii ndiyo maana
ya kupiga 911 wakati wa dharura.
ASANTE SANA KWA POST ZAKO!
ReplyDeleteNIMEKUA NIKIFUATILIA MAMBO MENGI SANA JUU YA HAWA MABWANA!TOKA 2012!
PIA UMENISAIDIA KUPATA VIPYA THAT I DIDNT GET BEFORE!
SASA NAWEZA PATA SABABU YA MICROSOFT WINDOWS KURUKA *WINDOWS 9* BADALA YAKE WINDOWS 10