Umewahi
kuitizama filamu iliyokwenda kwa jina la ‘Sugar Hill’, ni filamu ya siku
nyingi, na naweza kusema moja ya filamu za mwanzo kuchezwa na Wesley Snipes,
nimeitaja filamu hii kwa vile maudhui yake kwa namna fulani yanataka kuwiana na
posti yetu ya leo.
Katika
filamu hii familia ya ‘Skuggs’ ambayo ndiyo familia anayo toka Wesley Snipes,
imeathirika na dawa za kulevyea, kutoka Baba, Mama na baadaye watoto na hasa
kaka yake na Snipes.
Snipes
na ndugu yake walishuhudia mama yao akifa mbele ya macho yao baada ya kuzidisha
dozi ya dawa za kulevyea, badaye baba yake alipata ulemavu kutoka kwa wauza baada
ya kushindwa kulipa fedha alizokuwa akidaiwa, ulemavu huo ambao nusura uondoke
na maisha yake, lakini hata hivyo bado ni dawa za kulevyea ndizo zilizo kuja
kumua baba yao.
Ingawa
familia hii ya Skugg haikuwaandaa watoto wao wasiingie kwenye njia iliyo
wazamisha wao, lakini yalikuwa ni maombi, matumaini na tamaa yao kuona watoto
hao watasimama kwenye njia tofauti na ile waliyopita wazazi wao.
Lakini
hadithi ilikuwa ni tofauti kabisa...
Familia
hii ya Skugg, kwenye filamu hii ya Sugar Hilll, haina tofauti sana na hadithi
ya wapigania uhuru wa Afrika na wale walio zirithi nchi hizi baada ya uhuru.
Katika
Sugar Hill wazee wake na Snipes hawakuwaachia wanawe mwongozo wasiingie kwenye
dawa za kulevyea ingawa ilikuwa ni HAMU yao kuona HAWAINGII huko. Wakati Babu
zetu wanatukabidhi nchi zetu baada ya uhuru, ilikuwa ni HAMU yao kuona kuwa
watoto tulio zapokea nchi hizo KAMWE HATUTO ZIRUDISHA KWENYE MIKONO YA
WAKOLONI.’
Lakini
kama ilivyokuwa kwenye Sugar Hill, hadithi ya bara hili nayo ikawa ni tofauti
kabisa ...
Wakati
Snipes amekuwa mtu mzima na anajitambua, alimkumbuka mama yake siku moja, na
akasema maneno haya akiwa kwenye kaburi la mama yake ...
Dear
mother, seems like eternity since you have bee gone. So much has happened. So
many dreams turn into nightmares. You always wanted the best for me. But I
guess it wasn’t meant to be that way. The Sugar Hill where you always wanted us
to live, is now a memory, a burned out jungle, a ghost of a better days, like
my father- lost out of reach. And the Boy you loved has become the man you
feared, getting rich of the same poison that killed you and destroyed my
father. Partner with the same men that stripped away our family dignity. Uneasy
partners, tied together by time, fear, and greed ...
Maneno
hayo,
Maneno
hayo, yatizame tena, nadhani ni maneno ambayo tunaposimama kuwakumbuka wale
ambao walipoteza mali, familia na uhai kupigania uhuru wa mataifa yetu, kama
basi hatutaweza kuyatamka maneno hayo kwa haya tulizo nazo, basi tuyakiri
mioyoni mwetu, kwamba tumewasaliti.
Kwamba
zile ndoto za uhuru zimegeuka na kuwa jinamizi, kwamba tumegeuka na kuwa watu
ambao wao waliwaogopa, tunajitajirisha kwa kile ambacho kilicho wauwa wao na
kuzichana familia zetu, tunashirikiana na watu ambao walizivua heshima nchi
zetu, katika ushirika mgumu unao lindwa na muda, hofu na tamaa ...
Hivyo
ndivyo Afrika yetu ilivyo leo, hatukukabidhiwa uhuru, kwa maana ya uhuru
uliopiganiwa na wazee wetu ...
Kwenye
hili nataka tuitizame Afrika ya kati halafu ni kuache na maswali ya nini hatma
ya Afrika Mashariki.
Utakuwa
umelala usingizi wa pono kama bado unaamini au unafikiri kuwa kile kilicho
tokea Rwanda ni kwa sababu ya ‘Ukabila’ kati ya Wahutu na Watusi, kama ambavyo
vyombo vya habari vya kimagharibi na vile vya kwetu vya ku-copy n paste vilivyo
ripoti.
Ingawa
kweli kuliwa na chuki za kibaguzi baina ya Wahutu na Watusi, tena chuki ambazo
zilitengeneza makusudi na wakoloni katika kipindi cha ukoloni, lakini hiyo
haikuwa sababu kuu iliyopelekea ndani ya siku 100, watu takribani 1000000
wapoteza uhai, na dunia nzima ikitizama kama vile wanao uana si binadamu.
Mikono
na sura ambazo zilikuwa hazionekani, lakini zilizo kuwa zikishughulika kwa
kiasi kikubwa kufanikisha mauaji hayo ni IMF na World Bank.
Vyombo vya magharibi katika kuelezea mauaji haya vilitumia misamiati kama vile “countries
in transition,” “A painful stage in their evolution from one party state
towards democracy and the free market”
Wakati
vikisema hayo ‘havikukumbuka’ kuuambia ulimwengu kuwa ni mpango na sera mpya za
kilimo chini ya IMF na World Bank ambazo ziliwapelekea wakazi wa maeneo hayo kupotelea
kwenye kiza cha umasikini.
Kuharibika
kwa hali ya uchumi ambako, nako kulipelekea kuanguka kwa soko la kimataifa la
kahawa, na kile kilicho fahamika kama ‘macro-economic reforms’ kutoka kwa
Bretton Woods, kiliongeza msuguano baina wa kitabaka.
Utaratibu
ulio wekwa na ‘International Coffee Agreement’ (ICA) kufahamika kama ‘quotas’
ulianza kuparanganyika. Wanunuzi wa kahawa ya Burundi, ambao waliinunua kwa bei
‘maalum’ waliyo taka wao hawakuwa wakilipa fedha zao kwa wakati, halafu soko la
kahawa kimataifa likaporomoka kabisa na bei yake kushuka.
JINAMIZI
LA UKOLONI
Kwanza
ikumbukwe kabisa kuwa, chuki za baina ya Watusi na Wahutu ni matokeo ya mbegu
ya mgawanyiko iliyo pandwa na wakoloni kwa faida na maslahi yao.
Utawala
wa wa Belgiam wakati wameikalia nchi hiyo, ndiyo hasa ulio zaa chuki hiyo ya
kikabila. Machifu walio teuliwa na wakoloni hao, walipewa mamlaka ya
kuwalazimisha wananchi wao kufanya kazi za mkoloni kwa lazima, walipewa mamlaka
ya kuwapiga na kuwanyanyasa wale ambao waligoma, kwa vile machifu walikuwa
wakitoka kwenye kabila moja, hii ilitengeneza mazingira ya kuonewa kwa kabila
jingine. Lakini hicho ndicho mkoloni alikitaka ili aweze kuvunja ule umoja wao
wa kitaifa walio kuwa nao hapo kabla.
Mpaka
hapo mkoloni hakuonekana kama ndiye adui wa Wanyarwanda, bali Mnyarwanda
alimuona mwenzae ni adui kwa misingi ya kikabila. Katika kipindi hichi, Watusi
ambao walikuwa ni wachache, ndiyo walio pewa mamlaka dhidi ya Wahutu walio
wengi.
Mkoloni
huyo akatengeneza vitambulisho, ambapo vilikuwa vikimtambulisha ‘HUYU NI MTUSI’
na ‘HUYU NI MHUTU’ Lakini zaidi ya hapo vitambulisho hivyo vikisema kuwa ‘Mtusi
ni mfugaji’ na ‘Mhutu ni Mkulima.’ Katika kuongeza mgawanyiko huo, mkoloni
alijenga shule ambazo walisomeshwa watoto wa machifu tu.
Utaratibu
huu wa kikoloni wa kuwasomesha watoto wa machifu, au watoto wa tabaka aua
kabila fulani, ulikuwa ni kote kwa sehemu zote wakoloni hawa walipokuwepo. Na
hao watoto wa machifu walio someshwa, kama vile zilivyo kuwa, shughuli
mbalimbali za mkoloni, kuwa ni kwa faida yao na nchi zao, na hata watoto hawa
wa machifu walikuwa wakipatiwa elimu mahususi kwa ajili ya shughuli mbalimbali
kwa manufaa ya wakoloni hapo baadaye.
Lakini
kubwa zaidi, WAKOLONI WALIKUWA WAKIWATENGENEZA WATU WATAKAO WAACHIA NCHI WAO
WATAKAPO ONDOKA, WATU HAO AMBAO WATAONEKANA NI WAAFRIKA WENZETU, LAKINI FIKRA
NA MITAZAMO YAO ITAKUWA NI ILE YA KIKOLONI.
HII NDIYO
MAANA NASEMA KUWA ‘AFRIKA HAIJAPATA UHURU WAKE BADO KUTOKA KWA MKOLONI.’ SABABU
NI WATOTO WA MACHIFU WALIOANDALIWA NA MKOLONI NDIYO WALIOPEWA NCHI.
PIA
UTAONA WAPIGANIA UHURU WENGI HAWAKUTOKA KWENYE LILE TABAKA AMBALO LILIKUWA NI ‘TABAKA’
TEULE LA MKOLONI, MFANO MZURI NI HISTORIA YA KUPIGANI UHURU WA TANZANIA ILIYO
POTOSHWA.
WATOTO
HAWA WA MACHIFU BAADA Y KUIPOKEA NCHI KUTOKA KWA WAKOLONI, WAKAIENDESHA KWA
KUFUATA NJIA, NA MIPANGO NA MIKAKATI ILEILE YA MKOLONI, NA HATA HALI ILIZIDI
KUWA MBAYA KATIKA KIPINDI HICHI CHA MKOLONI ‘MWEUSI.’
WALE
AMBAO WALIKUWA WABISHI NA WALIKATAA MAONO HAYO YA WAKOLONI, BASI WALIONJA JOTO
YA JIWE, TUNAMKUMBUKA, SAMORA MACHELE, PATRICE LIMUMBA, STEPHEN BIKO, ANWAR
SADAT,WALTER RODNEY na wengine wachache ambao sijawataja...
HAWA
NDIYO WALIO KUWA WATOTO WA AFRIKA.
WENGINE
WENGI WALIOBAKIA NA WENGINE AMBAO BADO WAPO MADARAKANI MPAKA HIVI SASA,
WANACHEZA NA KUIMBA WIMBO MMOJA NA WALE WALIO ITWA WAKOLONI, KAMA ALIVYO SEMA
SNIPES KWENYE ‘SUGAR HILL’ ... Partner with the same men that stripped away our
family dignity. Uneasy partners, tied together by time, fear, and greed ...’
WAKABADILISHA
HISTORIA ZA NCHI ZAO ILIWAONEKANE KUWA WAO NDIYO WATOTO WA AFRIKA, LAKINI lies
never stand the taste of time au kama wanavyo sema waswahili ... penye ukweli
uwongo hujitenga ... LEO TUNAWAONA KWA SURA ZAO ZA HALISI, LEO TUNAJUA KUWA
WAMETUFIKISHA HAPA TULIPO KWA VILE WAO NA WALE WAKOLONI LAO LILIKUWA NI MOJA.
KAMA
TUNAZUNGUMZA KWA KUTUMIA MISEMO, BASI NI KWELI KABISA TANZANIA NI NCHI YA
MAZIWA NA ASALI ... LAKINI LEO IKO WAPI, MIAKA 52 YA UHURU NA NCHI INAZAMA KILA
UCHAO KATIKA KILA AINA YA SHIDA, CHUKI,MATATIZO NA DHIKI. YUKO WAPI YULE ALIYO
ITWA ‘BABA WA TAIFA?’ MIAKA 25 BAADA YA KUMTUMIKIA MKOLONI NA KUHARIBU HATA
VILE VILIVYO ACHWA NA MKOLONI MWENYEWE AKAAMUA ‘KUNG’ATUKA.’ LAKINI HISTORIA
IMEBADILISHWA NA YEYE ANAONEKANA KAMA NDIYE MPIGANIA UHURU NAMBA MOJA WA NCHI
HII, WAKATI SOTE WENYE AKILI TUNAFAHAMU, WAKATI YEYE ANAZALIWA WATU WALISHAANZA
KUPIGANIA UHURU, MBONA HAWATAJWI HAO MASHUJAA WENGINE WA KWELI?
MBONA
HAPAULIZWI NI VIPI MWALIMU ALIFIKA PALE ALIPOFIKA, LAKINI SWALI LA MSINGI
KULIKO YOTE KWANINI ALIISALITI TANZANIA? ...
ANY WAY
TURUDI RWANDA ....
Tangu
nchi hiyo ilipo pata uhuru wake mwaka 1962, mahusiano yake na wale walioitwa
wakoloni na ‘donors’ yakawa ya ajabu zaidi. Wakati wa ukoloni walio pewa nafasi
kubwa kimamlaka walikuwa ni Watusi, lakini ‘walipoondoka’ wakoloni, madaraka
wakayaacha kwa Wahutu, hii ilikuwa ni muhimu ilikuchochea moto unao waka!
Wahutu wanapewa nafasi ya kulipiza machungu yao wakati wa Ukoloni.
WAPO PAMOJA NA MABWANA WAKUBWA ....
Pamoja
na kuwa nchi ya Rwanda ilibaki kwa Wanyarwanda wenyewe, lakini mbegu ya chuki
ya kikabila iliyo pandikizwa na mkoloni ilishamea vizuri. Sasa chuki hiyo
ilianza kuonekana kwenye sekta za serikali kama vile kwenye jeshi, kwenye mambo
ya kiuchumi na kwenye mambo ya kijamii pia.
Mwaka
1990, mbegu ya chuki ya kikoloni ikaanza kutoa matunda yake, machafuko ya ndani
ya kazuka, baina ya Watusi dhidi ya Serikali ya Wahutu. Kama kawaida ‘Donors’
na aliyekuwa mkoloni wakaingilia kati mzozo huo, wakataka mapigano yamalizwe na
watu warudi mezani wazungumze. Donors wakaweka masharti yao wanayo taka
yafuatwe ili waweze kutoa chochote ‘kuijenga’ nchi na uchumi wake.
Walicho
kitaka ‘Donors’ kwa Rwanda ili waweze kuwapatia hiyo ‘misaada’ ni kile walichokiita
‘Democratization.’ Walitaka kile wanacho
kiita ‘mfumo wa vyama vingi.’
Lakini
walifahamu hilo halitoweza kuwezekana kwa nchi ambayo tayari imeshagawanywa
kwenye misingi ya kikabila, kwa nchi ambayo tangu kuanguka kwa bei ya kahawa
kwenye soko la kimataifa, imefanywa kuwa ni tegemezi kwenye mifuko ya Donors
chini ya IMF NA WB.
Nchi
hiyo ili iweze kuendelea kupokea ‘misaada’ kutoka Marekani, ilikuwa ni lazima
ibadilishe sera zake za kiutawala na uchumi pamoja na kuonesha ukuaji wa ‘demokrasia.’
Maisha
magumu na mazingira magumu ya kiuchumi kwa Wanyarwanda, yaliyosababishwa na
vita pamoja na sera za IMF, vilikuwa ni vikwazo vigumu kabisa vya kuelekea
kwenye hiyo demokrasia ambayo mataifa wahisani walikuwa wakiitaka Rwanda ieleke
huko. Wahisani hao wakaja na msamiati mwingine, ‘Good Governance,’ msamiati huu
ulitilia mkazo kwenye ‘democratization’ ambayo ilipandikiza mfumo wa vyama
vingi kwa gharama za nchi wahisani!
UCHUMI
BAADA YA UHURU
Zao kuu
la biashara ni kahawa, ambapo Rwanda ilivuna 80% ya pato lake la kigeni huko.
Kama zilivyo nchi nyingine za Afrika, mazao yake ya biashara ni yale ambayo
mkoloni aliyateua, na yaliendelea kulimwa baada ya yeye kuondoka, na
yaliendelea kuuzwa kwa wanunuzi walewale, ambao walinunua kwa bei waliyo taka
wao kama ilivyo kuwa katika ukoloni.
Uchumi
uliachwa kwenye bidhaa moja tu, Kahawa, bei ya bidhaa hiyo ilipo anguka kwenye
soko la dunia, uchumi wa Rwanda ulibaki matatani, lakini zaidi hata hicho
kidogo kilicho kusanywa kilirudishwa kwa nchi wahisani kulipa madeni yao.
IMF
mmoja kati ya wale walio iletea nchi hiyo matatizo, akaja na ‘suluhisho,’ la
tatizo walilosababisha. Kwenye ‘suluhisho’ jipya 50% ya sarafu ya Rwanda ilishushwa
thamani yake Novemba 1990, wiki sita tu baada ya jeshi la waasi wa Rwanda
kutoka Uganda kuivamia Uganda, jeshi hilo ni
Rwandan Patriotic Front (RPF) chini ya Paul Kagame.
Kushushwa
kwa thamani sarafu ya Rwanda, IMF walisema kungewezesha usafirishaji wa Kahawa
kwa wingi nje na hivyo kuingizia Rwanda pato kubwa zaidi, na kuondoa vita.
Lakini kinyume chake ndicho kilicho tokea, vita vya wenyewe kwa wenyewe
vikapamba moto, kipato cha wananchi mmojammoja kikapungua kutokana na kuanguka
kwa thamani ya sarafu. Lakini wiki chache tu baada ya sarafu hiyo kushushwa
thamani, bei ya mafuta na bidhaa nyingine muhimu ikapanda juu. Deni la nchi
hiyo ambapo mwaka 1985 lilikua kwa mara mbili zaidi, na baada ya sarafu
kushushwa thamani yake, DENI HILO likaongezeka kwa 34% kati ya mwaka 1989 na 1992.
Serikali haikuwa na pesa za kuendesha mambo yake, shughuli za kijamii
ziliporomoka. Wananchi wenye hasira wakaanza kuing’oa miche ya mikahawa,
takribani miti 300,000 ya kahawa iling’olewa.
Wananchi hawakuwa tayari kurudi kulima chakula.
IMF
hawakuridhika, mwaka 1992 wakatoa amri tena kwamba sarafu hiyo ya Rwanda lazima
ishushwe tena thamani kwa mara nyingine. Hili likaongeza gharama kwenye bidhaa
muhimu na mafuta. Pesa iliota mbawa kwenye mifuko ya Wanyarwanda.
Septemba
1990, wakati nchi ipo kwenye hali mbaya na inaelekea kwenye machafuko, yaani
wiki chache tu kabla ya uvamizi wa waasi kutoka Uganda, kulikuwa na kikao
kizito ndani ya Washington DC, kati ya IMF na waziri wa mambo ya uchumi wa
Rwanda, ambapo IMF walishabariki kutoa kiasi kikubwa cha fedha kwenda Rwanda.
Oktoba
mosi, wakati mamilioni hayo ya dola yanaingizwa kwenye benki kuu ya Rwanda, ni
siku hiyohiyo waasi kutoka Uganda wanavuka boda kuingia Rwanda na kuanza
machafuko. Ni kama waasi waliambiwa subirini kwanza fedha ziingie ... Fedha
hizo za ‘msaada’ kutoka kwa nchi wahisani zilitolewa kwa madhumuni ya ‘kuingiza
bidhaa kutoka nje,’ bidhaa za kijamii ilikupunguza makali ya kiuchumi. Hata
hivyo kiasi kikubwa cha mkopo huu wa harakaharaka, kilitumiwa na serikali kwa
mahitaji tofauti na yale yaliyo lengwa.
Zilitumika kununulia zana na vifaa vya
kijeshi kutoka South Africa, Egypt, na Ulaya Mashariki. Kuanzi Oktoba mosi
jeshi la Rwanda lilipanuka ghafla kutoka askari 5000 mpaka askari 40,0000,
vijana wasiokuwa na ajira kutokana na kuanguka kwa uchumi ndiyo walioandaliwa
na hatimaye kuingizwa jeshini.
Wakati nchi ikiwa imechanika chanika kutokana
na hali mbaya ya uchumi, kiasi cha dola za Marekani Milioni 260, zilimwaga
kwenye benki kuu, kutoka nchi wahisani ambao ni Ufaransa, Ujerumani, Ubelgiji,
European Community, na Marekani. Fedha hizi hazikwenda kurekebisha hali ya
uchumi iliyo kuwepo, bali kusaidia kulipa deni la Rwanda lililo tangulia pamoja
na kununua zana za kivita. Hivyo ndivyo nchi wahisani walivyo taka pesa zao
zitumike.
Pia
ikumbukwe kwamba IMF kupitia kwa mshirika wake Interanational Development
Association (IDA) ilitoa amri kwa serikali ya Rwanda kubinafsisha shirika la
umeme na maji, Electrogaz. Sababu ya kubinafsishwa ni ili liweze kutumika
kulipia deni la nchi hiyo. Haikuwa ajabu baada ya shirika hili kubinafsishwa
bei ya umeme ilipandishwa maradufu, wananchi walizidi kukamuliwa ili deni
liweze kulipika.
Septemba
1993, mwaka mmoja kabla ya mauaji ya kimbari shirika la mawasiliano na simu nalo
likabinafsishwa, mwongozo mwingine kutoka IMF na WB.
Kama
nchi wahisani wakishirikiana na WB na IMF, ni WABAKAJI, na nchi ya Rwanda ni MWANAMKE
anayetaka kubakwa, basi mpaka hapo MWANAMKE HUYO ALIKUWA KISHA VULIWA NGUO ZOTE
NA WABAKAJI WALIKUWA WAMESHAPANGA MSTARI KUIANZA DHAMBI YAO ....
TUKUTANE
TENA HAPO, KUTIZAMA NAMNA DHAMBI HIYO ILIVYO TENDEKA ...
pamoja kk
ReplyDelete