Thursday, January 2, 2014

MALIGHAFI ZA AFRIKA NA DAMU YA WAAFRIKA

Tangu yalipo anza machafuko Rwanda 1990, Washington walikuwa na ajenda ya siri ya kusimamisha NGOME YA MAREKANI ndani ya Afrika ya kati, eneo ambalo kihistoria lilimilikuwa na Ufaransa na Ubelgiji.

Mpango wa Marekani ulikuwa ni kumuondoa Ufaransa ndani ya Afrika ya kati (WASOMI NA WALE WENYE AKILI TUJIULIZE IKIWA RWANDA ILIKUWA NCHI HURU, KWANINI MAREKANI IPIGANE KUMUONDOA MFARANSA?) Mpango huo ulilenga kuwatumia Rwanda Patriotic Front (RPF), Washington ikawadhamini RPF kwa silaha, mafunzo na mbinu za kijeshi na vifaa.



Kutokea katikati ya miaka ya kwenye miaka 1980, serikali ya Kampala chini ya Yoweri Musaveni, ilitumia na Washington kama mfano wa kuigwa kwa ‘demokrasi.’ Lakini pia Uganda ikawa ndiyo kituo ambacho waasi waliokuwa wakidhaminiwa na Washington, waliondokea hapo kwenda kufanya uasi wao kwenye nchi za Sudan, Rwanda na Congo.
WANAWAFUNDISHA WAAFRIKA NAMNA YA KUUWANA

Meja Jenerali Paul Kagame, alikuwa mkuu wa intelejensia kwenye jeshi la Uganda, Kagame amepata mafunzo ya kijeshi kupitia jeshi la Marekani kwenye chuo cha Marekani Command Armed Forces (CGSC). Kagame alirudi kutoka kwenye chuo hicho na kuja kuliongoza jeshi la RPA, muda mfupi tu baada ya machafuko ya 1990.

KUDHAMINI PANDE MBILI ZA VITA

Ni kawaida kwa mataifa ya magharibi, kudhamini pande mbili za vita. Kuna faida kubwa kwao kwa vita kuendelea kuwepo kwa muda mrefu. Serikali ya Habyarimana ilipokea mkopo kwa ajili ya kuboresha jeshi lake kutoka kwa nchi wahisani na taasisi za kifedha za kimataifa.

Kuiwezesha Uganda kijeshi ilikuwa ni moja ya mipango muhimu kwenye sera za mambo ya nje za Marekani. Jeshi la Uganda UPDF na RPA, Rwandan Patriotic Army yalijengwa kwa msaada mkubwa wa Marekani na Uingereza.

“Kutoka 1989 na kuendelea, Marekani amewasaidia RPF (Rwanda Patriotic Front) na Uganda katika kuivamia Rwanda. Mahusiano baina ya Uingereza na Marekani yalipokuwa katika kuwasaidia Uganda na RPF, NDIVYO UHASAMA BAINA YA Rwanda na Uganda ulivyozidi kukua. Mpaka ilipofika mwaka 1990, RPF walianza maandalizi ya kuivamia Rwanda na wakiwa na kibali cha kufanya hivyo kutokwa kwa Shirika la kijasusi la Uingereza. (Written in 1999, the following text is Part II of Chapter 5 on the Second Edition of The Globalization of Poverty and the New World Order. The first part of chapter published in the first edition was written in 1994. Part II is in part based on a study conducted by the author and Belgian economist Pierre Galand on the use of Rwanda's 1990-94 external debt to finance the military and paramilitary.)


Wanajeshi kutoka Rwanda chini ya mwavuli wa RPA na Uganda kupitia UPDF walimsaidia John Garang na jeshi lake la People’s Liberation Army kwenye vita Sudan Kusini. Washington walijishughulisha kikamilifu kwenye michakato hiyo, nyuma ya shughuli vivuli za CIA. (Africa Direct, Submission to the UN Tribunal on Rwanda, http://www.junius.co.uk/africa- direct/tribunal.html)

Kukuwa kwa deni la nje la Uganda katika kipindi cha raisi Museven, kulikwenda sambamba au kuliwiana na kipindi cha machafuko ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya Rwanda na Congo.

Wakati Museven anayapata madaraka ya uraisi mwaka 1986, deni la nje la Uganda lilikuwa ni dola bilioni 1.3. Halafu ghfla deni hilo likakuwa mara tatu na kufikia dola bilioni 3.7 mnamo mwaka 1997. (Ibid)

Pesa hizi za Museven zilikwenda wapi? Mikopo hiyo kutoka kwa wahisani ililenga ‘kusaidia uchumi na shughuli za kijamii. Ni katika kipindi cha machafuko kwenye eneo la Afrika ya kati ndicho kipindi IMF walicho chagua ‘kuisaidia’ Uganda kiuchumi.
World Bank ndiyo walio kuwa wasimamizi wa fedha hizo kwa niaba ya nchi wahisani waliotoa fedha zao hizo. Serikali ya Uganda ilitakiwa kuweka hadharani kila sumuni ilivyotumika ya fedha hizo, mpaka kwenye wizara ya ulinzi, kila kipengele. 

Hata hivyo matumizi kwenye wizara ya ulinzi yalipozidi, World Bank hawakusema chochote. Baadhi ya fungu lililotakiwa kutumika kwenye shughuli za kijamii lilikwenda moja kwa moja kutumiwa na United People’s Defense Force (UPDF) ambayo ilikuwa ikijishughulisha na shughuli za kijeshi nchi Rwanda na Congo.
Hivyo utaona sehemu ya deni la nje la Uganda lilikwenda kudhamini shughuli za kijeshi ambazo zilikuwa zinayo maslahi kwa Washington.


Wakati waasi wakidhaminiwa kupitia serikali ya Uganda, serikali ya Rwanda nayo haikuwachwa nyuma, nayo pia ilipokea misaada kutoka kwa ‘WAHISANI’ walewale, na World Bank akiwa kama mwangalizi kuwa fedha hizo zinaingizwa mahala panapo takiwa.
Serikali ya Habyarimana ilipokea fedha hizo nayo kama ilivyo fanya Uganda, kiasi kikubwa kikatumika kwenye Wizara ya ulinzi pamoja na kuagiza silaha mbalimbali, yakiwemo mapanga yaliyo tumika kufanyia mauwaji hayo, unadhani Wahutu na Watusi walikuwa na mapanga ya kutosha kuchinjana? Hapana yaliagizwa kama bidhaa ‘muhimu za kijamii’ na World Bank akitazama. (Jim Mugunga, Uganda foreign debt hits Shs 4 trillion, The Monitor, Kampala, 19 February 1997.)


Walipo tumwa wachunguzi na wakaguzi, kutizama ni namna gani serikali ya Habyarimana imezitumia fedha zile za mkopo, hasa kulingana na masharti iliyo wekewa na nchi wahisani. Katika ripoti yao wakaguzi hao, hakuna hata sehemu moja waliyo zungumzia kuhusu fedha hizo kutumika kuingiza mapanga takribani milioni moja (Michel Chossudovsky and Pierre Galand, L'usage de la dette exterieure du Rwanda, la responsabilité des créanciers, mission report, United Nations Development Program and Government of Rwanda, Ottawa and Brussels, 1997.)na zana zingine zilizo tumika kwenye mauaji hayo ya kimbare. Wakaguzi hao walikuwa chini ya jicho la World Bank na Serikali, ingawa vitabu vya serikali vilithibitisha matumizi hayo, lakini kwenye ripoti hiyo haikuwekwa. Hata suala la nchi hiyo kuwa ilikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kabla ya 1994, halikutajwa (See also schedule 1.2 of the Development Credit Agreement with IDA, Washington, 27 June 1991, CREDIT IDA 2271 RW.)


Mwaka 1995, yaani karibu mwaka mmoja baada ya mauaji ya Kimbari, ‘WAHISANI’ ambao walitoa fedha zao kwenye utawala ulio tangulia, wakarudi Kigali kuzungumza na serikali mpya ya Kagame kuhusiana na fedha ambazo waliikopesha serikali iliyotangulia, fedha ambazo zilitumika kununulia zana ambazo Wanyarwanda walichinjana, kuchinjana ambako hata hao ‘WAHISANI’ hawakutambua kwenye ripoti zao kama tukio hilo limetokea (Huenda waliokufa si Binadamu), leo wametuma wawakilishi wao kuzungumzia namna gani fedha hizo zitalipwa. Inauma sana, hata majeraha ya vita vile hayajakauka, tena fedha zilitumika kutuchinjia sisi, leo wanakaa mezani na serikali ‘teule’ na wanazitaka hizo fedha.

Kagame ilibidi akubali juu ya kuwepo kwa deni hilo. Mwaka 1998 ‘WAHISANI’ wakakakutana tena Stockholm, dola milioni 55.2 zikatengwa, na akaunti maalum ikafunguliwa, kama ‘postwar reconstruction’ (World Bank completion report, quoted in Chossudovsky and Galand, op cit) Lakini pesa hizo hazikuenda Rwanda, bali zilitumika kulipia deni ambalo serikali iliyo tangulia ililiingia kwa kununulia silaha za kuwachinjia raia wake.

Baada ya Kagame kukabidhiwa nchi mwaka1994, chaguo la Washington D.C, WANAJESHI KUTOKA Rwanda na Uganda wakaivamia Zaire, ambayo kabla kama ilivyo kuwa Rwanda ilikuwani ngome imara ya Ufaransa na Belgiam. Si unajua lugha ya taifa ya Rwanda siyo KIFARANSA tena ni KINGEREZA, Mfaransa nje, sasa Marekani kwa kutumia askari wake wawili watiifu, Rwanda na Uganda, anaisogelea Zaire, moja ya nchi kubwa Afrika.

MOVIE MPYA, DIRECTOR AKIWA NI WASHINGTON, AMEBAKI STEKINGI MMOJA ...

Wanajeshi wa Kagame walio pokea mafunzo kutoka kwa wanajeshi maalum wa Kimarekani, wakishirikiana na wale wa Uganda, wanakwenda Zaire kupambana na ‘WAASI’ waliokimbilia Zaire na ambao wanaitishia usalama wa serikali mpya ya Rwanda.

Lakini wakati wanajeshi wa Rwanda wakipokea mafunzo kutoka kwa kikosi maalum cha Marekani, kwa siri wanajeshi wa Rwanda waliyatoa mafunzo hayo kwa waasi wa Kinshasa ndani ya Rwanda. Mpango wa Museven na Kagame ni kuwasaidia waasi wa Kinshasa walio kuwa wakiongozwa na Kabila dhidi ya serikali ya Mobutu seseko.

Mchakamchaka ukaanza, waasi wakaanza kusonga mbele, nyuma yao zipo baraka za Rwanda, ambaye yeye anazo baraka za Washington, ndani ya miezi saba, kwenye nchi kubwa kuliko zote Afrika, waasi wakiwa wanapata upinzani mchache, Mobutu akakimbia Kinshasa, Kabila akaichukua nchi, akabadilisha jina na kuiita Congo. Kama kawaida, Marekani wakakana kujihusisha kwao na vita hivyo, ingawa kulikuwa na ushahidi wa kila namna wa Washington kuweka mkono wake kwenye vita hivyo. (A ceiling on the number of public employees had been set at 38,000 for 1998 down from 40,600 in 1997. See Letter of Intent of the Government of Rwanda including cover letter addressed to IMF Managing Director Michel Camdessus, IMF, Washington, http://www.imf.org/external/np/loi/060498.htm , 1998.)

MASLAHI YA MAREKANI

Kilicho kuwa kikitakiwa Congo na Washington si kingine bali ni hazina ya madini Kusini Mashariki mwa Zaire, na maeneo mengine yanapo patikana madini mengine. Wakati wa vita hivyo, miezi kadhaa kabla ya kukimbia kwa Mobutu, Laurent Desire Kabila kwenye ngome yake ya Boma, alishaanza kuingia mikataba ya makubaliano na wachimbaji wa makampuni ya Uingereza na Marekani, mataifa mawili ambayo hazina za madini hayo ni muhimu sana kwao kwenye upande wa viwanda vyao vya silaha. (Ibid)


Wakati huohuo ndani ya Washington, Kiranja mpya wa Afrika au wa nchi za Dunia ya Tatu, IMF walikuwa Bize kupanga uchumi wa Zaire baada ya vita, hakuna muda wa kupoteza. Mpango mzima upo mezani unasubiri serikali mpya.

Mwezi mmoja tu kabla Mobutu hajaikimbia nchi yake, IMF ikatoa mapendekezo yake, ‘sarafu ya Zaire ikawekwa msalabani,’ kama njia ya kufufua uchumi. (Lynne Duke Africans Use US Military Training in Unexpected Ways, Washington Post. July 14, 1998; p.A01.

) Miezi michache baadaye, baada ya Laurent Desire Kabila kupewa nchi, IMF wakampatia Kabila amri nyingine, kwamba mishahara ya wafanyakazi wa serikali wote isimamishwe, kwa ajili ya ‘kuimarisha uchumi.’ Ulioharibiwa na mfumuko wa bei. (Musengwa Kayaya, U.S. Company To Invest in Zaire, Pan African News, 9 May 1997. Kumbuka walifanya hivyohivyo Rwanda kabla ya mauaji wa ya Kimbari, kitu kilichoiweka uchi Rwanda kufanywa wanavyo taka nchi wahisani.


Sera hizo za IMF zilikuwa ni mafuta kwenye moto unao waka, nchi haikuweza kukalika tena, vita vya wenyewe kwa wenyewe vikala maisha ya watu zaidi ya milioni 2.

Mwaka 1998, RPA na UPDF wakaivamia DRC tena, baada ya Laurent Kabila kusahau nafasi yake, nafasi yake kwenye mchezo mzima wa ‘nchi huru’ za dunia ya tatu. Alisahau kwamba yeye ni MCHEZESHWAJI kama walivyo wanasiasa wengine na akajifanya kwamba yeye ni MCHEZESHAJI. Aliikataa mipango ya Washington, na akaivunja mikataba aliyo isaini Goma na nchi wahisani, kabla hajapewa nchi, akawakana vibaraka wa Rwanda na Uganda walio mweka Madarakani.

Kwa vyombo vya habari vya magharibi. Vita hivi vinafahamika kama ‘Africa First World War’ Kwa sababu vinahusisha mataifa sita ya Afrika pamoja na mataifa ya magharibi kwa upande mwingine.

Wawakilishi wa nchi za Magharibi kwenye vita hivyo wananufaika kwa kusafirisha rasilimali za nchi hiyo kwenye soko la kimataifa, wakati vikundi vya waasi vikinufaika kwa soko la ndani.
Rasilimali za Congo zimegeula sufuria la Pilau kwenye sherehe, mwenye mwiko, mwenye sahani, mwenye kijiko, mwenye mfuko, aliye mikono mitupu, kila mtu anacho chake, na tunajua uhitaji wa madini yanayo tumika kutengenezea vifaa vya kielektronik, kama simu, laptop, na mengineyo, mashirika na makampuni ya kimataifa yanachukua rasilimali hizo kwa bei ya kuwachinja wananchi wa Congo.



Wakati hayo yanaendelea nchi kama Uganda na Rwanda zinaendelea kuneemeka na mipango mbalimbali na hata zana za kijeshi kutoka Marekani. Uganda inatajwa kama ngome ya Marekani ndani ya Afrika ya kati.


6 comments:

  1. Habari za saahzi kaka hope umzima kabisa asante kwa post zako nimekua nikifatilia sana ila mbona kimya alaf ningependa utuelezee vifo vya aaliyah na 2pac coz vinahusishwa sana na hawa jamaa af kuna faida gani na hasara m2anayopata pindi anapojiunga?!

    ReplyDelete
  2. Kaka mbona kimya?! Swali langu hapo juu ujanjbu

    ReplyDelete
  3. vp mbona kimya bongo zimelala

    ReplyDelete
  4. Kaka naona blog yako ishakufa 2ambiane bhasii

    ReplyDelete
  5. Pole kwa ukimya, ni majukumu tu.
    Kuhusu 2pack na Aaliya hope siku moja nitaandaa post yao, lakini kwanza ninavyo viporo ambavyo ningependa kuvimalizia.
    Utakapo endelea kuitembelea hii post na hata sasa kwa idadi ya post nilizoziweka inatosha kukuambia mbivu na mbichi ni ipi.
    Kifupi usijaribu kujiunga nao.

    ReplyDelete