Thursday, April 24, 2014

UJIO WA BENKI MOJA YA DUNIA


Safari ya kuelekea kwenye New World Order, kwa kiasi kikubwa imebebwa na mfumo huu wa kiuchumi ambao unategemea mabenki. Rejea posti hii kuhusiana na mabenki ya Illuminanti. Kama nilivyo sema awali aihitaji kufikiri sana kuona kuwa wale wenye mamlaka juu ya pesa, mzunguko wake na thamani yake ndiyo wenye mamlaka juu ya dunia hii. Hichi ndicho Illuminanti kwa kiasi kikubwa wameweza kukifanikisha.


Katika zama za kati wakati utajiri ukipimwa kwa mali kama vile dhahabu na fedha. Illuminanti wakiwa wamjifinika shuka la Knight Templar, waliweza kijiweka kwenye nafasi ya juu ya uchuuzi wa bidhaa hiyo muhimu ambayo leo tunaiita ‘PESA’. Matajiri na wafalme wa zama za kati hawakufanya biashara hiyo na yeyote zaidi ya Knight Templars.

Brotherhood wakagundua kwamba kiasi kikubwa cha dhahabu kinaweza kukopeshwa kwa kutumia makaratasi yenye sahihi yao na thamani ya dhahabu halisi ikiwa imeandikwa kwenye makaratasi hayo badala ya dhahabu yenyewe. Kama ambavyo leo mtu anavyo weza kukuandikia hundi badala ya kukupa pesa halisi. Juu ya hapo Brotherhood walipo kopesha makaratasi hayo ambayo ‘yaliwakilisha’ dhahabu waliyonayo, waliwatoza riba wale wakopaji. 



Wakati mwingine hawakuwa na hizo dhahabu halisi, ispokuwa walikuwa na makaratasi tu, hivyo waliwakopesha watu makaratasi hayo na kuwachaji riba kwa makaratasi hayo bila wao kuwa na hizo dhahabu halisi, tizama posti hii kwa http://salimmsangi.blogspot.com/2013/10/mfumo-wa-mabenki-na-hatma-yetu. 

Lakini mwiso wa siku wakopaji walipokuja kulipa madeni yao, hawakulipa makaratasi yale waliyo pewa awali, ispokuwa walilipa dhahabu halisi. Kwa utaratibu huu hazina ya dhahabu ikaangukia kwenye mikono ya Illuminanti na imekuwa ikiongezeka tangia hapo. Sasa dunia inautambua mfumo uo kuwa ni halali, na ndiyo utaratibu wa uchumi wetu leo, ambapo makaratasi yanatumika kama ‘kiwakilishi’ cha utajiri halisi ambao upo mikononi mwa wa chache, lakini wakati huu ukiwa hauwakilishi dhahabu, ispokuwa mali halisi zinazo milikiwa na masikini, na mwisho wa siku tunaposhindwa kulipa madeni hayo wanakuja kuchukua nyumba, gari na mengineyo, mfumo huo leo unatumiwa na taasisi zinazo itwa benki.


Tangu kipindi cha Babiloni, ukopeshaji wa kutumia riba umekuwa ndiyo hasa chanzo cha vurug, vita na hata kuanguka kwa dola mbalimbali. Dola kama ya Persia na Roma zilitanuka na kuwa kubwa kutokana na madeni makubwa waliyo kopa.

 Mwisho wa siku yanaposindwa kulipa madeni hayo huanzisha vita na mataifa ambayo yanawadai ili kulizima deni hilo kabisa. Hili linaendelea mpaka sasa. Utajiri wa Marekani umejengwa na matrilioni ya mikopo, mikopo kutoka kwenye benki za watu binafsi, na kinyume chake Barack Obama na marais wengine wote duniani SI MARAISI HALISI, BALI VIBARAKA VYA WAMILIKI WA MABENKI. KIFUPI NI KUWA NCHI ZOTE DUNIANI ZIPO KWENYE MIFUKO YA WAMILIKI WA MABENKI.


Moja ya sababu ya Ufaransa kushinikiza uvamizi wa Libya ni deni ambalo Ufaransa ilikuwa ikidaiwa na Libya, hivyo kwa kuong’oa utawala ule na kuweka utawala wanao utaka ni sawa na kulifuta deni hilo. Moja ya sababu kuu ya machafuko ya Rwanda ni madeni kutoka IMF na World Bank, tizama posti hii http://salimmsangi.blogspot.com/2014_01_01_archive.

Utozwaji wa Riba unasababisha kupaa kwa bei ya bidhaa kwa sababu asilimia kubwa ya gharama ya bidhaa inakwenda kulipia deni la muuzaji/msambazaji/mzalishaji/n.k. Deni linavyo kuwa kubwa, ndivyo inavyokuwa bei ni kubwa kwa bidhaa. Benki zinaongeza kiwango cha riba ilikupunguza idadi ya wakopaji lakini wakati huohuo kuifanya mikopo iliyopo kwenye mzunguko kushindwa kulipika, sababu kwenye mfumo tulio nao deni linapwa kwa deni, watu wasipo kopa, hakuna fedha kwenye mzunguko, pesa ikitoweka kwenye mzunguko madeni hayalipiki, madeni yasipo lipika, benki zinakuja kuchukua utajiri halisi ulio wekwa kama dhamana.


Ili taifa liweze kuendelea kiuchumi katika kiwango cha kitaifa na kimataifa, inabidi kwa serikali kukukopa fedha kwenye taasisi za fedha za watu binafsi, inakopeshwa pesa ambayo kimantiki hasa haipo. Taifa ili kuweza kulipa deni hilo inabidi kuchukua utajiri halisi kutoka kwa wananchi wake na kuwapelekea wakopeshaji ambao mara nyingi ni taasisi za fedha za kitaifa na kimataifa. Kwa wakati huohuo wananchi wanakopa kutoka kwenye taasisi hizohizo ili waweze kulipa mikopo, kodi na kuendesha maisha yao. 



Hii inatuambia kwamba, wamiliki wa mabenki katu hawawezi kupata hasara, hii inaamaanisha kwamba utajiri wote unao uwona kwenye maisha ya watu, kiuhakika eidha ni wa kwao wamiliki wa mabenki, au wameukopesha wao au utakwenda kwao baada ya muda. Mwaka 1993 serikali ya Uingereza ililipa £ 24.5 bilioni kama riba, hii ilikuwa ni mara mbili zaidi ya bajeti ya elimu kwa UK, na hii ilikuwa ni riba tu. Lakini hilo halitoshi kuifanya serikali kuprint fedha zake yenyewe na kuzikopeshaa bila riba!
Historia inatuambia kunao viongozi waliojaribu kufanya hivyo katika kipindi chao cha kiutawala. Abraham Lincoln alisema baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya Marekani, atarudi na kuitizama Federal Reserve, na kweli alianza kuprint fedha zake mwenyewe, lakini haikumchukua muda, aliuwawa. J.F. Kennedy naye alikuja na wazo kama hilo la Lincoln, naye kilimpata kilicho mpata mwenzake.


Leo utaziona serikali zetu zikitoza kodi katika kila kitu, maeneo mengine yanatozwa kodi zaidi ya mara mbili, serikali zinakusanya pesa kuliko zilivyo pata kukusanya hapo, serikali zinatoa ahadi nzuri nzuri kwa wanachi wake, lakini hali ya uchumi bado inazidi kuzorota, na tunajiuliza ni wapi fedha zote hizi serikali inapozipeleka? Rasilimali za nchi zinauzwa kwa kutumia neno ‘ubinafsishaji’ na ‘uwekezaji’ lakini hali bado duni, shida nini? Matumbo yasiyo ridhika, yasiyo shiba, yasiyo kinai ya wamiliki wa mabenki ndiyo wanao pelekewa utajiri huo, na hawawezi kuacha mpaka nchi yote iwe kwenye mifuko yao.

Jiulize kwanini dunia hii iliyo jaa rasilimali kutoka angani, aridhini, baharini na kila unapo pafikiria, lakini bado kuna watu wanava nguo moja na hawana ndoto kwamba kuna siku wataweza kubadilisha, mamilioni wanakufa kwa njaa, vita  na ukame kila mwaka. Dunia nzima imetiwa minyororo ya madeni kutoka kwa wamiliki wa benki. Serikali zinabidi zikope fedha kutoka kwenye taasisi za fedha, kisha zizalishe bidhaa za kuuza kwenye mataifa mengine, ili ziweze kupata fedha za kulipa madeni yake pamoja na riba, au vinginevyo rasilimali zake zibinafsishwe kwenye mashirika ya kimataifa kwa kutumia maneno mazuri kabisa, ‘uwekezaji’.


Kiukweli kabisa ni watu wachache tu ndiyo hasa wame ishikilia dunia kwenye ncha ya kisu. Dunia inadhikika na walimwengu wake kwa sababu ya maamuzi ya watu wachache. Wameweka mfumo huu wa kibenki kuwa ndiyo uti wa mgongo kwa uchumi wetu na hakuna ambaye anasalimika na mfumo huo. 

Huyu mungu mkubwa wa uchumi anayeitwa ‘Benki’ na mitume wake kama ‘ukuaji uchumi’ na ‘uzalishaji bidhaa’ wakiwa tumia maandiko matakatifu ya ‘ubinafsishaji’ na ‘uwekezaji’ imekuwa ni ‘pepo’ kwa wateule wachache na ‘moto’ kwa mabilioni ya walimwengu. Mfumo huu unaizamisha dunia kwenye bahari ya madeni wakati wateule wakielea kwenye utajiri usio pimika.


Wakati dunia ikiwa imeshikiliwa na wamiliki wa mabenki, na kusalimika kwake kumewekwa katika ukopeshaji wa kutoza riba, daima kutakuwepo na hitajio la vita kutoka kwa watawala kwenda kwa watawaliwa. Hii ni kwa sababu katika mzunguko kutakuwa na kiasi kikubwa cha fedha kuliko utajiri halisi kama dhamana ya fedha hizo; pale ambapo mkopaji anapokosa fedha za kulipa deni lake na riba, anakuwa na vitu viwili tu; eidha awe mtumwa wa MKOPESHAJI, au ADUI YAKE, na chochote kati ya hicho hakina matokeo mazuri. 

Ni kwa sababu hii mabenki haya ya kimataifa ndiyo wadau wakubwa na wenye hisa kubwa zaidi kwenye Majeshi, sheria, nishati, madawa, elimu, vyombo vya habari n.k.

Ili mabenki yaendelea kukaa pale juu milele, wakopaji lazima wabakishwe kwenye lindi la ujinga na wasifahamishwe kwamba wao ni zaidi ya watumwa kwa wakopeshaji wao. Historia ya kweli, ikiwemo upotoshwaji na ulaghai wa mfumo wa kibenki, katu na lazima usifundishwe. Kiuhakika ni lazima, ni lazima usifundishwe. Tizama vitabu vya kihistoria vimejaa hadithi za wafalme na malkia, kuanguka na kukua kwa mataifa, vita na ushindi. Lakini ni zimwi gani hilo lililo nyuma ya hayo yote, hapati hata neno moja juu ya hilo, lakini siku zote zimwi hilo si jingine bali ni mfumo wetu wa uchumi ambao benki au kwa lugha nyingine ‘makaratasi’ ndiyo yamefanywa kipimo cha thamani ya vitu halisi, badala ya utajiri halisi wa vitu hivyo.

NEXT TIME PLEASE NA TUTAANGALIA HATUA KUELEKEA KWENYE BENKI MOJA YA DUNIA...........................  kumbuka tunatakiwa kuwa na SERIKALI MOJA!
KIONGOZI MMOJA!
DINI MOJA!
BENKI MOJA!
Na JESHI MOJA ..... TCHAOOOO

No comments:

Post a Comment