Wanamuziki
wengi, wanauwawa tarehe 25, au wakiwa kwenye umri wenye nambari 25.
Michael
Jackson tarehe 25 Juni 2009
Farrah
Fawcet Tarehe 25 Juni 2009
Sky
Saxon Tarehe 25 Juni 2009
James
Brown Desemba 25 2006
Dean
Martin Disemba 25 1995
Eartha
Mae Kitty Disemba 25 2008
Lisa
Lopes (Left Eye) Aprili 25, 2002
Rouger
Troutman Aprili 25, 2009
Aaliyah
Haughton Agosti 25 2001
Static
Major Februari 25 2008
Tupac aliuwawa akiwa na miaka 25
Ni
kweli vifo vya wanamuziki hawa kwenye tarehe ishirini na tano (25) ya mwezi
vimetokea kwa nasibu au ni kwa makusudi kwa wanamuziki hao kuwa wameuwawa kwenye tarehe
hiyo?
Unaweza
kusema kuwa vifo hivyo vimetokea kwa bahati mbaya, kwa sababu wanamuziki wengi
pia wamekufa lakini si kwenye tarehe 25 ya mwezi, kitu ambacho unaweza kuwa
sahihi, lakini unapoitizama historia ya Illuminanti na matumizi yao ya nambari
na jinsi inavyotumiwa kwenye vitu mbalimbali dhidi ya umma, hutasita kuona kile
ambacho wengi hawakioni, kwamba kuna ambacho kinaendelea, kuna ambacho kimebeba
baraka za kishetani kinaendelea.
Unakumbuka
tukio la 9/11?
911 ni
sawa na 9+1+1 11
Septemba
11 ni siku ya 254 ya mwaka na unapo chukua nambari hii yaani, 254 ni sawa na
2+5+4 = 11
Baada
ya tukio zima la 9/11 zinabaki siku 111 kabla ya mwaka kumalizika.
Majengo
yote mawili yalikuwa na ghorofa 110.
Jengo
la tatu kuanguka linalo julikana kama ‘BUILDING 7” na ambalo watu wengi
hawafahamu kama nalo lilianguka siku hiyo, lakini ni kweli lilianguka kama
yalivyo anguka mengine, ingawa halikugongwa na ndege, jengo hili lilikuwa na
ghorofa 47.
Chukua
4+7= 11
Idadi
ya madirisha kwenye majengo yote mawili ilikuwa ni 21,800 hivyo basi 21,800 ni
sawa na 2+1+8+0+0= 11
Ndege
ya kwanza kugonga mnara, ilikuwa ni ndege nambari 11.
Ndege
nambari 11, ilikuwa na abiria 92 kitu ambacho ni sawa na
9+2=11
Lakini
pia ndege hiyo ilikuwa na wafanyakazi 11 tu.
Mnara
wa kwanza kugongwa iliporomoka na kuwa mavumbi matupu ilipofika saa 10:28 AM
sawa na 1+0+2+8= 11
Majengo
pacha hayo yalianza kujengwa mwaka 1966 mpaka mwaka 1997, kwa maneno mengine
ujenzi huu ulichukua muda wa miaka 11 kumalizika.
Kwa
uchache tu hii itoshe kukuambia kwamba nambari ni muhimu sana kwenye matukio na
shughuli za maadui zetu.
Nambari
hii 11 ni nambari ya muhimu sana kwa Illuminanti. Nambari hii haipunguzwi na
kufanywa kuwa ni tarakimu moja, yaani 1+1 = 2 hapana, katika posti zilizo
tangulia nimeeleza maana hasa ya nambari hii na kwamba ukiipunguza na kuwa
tarakimu moja, maana yake inapotea.
Wanafahamu
kuwa maumbile ya dunia yamesimamia katika nambari, hivyo athari ya nambari
katika mazingira na mrengo fulani unayo matokeo mahususi kwa mtumiaji.
Turudi
kwenye vifo vya wasanii na nambari 25.
Watu
watatu maarufu, au wasanii watatu walikufa 25 Mei 2009, wakiwa ni Michael
Jackson, Farrah Fawcett na Sky Saxon.
Kikawaida
Illuminanti wanapo mtoa kafara mtu maarufu, lazima wafanye mara tatu, yaani
lazima kifo chake kiambatane na vifo vya watu wengine wawili, ambao ingawa si
maarufu sana, lakini majina yao yanayo nafasi kwenye jamii. Hivyo macho ya watu
yatabaki kwa yule mwenye jina kubwa zaidi kama ilivyo kuwa kwa Michael Jackson.
Jumla ya nambari, yaani 25 ni sawa na 2+5=7
Nambari 7 ambayo nayo ni moja ya nambari mahususi zinazo tumiwa na Illuminanti.
Katika tarehe hiyo ya mwezi, yaani tarehe 25 walikufa watu watatu maarufu kwenye jukwaa la muziki, hiyo ni sawa na kusema,
(2+5)(2+5)(2+5)=777
Unakumbuaka 'London Bombing' Ilitokea tarehe 7 ya mwezi wa 7 mwaka 2005, saba ya mwisho imefichwa kwenye mwaka ambao ni sawa na 2+0+0+5=7 hivyo ni 777. Pia milipuko iliyo rikodiwa siku hiyo idadi yake ilikuwa ni 7 kwa ujumla.
Vifo vya wanamuziki hawa kwenye tarehe husika, hapana shaka vilikuwa ni kafara ya kishetani, na mlengwa hapa alikuwa ni Michael Jackson.
Swali kwanini Michael Jackson ????????????????
Tukutane tena hapa kumalizia the rest of the story.
No comments:
Post a Comment