Wednesday, September 11, 2013

NAMBARI NA VIFO VYA WASANII

Wanamuziki wengi, wanauwawa tarehe 25, au wakiwa kwenye umri wenye nambari 25.

Michael Jackson tarehe 25 Juni 2009


Farrah Fawcet  Tarehe 25 Juni 2009



Sky Saxon Tarehe 25 Juni 2009


James Brown Desemba 25 2006


Dean Martin Disemba 25 1995


Eartha Mae Kitty Disemba 25 2008


Lisa Lopes (Left Eye) Aprili 25, 2002


Rouger Troutman  Aprili 25, 2009


Aaliyah Haughton Agosti 25 2001


Static Major Februari 25 2008


Tupac aliuwawa akiwa na miaka 25
Ni kweli vifo vya wanamuziki hawa kwenye tarehe ishirini na tano (25) ya mwezi vimetokea kwa nasibu au ni kwa makusudi kwa wanamuziki hao kuwa wameuwawa kwenye tarehe hiyo?

Unaweza kusema kuwa vifo hivyo vimetokea kwa bahati mbaya, kwa sababu wanamuziki wengi pia wamekufa lakini si kwenye tarehe 25 ya mwezi, kitu ambacho unaweza kuwa sahihi, lakini unapoitizama historia ya Illuminanti na matumizi yao ya nambari na jinsi inavyotumiwa kwenye vitu mbalimbali dhidi ya umma, hutasita kuona kile ambacho wengi hawakioni, kwamba kuna ambacho kinaendelea, kuna ambacho kimebeba baraka za kishetani kinaendelea.


Unakumbuka tukio la 9/11?

Katika utaratibu huu wa nambari kwa Illuminanti, mathalani 34095 ni sawa na 3+4+0+9+5 = 21 na 21 ni sawa na 2+1=3 kama nilivyo elezea kwa kina kwenye posti hii, http://salimmsangi.blogspot.com/search/label/13 ambayo hiyo nambari 11 haijatumika hapo kwa bahati mbaya, zaidi kuhusu nambari 11 na 9/11 tizama posti hii http://salimmsangi.blogspot.com/p/leotutazungumziaalama-nembo-za_27.html utaweza kuona kwa nini 11 Imetumika hapo, laki kwa nyongeza tu fanya hivi,
911 ni sawa na 9+1+1  11
Septemba 11 ni siku ya 254 ya mwaka na unapo chukua nambari hii yaani, 254 ni sawa na 2+5+4 = 11

Baada ya tukio zima la 9/11 zinabaki siku 111 kabla ya mwaka kumalizika.
Majengo yote mawili yalikuwa na ghorofa 110.
Jengo la tatu kuanguka linalo julikana kama ‘BUILDING 7” na ambalo watu wengi hawafahamu kama nalo lilianguka siku hiyo, lakini ni kweli lilianguka kama yalivyo anguka mengine, ingawa halikugongwa na ndege, jengo hili lilikuwa na ghorofa 47.
Chukua 4+7= 11
Idadi ya madirisha kwenye majengo yote mawili ilikuwa ni 21,800 hivyo basi 21,800 ni sawa na 2+1+8+0+0= 11
Ndege ya kwanza kugonga mnara, ilikuwa ni ndege nambari 11.
Ndege nambari 11, ilikuwa na abiria 92 kitu ambacho ni sawa na
9+2=11
Lakini pia ndege hiyo ilikuwa na wafanyakazi 11 tu.
Mnara wa kwanza kugongwa iliporomoka na kuwa mavumbi matupu ilipofika saa 10:28 AM sawa na 1+0+2+8= 11

Majengo pacha hayo yalianza kujengwa mwaka 1966 mpaka mwaka 1997, kwa maneno mengine ujenzi huu ulichukua muda wa miaka 11 kumalizika.

Kwa uchache tu hii itoshe kukuambia kwamba nambari ni muhimu sana kwenye matukio na shughuli za maadui zetu.
Nambari hii 11 ni nambari ya muhimu sana kwa Illuminanti. Nambari hii haipunguzwi na kufanywa kuwa ni tarakimu moja, yaani 1+1 = 2 hapana, katika posti zilizo tangulia nimeeleza maana hasa ya nambari hii na kwamba ukiipunguza na kuwa tarakimu moja, maana yake inapotea.

Wanafahamu kuwa maumbile ya dunia yamesimamia katika nambari, hivyo athari ya nambari katika mazingira na mrengo fulani unayo matokeo mahususi kwa mtumiaji.
Turudi kwenye vifo vya wasanii na nambari 25.

Watu watatu maarufu, au wasanii watatu walikufa 25 Mei 2009, wakiwa ni Michael Jackson, Farrah Fawcett na Sky Saxon.


Kikawaida Illuminanti wanapo mtoa kafara mtu maarufu, lazima wafanye mara tatu, yaani lazima kifo chake kiambatane na vifo vya watu wengine wawili, ambao ingawa si maarufu sana, lakini majina yao yanayo nafasi kwenye jamii. Hivyo macho ya watu yatabaki kwa yule mwenye jina kubwa zaidi kama ilivyo kuwa kwa Michael Jackson.
Jumla ya nambari, yaani 25 ni sawa na 2+5=7
Nambari 7 ambayo nayo ni moja ya nambari mahususi zinazo tumiwa na Illuminanti.


Katika tarehe hiyo ya mwezi, yaani tarehe 25 walikufa watu watatu maarufu kwenye jukwaa la muziki, hiyo ni sawa na kusema,
(2+5)(2+5)(2+5)=777

Unakumbuaka 'London Bombing' Ilitokea tarehe 7 ya mwezi wa 7 mwaka 2005, saba ya mwisho imefichwa kwenye mwaka ambao ni sawa na 2+0+0+5=7 hivyo ni 777. Pia milipuko iliyo rikodiwa siku hiyo idadi yake ilikuwa ni 7 kwa ujumla.





Vifo vya wanamuziki hawa kwenye tarehe husika, hapana shaka vilikuwa ni kafara ya kishetani, na mlengwa hapa alikuwa ni Michael Jackson.
Swali kwanini Michael Jackson ????????????????
Tukutane tena hapa kumalizia the rest of the story.

No comments:

Post a Comment