Thursday, August 29, 2013

FREEMASON NA MUZIKI


Sauti ya muziki leo ipo kila mahali, kila kona na uchochoro wa dunia yetu ya leo, watu wengi mno wanasikiliza muziki leo hii, kwa sababu mbalimbali, lakini ni watu wachache mno ambao kiuhakika wanafahamu maana ya mashairi, au sababu ya aina fulani ya mashairi na aina fulani ya ala ya muziki kutumika katika muziki husika.

 Ni wachache mno wanao fahamu athari mbalimbali zinazo oneshwa katika video za miziki mbalimbali, nalo hili ni jambo la kusikitisha mno.


Kumekuwa na minong’ono kuhusiana na kile kinacho endelea kwenye tasnia ya muziki na nani wanao tawala tasnia hiyo, mienendo mibovu ya wasanii wenyewe, unywaji wa pombe, utumiaji wa dawa za kulevyea, mazingira ya ‘mind control’ kwa wanamuziki na vifo vya ghafla vinavyo achwa maswali yasiyo na majibu.

Miziki mbalimbali unayo sikiliza redioni na kuitizama kwenye luninga, inabeba maana mahususi kwenda kwa wasikilizaji wake, kutoka kwenye vyombo vilivyo tumika, aina ya mashairi yanayo imbwa, vile vinavyo onekana kwenye vidio za miziki hiyo utakuta kuna jumbe zinazo husu mambo ya ushetani, ngono, mauwaji, uchawi, ushirikina na mengine ambayo sikio na jicho la mtazamaji huyadharau kwa vile eidha hawayafahamu au yamekuwa ni mambo ya kawaida kwenye jamii.

Mtiririko wa posti hizi za ‘muziki’ huenda zikawa na zakushtushwa kwa baadhi na kuwaweka njia panda wengine, lakini mwisho wa yote , ‘ukweli ndiyo utakao kuwacha huru.’ Kama zilivyo posti zangu zingine na zitakazo kuja, zisome kwa akili huru, tumia muda wako wa ziada kutafiti juu ya haya ninayo yaandika, na ninajua kuwa mwisho wa yote hutajutia muda wako. 

Hupaswi kuamini haya ninayo andika, unapaswa kuelewa haya ninayo andika, na ili uelewe unapaswa kuishirikisha akili yako huru, tuendelee.


Katika baadhi ya nyimbo, na hapa nazungumzia nyimbo kutoka nchi za magharibi, lakini pia kutoka nchi za Asia na pia kutoka nyumbani ambazo nazo kila uchao wasanii wetu wanajitahidi kila wawezalo ku-copy na ku-paste kila wanacho kona toka nchi za magharibi na Asia.

Utaona basi, katika nyimbo hizo, kuna baadhi ya maneno au majina ambayo yanatumika sana, na mara kwa mara katika nyimbo hizo, wakati mwingine ‘maneno’ au ‘majina’ hayo yanafichwa kwenye kiitikio (chorus) au kwenye kile kinacho fahamika kama ‘catch up’ ya wimbo.

Tuanze na baadhi ya nyimbo tuone maneno na majina hayo ...

Eminem -  kwenye wimbo unao kwenda kwa jina la ‘RAIN MAN,’ ametumia sana jina hilo RAINMAN
Rihanna – Kwenye wimbo unao kwenda kwa jina la ‘Umbrella’ neno ‘Umbrella limetumika sana.
Fat Joe akimshirikisha Lil Wayne – Kwenye wimbo unao kwenda kwa jina la Make it Rain.
Savage – Kwenye wimbo unaokwenda kwa jina la Wild Out, jina la RAIN MAN limejitokeza.
Black Stone Cherry – Kwenye wimbo wa Blind Man, jina la RAIN MAN limejitokeza tena.
Jamie Foxx – kwenye Wimbo Rain Man jina ‘RAIN MAN ‘ limetajwa maradufu.

The Game – Kwenye wimbo wa Cali Sunshine, jina RAIN MAN limejitokeza.
Jay Z akimshirikisha Usher Rymond na Pharrell – kwenye wimbo ‘ANYTHING’ jina la ‘RAIN MAN’ Limetajwa.
Eminem akimshirikisha Dr. Dree – Kwenye wimbo ‘OLD TIME’S SAKE’ jina ‘RAIN MAN’ limetajwa.
W.A.S.P – Kwenye wimbo ‘THE BURNING MAN,’ jina RAIN MAN lipo.

BOB DYLAN – Kwenye wimbo wa ‘STUCK INSIDE OF MOBILE WITH THE MEMPHIS BLUES AGAIN; Jina ‘RAIN MAN’ Limetajwa tena.
MIMS – Kwenye wimbo Doctor Doctor, jina ‘RAIN MAN’ Limetajwa tena.

Eminem – Kwenye wimbo wa RHYMIN’ WORDZ FREE STYLE’
H-Blockx kwenye wimbo wa ‘RAIN MAN’ jina RAIN MAN’ Limejitokeza.
NAS – Kwenye wimbo ‘DONT BODY YA SELF’ jina ‘RAIN MAN’ limo.



YA BOY- Kwenye wimbo ‘RAIN MAN’ jina ‘RAIN MAN’ na ‘UMBRELLA’ yametajwa.
TANYA TUCKER – Kwenye wimbo wa ‘LIZZIE AND THE RAIN MAN’ Jina ‘RAIN MAN’ limejitokeza.
Bob Dylan – Kwenye wimbo ‘I WANNA BE YOUR LOVER’, jina ‘RAIN MAN’ kama kawa, limo.

Maneno mengine yanayo tajwa ni ‘ILLUMANATI, SECRET SOCIETY, NEW WORLD ORDER, NA ORODHA YA WANAMUZI WANAO TAJA MAJINA NA VITU HIVYO NI KUBWA, SIJUI KUNA HAJA YA KUENDLEA WAKUU?

Hivyo basi ukitizama au kusikiliza muziki wa leo, kwa mtu mwenye akili huru, utaoana kuna kitu ambacho hakipo sawa, ama kitu ambacho hatuambiwi kuhusiana na tasnia hii ya muziki.
Swali, ni nani huyu ‘RAIN MAN?’


Tukutane hapahapa kwenye posti zitakazo fuata.




No comments:

Post a Comment