Freemason
wanaficha siri zao hadharani, yaani wanacho ficha wanakiweka hadharani, kweupe,
kila mtu aone, lakini ni wachache wanao ona, ni kima kuficha mbao kwenye msitu,
au kama wanavyo sema Waswahili, ‘mchawi mpe mwanao amlee,’ alama, majina na
maumbo yaliyo fichwafichwa, lakini kweupe hadharani yanakuwa yameandaliwa kwa
ajili ya kupokelewa na ubongo wa nyuma ambao hufanya kazi bila idhini ya
muhusika, na hii ndiyo sababu vitu hivyo huwa havionekani au kung’amuliwa na
wahusika sababu ni vitu ambavyo kwenye macho na kwenye akili vinaonekana kuwa
havina maana, lakini haimanishi kuwa kwenye ubongo wa nyuma havijarikodiwa,
vipo vimekaa vizuri.
Katika
vidio au sauti ya muziki alama hizi za siri hutokea au husikika kama kitu
kilicho ingia hapo kwa bahati mbaya na hakina maana yeyote, ni sawa na kusiliza
muziki kisha katikati ya wimbo jina ‘RAIN MAN’ linatajwa, kiukweli si kitu
chenye maana kwa msikilizaji wa kawaida, au picha ya kichwa cha mbuzi mwanzoni
mwa nyimbo ya Rihhana, lakini ingawa kwenye ubongo wa mbele hakuna kilicho
rekodiwa, ubongo wa nyuma ni kama ‘BLACK HOLE’ Hakuna kinacho pita kisirekodiwe
hapo uwe macho au umelala, hakikitatizi kitu hapo, na nyingi ya alama za
kimasoni hulenga kwenye ubongo wa nyuma.
Wakati
mwingine maumbo na alama hizo huwekwa wazi mbele ya macho yetu, lakini maana
yake inakuwa haifahamiki na wanao tizama, mara kadhaa alama ya jicho moja
huwekwa mbele ya hadhara, na kila mtu anaiona, lakini si kila mtu anayefahamu
maana ya nembo hiyo. Utasikia neno ‘NEW WORLD ORDER’ katikati ya wimbo lakini
huwezi jua maana halisi ya neno hilo ni nini.
Wakati
mwingine alama, nembo na maneno na majina huwekwa kweupe hadharani lakini kwa
ajili ya mawasiliano baina ya wanachama wa jumuiya hizi tofauti za siri. Hivyo
hulazimika kufanya hivyo, kama walipo fanya wakati walipo mchinja Nick Berg
live kwenye luninga, ule ulikuwa ni ujumbe mahususi kwa Illuminanti na mason
wote duniani kuanza kutekeleza majukumu yao kuelekea kwenye NWO, tizama post
hii kwa kina zaidi http://salimmsangi.blogspot.com/p/leotutazungumziaalama-nembo-za_27.html
Kwenye
hii vidio ya Rihanna, kile kinacho onekana kama maji yaliyo rushwa kwa mikono
na kutengeneza mfano wa kichwa cha mbuzi, ni wazi kuwa umbo hilo haliwezi
likaja kwa kitendo cha mwanamuziki huyo kuirusha mikono yake hivyo, ISPOKUWA
MTU FULANI ANAYEFAHAMU NINI ANACHO KIFANYA, NA ANAYELIPWA VIZURI TU KWA KUFANYA
KAZI HIYO, ALIFANYA KILE KINACHO ITWA ‘edit’ KWENYE VIDIO HIYO NA KUTENGENEZA
UMBO HILO LA KICHWA CHA MBUZI, ambalo kama tulivyo ona haliwezi kunaswana
ubongo wa mbele, bali wa nyuma.
Kumbuka
kwamba vidio hizi zinatengenezwa kwa macho yote, yaani chini ya uangalizi na
usimamizi mkubwa na wa umakinifu, hivyo basi chochote unacho kiona kwenye vidio
hizo, ujue hakipo hapo kwa bahati mbaya, bali kimedhamiriwa kiwepo hapo.
Kwanini
basi Freemason wanaficha mambo yao kweupe hadharani?
Utaona
kwamba Illuminanti na freemason na asasi zingine za siri na zile za kishetani
hawakatai juu ya kuwepo kwa MUNGU MMOJA, isipokuwa wameona kuna ambaye
anastahiki haki na sifa hiyo zaidi ya MUNGU MMOJA (Najilinda kwa Allah kutokana
na hayo) naye ni shetani, na hii ndiyo maana ya nambari 101 au 11 kama nilivyo
zungumzia kwenye posti hii http://salimmsangi.blogspot.com/p/blog-page.html
hivyo basi alama hizo za kishetani wanaamini
zikitumiwa ipasavyo na haswa kinacho lengwa ni ubongo wa nyuma, inakuwa ni
rahisi sana kurubuni umma kuanza kufuata na kushabikia na hatimaye kukubali
vitu hivyo kuwa ni vitu vya kawaida kwenye kijamii.
Illuminanti
wanapo weka alama hizi kwenye vyombo vya habari wanavyo miliki, makampuni,
mashirika, filamu na muziki ni kumkashifu Mungu, lakini zaidi wanawaambia
walimwengu kwamba wao ni ‘mungu’ kwamba wanaweza kufanya lolote. Kokote vyovyote
na asiseme yeyote chochote.
Kwamba shetani yupo pamoja na wao, na anawasaidia
wao kwa kila hali. Lakini
zaidi, Illuminanati wanapo tandaza alama zao za kishetani kwa kila mtu kuona,
huwa na malengo mengine mabaya, Illuminanti wanafahamu kuwa ulimwengu wote
umeumbwa kwenye misingi ya nishati (energy) nishati hizi zimegawanyika katika
makundi makuu mawili, hasi na chanya, lakini zaidi wanafahamu ni kwa namna gani
wanaweza kuzichezea hizo nishati kwa manufaa yao binafsi, lakini pia dhidi ya
umma.
Elimu
hii ni moja ya elimu zao za siri zinazo fahamika kwa wateule wachache. Ili wao
waendelee kuwa na nguvu, na ili waendelee kusimama dhidi ya umma, nishati hasi
lazima zitiririke kwa wingi kwenye uso wa dunia, utaona basi majengo yanayo
jengwa sasa na aina nyingine za miundo mbinu zinabeba maumbile mahususi ambayo
malengo yake ni kutiririsha ‘nishati hasi’ dhidi ya umma, mauajia yanayo
shabikiwa kote duniani, maasi na maovu mengine kupitia vyombo vya habari na
michezo ya kompyuta, yote ni mahususi kwa ajili ya kufungua milango hasi ya
nishati dhidi ya umma, ili wao waendelee kuwa na nguvu dhidi ya nguvu chanya
ambazo zinazalishwa na walimwengu wengine wanao ishi kwa kufuata njia sahihi ya
maisha iliyo elekezwa na MUUMBA mwenyewe.
Elimu
hii mahususi imekusanywa na illuminanti kutoka kizazi hadi kizazi kwa
kushirikiana na mashetani, wanafahamu njia za nishati zote mbili kwenye uso wa
dunia, na jinsi ya kuzitumia, wanafahamu ni maumbo gani yakitumiwa na
yakitumiwa vipi yataleta madhara au tija gani kwa umma, wanafahamu vitu kama ‘star
gate’, elimu maalum ya nambari na mengine mengi ya kucheza na fikra za watu kwa
kutumia nishati hizi.
HII NI RAMANI KATIKA MOJA YA MAENEO YA WASHGTON DC, UKITAZAMA VIZURI NA KULINGANISHA NUKTA ZA MAJENGO KADHAA YA SERIKALI UNAPATA PICHA YA BUNDI, NA PIA PYRAMID NA HATA NYOTA YENYE NCHA TANO!!!!!!!!!!!!!!!!
Lakini
pia Illuminanti wanapo weka alama hizi katika kona mbalimbali, kama vile kwenye
vituo vya luninga, kwenye mashirika, majumba ya serikali, siku maalum katika
mwaka na kwengineko, wanamaanisha kukuambia kuwa wao ndiyo wanao miliki maisha
yako na hatma yako, wanakuambia kuwa wao ndiyo watawala, wanatazama na kuona
kila kitu, lakini yote hayo si kweli ila wanajitahidi wawe kwenye mamlaka kiasi
kwamba mtu akipiga chafya wajue fulani mahala fulani kwenye nyumba fulani
kapiga chafya, huko ndipo wanapo taka kwenda ...
LAKINI NI MIMI NA WEWE NDIYO
TUTAKAO AMUA KUWA WAO WAFANIKIWE AMA LA, TUPO WENGI NA WAPO WACHACHE NA TAARIFA
KAMA HIZI ZINALENGA KUKUAMBAI KUWA CHUKUA MAMLAKA YA MAISHA YAKO MWENYEWE,
SIMAMA DHIDI YA NEW WORLD ORDER ... NAKUMBUKA NILIKUAMBIA KUWA NITAKUAMBIA
MAANA YA ‘RAIN MAN’ SIJASAHAU, TUENDELEE KUWA PAMOJA HAPAHAPA ....
No comments:
Post a Comment