Sauti
ya muziki leo ipo kila mahali, kila kona na uchochoro wa dunia yetu ya leo,
watu wengi mno wanasikiliza muziki leo hii, kwa sababu mbalimbali, lakini ni
watu wachache mno ambao kiuhakika wanafahamu maana ya mashairi, au sababu ya
aina fulani ya mashairi na aina fulani ya ala ya muziki kutumika katika muziki
husika.
Ni wachache mno wanao fahamu athari mbalimbali zinazo oneshwa katika video
za miziki mbalimbali, nalo hili ni jambo la kusikitisha mno.
Kumekuwa na minong’ono kuhusiana na kile kinacho endelea kwenye tasnia ya muziki na nani wanao tawala tasnia hiyo, mienendo mibovu ya wasanii wenyewe, unywaji wa pombe, utumiaji wa dawa za kulevyea, mazingira ya ‘mind control’ kwa wanamuziki na vifo vya ghafla vinavyo achwa maswali yasiyo na majibu.
Miziki
mbalimbali unayo sikiliza redioni na kuitizama kwenye luninga, inabeba maana
mahususi kwenda kwa wasikilizaji wake, kutoka kwenye vyombo vilivyo tumika,
aina ya mashairi yanayo imbwa, vile vinavyo onekana kwenye vidio za miziki hiyo
utakuta kuna jumbe zinazo husu mambo ya ushetani, ngono, mauwaji, uchawi,
ushirikina na mengine ambayo sikio na jicho la mtazamaji huyadharau kwa vile
eidha hawayafahamu au yamekuwa ni mambo ya kawaida kwenye jamii.
Mtiririko
wa posti hizi za ‘muziki’ huenda zikawa na zakushtushwa kwa baadhi na kuwaweka
njia panda wengine, lakini mwisho wa yote , ‘ukweli ndiyo utakao kuwacha huru.’
Kama zilivyo posti zangu zingine na zitakazo kuja, zisome kwa akili huru, tumia
muda wako wa ziada kutafiti juu ya haya ninayo yaandika, na ninajua kuwa mwisho
wa yote hutajutia muda wako.
Hupaswi kuamini haya ninayo andika, unapaswa
kuelewa haya ninayo andika, na ili uelewe unapaswa kuishirikisha akili yako
huru, tuendelee.
Katika
baadhi ya nyimbo, na hapa nazungumzia nyimbo kutoka nchi za magharibi, lakini
pia kutoka nchi za Asia na pia kutoka nyumbani ambazo nazo kila uchao wasanii
wetu wanajitahidi kila wawezalo ku-copy na ku-paste kila wanacho kona toka nchi
za magharibi na Asia.
Utaona
basi, katika nyimbo hizo, kuna baadhi ya maneno au majina ambayo yanatumika
sana, na mara kwa mara katika nyimbo hizo, wakati mwingine ‘maneno’ au ‘majina’
hayo yanafichwa kwenye kiitikio (chorus) au kwenye kile kinacho fahamika kama ‘catch
up’ ya wimbo.
Tuanze
na baadhi ya nyimbo tuone maneno na majina hayo ...
Eminem - kwenye wimbo unao
kwenda kwa jina la ‘RAIN MAN,’ ametumia sana jina hilo RAINMAN
Rihanna – Kwenye wimbo unao kwenda kwa jina la ‘Umbrella’ neno ‘Umbrella
limetumika sana.
Fat Joe
akimshirikisha Lil Wayne – Kwenye wimbo unao kwenda kwa jina la Make it Rain.
Savage – Kwenye wimbo unaokwenda kwa jina la Wild Out, jina la RAIN MAN limejitokeza.
Black
Stone Cherry – Kwenye wimbo
wa Blind Man, jina la RAIN MAN limejitokeza tena.
Jamie
Foxx – kwenye Wimbo Rain Man jina ‘RAIN MAN ‘ limetajwa
maradufu.
The
Game – Kwenye wimbo wa Cali Sunshine, jina RAIN MAN limejitokeza.
Jay Z
akimshirikisha Usher Rymond na Pharrell –
kwenye wimbo ‘ANYTHING’ jina la ‘RAIN MAN’ Limetajwa.
Eminem akimshirikisha Dr. Dree – Kwenye wimbo ‘OLD TIME’S SAKE’ jina ‘RAIN MAN’ limetajwa.
W.A.S.P
– Kwenye wimbo ‘THE BURNING MAN,’ jina RAIN MAN lipo.
BOB
DYLAN – Kwenye wimbo
wa ‘STUCK INSIDE OF MOBILE WITH THE MEMPHIS BLUES AGAIN; Jina ‘RAIN MAN’ Limetajwa
tena.
MIMS – Kwenye wimbo Doctor Doctor, jina ‘RAIN MAN’ Limetajwa
tena.
Eminem – Kwenye wimbo wa RHYMIN’ WORDZ FREE STYLE’
H-Blockx
kwenye wimbo wa ‘RAIN MAN’ jina RAIN MAN’ Limejitokeza.
NAS – Kwenye wimbo ‘DONT BODY YA SELF’ jina ‘RAIN MAN’ limo.
YA BOY- Kwenye wimbo ‘RAIN MAN’ jina ‘RAIN MAN’ na ‘UMBRELLA’ yametajwa.
TANYA
TUCKER – Kwenye wimbo
wa ‘LIZZIE AND THE RAIN MAN’ Jina ‘RAIN MAN’ limejitokeza.
Bob
Dylan – Kwenye wimbo
‘I WANNA BE YOUR LOVER’, jina ‘RAIN MAN’ kama kawa, limo.
Maneno
mengine yanayo tajwa ni ‘ILLUMANATI, SECRET
SOCIETY, NEW WORLD ORDER, NA ORODHA YA
WANAMUZI WANAO TAJA MAJINA NA VITU HIVYO NI KUBWA, SIJUI KUNA HAJA YA KUENDLEA
WAKUU?
Hivyo
basi ukitizama au kusikiliza muziki wa leo, kwa mtu mwenye akili huru, utaoana
kuna kitu ambacho hakipo sawa, ama kitu ambacho hatuambiwi kuhusiana na tasnia
hii ya muziki.
Swali,
ni nani huyu ‘RAIN MAN?’
Tukutane
hapahapa kwenye posti zitakazo fuata.
No comments:
Post a Comment