Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Sunday, August 4, 2013

BALAA LA PICHA ZA NGONO NA KIZAZI CHETU

Kwa sasa filamu za ngono zinafanya kazi nzuri sana katika kile tunachoweza kukifananisha na ‘MIND CONTROL’ kama hufahamu msamiati huo unayo maana gani basi nenda kagoogle, na utapata somo.



 Masaa yote sasa tunafikiria ngono, na kila kazi yeyote ya sanaa inayofanywa haijakamilika kama ndani yake haijakuwa na maudhi ya ngono, mavazi hayajauzika kama hayajabeba dhana ya ngono, ilimradi hakuna kinachoweza kufanyika bila kuwekwa viashiria vya ngono, si kwenye siasa, wala kwenye dini, si kwenye utamaduni wala kwenye sanaa. Ni kana kwamba jamii yetu imegundua kitu kipya.


Hatufikiri wala kutizama hata kuhoji ni namna gani uhuru wetu na haki zetu zinavyo porwa, namna gani sheria zetu zimegeuzwa na kuwa ni fimbo kwa watu fulani na ngao kwa wengine.
Jiulize MWANAUME anaona nini, pale anapo mtazama MWANAMKE? Hakuna ambacho anacho kiona zaidi ya kifaa cha ngono. Jarida la Playboy lilipoanzishwa kwanza lilianza na kuwapandikiza wanaume fikra za ngono kwa msichana aliye jirani naye, ‘Girl Next Door’ sasa hivi wamehamia kwa watoto, na kwenye mitandao ya ngono kumejaa picha za ngono za watoto wadogo, na watoto wetu ambao bado hawajaweza hatakuumba maneno wanayo ‘section’ yao ya ngono kwenye katuni mbalimbali.



Lengo ni moja tu, kuleta fikra na mawazo yetu kwenye kitu kimoja tu, NGONO NA VIUNGO VYETU VYA UZAZI.


Kama kawaida PlayBoy inafanya kazi nzuri kwenye kupunguza idadi ya watu duniani, kwa sababu mawazo na fikra za watu zimehamishwa kutoka kwenye, mahusiano ya muda mrefu kwenye ndoa na familia na kuletwa kwenye mahusiano ya muda mfupi ya Boy Friend na Girl Friend au mbaya zaidi mahusiano ya ngono kama bidhaa. Hivyo dhana nzima ya ngono kama tendo la ndoa imeharibika na badala yake ni ngono kama bidhaa na hapo huwezi kukuta msamiati unao itwa Familia.



Filamu za ngono ni silaha ya maangamizi kwenye ndoa na mtazamo wa tendo la ndoa kwenye jamii. Mpaka kwenye miaka ya 1950 bado jamii mbalimbali duniani ziliona tendo la ndoa ni kitu kitakatifu na hakiwezi kufanyika kokote zaidi ya ndani ya ndoa, kwa wanandoa wa jinsia mbili tofauti. Lakini baada ya bidhaa zenye maudhi ya ngono na filamu zake kuanza kutiririka kwenye mitaa ya majiji mbalimbali duniani na sasa hata vijijini, dhana ile imetoweka kabisa na sasa ubongo wa wanaume wengi haufikiri chochote zaidi ya ngono wakati ule wa wanawake ukitumia ngono kama zana ya kumshinda mwanaume.

Ndoa nyingi zipo njia panda, na nyingi zimevunjika na vijana wengi suala la ndoa ni suala la mwisho kabisa katika orodha ya malengo yao ama halipo kabisa, kutokana na kwamba kazi kama za kina Play Boy na tasnia nzima ya filamu za ngono, inawaambia wanaume wote duniani kwamba, ‘NDANI YA NDOA HAKUNA KILE UNACHO KITAKA’, Wanaume sasa wapo radhi wapige punyeto wakitizama filamu za ngono kuliko kulala na wake zao.

“Play Boy ndiyo jarida la kwanza la kitaifa kuwa-brainwash vijana wa vyuo kuanza kuwaogopa wanawake na kuiogopa ndoa na familia. Play Boy imekuwa ni mbadala wa tendo la ndoa na burudani kwa wanandoa” ( Soft Porn Plays Hardball, uk 47)


Jamii imefika mahala pabaya sana kwa sasa, wanaume kwa wanaume wanaowana, na wakati huohuo wanawake kwa wanawake wanaowana, Yaani wanaume wanafundishwa na kuelekezwa jinsi na namna yakuwa wanawake kupitia kampeni za USHOGA na wanawake nao wanafundinshwa na kuelekezwa jinsi ya kuwa wanaume kupitia kampeni za ‘Gender Senstive’ haki sawa, haki za wanawake na lesbianisim (ushoga kwa wanawake).

Kwa kasi sana kisaikolojia wanaume wa kizazi hiki wanageuzwa kuwa mashoga, mpaka wengine wamefikia kujiita kuwa wao ni mashoga lakini bado ni bikira, yaani mwanaume keshaikubali ile dhana ya yeye kuwa ni shoga ingawa bado hajaingiliwa na mwanaume mwenzake, wengine wanaona hayo ni maumbile kazaliwa hivyo, kwa hiyo hana makosa, siyo kosa lake, hivi ndivyo filamu za ngono, majarida ya ngono, vitabu vya hadithi vilivyo na maudhi ya ngono, filamu za kawaida zilizobeba vionjo vya ngono na ushoga, muziki, mavazi, katuni za watoto zinavyo itengeneze jamii yetu ya sasa kuwa. 



Leo thamani ya mwanamke ipo kwenye kutembea uchi wakati ile ya mwanaume ipo kwenye kufanya ngono holela na wanawake wengi.

Kwa sasa wanaume hawawatizami wanawake kama, Mama, dada au wake, bali kama kifaa cha ngono. Wanaume wengine hawatizami wanaume wenzao kama Baba, kaka au ndugu, lakini kama chombo cha kufanyia liwati.

Wanawake ambao jamii inawaona kama ‘wabaya’ yaani wasio na mvuto, hawaonekani tena kwenye macho ya wanaume; ila kama watajitoa mhanga na kuanza kutembea uchi na kujirahisisha mbele ya wanawake, basi wataonekana na thamani yao kama chombo cha ngono na starehe itaonekana.

Kuna ambaye kwenye jamii ya leo anaweza kutafsiri au kutoa dhana ya MAPENZI ni nini baina ya mke na mume?

Hakuna.

Lakini si hivyo tu, huu ni ushindi kwa Illuminanti, huu ni ushindi kwa maadui zetu, familia zimechanikachanika, vijana hawataki tena mambo ya ndoa, na wachache wanao ingia wanawaogapa wa kupata watoto, na hata wakipata basi wasizidi wawili.

Wanakuambia maisha magumu, wanakuambia mtoto wako lazima umuandalie maisha mazuri, elimu nzuri, ‘future nzuri’ wakiwa zaidi ya wawili hutaweza. Hii ndiyo inayo itwa ‘social engnineer’ jamii inapangwa, inaundwa na kutengenezwa upya. Kuwa na mtoto imekuwa ni sawa na kuwa na bomu mkononi muda wowote litakulipukia.
Lakini sikweli, tangu lini binadamu tumekuwa MUNGU, Mbona tunajitwisha jukumu lisilo letu. Hivi ni kweli kwamba tatizo ni kuwa na watoto wengi???????????????????
Kutokana na juhudi mbalimbali za ‘social engineer’ kama vile haki za watoto, haki za wanawake, haki za mashoga, haki za wanyama, harakati za wanamazingira, jamii yetu haiwezi tena kufikiria tatizo ni nini, tumefanywa vilema wa kufikiri, kuona, kusikia na kuchambua matatizo yetu kama watu huru. Tatizo si kuwa na watu wengi, fanya homework yako mwenyewe na utajua tatizo nini!!!!!!!!!!!!!!



Porn kama zana ya ‘social engineering’ inawageuza wanaume wote kuwa kama mashoga, wanaume hawataki kuowa na wala hawataki watoto. Badala ya kuwa na familia, tunakuwa na ‘ngono’ kuanzia tukuwa watoto kupitia katuni mbalimbali tunazoachiwa kutizama tukiwa wadogo, tukiwa vijana kupitia mitandao mbalimbali ya ngono na majarida yake na mashuleni kwetu siku hizi tunafundishwa elimu ya ngono, mpaka tunaingia makaburini, ubongo wetu ni ngono, ngono, ngono, porno, porno, porno. Ngono sasa ipo kila mahala unapotizama, kila wakati, ni kama tumefungwa minyororo ya ngono, hatukui, hatuendelei, hatusogei. 

Tumekwisha kabisa.


Tatizo ni kubwa, na wewe unaweza kuwa ni sehemu ya tatizo au sehemu ya suluhisho la tatizo. Kwakutizama picha za uchi unakuwa ni sehemu ya tatizo, unatia nguvu kwenye tatizo, unakuwa ni mafuta kwenye moto unao waka, na kinyume chake ni sahihi.
Hii ni biashara kama zilivyo biashara nyingine. Hivi sasa biashara ya kwanza kwa kutengeneza fedha duniani ni ‘HUMAN TRAFICK’. Hii ni kama ilivyo kuwa biashara ya ‘UTUMWA’, Slave Trade, lakini sasa hakuna mashamba ya kulima, mashine na maendeleo yake yamekuwa makubwa hata maofisini watu wanapunguzwa kwa ajili ya mashine, sasa watu wanao safirishwa wanapelekwa wapi? Biashara hii ya kusafirisha watu inakadiriwa kwa mwaka inazalisha faida ya dola za marekani bilioni 32. Hii ni faida, yaani ikimaanisha gharama zote zimeisha ondolewa, hii ni faida tu.


Watu kutoka nchi masikini, watu kutoka kwenye maneno ya vita, waathirika wa dawa za kulevyea na wahanga wengine wanapelekwa wapi?
Wengi kati ya hawa wanao safirishwa hupelekwa kutumikishwa kwenye miradi mipya ya Illuminanti ya ambayo inahusisha kujenga majiji makubwa, makubwa chini ya aridhi. Jiji kama unavyoweza kuliona jiji la Dar es Salaam au Nairobi, yanajengwa chini ya aridhi yakiwa na miundo mbinu mbalimbali, lakini wengi wao huishia kwenye TASNIA YA FILAMU ZA NGONO.



Wengi wao wakati wa kurekodiwa kwenye filamu hizo huwa tayari ni walemavu wa akili kwa ajili ya kumezeeshwa dozi za kutosha za dawa za kulevya au tayari ni mtumwa wa MIND CONTROL.

No comments:

Post a Comment