Tuesday, June 25, 2013

TAHADHARI NA CHANJO!!!!!!!!



Kipi ni kipi kwenye suala la chanjo,?
Madhara ya kuipokea ni makubwa kushinda madhara ya kutoipokea?
Vipi kuhusu magonjwa, je usipo pokea chanjo magonjwa yanayo taja yanaweza kuwa na balaa zaidi kwako kushinda hiyo chanjo yenyewe?
Uwiano baina ya faida na madhara ya chanjo ni muhimu kwa kila ambaye anadhania kufanya chanjo, ili kujiweka katika nafasi iliyo nzuri ya kukubaliana au kutokukubaliana na zoezi zima la chanjo.

Ni muhimu tukafahamu ikiwa magonjwa ya watoto tunao ambiwa kuwa yanahitaji chanjo kama ni kweli yanayo madhara au kama ni makubwa kama ambavyo yanavyo elezwa na watu wanao fanya kampeni za chanjo.

Pia kunatafiti ambazo zinafungiwa macho na watu wanaoa fanya kampeni za chanjo ikiwa chanjo zina madhara makubwa hata kushinda magonjwa ambayo inadai kuwa yanakwenda kutibu.


Mathalani USA madhara ya chanjo yamekuwa makubwa kiasi kwamba zimtumika dola bilioni 1.8 kwa ajili ya kuwalipa wale ambao wamepatwa na madhara kutokana na chanjo. (HRSA Statistics report June 1, 2009, awards paid)

FDA (Food and Drug Administration) imekiri kwamba ripoti 12,000 zinazo pokelewa kila mwaka kwa upande wa madhara ya chanjo, inawakilisha sehemu ndogo sana ya kile ambacho kinachotokea kama madhara ya chanjo hizo.( Reported by KM Severyn, R.Ph.D. in
the Dayton Daily News, May 28, 1993. Ohio Parents for Vaccine Safety, 251 Ridgeway Dr., Dayton, OH 45459) Takeimu hizo pia zimethibitishwa kuwa ndivyo na wachunguzi wa NVIC (National Vaccination Information Center "Investigative Report on the Vaccine Adverse Event Reporting System")



Taarifa ya NVIC imeripoti kuwa ni New York peke yake, ambako ni mmoja kati ya madaktari 40 tu, yaani 2.5% ndiyo wanao ripoti vifo na madhara ya chanjo.

Haina mashaka kabisa kuwa chanjo zinayo madhara, sasa upo tayari kumtoa muhanga mtoto wako? Ingawa hujaambiwa kuwa unamtoa mwanao mhanga, lakini hivyo ndivyo kila wakati unapo mpeleka mwanao kuchukua chanjo.

Statistiki ni moja ya zana inayo tumika kutuonesha kuwa chanjo inafanya kazi...
Majendwali yanakuwa yanatumika kuonesha uwiano baina ya kitu kimoja na kingine kwenye vipindi tofauti vya muda, lakini watu wa chanjo wamekuwa wakitumia majedwali ambayo yanaonesha kuwa magonjwa fulani yamepungua na kunasibisha athari hizo na chanjo zao.
Wakati mwingine magonjwa yalishaanza kutoweka kabla hata ya chanjo kuanza lakini wao watasingizia ni chanjo ndiyo iliyo leta mageuzi hayo.

Njia nyingine wanayo tumia pale wanapo weka ubaoni taarifa zao ni kuzitaja kiujumla wake zaidi, yaani kama vile taarifa za ulimwengu kwa ujumla badala ya nchi au mkoa au kitongoji. Hii hutumika mara nyingi mno, yaani taarifa za kiujumla zinazo tumika huenda hata hazimgusi mtoto wako kwenye nchi, mkoa achilia mbali kitongoji chako, lakini wanatumia ujumla huo kwa ajili ya kukutisha ili uweze kumsalimisha mwanao kwenye kituo cha chanjo.


Mathalani wanaweza kusema watoto “242,000 wanakufa kila mwaka kutokana na utapiamlo”. Hawato kuambia au hawatokupa takwimu za wapi na eneo husika wanazitoa kwa ujumla wake tu.

Unapo ona takwimu za mlipuko wa magonjwa kuwa makini nambari ya idadi inayo tajwa, ni nadra sana kusema ni wangapi katika waliopata magonjwa hayo ya mlipuko kuwa wamepatiwa chanjo. Chanjo haikupatii wewe kinga.

Utakuta kuwa magonjwa au ugonjwa ulishaanza kupungua kabla ya chanjo kutolewa lakini watoa chanjo hawawezi kukiri hilo. Pia watoa chanjo baada tu yakufanya zoezi lao moja kwa moja wanakimbilia kusema kuwa ugonjwa umepungua kutokana na chanjo. Lakini kile ambacho hawakisemi ni kuwa chanjo haiwezi kufanya kazi mpaka baada ya mwaka mmoja ndiyo takwimu zitizamwe ilikuweza kuona kama kweli chanjo zimeleta mabadiliko yoyote.


Bado wapo wale ambao wanao amini kuwa juu ya chanjo. Kawaida huwa ni wakali mno unapo jaribu kuwaelezea ubaya wa chanjo. Imani kuu watu wengi waliyo nayo ni kwamba haya magonjwa ni hatari yanauwa na chanjo ndiyo pekee inayo weza kubadilisha hali hiyo. Mtu yupo tayari mtoto wake apate madhara ya chanjo, lakini asimnyime chanjo kwa vile dakitari kasema, kwa vile imetangazwa kwenye luninga, kwa vile kiongozi filani kasema ...
Kikubwa unapo kutana na mtu wa aina hii kama hana ushahidi wowote wa namna gani chanjo inasaidia kinga ya mwili zaidi ya maneno aliyo msikia fulani kasema, basi jaribu kumuelimisha au achana naye ...


Ukweli hauwezi kuogopa upekuzi pekuzi, kama kweli chanjo zinaleta tija kwa watoto wetu na mama wajawazito, basi madaktari na viongozi wanaogopa nini na kuwatishia watu pale wanapo hoji uhalali wa chanjo?
Dakatari atakuambia mimi ni dr. Na nimekwenda shule miaka kadhaa kusomea hichi kitu so hufahamu chochote wewe...  lakini hili halimafanyi dr kuwa juu ya kila kitu, hapa siyo ishu ya umesomea nini na umesomea miaka mingapi, hapa ni ishu ya fact na ukweli, hii ni ishu ya uhai na kifo ...
Ni watu wangapi kila mwaka wanakufa kutokana na makosa ya madaktari?

Makala moja kwenye ‘Journal of the American Medical Association (JAMA) inasema kuwa madaktari ndani ya USA wanashikilia nafasi ya tatu kwa kuuwa watu, kila mwaka wanauwa watu 225,000 na 106,000 ya vifo hivyo ni kutokana na madhara ya dawa wanazo pewa wagonjwa.
Watu hao wameuwawa na madakatari ambao wamfenya makosa, suala la afya ni biashara kwa sasa, na daktari hakutizami kama mgonjwa, bali mteja ambaye atapenda uende na urudi tena kwake, ukipona atapata wapi pesa?
Takwimu hizo ni za mwaka 2000, kwa sasa ndani ya Marekani madaktari wanashikilia nafasi ya kwanza kwa kuuwa watu, wanauwa watu kushinda hata watu wanao kufa kutokana na kupigwa risasi!

Bado unaamini kuwa ni sawa kwa mtoto wako kupokea chanjo kwa vile Dr. Kasema hivyo?
 ITAENDELEA ...

1 comment:

  1. Binafsi sina mtazamo tofauti na kile ulichoeleza. Nimevutiwa sana na mtu kama wewe. Naogopa tuu kwamba watakuondoa mapema. Na huenda tayari walishakuondoa duniani, maana sijui. Lakini kama ungalipo hai, basi jikabidhi kwa Mungu aliye hai ili akulinde kila utokapo na uiingiapo.

    ReplyDelete