Friday, June 21, 2013

ONYO! CHANJO NI HATARI KWA UHAI WAKO ...

WAPENDWA NAJIHISI NINAKAZI KUBWA MNO YA KUFANYA, KAZI YA KUWAELIMISHA WATANZANIA WENGI, NDUGU ZANGU JUU YA UBAYA NA NJAMA ZA MAADUI ZETU, HAKUNA MWINGINE WA KUIFANYA KAZI HII ILA MIMI, NA NIPO HAPA KWA AJILI HIYO ... NINACHO HITAJI KUTOKA KWENU WASOMAJI WANGU SI KINGINE BALI MUDA WENU MCHACHE KUPITIA POST HIZI NA KUWAARIFU WENGINE JUU YA HILI KWA NJIA YOYOTE ILE INAYO WEZEKANA ...

CHANJO NI HATARI KWA AFYA YAKO ... 

“Chanjo ya pekee iliyo salama, ni chanjo ambayo haijawahi kutumika.” (James R. Shannon, National Institute of Health)

Kabla hasa ya kutizama nini hasa maana ya ‘chanjo’ kwanza hebu tutizame kazi hasa ya chanjo ni nini. Kama kilivyo kitu kingine chochote, kazi yake lazima ifanane na maumbile, muundo au sifa ya kitu chenyewe. Namna ambavyo sifa au maumbile ya hichi tunacho kiita chanjo yalivyo, tunaweza kuziona kwa maneno rahisi kabisa kazi za chanjo ni zipi, na kwenye kazi ya chanjo ndipo palipo na maana halisi ya chanjo. Chanjo imetengenezwa kwaajili 
ya,




i)         Kusafirisha,
ii)        Kujenga, na
iii)       Kubomoa au kudhoofisha.

Sasa tuzitizame kwa ufupi hizi kazi tatu za chanjo,
tukianza na KUSAFIRISHA, kama chombo cha usafirishaji, chanjo zimetengenezwa katika maumbile ambayo yataziwezesha kubeba kitu na kukipitisha katika mwili bila kitu hicho ‘kukaguliwa’ au kuzuiliwa na seli hai za mwili zinazofanya kazi ya ulinzi mwilini. Hivyo kama ni gari basi chanjo zimetengenezwa kupitisha mizigo isiyo faa kwenda ndani ya mwili na kwenda kuidondosha sehemu fulani ya mwili, lakini vifurushi hivyo katika kila tone la chanjo vinafikia mamia ya vifurushi na ndani ya hivyo vifurushi kuna mabilioni ya bidhaa ‘haramu’ zinazo kwenda kusambaza ndani ya mwili.

KUJENGA, tunapoitazama kazi hii, wengi huamini kuwa kazi ya chanjo ni kujenga mfumo bora wa ulinzi na kuupatia mwili afya kwa kusaidia kuzuia mashambulizi ya baadaye ya virusi ndani ya mwili. Na hili ndilo tunalolisikia kila wakati wanapo fanya kampeni za watu kwenda kuchukua chanjo, wanasisitiza ni kwa ajili ya kuzuia mashambulizi ya baadaye ya aina fulani ya virusi au magonjwa. Lakini kinyume chake ndiyo sahihi kama tuakavyo ona.

KUBOMOA au KUDHOOFISHA, eidha kwa kuuwa virusi, seli au kudhoofisha aina maalum ya kazi fulani ndani ya mwili.


Kwenye wovuti wa United State Geological Survey, tunakutana na tafiti zilizokuwa zikifanywa na kitengo hicho kwenye miaka ya 78 mpaka 80, tafiti hizo zilielezea kuhusiana na ongezeko kubwa la farasi pori, wovuti huo au tafiti hizo zilielezea kuwa farasi pori hao waliongezeka kwa kasi ya asilimia 18 -25 kwa mwaka. Wovuti huo ulidai kuwa ongezeko hilo lingeathiri mazingira na ukuaji wa wanyama pori wengine. Sheria ya Marekani ya mwaka 1971 ihusiayo mambo ya wanyama wanao zagaa – The Wild Free Roaming Horses and Burros Act of 1971 – sheria hii iliitaka The US Bereau of Land Management (BLM) na USDA Forest Services kusimamia ongezeko hili la farasi ili kuzuia na kusimamia usawa wa kimazingira. Katika kuhakikisha usalama wa aridhi, wa farasi wenyewe na wanyama pori wengine, tafiti zikapendekeza zoezi la kufanyiwa UGUMBA kwa wanyama hao.

Hivyo kutoka mwaka1978 mpaka kwenye miaka ya 80 BML ikasimamia tafiti mbalimbali ambazo malengo na maono yake makubwa yalikuwa ni kutengeneza CHEMOSTERELANT, hii ni aina ya kemikali ambayo malengo yake ni kupunguza idadi ya wanyama au kuwamaliza kabisa kwa kuwafanya wagumba, au kuwanyima uwezo wa kuzaliana. Ingawa njia hii ilifanikiwa kupunguza uzaaji ‘ovyo’ wa farasi wa porini lakini ilikuwa na mapungufu kadha wa kadha na hivyo waliachana nayo.

Lakini kazi haikuishia hapo, watafiti kutoka National Park Service na Assateague Island National Seashore wakahamia kwenye vitu ambavyo vinaweza kuzuia moja kwa moja yai la kike kukutana na mbegu za kiume, vitu hivyo ambavyo vilionekana kufanikiwa kwa viumbe kama mbwa, panya na wanyama wengine. Mbinu hii mpya ambayo ilijumuisha Porcine zona oellucid (PZP) ilifanikiwa sana kwa farasi pori hao tangu walipoanza kuitumia mwaka 1988 na ilipofika mwaka 1994, ukuaji wa ongezeko la farasi pori ulianza kupungua na kwenda sambamba na idadi ambayo ‘mtaalam’ binadamu aliitaka. (http://www.fort.usgs.gov/wildhorsepopulations/contraception.asp)
Tutizame ni vipi PZP inavyo fanya kazi katika zoezi hili la kusababisha ugumba kwa wanyama. PZP inapo ingizwa kwa mnyama husika, moja kwa moja inahesabika kama kitu geni ndani ya mwili, kwa vile hii imelengwa kwenda kufanya kazi yake kwenye eneo ambalo mbegu ya kiume itakutana na yai la kike, mnyama aliyepatiwa aina hii ya chanjo, ajenti wa PZP wanasababishwa kuzalishwa kwa ANTIBODY ambazo zitakwenda kujishikiza kwenye uso au ukuta wa yai ambapo hutoa aina fulani za kemikali zinazo wezesha mbegu za kiume kutambua sehemu yai lilipo, antibodi hizo huzuia ufanyaji kazi wa vikemikali hivyo kutoka kwenye yai na hivyo zoezi zima la kuungana kwa yai na mbegu ya kiume linashindikana, na hivyo hakuna ujauzito, hakuna kushika mimba.
Ovari kutoka kwenye nguruwe wa kufugwa (hukusanywa kutoka kwenye machinjio ya nguruwe) zinakatwa katwa katika vijipande vidogo, vidogo kisha huchujwa na kupatikana PZP, farasi anapochomwa hii kama chanjo, moja kwa moja mfumo wa ulinzi unazalisha antibodi ambazo zitakwenda kusababisha ugumba, endapo zoezi hili litafanyika kwa miaka minne mfululizo kwa mara moja kila mwaka, inatosha kutengeneza tatizo la ugumba la kudumu, yaani kiumbe husika hatozaa tena.
“Heyi, mbona mada inahusu kupunguza idadi ya watu kwa asilimia tisini, farasi wanahusika vipi?”
Tulia wewe, ngoja kidogo tutafika huko, unaonaje nikikuambia aina hiyo ya chanjo ya PZP kwa farasi ipo kama hiyo, hiyo kwa ajili yako wewe msomaji wa BLOG HII?”
“Unasema kweli?”
“Ndiyo maana nimekuambia tulia ...”
Unaweza kubadilisha neno FARASI na kuweka BINADAM katika maelezo ya hapo juu, lakini kama inakuwa vigumu kukubaliana na hilo, nenda kwenye mtandao na andika ‘HUMAN STERILIZATION’, lakini kama na hili unadhani litachukua muda wako mwingi, basi tuendelee kufunua kurasa za blog.
Machi 10, 2011, kilichapishwa kile ambacho kinaelezea ni namna gani zoezi hilo la farasi kuwa wagumba limefanikiwa kwa binadamu pia. Chapisho hilo lilikuwa na kichwa cha habari ‘LONIDAMINE ANALOGUES FOR FERTILITY MANAGEMENT’, lilielezea kuwa mpango wa kudhibiti uzazi unahusisha kumpatia muhusika dozi moja au zaidi ya mchanganyiko ambao utamsababishia muhusika kupata ugumba. Pia inaweza kutolewa kwa ajili ya kumaliza ufanyaji wa kazi wa SERTOL CELL ambazo hizi hufanya kazi ya kuzinawirisha mbegu za kiume iliziweze kuwa na afya ya kurutubisha yai. Pia kuzuia kuzalishwa kwa mbegu za kiume kwa muhusika, kupunguza uzito wa korodani ambao ni muhimu katika kuzalisha mbegu, kupunguza uzito wa ovari kwa mwanamke, kumaliza kabisa ufanyaji kazi wa ovari kwa mwanamke, kusababisha ugumba usiotibika kwa muhusika.
Kumbuka tumeshahama kutoka kwa farasi na aya hiyo hapo juu haimzungumzii farasi, bali mtu, mwanamke au mwanaume. Chapisho hilo kutoka kwa watafiti BML limetaja kuwa taarifa hiyo ni mwendelezo wa taarifa zilizo tangulia kuhusiana na somo husika, na likataja nukuu rejea za taarifa zilizo tangulia. Aya ya pili ya chapisho hilo likazungumzia uhusikaji wa moja kwa moja wa serikali ya Marekani katika kufanikisha tafiti hizo, hivyo kwa maneno mengine tafiti hizo ziko sawa kisheria na zinayo baraka za serikali.
Aya ya nne kwenye chapisho hilo inasema kuwa,
Uzuiaji wa mimba zisizo tarajiwa kwa wote, wanyama na binadamu, ni jambo linalo zishughulisha zote, nchi zinazo endelea na zile zilizo endelea. Bidhaa mbalimbali na njia zimekuwa zikipendekezwa na kutumika kwa ajili ya kuzuia mimba zisizo tarajiwa. Baadhi ya bidhaa na mbinu hizo ni, upasuaji unaohusisha kufunga au kukata mirija ya uzazi kwa mwanamke, matumizi ya kondomu, vidonge vya uzazi wa mpango, vipandikizi vinavyo zuia au kucheleweshwa kutolewa kwa homoni zinazo andaa yai kwa ajili ya urutubishwaji ...” (story of vaccination)

Aya ya 231 kwenye chapisho hilo inasema kuwa UGUMBA ulifanikiwa kwa 100% kwa panya saba wa kiume ambao walijaribiwa na kuonekana kuwa siyo wagumba, na walipo patiwa tone moja la chanjo, liliwasababishia ugumba wiki tatu tu baada ya kupata tone hilo la chanjo. Jaribio hilo likafanyika kwa wanyama wengine nane na matokeo yake yalikuwa ni 100% kama yale yaliyo tangulia.

Kijitabu cha kimasoni kinachoitwa “In Gold and Sky Blue” cha mwaka 1992 kinasema hivi,
“Freemasons ndiyo watu wa kwanza na washangiliaji wa chanjo”.( In Gold and Sky Blue" Turku, 1992, Uk. 25)
 Alikuwa ni mwanafisikia wa kimasoni bwana Edward Jenner, ambaye mwaka 1796 alianza kulipa nguvu suala la kinga kwa kutumia chanjo, jambo ambalo Freemasons wanajivunia
Dr. Viera Scheibner wa Australia, mtaalam anafahamika kwa ujuzi wake kutokana na mambo ya chanjo, aligundua kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya chanjo mbalimbali zinazofanyika na kuwepo kwa maradhi ya diphtheria, whooping cough, TB ambayo kwa sasa yamethibitishwa kisayansi kuwa ni kweli. Na pia utafiti wake huo umegundua kuwa watoto wengi wamekuwa vilema wa maisha kutokana na chanjo hizo. Anasema:
 ‘Hakuna ushahidi wowote kwamba chanjo zinayo uwezo wa kuzuia maradhi yoyote, ila kinyume chake kunayo ushahidi wa kutosha kuwa chanjo zinayo madhara makubwa (Mark Sircus Ac., OMD ‘Cry of the Heart’ - Stop Hurting the Children -)
Watoto wengi wamepata maradhi ya Autistic mara baada ya kupokea chanjo hiyo. Madaktari wasio werevu na wenye kufuata mkumbo pamoja na viongozi wa kisiasa wamekuwa wakisambaza habari zisizo sahihi kuwa chanjo hazina madhara. Ukweli ni kuwa chanjo imesababisha vifo vingi na ulemavu mkubwa kwa walipa kodi.
Makampuni ambayo yanatengeneza na kuzalisha dawa zinazotumika kwa chanjo hizo wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Karibia asilimia 80 ya dawa zote za chanjo zinatengenezwa katika maabara zinazotawaliwa na kuongozwa na familia ya kimasoni ya Rockefeller
Bill & Melinda Gates Foundation imewapatia wanasayansi kutoka nchi 22 kila mmoja  dola za kimarekani 100,000 kwa ajili ya kufanya utafiti wa kuweza kumtengeneza mbu ambaye atafanya kazi ya kuwadunga binaadam chanjo. Hili linakuja kwa sababu kumekuwa na muumko mkubwa wa watu kupinga chanjo hizi, hivyo mbu huyu wa kimaabara atakapo kudunga na sindano yake ni kuwa anakupatia matone ya chanjo bila wewe kujua, halafu huyo anaondoka zake. Jamaa wamedhamiria lazima wakuondoe kwa bei yoyote ile, hivyo kaa chonjo baba, kwani ndiyo kwanza kunapambazuka.
Wanasema ukitaka kula rushwa basi tengeneza chombo cha kuzuia rushwa, Ukitaka kuuza dawa za kulevyea tengeneza chombo cha kuzuia dawa za kulevyea, ukitaka kusambaza UKIMWI tengeneza chombo cha kupambana na Ukimwi na ukitaka kueneza Polio tengeneza chombo cha kuzuia Polio, na safari hii chombo hicho ni chanjo.
Februari 14, 1999, London Telegraph lilikuwa na habari hii:
“Kampeni kubwa ya chanjo ya miaka ya 50 na 60 zinaweza kusababisha mamia ya vifo kila mwaka kwa sababu ya virusi vinavyo sababisha saratani kuwemo ndani ya chanjo hizo za mwanzo kabisa kwa ajili ya polio (virusi walichanganywa maksudi ndani ya chanjo ) kutoka kwa wanasayansi virusi hao wanajulikana kama  SV40, virusi hao wanatolewa kwenye nyani walio kufa ambao seli kutoka kwenye vibofu vya nyani hao zilitumiwa katika utengenezaji wa chanjo. Madaktari wanaamini kuwa makumi milioni ya watu walichomwa chanjo hizo kabla ya virusi hao ‘hawajagundulika’ na ‘kutolewa’ mwaka 1963.”
“Kwa sasa utafiti unaonesha madhara ya SV40 yanatisha, kwamba virusi hao kutoka kwa nyani waliokufa wanasababisha aina tofauti za maradhi ya saratani ... aina hii ya virusi hawa wanao sababisha  saratani vinaweza kusafirishwa kutoka kwa wazazi kwenda kwa mwana”
Chanjo ya Polio iliandaliwa kwenye miaka ya 1940, kutoka kwenye figo za nguruwe walio kufa na nyani …  Chanjo hii iliyo tiwa virusi vilivyo hai ilijaribiwa maabara na ilikutwa na virusi 149 vilivyo hai pamoja na bakteria. Virusi waliopatikana ni pamoja na SV40 ambao pia wanapatikana kwenye seli zilizo athiriwa na saratani. 

Kati ya mengi chanjo hizo zinaweza kusababisha homa ya matumbo, maradhi ambayo yanasababisha mfumo wa ulinzi kuzishambulia seli hai za mwili kama wavamizi, kifupi hapa mwili wako unajimaliza wenyewe (autoimmune diseases). Type 1 diabetes, au kisukari cha 1 ni hii huwa ni kwa watoto nalo hutokana na hali ya mfumo wa ulinzi kuzishambulia seli  za insulini zinazo zalishwa kwenye kongosho au utasema hili huletwa na (autoimmune, au huu ni moja ya ugonjwa wa autiimmune unao patikana katika chanjo hizo). Ugonjwa wa matatizo ya mifupa kwa watoto ( rheumatoid arthritis).

Marekani kitengo cha Center for Disease Control (CDC) kiliripoti kuwa kutoka mwaka 1973 mpaka 1983, asilimia themanini na saba (87%) ya wagonjwa wa polio walipata ugonjwa huo kutoka kwenye chanjo za polio zenyewe ambazo watu hao walichomwa na kutoka mwaka 1980 mpaka 1983 chanjo za polio kwa asilimia mia moja (100%) zilisababisha matokeo yote ya maradhi ya polio yaliyo tokea nchini humo.


“Mtoto wako anapo chomwa chanjo ya Polio huwezi kulala kwa vizuri kwa wiki mbili mpaka tatu” 

1 comment:

  1. These are in fact impressive ideas in about blogging.
    You have touched some fastidious points here. Any way keep up
    wrinting.

    Feel free to visit my web site :: Louis Vuitton
    Discount [http://thorstromphotography.com]

    ReplyDelete