Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Wednesday, May 1, 2013

WAO NI AKINA NANI?


FREEMASON NI AKINA NANI?
Swali hili limekuwa likiulizwa na mimi binfsi mara kadha tangu na baada ya kuanza kuchapisha makala zangu kwenye gazeti la Mtanzani, nimekuwa nikiulizwa swali hili. Ni swali ambalo muulizaji hulidhani ni jepesi tu na lenye majibu ya haraka haraka, lakini ukweli ni tofauti kabisa.

Kwanza kubaliana na mimi kuwa tunao freemason wa aina mbili kote duaniani. Kuna jumla ya wanamasonia wanao karibia milioni sita kote duniani, ambao kama nilivyo sema tunaweza kuwagawa katika makundi mawili tu.
 Kundi la Kwanza ni Freemason wanao onekana (Visible Freemason)
 Kundi la Pili ni Freemason wasio onekana  (Invisible Freemason)

Asilimia tisini na tani mpaka tisini na nane (95-98%) ya freemason wote duniani wapo kwenye kundi la pili 'Visible Freemason' na Asilimia tano mpaka mbili (2%) ya freemason wote ni Invisible freemason.

Hivyo basi mpaka utakapo yaelewa makundi haya mawili ya kimasonia ndipo utakapo weza kuja na tafsiri sahihi au definition ya freemason.



Definition au tafsri inayotumika kwa sasa kuhusiana na freemason sehemu mbalimbali duniani imeegemea kwenye kundi la kwanza la Visible Freemason. Tafsiri hiyo ni sahihi kabisa lakini tafsiri hiyo siyo ukweli wote kuhusiana na freemason.

Tafsiri nyingi kuhusiana na freemason zinawataja kama (1) kikundi au taasisi au jumuiya (2) Ambayo asili yake ni kutoka kwa wajenzi wa zama za kati Ulaya (4) Ambayo sasa inawakaribisha wanachama ambao hawana taaluma ya ujenzi kujiunga (5) Aambayo inajihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii.

Hayo kwa uchache utayakuta kwenye tafsiri nyingi za sasa kuhusiana na freemason, lakini kama nilivyo sema huo siyo ukweli wote kuhusiana na freemason.

Ukitaka kuwafahamu freemason vyema, watizame kama mfano wa jengo zuri lililo nakshiwa vizuri. Jengo linapokamilika kujengwa, hufatiwa na kupakwa rangi na kutiwa nakshi mbalimbali. Visible Freemason ni kama nakshi juu ya jengo, ni kama mauwa mazuri kwenye ukuta wa jengo, halafu Invisible Freemason ndiyo haswa jengo lenyewe. Hivyo ni wazi utafanya makosa makubwa ya kimsingi utakapo litafsiri jengo kwa mujibu wa mauwa yaliyo chorwa juu ya ukuta wake, ni lazima tukwangue mauwa yale, rangi yenyewe, halafu ndipo tutakapo kuta jengo lenyewe limejengwa na kitu gani, juu ya kitu gani na muhimu kabisa kwa madhumuni gani.

Hivyo basi Visible Freemason wanatumika kama ngao dhidi ya Invisible Freemason, lengo na kazi yao ni kuyafinika yale ambayo yanafanywa na Invisible Freemason.



Jesse Jackson, huyu ni mfano mzuri wa Visible Freemason



Nadhani huyu sote tunamjua, Mtanzania, freemason ambaye naye anawakilisha kundi la VISIBLE FREEMASON.

 

Mazzini na Mwenzake Pike vinara wawili katika ulimwengu wa kimasonia, hawa ni Invisible freemason. Pike na mwenzake Mazzin wanatajwa katika maandishi mengi kuwa ndiyo waandishi wa mapinduzi makubwa Ulaya pamoja na vita vya I na II vya dunia na pia vita vya III vya dunia vinavyo andaliwa hivi sasa.

Hivyo basi wakati visible freemason wakiwaficha ngugu zao Invisible freemason kwa kuchangia madawati, vifaa vya hosipitali, miundo mbinu na kazi mbalimbali za kijamii, kaka zao Invisible freemason nyuma ya mapazia ya kiza kwenye mahekalu ya kimasonia wanapanga na kutekeleza njama za kusimamisha utawala wa kishetani juu wa wanadamu wote.


Jumuiya ya kimasonia inayo madaraja 33 au 33 degrees, lakini asilimia 98 ya freemason wote duania hawavuki daraja la 3 ambayo pia ni maarufu kama blue degrees. N a wengi kati yao hawa asilimia 98 hawafahamu kabisa juu ya kuwepo kwa Invisible freemasoni.

“Umasonia kama zilivyo dini zingine zote … unaficha siri zake isipokuwa kwa wateule, wajuzi na wenye hekima na inatumia maelezo ya uwongo ya nembo na alama zake kuwapotosha wale ambao wanaostahiki kupotoshwa ili kuficha ukweli, ambao ni nuru na (kutumia maelezo hayo) tunawaweka mbali na nuru hiyo” (Albet Pike, Morals and Dogma, uk. 104-5, 3rd Degree)


Pike hapi kaweka nukta moja ya msingi kuwa Umasonia ni dini, ni dini ya nini, nitalijibu swali hilo baadaye kwa urefu wake, ila ni dini ya kishetani kwa kifupi. Freemason kama jengo la shule lengo lake ni kuuficha ukweli Fulani kwa watu Fulani, ambao hawa ni lile kundi la freemason wanao fahamika, ambao wao ni kama mauwa mazuri juu ya ukuta usio fahamika asili yake ni nini. Wateule wachache kama alivyo sema Pike ndiyo makhususi siri hizo na mambo yake ya maajabu wanafunuliwa wanapo yafikia madaraja ya juu kabisa.
Mathalani mwana masonia ambaye anaona kuwa dini yake labda Ukristo au Uislamu ndiyo sahihi na hawezi kuziacha basi huyu atabakizwa katika ile sehemu ya jumuiya inayoonekana, huyu atakuwa ni mauwa kwenye jengo la kimasoni, huyu atakuwa ni yule freemason anayo julikana na wanajamii na wala hafichi umasonia wake, na wapo wengi hawa tunawaona kila mahala. Huyu hatofanikiwa kuufahamu ukweli labda autafute mwenyewe binafsi lakini si ndani ya hekalu la kimasoni, huyu ni katika wale ambao Pike anasema wanastahiki kupotoshwa. Lakini mtu huyu atajihisi anafahamu kuwa anaujua ukweli kumbe la hasha, sivyo hivyo.
Utakumbuka Milton Copper kwenye kitabu chake 'BEHOLD A PALE HORSE'  ametuambia kuwa daraja la 33 limegawanyika sehemu mbili, hivyo mtu huyu anaweza kafikishwa mpaka daraja 33 lakini akawa ni miongoni mwa wale wanaofaa kupotoshwa, hivyo hatoujua ukweli daima.

Hivyo freemason ni jumuiya ambayo inawagawanya wanachama wake katika makundi mawili, kundi la wale wanao faa kuambiwa kila kitu na wale ambao wanastahiki kupotezwa, hawafai kuambiwa kila kitu.

Freemason kutokana na kazi zao kuna mahala utawasikia wakifahamika kama BABILON BROTHERHOOD, BIG BROTHER, AU ILLUMINANTI, lakini majina haya siyo ya kwao, majina haya yanakuja kutokana na aina fulani fulani za shughuli zao chafu za kimataifa walizo pata kuzifanikisha au wanazo lenga kuzifanikisha na shughuli hizo asili yake ni za kale zaidi kuliko freemason yenyewe.


Freemason imekuwa ikitajwa kwenye maduara ya majina hayo hapo juu na mfano wa hayo si kwavile wao ni 'WACHEZAJI MAHIRI' kwenye mchezo mzima, bali zaidi kutokana na ufahamu finyu wa asili ya matukio hayo na freemaso wenyewe. Freemason katika hili duara la matukio makubwa na mazito ya kidunia kitu kidogo mno, au ni sehemu ndogo sana kwenye duara la nyuzi 360.

13 comments:

  1. kaka unaniogopesha unapo sema kuwa freemasonry ni kitu kidogo sana, mbona wao ndiyo wanao tawala dunia, bado sijakuelewa hapo, hebu nieleweshe hapo vyema.

    ReplyDelete
  2. Kaka hata mimi ninawali kama hilo hilo hapo juu naomba muongozo wako tafadhali

    ReplyDelete
  3. kaka eti nikitaka kujiunga na hawa jamaa nifanye nini?

    ReplyDelete
  4. Kaka salim kwanza nikupe hongera kwa hili, ningependa kujua eti nikweli freemasonry wanakula nyama za watu? Na je ukitaka kujiunga ni lazima utoe kafara ndugu yako au watu wako wa karibu.

    ReplyDelete
  5. Kwa hiyo kaka unamaanisha kuwa Ande chande yeye ni visible freemasonry na hafahamu chochote juu ya invisible freemasonry?

    ReplyDelete
  6. Eti kaka je kANUMBA ALIKUWA NI FREEMASONRY na wao ndiyo walio muuwa? Vipi kuhusu Sharo Millionea na je na yeye alikuwa freemasonry na wao ndiyo walio muuwa? Na Diamond Je ni freemasonry, Je Mzee Ali Yusuph pia ni freemasonry?

    ReplyDelete
  7. Habari yako ndugu msomaji,
    Ukweli wala sikuogopeshi, ispokuwa huo ndiyo ukweli halisi, kuna msemo maarufu wa kiswahili usemao 'waona vuma baharini papa lakini ...'
    Freemasonry ni sehemu ndogo sana kwenye mtandao huu mpana wa Babilon brotherhood, lakini inayo nafasi muhimu na ya kipekee kwenye mtandao wenyewe.

    Nafasi ya freemasonry kwenye mtandao huu ni sawa na nafasi ya tofali katika jengo, kila tofali kwenye nafasi yake ndipo yanapo kamilisha jengo, na ndivyo walivyo freemasonry.

    Mtandao huu ni mpana unahusisha tasisi za kitaifa na kimataifa, mashirika ya umma na yale ya watu binafsi, makampuni, familia, watu binafsi na mengine na mengine.

    Lakini wote hao, muundo wa mtandao ni kama Jengo la Piramidi, ni lipana mno chini, na jembamba kadiri linavyo kwenda juu,hivyo kuna tasisi au mashirika, au makampuni, au familia au watu binafsi kwenye mtandao huu ambao nafasi yao ni chini kabisa, wengine wapo katikati na wengine juu kileleni.

    Visible freemasonry ni miongoni mwa wale waliopo chini kabisa, wakati ndugu zao Invisible freemasonry wakiwa juu kileleni.

    ReplyDelete
  8. Itakuwa vyema kabla ya kuulizwa swali ukajitambulisha hata jina lako, nadhani aliyeuliza swali hapo juu alikuwa akimaanisha kuwa *ninaswali* na kama hivyo ndivyo, basi thani nitakuwa nimeshamjibu.

    ReplyDelete
  9. Ndugu yangu uliye uliza ni namna gani unaweza kujiunga na hawa freemasonry, ningependa uniulize tena swali hilo baada ya mimi kutupia post zingine kadhaa kuhusiana na freemasonry, halafu tuone kama bado utakuwa na hamu ya kujiunga nao ama la, hivyo nitupie tena hilo swali baada ya wiki mbili hivi kutoka leo.

    ReplyDelete
  10. Ndugu uliye uliza swali ikiwa kama moja ya masharti ni kuwatoa kafara na kama wanakula nyama za watu, ningependa kukujibu hivi,

    Karibuni hivi nitaweka post ambayo ndani yake itaelezea tofauti ya Freemasonry na imani nyingine za kiza, sababu watu wengi wanashindwa kutofautisha baina ya yale wanayo yafanya freemasonry na washirikina wengine ...

    ReplyDelete
  11. Ndugu uliye uliza swali kuhusiana na Ande Chande, ningependa kushea na wewe kitu kimoja kuhusiana na freemasonry.

    Kutokana na maelezo ya Albert Pike kwenye kitabu chake maarufu ambacho ni kama muongozo kwa mason wote 'Moral and Dogma' ameutaja umasonia kama dini lakini mahala pengine akawataja 'Visible freeasonry' kama wasiyo stahiki kuambai ukweli.

    Lakini pia freemasonry atakapofikia daraja la 28 kutokana na maelezo ya mwandishi mwingine William Cooper ni kwamba freemasonry ndipo anapoambiwa kuwa yale yote aliyo jifunza ndani ya umasonia kabla ya kufikia daraja hiyo ni uwongo na ayasahau na kuanzia hapo awemakini maana ndiyo mambo yanapoanza. Pia ni katika daraja hilo ndipo freemasonry anapo ambiwa kuwa utabiri uliofanywa na Jacob de Molei, aliyekuwa kiongozi wa Knights Templer kabla hajachomwa moto, iutabiri ule haukutokea bali freemasonry ndiyo walio tekeleza mauwaji ya Papa na Mfalme ili kutimiza maono yaliyo tolewa na Grand Master De Moley.

    Lakini pia Cooper anatuambia kuwa daraja la 32 limegwanyika sehemu mbili kwenye kitabu alicho kiita 'Be Hold the Pale Hourse' kwamba kuna ambao wanafiki daraja la 32 na bado hawajui kitu, au bado hajaaminiwa kupewa fungu za siri hizo nzito, hivyo anapandishwa daraja lakini kama visible freemasonry ambaye hatofunuliwa siri za ndani za mtandao mzima.

    Imenibidi kutoa maelezo hayo marefu ili kuweza kukujibu swali lako hivyo basi kutokana na swali lako inabidi kwanza kujua Chande yupo daraja la ngapi katika madaraj 33 ya freemasonry, lakini juu ya yote huyu ni visible freemasonry, na kazi yao ni kupaka mauwa juu ya ukuta kuficha madhila ya bwana wakubwa, na visible freemasonry ndiyo wanao stahiki kudanganywa kutokana na maelekezo ya kiongozi wao wa zama zote, Albert Pike.

    ReplyDelete
  12. Kuhusiana na hilo la wasanii wabongo kuhusishwa na zahama hili, ningependa munipe muda kidogo, na ndani ya wiki ijayo nadhani nitaweka post juu ya hili, lakini kutokukuweka njia panda ni kwamba hakuna kati yao aliye freemasonry, na vipi nimefikia kwenye hitimisho hilo, tukutane kwenye blog hii hii nitakupatia 'details'

    ReplyDelete
  13. umenigusa sana....tangu mwanzo sikutaka ku coment ila kwa kweli upo vizuri kwenye "quotes"

    ReplyDelete