Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Saturday, May 4, 2013

FREEMASONRY ILIANZIA WAPI Part I





Freemasons ni jumuiya ya kale mno, lakini kabla ya 1717 haikuwa ikifahamika rasmi kama Freemasons, ni kiuhakika FREEMASONRY walikuwa ni waashi ambao walikuwa na utaratibu wao wa namna ya kufanya ujenzi wao, walikuwa huru katika Ulaya ya zama za kati wakiruhusiwa kuzunguka kila mahala kote duniani kama wangeweza, hawakuwa watu ambao wakijihusisha na mambo ya maajabu kama wanavyo fanya Freemasons wa sasa, mpaka pale mafundisho ya kipagani na uchawi kutoka Mashariki ya Kati kupitia kwa Knights Tampler yalipochomokwa kwenye asasi hii ambayo awali haikujua chochote zaidi ya ujenzi.
Hawa wajenzi wa zama za kati ndani ya Ulaya walifahamika kwa jina la kazi yao, yaani masoni au kwa lugha yetu fundi mwashi. Masoni walikuwa na utaratibu maalum wa kulinda siri hizi zinazo endana na kazi yao, walikuwa na mahekalu yao, ambapo humo wanajumuiya walifundisha maajabu na siri za kazi zao za ujenzi, lakini haya hayakufunuliwa kwa mtu baki. Hivyo majengo mbalimbali ya ibada zama hizo, majengo ya kiserikali, makasiri ya kifalme na nyumba za watu binafsi wenye ushawishi wa kiuchumi katika jamii zilijengwa na watu hawa, masoni. Hii ndiyo maana Ulaya ya zama hizo haikunufaika na maarifa haya kwa haki yake kwa vile haikuwa elimu aliyo pewa kila mtu, bali ni kwa watu maalum na walitumia kwa majengo ya watu na vikundi makhususi. Siku zote Freemasons walicho nacho ni cha kwao na ulicho nacho pia wanataka wakichukue, daima wako kinyume na jamii inayo wazunguka, hivyo lolote la kuinufaisha jamii halielezwi kwa wanajamii na wanafanya kila wawezalo kuhakikisha wanajamii hawayapati maarifa hayo. Desturi hii wako nayo mpaka leo hii, kila shida unayo iona duniani au maradhi ujue kuna tiba yake, kuna tiba ya kansa, kuna tiba ukimwi kutaja kwa uchache, kuna suluhisho juu ya tatizo la uchumi, kuna suluhisho juu mmomonyoko wa maadili lakini katu hayatatolewa, kwa sababu wewe unaye soma kitabu hichi ndiye adui yao nambari moja!


Moja ya masalio ya majengo yaliyo jengwa na MASONI wa zama za kati na ambayo pia lilitumika kama ofisi yao.

Masoni hawa wa zama za kati katika mahekalu yao walihifadhi zana zao za kazi, walipumzika humo na pia kula chakula humo. Katika mahekalu hayo wanajumuiya walisimikwa katika madaraja ya kimasoni, zama hizo kulikuwa na madaraja matatu tu, yaani Apprentices, Journeymen na Grandmaster. Mason, hawa walikuwa wakijikusanya kama kikundi cha ushirika ili waweze kupata kazi husika, walitambuana kwa salamu zao za siri na ishara mbalimbali zilizo kuwa hazifahamiki kwa watu wengine.



 Mwaka 1347 mpaka 1351 wakati Ulaya ikipambana na janga la Black Death, mambo mengi yalikwenda mrama, taratibu na mipango mingi iliharibika, shughuli za ujenzi zilipigwa marufuku, MASONI ambao walikuwa na taaluma ya ujenzi nao walikuwa kwenye wakati mgumu.





Alama ya MASONI wa zama za kati Ulaya inayo tambulisha eneo lao au ofisi yao ya kufanyia kazi, hapa ni kabla jumuiya hiyo haijaingiliwa na kuigeuzwa na kufanywa kuwa FREEMASONRY.

Lakini wakati Ulaya inapambana na Black Death, kitu kilicho pelekea mabalaa mengi likiwemo kwa jumuiya mbalimbali kupigwa marufuku kabisa au kunyimwa kufanya kazi katika utaratibu walio uzoea, takribani miaka 70, kabla ya Black Death, sehemu Fulani ya Ulaya ilikumbana na kitimtim kingine ambacho athari yake ilisubiri kwa takribani miaka 70 iliweze kuonekana, athari ya kile kilicho tokea mwaka 1307, sehemu Fulani kwenye jiji la Ufaransa, ilisubiri mpaka balaa la Black Death lilipokuja na fursa mpya ambayo kwayo, freemasonry ya leo ilizaliwa rasmi.

Lakini ni nini kilichotokea mwaka 1307, na kwa nini ilibidi kusubiri kwa takribani miaka sabini kupata fursa ambayo kwayo freemasonry imezaliwa?

Punde tutakifahamu hicho, lakini kwanza tutakuwa hatujatendea haki, tafiti mbalimbali kama tutasimamia hapo kwamba  freemasonry ilizaliwa rasmi mwaka 1717, London Uingereza.

Hapana kama nilivyo sema hapo juu ni kwamba 1717, freemasonry ilikuwa imezaliwa rasmi, lakini si maanishi kuwa kabla ya 1717 hatukuwa na freemasonry.

5 comments:

  1. kaka unaonekana uko vyema tafadhali endelea kutupa vitu

    ReplyDelete
  2. ningependa kujifunza zaidi kuhusiana na ahwa jaamaa je niende wapi?

    ReplyDelete
  3. sehemu inayo fuata itatoka lini kaka salimi, halafu big up sana

    ReplyDelete
  4. thank you guys,
    Kama unapenda kujifunza zaidi kuhusiana na freemasonry tembelea blog hii kila wakati, utapata vitu tele tele hapa

    ReplyDelete
  5. sehemu inayo fuata ipo tayari just soon nitaiweka hapa kwenye blog yetu kila mtu aone.

    ReplyDelete