Wednesday, April 11, 2018

JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? Season Finale, Ep1 (Tunabisha hodi Mlangoni kwa Mwalimu wa Walimu Wetu..



Kwenye mfululizo wa Makala hizi, kwenye season 1 na 2, juhudi kubwa imefanyika kuonesha kwamba, kabla historia tunayo ijua haijaanza kuandikwa palikuwepo na jamii iliyo ishi na iliyo endelea kwenye nyanja zote unazo zijua, kwa maendeleo makubwa ambayo leo kwenye karne ya ishirini na moja, ya sayansi na teknolojia hatuja ‘ota’ kuyafikia!




Maarifa waliyo kuwa nayo, japokuwa ushahidi tulio nao dhidi ya maarifa na elimu yao ni wa vipande vipande, lakini unashangaza na kumuacha kila mmoja na maswali pasina majibu.
Mathalani ni vipi watu wa Maya walikuwa na kalenda makini, sahihi na bora kushinda kalenda tunayo itumia leo karna ya ishirini na moja.

Ni vipi Pyramid la Khufu linabakia kuwa moja ya majengo makubwa, mazito kuwahi kusimamishwa kwenye uso wa dunia, n ahata leo kwa taaluma zote tulizo nazo hatuwezi kusimamisha mfano wake?
Ni kipi kilicho wapelekea watu wa Babilon kutengeneza betri za umeme miaka 4000 iliyopita?

Ni wapi Wagiriki na Waroma wa kale walipata taaluma ya kuwa kuna sayari nyingine Zaidi ya Sartun?

Tunaweza kweli kuikana dhana na Zaidi ukweli wa msingi kwamba, kabla historia haija anza kuandikwa, palikuwa na historia nyingine kubwa kushinda ya kwetu ambayo imefichwa?
Ni vipi mtu utaweza kujibu maswali haya pasina kukubali uwepo wa historia nyingine tofauti na hii ya Mjomba Darwin?

Ni kipi kilicho kuwa kikiwasukuma wanfalsafa wa Kigiriki na watawa wa Brahmin India, kuzungumzia uwezekano wa kwenda kuishi kwenye sayari nyingine? Kumbe hata kwenye hili sisi si wa kwanza?

Je watu wa kale walikuwa na taaluma ya ‘dhahabu’ kuhusiana na usafiri wa angani, hasa kile kinachoitwa, ‘antigravitation’ au ni vipi basi utaelezea ujenzi wa Pyramid na mfano wako ambao ulihusisha ubebaji wa mawe yenye Zaidi ya tani 1000! Ni vipi utaelezea ngano za waungu kama Isis na wengineo walio kuwa wanarukwa angani?

Ni vipi kuhusu taaluma ya taa zinazo waka maelfu ya miaka na hata milele, je ni nishati ipi waliyo itumia, ni wazi ni zaidi ya umeme na hata zaidi ya nyuklia, nadhani dunia ingekuwa wapi leo kama na sisi tungekuwa na nishati hiyo? Je taa inayo waka kwenye kaburi la Kennedy mpaka leo inatumia nishati hiyo, au imechagizwa (inspired) na hadithi ya taa zilizo waka milele?

Vipi kuhusu hadithi za marobotika, tumejua Sophia siyo robotika wa kwanza kuwa na ‘artificial inteligence’ duniani, Plato alikuwa na robotika wake ambaye ilibi amfunge asije kukimbia. Je tumeiga hili kutoka kwenye historia iliyo fichwa kama taa ya kwenye kaburi la Kennedy na kisha kujinadi ‘tumevumbua’?

Mbona taaluma ya kutengeneza na kuendesha ndege imeandikwa vya kutosha na kwa lugha rahisi kwenye historia ya kale, kuliko tunavyo andika historia ya binadam wa Darwin? Ni vipi pawepo na maelezo juu ya ndege na aina zake kama hawakutengeneza na kuzitumia ndege hizo?

Kama binadam wa Darwin ndiyo kwanza yupo kwenye hatua ya juu Zaidi ya kimaendeleo ni nani aliyefanya kazi zile za Sanaa zinazo toa nuru ya kuififisha Sanaa yetu isionekane ni kitu chochote mbele ya kazi hizo za kale za Sanaa?
Ni vipi karne arobaini na tatu zilizopita ‘wanaanga’ wa China waliweza kuuelezea mwezi kwa taarifa ambazo ndiyo kwanza tunazithibitisha leo, na BADO HATUJAWEZA KWENDA MWEZINI.


Kwa kila hali walikuwa wameendelea kivitu kuliko tunavyo weza kusema sisi tumeendelea.
Lakini haikuwa habari ya kona moja ya dunia, na kona nyingine ni giza, hapana, maendeleo hayo yalikuwa kwenye pembe zote za dunia, kila jamii, kwenye kila bara wanazo hadithi za kale zinazo fanana, kuhusiana na ‘golden age.’

Unafaham kuwa ‘mvumbuzi’ wa simu Alexander Graham Bell, baada ya ‘kukivumbua’ kifaa hicho alisema, ‘The old devices have been reinvented’. Yes, ndivyo alivyo sema Bell.

 Lakini mshindi wa ‘Nobel Prize’, kwenye fizikia, ambaye ni mwanasayansi mkubwa wa Uingereza Frederick Soddy naye alisema kuhusiana na taaluma hiyo ya kale, ‘not only have attained our present knowledge, but a power hitherto unmastered by us?

Kanakwamba Bell na Soddy hawajasoma kuhusiana na evolution, ama wamesoma vyanzo vingine vya sayansi na historian a vya kale zaidi, vyinginevyo wasinge kuwa na mawazo hayo.

Tumeona kwenye safari yote hii, tunacho kisaka, si kwamba kimeegemea kwenye taarifa na nyaraka za kale tu, lakini pia kwenye uvumbuzi wa kisayansi wa masalio yenye kuonekana na kushikika!

Ushahidi huo unaongezeka siku hadi siku, kwamba siri zote za sayansi na teknolojia ya leo, vilikuwepo, vilifanyika, vikatumika kale kwenye zama zilizo sahaulika au kwenye ukurasa uliofuta kwenye historia.
Itazame Egypt, miaka 3000 KK, ghafla kutoka kusiko julikana Egypt ile pale, imeendelea, kiuchumi, kiasa, kijamii na hata miundo mbinu yake.

Hakuna jamii inayo endelea ghafla namna hiyo, hatuoni kiunganishi baina ya binadam wa Darwin na Egypt.
Hakuna kipindi cha mpito, labda imeanzia pale, ikafika hapa ndiyo ikasogea pale, hakuna, ghafla tu Egypty inayo mahekalu, Pyramid ambazo mpaka leo hatuwezi kuzijenga, Sanaa ya hali ya juu, mitaa na barabara zilizo pangika, matumizi ya kuandika kwenye karatasi, matumizi ya desimali kwenye hesabu, na matumizi ya sifuri.

 Jamii tayari inayo mgawanyo maalum, wanasiasa, wafanya biashara, wanajeshi, wafanyakazi wa kiserikali. Yote hayo ghafla ndani ya 3000 KK?

Utazame Sumeria, Mesopotamia nazo ndani ya 3000 KK, kama zimeshuka kutoka mbinguni, zote zimekamilika, bila zile hatua za kihistoria za kutoka kwenye hatua moja kwenda nyingine.
Nazca Peru, Uru Iraq ya leo, na miji mingine ya kale tuliyo ipitia kwenye posti zilizo tangulia. Huoni zama za mawe, za chuma au ujima, hakuna, wala humuoni binadam wa Darwin wala nyayo zake kwenye jamii hizo, ni ghafla kama miji hiyo imeshushwa kutoka mbinguni ikiwa  kamilifu.

Lakini ukiacha uwiano wa muda kwa maana ya 3000 KK, kwa jamii hizi pia bado pamoja na umbali na maelfu ya maili yaliyo kuwa yaki zitenganisha jamii hizi, bado zilifanana mambo mengi kana kwamba asili yake zote ni moja tu.
Alama na Michoro

Kote kwenye jamii hizi za kale, alama na ichoro mbalimbali imekuwa inafanana, hadithi ya mungu nyoka, mungu jua, swastika, gharika kuu, waungu wanao ruka kwa ungo na mengine mfano wake, nenda China, Egypt, India, Mexico kote utakutana na hadithi hiyohiyo.

Mfumo wa kuandika
Dunia nzima tukitamza mfumo wa kuandika kwa maana ya tarakimu, herufi na alama, tukirudi nyuma 3000 KK au wakati na baada ya 3000 KK tunakuta kote walifanana, kanakwamba tayari walikuwa na ‘globalization’ aka Utandawazi!

Lugha.
Maneno, matamshi, mizizi ya maneno na majina kwenye jamii hiyo ya kale ni kanakwamba yote yalikuwa na asili moja. Asili ipi, iliyo tokea wapi, lakini sote tunajua haikuanzia 3000 KK!
Ujenzi wa mahekalu na majengo mengine mfano wa Pyramid, ulifanana si kwa muundo tu, lakini pia mali ghafi zilizo tumika, mahesabu ya vipimo na muelekeo wake. Pyramid za Peru na Gaza zote zinazilenga nyota fulani za angani.

Mila na desturi pia zilifanana, mathalani, Egypty, Maya, Incas, Celts kutaja kwa uchache, walivifunga vichwa vya watoto wakiwa wachnga ili kutengeneza fuvu la kicha kuwa kubwa kwa urefu. Mafuvu hayo yapo, kwanini walifanya hivyo, hiyo ni habari nyingine pana. 

Jamii nilizo taja hapo juu waliwafunga maiti wao na kuwapaka vitu na madawa maalum ili wasioze, teknolojia hii hatunayo sisi, lakini tena nukta hizi zinathibitisha kuwa jamii hizo zilikuwa zina muingiliano wa kidunia, leo tunaita globalization.

Tunaitafuta ‘X’, tunaitafuta nukta ya msingi iliyo anzisha yote haya, ambayo tunajua haikuwa mwaka 3000 KK.

Mwanahistoriam mwanajiografia, mwanasayansi, na wana fani zingine wote ukiwauliza ni wapi chemchem ya taaluma aliyo nayo imeanzia, kama hata anzia 3000 KK, basi atakuja kuanzia Egypt, Roma, Ugiriki na mfano wa hao kama ndiyo walimu au waanzilishi wa taaluma husika, lakini swali ambalo linakwepwa kwa makusudi na ambalo halijibiki ni yupi huyo mwalimu wa walimu wetu?

Makala hizi zimeingia season 3 sasa, na kote huko tulikuwa tukimtafuta huyo mwalimu wa walimu wetu na hapa tupo karibu kabisa na mlango ambao ukifunguka, tutaona maajabu ndani ya maajabu na tutakutana uso kwa uso na mwalimu wa walimu wetu.

Mifupa, mirefu kama nyumba na kimo kama bati lake, imekutikana kwenye kingo za mto Amazoni, Amerika ya Kusini. Wataalam wetu wanakadiria binadam mwenye mifupa hiyo, fuvu lake la kichwa linaweza kutosha ndani ya chumba cha mita 1.5 kwa 2.5 na mwenyewe kuwa na urefu wa mita 12! Profesa Carl Frailey, kutoka Ovreland Park, Kansas, anasema binadam huyo anaweza kuwa na uzito wa tani 120! Hii itamfanya kuwa mzito kushinda Tyrannosaurus rex… jinyama dinosari lilikokuwa zito kushinda wote”, alisema. (The Sunday Mail, Brisbane, November 17, 1991)
Masalio haya hayapo kwenye vitabu vya Darwin, lakini haimaanishi kuwa hayopo, au hayajapata kuwapo, kifupi kila cha kale kilicho kusanywa kwenye historia ya kweli kilikuwa ni kikubwa kuliko tunavyo kiona sasa. Si chura wala farasi, siyo ndege wala jongoo, historia yao ya kweli iliyoandikwa kwenye udongo viumbe hao walikuwa wakubwa maradufu kuliko tunavyo waona leo, na pia binadam.

Karibu kwenye historia mpya ya ulimwengu, historia ambayo huenda ndiyo mara ya kwanza unaisoma, au uliisikia, lakini huku isadiki, na wala mimi si kazi yangu kukufanya uisadiki, ila nitakuonesha Ushahidi, wa maandishi na ule wa kushikika, eidha utaelewa, utaamini, au utasadiki hilo ni lako na ubongo wako …..

Guys, Google wamenipa tabu sana, kwa mambo yao hayo ya ‘security’ flow ya blogi imevurigika, hasa kwenye page yetu ya ‘facebook’ hivyo nilikuwa na kazi ya kuihamisha, imenichukua muda, nadhani itanichukua muda zaidi, lakini tunahama ‘blogspot’ wapi tunakwenda soon tutajua ….

Stay tune as always ... tunakaribia kuhitimisha mtanange huu ... Tchaooo


4 comments: