Thursday, April 19, 2018

JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? Season Finale, Ep 2 (Binadam wa kwanza..)



Kwenye tamthilia ya Lost, Eko alipoamua ‘kumpokea’ Bwana, Lock alikuwa amevutika sana akataka kujua ni kwanini Eko kaamua hivyo, na Eko naye alitaka wafuasi kwenye ‘kanisa’ hivyo alikuwa na hamasa kumuelezea Lock, akamuambia, “Nitaanzia mwanzo”, Lock akasikiliza baada ya kitambo akamuambia Eko, “Sikujua kwamba uliposema unaanza, mwanzo ulimaanisha MWANZO, (kitabu cha mwanzo kwenye biblia). Lock  akaondoka zake …..

Na mimi naanzia ‘mwanzo’, lakini haitakuwa mwanzo kama ya Eko msije mkaondoka … ila nitapita kwa nukta moja ama nyingine kwenye kitabu cha biblia pia.

Karibu jamvini tupo darasani na mwalimu kesha fika.


Nukta moja ya msingi ningependa tuifaham kabla hatujaanza darasa letu. Tukiachana na Darwin na wafuasi wake, nadhani sote tuliobakia tunakubaliana juu ya uwepo wa vitu vitatu; 
yaani, Roho, kiwiliwili, na akili. Darwin na watu wake wanakubali viwili tu, yaani Kiwiliwili na akili, roho wanasema haipo.

Kuhusiana na mtanange huo, rudi kwenye posti, iliyokwenda kwa jina la ‘Namtafuta Mungu’, nilielezea kwa kina juu ya hili.
Turudi kwenye nukta ninayo taka kuitambulisha kabla ya kupiga hatua nyingine mbele. Vitu vitatu nilivyo vitaja hapo juu, ingawa viko pamoja lakini vina tofautiana sana kama mchana na usiku. Moja ya vingi vinavyo tofautiana ni lugha.

 Lugha ya akili na lugha ya roho, ni lugha mbili tofauti. Asili ya vitu viwili hivi kama tutakavyo ona punde ni asili mbili tofauti, hivyo tabia na maumbile yao ni tofauti na pia lugha ni tofauti.
Sababu dunia tunayo ishi imetawaliwa na nadharia ya Darwin ambayo inaikataa Roho, lugha nayo tunayo itumia kwa kiasi kikubwa nayo imegemea upande mmoja, ingawa Roho inaifaham vyema lugha ya Akili/kiwiliwili, lakini Akili/Kiwiliwili kinapata tabu sana kuielewa lugha ya Roho na ama haielewi kabisa; yaani ni dunia mbili tofauti.

Mwili/Akili/Kiwiliwili ni ‘Three Dimensional’ (3D) yaani Kimo, Urefu na Upana. Wakati Roho ni ‘Mult Dimensional’. Nikisema mult-didimensional kwa lugha nyepesi namaanisha ni zaidi ya 3D.
Sababu lugha tunayo itumia inaeleweka zadi kwenye 3D, au kwa uwazi zaidi kwenye akili zetu, kuna nukta zingine nitatoa maelezo ya ziada pale ambapo lugha ni ‘mult dimension’ lakini imetoholewa na kuingizwa kwenye 3D.

Katika vitabu vya dini, na hasa nikizungumzia dini kuu 3. Asili ya uumbaji ni moja.
KWAMBA ALIKUWEPO MUNGU NA HAKUKUWA NA CHOCHOTE KINGINE.

Kisha Mungu akaanza kuumba kimoja baada ya kingine.

Na kumbuka aliposema Mola wako kuwaambia Malaika kuwa anakwenda muweka msimamizi/kiongozi kwenye uso wa dunia …(Quran: 38:71)

Katika aya hiyo limetumika neno ‘Khalifa’ ambalo mzizi wake ni ‘Khalafu’ ambayo maana yake kilugha ni kuchukua au kushika nafasi ya fulani baada ya kuondoka kwake.

Mathalani baada ya Mtume (saw) kufariki na Abubakar Sidiq (ra) kushika nafasi yake, jina aliloitwa kama mtawala Abubakar Sidiq (ra) ni Khalifat Rasullullah … ikiwa na maana kuwa yeye sasa ndiyo kaishikilia ile nafasi ya utawala baada ya Mtume.

Hivyo aya hiyo kwenye Quran inatuambia kwamba binadam anakuja kuishika nafasi hiyo, lakini yeye si wakwanza kupewa nafasi hiyo, ila yeye anakuja baada ya aliye kuwa kwenye nafasi hiyo kuondolewa au kuondoka.
Mathalani baada ya Mtume (saw) kufariki na Abubakar Sidiq (ra) kushika nafasi yake, jina aliloitwa kama mtawala Abubakar Sidiq (ra) ni Khalifat Rasullullah … ikiwa na maana kuwa yeye sasa ndiyo kaishikilia ile nafasi ya utawala baada ya Mtume.

Hivyo aya hiyo kwenye Quran inatuambia kwamba binadam anakuja kuishika nafasi hiyo, lakini yeye si wakwanza kupewa nafasi hiyo, ila yeye anakuja baada ya aliye kuwa kwenye nafasi hiyo kuondolewa au kuondoka.

Kulingana na mafunzo ya dini ya kiislam, kabla ya kuja binadama katika mgongo wa aridhi, waliishi viumbe wengine waliofahamika kama majini.

Viumbe hawa ndiyo walio kuwa wasimamizi au viongozi kwenye uso wa dunia. Lengo la kuwepo viumbe hao kulingana na mafunzo ya dini ya kiislam linafanana na lengo waliloumbiwa binadam ambalo ni kumuabudu MUNGU MMOJA, BILA KUMSHIRIKISHA NA CHOCHOTE KILE NA KUSIMAMISHA UFALME WAKE AHAPA DUNIANI.

Viumbe hao, majini walifanya fisadi kwenye uso wa dunia na uharibifu kwenye nyanja zote za uchumi, kijamii na kiroho n.k, mwisho wa siku waliadhibiwa na cheo hicho wakanyang’anywa.

 Dunia ikabaki kitambo kirefu bila msimamizi mpaka MUNGU MMOJA, alipompa amana hiyo binadam.

Haifahamiki ni kwa muda gani hasa utawala wa Majini uliishikilia dunia kabla ya kuja binadam. Tofauti kubwa ya Majini na Binadam ni kuwa Binadam tunayo roho na kiwiliwili, ikiwa majini wao wanayo roho tu bila kiwiliwili. Majini japokuwa wanaishi kwenye uso wa dunia, lakini wanaweza kwenda kwenye zaidi ya 3D, wakati binadam tunaishia kwenye uwanda wa 3D tu.


Binadam kupitia elimu maalum na mafunzo mahususi anaweza pia kuifikia kwenye uwanda wa zaidi ya 3D, na mara nyingi tunakwenda zaidi ya 3D tunapokuwa usingizini au kwenye ibada maalum au ‘meditation’, na mtoto aliye chini ya umri wa miaka 3 na hasa miaka 2 kurudi chini wanao uwezo mkubwa wa kuufikia uwanda wa zaidi ya 3D na mara nyingi wanafanya hivyo.

Kwa watoto, sehemu ya ubongo wa mbele, unao husiana na mambo ya hiyari, kufanya maamuzi na kuhoji vitu inakuwa ndiyo kwanza inajengwa, hivyo kipindi hicho mwili wake unakuwa sehemu kubwa unatawaliwa na ubongo wa nyuma ambao kimaumbile hauathiriwi na sharia za kimaumbile kama vile za kibaiolojia, fizikia, kemia, kijamii, kidini n.k, ubongo huu unaitwa subconscious level, na ndiyo ubongo unao utawala mwili wetu tunapokuwa tumelala, au kwenye meditation, au tunapokuwa kwenye ibada flaniflani.

Hivyo kwa mtoto ni rahisi kuufikia uwanda wa zaidi ya 3D sababu yuko ‘free’, wakati anapokuwa kwenye miaka 3 na kuendelea, ubongo wa mbele, ‘front lobe’ unakuwa umeshika usikani, ubongo huu unasheria za kutosha hivyo mambo ambayo yalikuwa yanawezekana hapo kabla sasa hivi kupitia ‘front lobe’ unaambaiwa haiwezekani.

Mathalani mtu mzima akikaa na mtoto wakatizama filam ya Spiderman, mtu mzima atajua katu vile vitu haviwezekani, lakini mtoto usishangae akatoka hapo na kuanza kuparamia madirisha na kusema yeye ni Spiderman,  sababu mtu mzima anatumia, ‘logic’, ambayo inakuwa ni kama kifungo wakati mtoto kila kitu kwake ni ‘possible’ … 

unakumbuka ndoto zako za utotoni … ulitaka kuwa nani … je umezifikia … au Mr. ‘Logic’ kakuambia haiwezekani?

Turidi kwenye mjadala wetu,

Ukiacha tofauti hiyo ya kimaumbile binadama na majini hatutofautiani kitu kingine. Kulingana na mafunzo ya kiislam binadam na majini ndiyo viumbe wawili pekee wanao itwa ‘viumbe huru’, tofauti na hayawani wengine wote ambao wnafuata silka. Hayawani wengine wote hawana maamuzi binafsi au uhuru alio nao binadam au jinni.

Kwenye otofauti huo ndiyo unapokuta kwa binadam na jinni kuna lugha inayo itwa ‘halali’, ‘haram’, ‘takatifu’, ‘dini’, ‘ibada’, mungu, miungu na mfano wa hayo, lakini kati huwezi kuikuta misamiati hiyo kwa mnyama yoyote yule mbali na hawa wawili.

Makazi mahususi ya majini kwa ni mapangoni, kwenye mashimo na mahandaki.
Kutokana na mafunzo ya kiislam, wakati jua linazama (magharibi) wasilamu wana amrishwa kuwaingiza watoto wao ndani na kufunga milango kwa kutaja jina la MUNGU MMOJA, sababu kipindi hicho ndiyo mashetani wanatoka kwenye mashimo yao kuja kwenye uso wa dunia.

Unakumbuka hapo juu tumetaja kuwa watoto wadogo wanao uwezo wa kuufikia uwanda wa zaidi ya 3D, na hapa utaona ni watoto ndiyo wanatakiwa wafungiwe ndani tena kwa kutaja nina la MUNGU MMOJA, sababu watoto wanaweza kuwaona majini na mfano wa hayo ambayo jicho la mtu mzima limepigwa kufuli na ‘Mr. Logic’ hivyo hatuwezi kuona. 

Hii ndiyo maana nyumba ambayo imeathirika na mambo ya kichawi na ushirikina wa kwanza kuathirika anakuwa ni mtoto.
Hivyo basi ingawa majini wanaishi kwenye mapango na mashimo, lakini wanayo desturi ya kupanda juu ya mgongo wa aridhi, sababu baadhi ya mahitaji yao mengine yanapatikana juu ya uso wa dunia.

Kwa mujibu wa mfululizo wa Makala hizi, mpaka sasa hatujaona kiumbe mwingine mwenye maono huru na asiyefata silka peke yake zaidi ya binadam na majini. Lakini si hivyo tu, mpaka sasa sayansi inayo egemea mafunzo ya Darwin nayo haijaja na kiumbe huru zaidi ya binadam peke yake.

Ingawa uhuru wa binadam unatokana na yeye kuwa ni roho yenye mwili, sayansi ya Darwin inasema yeye ni mwili usiyo na roho, na hivyo uhuru wa binadam kwa upande wa sayansi ya Darwin siyo uhuru ulio kamili.

Hivyo ndiyo maana tunapata kitu kama, NWO, Bigbrother, Illuminanti n.k ambao wanaonelea binadam ni kama hayawani wengine isipokuwa binadam wachache kutoka kwenye familia chache mahususi wenye damu maalum ndiyo wanaweza kuwa watawala na kuwasimamia binadam wengine wote kama anavyo fanya mchunga kondoo kwa kondoo zake.

Mbali na filamu, vikaragosi, vitabu, tamthilia na hadithi mbalimbali mpaka sasa ulimwengu wa Darwin na ndugu zake hawajaweza kuthibitisha ‘beyound reasonable doubt’ juu ya kuwepo kwa kiumbe mwingine aliye huru kama binadam, na kila wanacho kifanyia utafiti na kuja nacho kinayo kila dalili ya kiumbe tunacho kiita ‘Jinni.’ Ingawa mbele ya hadhara sayansi hiyo ya Darwin na jamaa zake inakana juu ya kuwepo kiumbe hicho, kama inavyo kana juu ya kuwepo kwa roho, lakini nyuma ya mapazia mieusi wanakiri juu ya kuwepo kwa viumbe hao na kushirikiana nao kufanikisha NWO.

Hivyo kutoka sasa nitasimamia juu ya viumbe hawa wawili nay ale tuliyo yapita huko nyuma, sababu hadithi za ‘aliens’ na wenzao mpaka sasa hazina mashiko, na si kwenye mfululizo wa Makala hizi tu, lakini nenda kwenye chanzo chochote na tuletee Ushahidi ya kiumbe kilicho huru zaidi ya binadam na majini na utaona ushahidi huo  unaangukia pua kama siyo kwenye majini.

Sababu NOW na wenzao wamefanya na bado wanaendelea kufanya kazi kubwa ya kupotesha historia, na hili tutaligusia kwenye hitimisho, ni kwamba kumekuwa hakuna vyanzo huru vyenye rasilimali za kutosha kuweza kuzama kwenye bahari pana ya historia ya majini kabla ya kuja binadama na hata baada ya binadam. 

Kila tunacho kipata ni kipande cha karatasi, tukilinganishe na mwamba Fulani wa kale, tuchanganye na hadithi ile ya zamani ndiyo kwa mbali tupate picha ya nini hasa kilitokea, lakini pamoja na uduni wa rasilimali na zana hizo bado picha tunazo zipata zipo ‘clear’ kushinda sokwe wa Darwin.

Kutokana na mfululizo wa Makala hizi na kile tulicho kiona, kuhusiana na baadhi ya kazi ambazo tumeziona kuna ambazo ni za viumbe hawa, majini, kuna zingine ni za Binadam, na zingine wamefanya pamoja kama tutakavyo ona. 

Sehemu kubwa ya Maisha yao wanaishi chini ya aridhi na mapango, ingawa mwandishi hakatai dhana kuwa sehemu ya miundo mbinu hiyo ilikuja kutumiawa na kuendelezwa na vizazi vya Binadam baada ya kupewa funguo za mamlaka ya aridhi.

Sehemu kubwa ya mahandaki na mashimo hayo leo hayatumiki kwa sababu mbalimbali na iliyo kuu ni marufuku iliyopigwa na serikali katika maeneo ambayo yapo mashimo na mahandaki hayo.

Tutarudi kwenye athari za kazi za majini kwenye uso wa dunia, lakini kwanza turudi mbinguni kuliko tolewa taarifa ya kuwa katika aridhi sasa atawekwa ‘Khalifa.’
Malaika wakauliza …

 “... Je utawaweka wale ambao watafanya fisadi na kumwaga damu ilihali sisi tunakutaja na kukutukuza na kukushukuru ...?” (Quran: 2:30)

Swali la Malaika linakuja kutokana na historia ya Majini na kile walicho kifanya, hivyo kuja kwa kiumbe mwingine ambaye atayafanya aliyoyafanya mtangulizi wake haitakuwa sawa mbele ya Utukufu wa MUNGU MMOJA ambaye wao malaika wanamtaja, kumtukuza na kumshukuru.

MUNGU MMOJA, akawajibu Malaika wake kuwa ‘Nayafamu msiyo yafahamu.’

Allah mtukufu amemuumba Binadam kutokana na udongo uliyochukuliwa sehemu mbalimbali kote duniani. Hivyo watoto wadam wanakuja na rangi na maumbile kulingana na udongo ulipochukuliwa. Kuna ambao ni wekundu, weupe, weusi na wengine baina ya hao (kati na kati); wengine wembamba na wengine wanene, wengine wabaya (tabia) wengine wazuri (tabia), wapole na wakorofi, wengine wachafu na wengine wasafi.” (Saheeh, At-Tirmidh.)


Udongo huo alio umbiwa Adam, ulichanganywa na kufinywangwa na kutoa umbo la Adam akiwa mkamilifu likaachwa kwa kitambo fulani, mpaka likabadilika rangi na kuwa na weusi (dark) na mkavu kiasi ukiugonga unatoa sauti.


Ni katika weusi (dark) huo ndiyo tunapata jina la Adam, ambalo linamaanisha Ngozi yenye weusi (dark skin). Ingawa neno Adam kwenye baadhi ya mapokeo ya Mtume (saw) limekuja na maana mbili, ambapo maana ya kwanza ni hiyo ya asili, likimaanisha ngozi yenye weusi (dark skin), lakini maana ya pili, limetumika kuelezea ngozi yenye weupe (light skin). 

Wakati anatajwa Adam kwenye hadithi neno hilo linamaanisha Ngozi yenye weusi (dark skin), na wakati anatajwa Issa/Yesu kwa neno hilohilo linamaanisha Ngozi yenye weupe (light skin)
Hivyo basi baba yetu Adam Ngozi yake ni ‘dark skin’, kama tulivyo ona hapo juu. 

Lakini pia tumeona kwa nini watoto wake baadae wamekuja kuwa na Ngozi tofauti, kama hiyo ya Issa/Yesu ya kwake ni light skin, na hata ya kwako wewe msomaji ni tofauti na ya mwingine, hii ni kutokana na aina tofauti tofauti za udongo na tabia zake zilizo tumika kumfinyangia baba yetu, Adam (a.s).

Lakini tukirudi kwenye nukta ya msingi, hii haimfanyi mtu mweusi kuwa bora dhidi ya mtu mweupe n.k, sababu mtu siyo mwili au kiwiliwili chake, mtu ni Roho, na kiwiliwili ni jumba au chomb kinacho beba roho na ambapo Roho, hakuna nyeupe wala nyeusi, nyekundu wala njano, kipofu au kiziwi, kilema au mgonjwa, roho zote ni sawa kwa 100%.

N andiyo maana kwenye mafunzo ya dini ya kiislam tunafundishwa kuwa

… Mola wetu hatizami miili yetu, wala mali zetu, wala watoto wetu, lakini anatizama nafsi/roho zetu … na roho/nafsi iliyo bora dhidi ya nyingine ni ile iliyo karibu kwa Mola wake kwa kufanya matendo mema kwa ajili ya Mola wake ...

Ila kwasababu tunaishi kwenye dunia iliyo tawaliwa na kushikiliwa na nadharia ya Darwin, ambayo haitambui uwepo wa Roho, bali kiwiliwili tu, ndiyo maana leo hii, kila kitu thamani yake inapimwa kwenye vitu, ‘materialisim’ … hata kwenye baadhi ya nyumba za ibada mwenye nacho ndiyo anathaminiwa ambayo ni kinyume kabisa na hata malengo ya nyumba hizo za ibada.

WEWE NI ROHO YENYE KIWILIWILI NA SIYO KIWILIWILI CHENYE ROHO.

… yule atakaye ingia peponi (Allah tujaalie kuwa miongoni mwao), atapewa umbo kama la Adam, ambaye urefu wake ulikuwa ni kubiki 60, ila watu walio fuata baada yake ukubwa wa maumbo yao umekuwa ukipungua mpaka leo.” (Sahih Muslim)

Allah alimuumba Adam, na akampa urefu wa kubiki 60 … watu walio fuata baada yake ukubwa wa maumbo yao umekuwa ukipungua mpaka leo.” (Sahih Bukhar)

Kutaja hizo hadithi kwa uchache, zipo nyingi zinaelezea umbo la Baba yetu Adam, kuwa urefu wake ulikuwa ni kubiki 60.
Kubiki 60 ukizileta kwenye lugha rahisi tunayo ielewa ni futi 90 au mita 30!


Upo hapo?

Umbo la Baba yetu Adam, lilikuwa ni futi 90 au mita 30 kwa urefu, nadhani ukipiga hesabu zako kichwani mwako utapata upana wake ulikuwaje!
Mtu mrefu sana leo hazidi futi 8! Kwa maneno mengone ni kwamba tumepungua maumbile yetu kwa asilimia 90 na zaidi.

Ndugu yetu, mtanzania mwenzetu tunaye jivunia nae kwa urefu Hasheem Thabeet, urefu wake ni futi 7 na nchi 3! Sasa hebu fikiria kama Hasheem na urefu wote ule hauzidi futi 7, ni vipi basi ulikuwa urefu wa futi 90!

Nadhani unaanza kupata mwanga sasa.
Kwa hiyo umbo kamili la vizazi vya Adam vilikuwa kwenye futi 90, hawa tunaita ni MA-GIANTS.

Sema tena MA-GIANTS.

Umbo hilo la futi 90 likapuliziwa roho, ambapo roho ndiyo kiumbe hasa kilicho kusudiwa kuishi ndani ya umbo hilo la futi 90.

Umbo hilo la futi 90 bila Roho lilikuwa ni udongo mkavu unao toa sauti, na Roho inapohama, umbo hilo hurudi kuwa mavumbi matupu, hurudi kwenye asili yake, hufa.

Kinacho kufa siyo Roho, kinacho kufa ni mwili, roho inahama, ndiyo maana kwenye lugha ya Kiswahili, neno tulilo litohoa kutoka kwenye lugha ya kiarabu, ‘Mufarakah’ au ‘Amefariki’ ‘Kufariki’, lina maana ya kutengana, utengano, yaani mwili umetengana na Roho, na vinapo tengana ndipo kifo hutokea, nacho huwa ni kifo cha mwili, sababu Roho itaendelea kuwa hai kwenye kituo kinacho fahamika kama, ‘Barazaq’ kwa waislam, halafu itarudishwa kwenye kiwiliwili mara nyingine na kusimamishwa mbele ya Mola wake akiwa na umbo kama la awali, umbo la futi 90.

Kuna mengi yaliendelea hapo mpaka kufikia Adam na Hawa kuteremshwa kutoka mbinguni nakuja kwenye uso wa dunia, kwenye Makala haya nisingependa kwenda huko zaidi, ila ningependa kugusia nukta moja ya msingi sana.

Nukta hii ni mkataba baina ya binadam wote na MUNGU MMOJA. Kila mtu aliingia mkataba huu, wote waliokwisha pita kwenye uso wa dunia, wote ambao wapo kwenye usi wa dunia, na wote watakao kuja mpaka siku ya mwisho , tulisaini huu mkataba.

Kwenye Quran tunajifunza kuwa,

Na Mola wako mlezi alipo waleta katika wana wa Adam, kutoka migongoni mwa kizazi chao na akawashuhudia juu ya nafsi zao, akawambia: Je Mimi si Mola wenu Mlezi? Wakasema: Kwani! (kwanini isiwe hivyo) Tumeshuhudia. Msije mkasema siku ya kiyama sisi tumesahau makubaliano haya.” (     Quran 7:172)

Kwenye aya hiyo tunajifunza kuwa binadam wote au watoto wote wa Adam tulisimamishwa mbele ya Mola wetu, na kuulizwa na Mola wetu.

Je Mimi si Mola wenu Mlezi.”

Tukajibu,
 “Kwanini isiwe hivyo, hilo halina shaka kabisa, wewe ndiye Mola wetu Mlezi.

Tukaambiwa, 
Msije kusema siku ya kiyama kwamba mlisahau huu mkataba.

Je kuna yeyote anayekumbuka haya makubaliano?

Hakuna.

Swali kwanini, tusikumbuke mkataba muhimu kama huu?


Guys Tchaoo, that is your homework …

Lakini nitalijibu swali hilo kwenye nuru ya sayansi ya saikolojia na metaphysics …

Lakini mwalimu yoyote mzuri anapo toa ‘assignment’ kwa wanafunzi wake huwapa vitabu na rasilimali zingine zitakazo wasaidia kujibu swali hilo…

Hivyo wanafunzi wangu wapendwa … kwa wale wapenzi wa filamu ningeomba utizame filamu inayo kwenda kwa jina la, Déjà vu na ‘Manchuria Candidate’ zote zimechezwa na Danzel Washington, au Time Travelling Machine.



Wale wapenzi wa series katizame series ya Lost season 4 au 5.

Wale wapenzi wa kusoma, kasome kitabu kinacho kwenda kwa jina la ‘The Music of Time', kimeandikwa na Preston Nicholos.

Au Project Super Man kimeandikwa na Michael Andrew Pero, au Trance - Formation of America …

Till next time I say Tchaooo ...

8 comments:

  1. Anhaaa Mbona umekatisha utamu sasa??!! Mpk lini? Ninavyokujua ww mpk miezi 2 hapo ndo tutakupata

    ReplyDelete
    Replies
    1. Soon mdau, this time nataka niweke bandika bandua maana nina viporo vingi nataka viishe, so soon Inshallah ...

      Delete
  2. Nataka nikutafute private Akh: Salim

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapana shaka, tuanzie hapa salimumsangi@gmail.com .. then mengine yataendelea

      Delete
  3. Kaka umetoa ulibalikiwa na Allah, Allah akulinde na kila LA Shari wewe na kizazi chako

    ReplyDelete