Je kunayo uwezekano kwamba kamera na vinasia
sauti vilikuwepo katika zama zilizo sahaulika, zama za kale za ngano na hadithi
za kufikirika?
Ni uwendawazimu kuuliza swali kama hili, ama
sivyo? Lakini kwa ambaye amefuatilia mtiririko wa mabandiko haya ni swali
ambalo haliwezi kukwepeka.
Twende India, kwenye milenia ya pili KK, kunayo
rikodi zainazo toa mwanga wa majibu kwa swali letu. Lakini rikodi hizo
zinasemwa si za milenia ya pili KK, bali za kipindi cha nyuma Zaidi.
Kipindi
gani hicho, ziliandikwa na nani?
Kama yalivyo masalio na vipande vipande vya
taarifa za zama zilizo sahaulika, hizi nazo kutoka India ni moja kati ya
vipande vidogo vidogo ‘tulivyo’ achiwa kuvionganisha walau kupata mwanga wa
nini hasa kilikuwepo kabla ya ‘binadam wa Darwin’.
Taarifa hizo zilipoweza kufasiriwa mnamo karne
ya iliyopita, zilikutwa zinayo utajiri wa kutisha na kugofya kwenye nyanja za
sayansi na teknolojia, utajiri ambao kwa sasa ndiyo tunakimbizana nao, kama
bado tutakuwa hatuja ushika.
Tunayo yaona leo kwenye ulimwengu wa kamera na
ujasusi vimeelezea kwenye kurasa kongwe za India ambazo ni lini zimeandikwa, na
zimendikwa na watu au viumbe gani, bado hatujaweza kutoa alama ya kuuliza kwenye
sentensi hiyo.
Wanasayansi wetu wa inchi ‘mbalimbali’ kwa sasa
wanapitia tafsiri nzuri iliyo fanywa na Maharshi Bharadwaja na kupewa jina
la ‘Aeronautics’, na ikifahamika kuwa ni
nyaraka kutoka zama za kale mno, huenda kabla binadam wa Darwin hajaikanyaga
dunia lakini ikiwa inayo mambo ya ajabu na kushangaza kana kwamba imeandika
kwenye karne hii tunayo ishi sasa!
Yanayo tajwa kwenye ule ukurasa wa ‘Yaliyomo’
kwenye nyaraka hizo ni pamoja na:
-Siri ya kutengeneza ndege ambayo haitoweza
kuharibiwa na adui. Ambayo haitoweza kuvunjika, kushika moto, wala kuharibiwa.
Si dhani kama ndege zetu kubwa za biashara
zinayo teknolojia hii. Walikua mbali mno! Ndege zetu bado zinashika moto,
zinaweza kuharibiwa na adui na pia zinavunjika vipande vipande zikikumbwa na
dhoroba mbalimbali.
Walikuwa mbele yetu kwa teknolojia ya anga. Ni akina nani
hawa, waliishi kwenye zama zipi, yapi maarifa hayo, mbona binadam wa Darwin ana
evolve kurudi nyuma na siyo kwenda mbele. Ni kweli tumetokana na Sokwe? Je
teknolojia hiyo ilikuwa ni ya Masokwe? Au kuna ambacho mjomba Darwin amesahau
kutuambia?
Jingine kwenye orodha ya ‘Yaliyomo’ kwenye
nyaraka hizo za kale ni:
-Siri ya kutengeneza ndege inayoweza ‘kusimama/kunata’
anagani.
Hili ndilo tunalo fanya sasa kwenye karne hii
kwa kutumia ndege za kivita. Je tumevumbua hili au wanasayansi wali-‘copy n
paste’ kutoka kwenye nyaraka mfano hizi?
Jingine kwenye ‘Yaliyomo’.
-Siri ya kusikiliza mazungumzo na sauti nyingine
kwenye ndege ya adui.
Kama alivyo sema Friar Roger Bacon kwenye
bandiko lililopita kwamba “Vyombo vya kurukia angani kama hivi vilikuwa ni vya zamani sana, na hata sasa katika zama zetu bado vinatengenezwa”, ndivyo inavyo someka kwenye nyaraka hizi ambazo nazo za
kale mno kushinda kipindi alicho aliishi Friar Roger Bacon.
Utaona hapa ndege inatajwa kama kitu cha kawaida
kabisa, na cha ziada kinacho tajwa hapa ni ‘ujasusi’ wa teknolojia namna gani
utaweza kunasa mazungumzo na sauti zingine kwenye ndege ya adui yako bila yeye
kufaham.
Katika zama zetu hizi za ‘mbio’ za kulitawala
anga, teknolojia hiyo kijasusi ndiyo habari ya mjini.
Kingine kwenye ‘Yaliyomo’ ni:
Siri ya namna ya kupata picha za ndani ya ndege
ya adui! Jingine lenye kutuacha mdomo wazi. Hapa tena inatajwa ndege, lakini zaidi
inatajwa kamera, tena kamera ya kijasusi
yenye uwezo wa kupiga picha ndani ya ndege ya adui na kuirusha kwenda kwa mpigaji,
bila adui kufahamu, walitumia ‘internet’ pia kwa ajili ya mawasiliano hayo au …?!
Sidhani kama kwenye ulimwengu wetu wa ‘ujasusi’ tumefikia teknolojia hii, au
tumeishia kudukua sauti na picha za rai wetu. Ukweli ni kwamba walikuwa mbali
sana, kiasi kwamba ukiilinganisha teknolojia yao na yetu ni ‘Binadamu na Mdoli.’
Sasa hutoshangaa barabara za kurushia ndege
Nazca, ambazo tulizigundua karne iliyopita baada ya ndege za watalii kuanza
kuruka eneo hilo, hutashangaa kuhusu ramani za Reis ambazo zinaonesha bara la
Antaktika kwa ukamilifu wake, ambapo karne ya 19 Urusi wanachapisha ramani ya
Dunia haina bara la Antaktika sababu hatukujua kwamba kuna pande la aridhi
lililoganda kwa barafu kwenye kitako cha dunia!
Nadhani hutaweza kuziita ni ngano tena hadithi
za waungu wa Kigiriki na Egypt ambao walikuwa wanapaa angani, wala kuitilia
mashaka safari ya kwendaa mwezini liyo fanywa China na Chang Ngo. Au bado unayo
mashaka kwamba teknolojia tunayo jivunia tumeikopi mahala?!
Syria mwaka 1400 KK, walikuwa na maktaba ambayo
ndani yake kunayo vyumba kadhaa vilivyo jikita na vitabu vya kamusi na tafsiri
peke yake. Utajiuliza kulikuwa na lugha ngapi zama hizo kiasi maktaba iwe na
sehem maalum kwa ajili ya vitabu vya ‘kamusi’ na ‘tafsiri’?
Kumbuka hapo vitabu
vinatajwa, kwamba dhana ya vitabu hakuwa ngeni zama hizo, ni vipi binadam
alirudi chini na kuanza kuchora chora mapangoni na kuandika kwenye mawe kutoka
kwenye vitabu na makaratasi? Nini kilitokea kilicho sababisha mabadiliko hayo?
Egypt, China na India kama tulivyoona wao
walikuwa na vitabu vinavyo husiana na maarifa ya teknolojia.
Kwenye milenia kadhaa Kabla ya Kristo yapo
maandishi ya kutosha kuhusiana na nguo, marashi, viatu, nguo za kisasa kabisa
kama tunazo vaa leo, nguo za kuogelea, mawigi ya kisasa, nguo za ufukweni kwa
walimbwende, na mengine mfano wa hayo.
Lakini kwani hili litakushangaza? Kama
watu walitengeneza simu, vinasa sauti, ndege za kivita, kamera unadhani kwamba
walijifunika majani, na kutembea bila viatu? Hapana kila nyanja ya Maisha iwe
kiuchumi, kijamii, kisiasa ambayo tunaona tumesonga mbele kwenye zama zetu,
kwenye zama hizo zilizo sahaulika walikuwa mbele Zaidi yetu kwa namna nyingi
mno.
Sanaa na kazi zake. Walicho fanya watu hawa kwenye
nyanjaa hii, pia ni zaidi ya kile ambacho tumewahi kukifikiri na kukifanya
kwenye uwanja huo. Kwao, ‘The Sky was not the limit, only what they couldn’t imagine, and
perhaps they imagine almost everything’, mtanisamehe kwa
kukopa maneno hayo ya Malkia, ni katika kuweka msisitizo wa kinacho fuata.
Nani hajatizama filam maarufu, kwenye mambo ya
historia, iliyo igizwa na Indiana Jones iliyo kwenda kwa jina la ‘Crystal Skull’? Maudhui
ya filamu ile yameegemea kwenye tukio la kweli, la Indiana Jones wa kweli, ambaye aliitwa Mitchell
Hedges aliyevumbua, ‘Crystal Skull’ la kweli. Mpaka anakufa hakusema ni wapi
aliliokota fuvu hilo la ajabu.
Fuvu hilo moja ya mengi linalo husishwa nalo
kwamba linaweza kufanya ni pamoja na kutoa sauti nzuri, murua ya kuburudisha, yenye
kusawijisha moyo, akili na mwili kwa pamoja na kukufanya ujihisi mpya baada ya
kusikia sauti hiyo. Mwezi unapokuwa kwenye hatua Fulani katika moja ya vituo
vyake, fuvu hilo likitolewa nje katika wakati huo na kuhamiliana na mwezi huo
basi ndipo sauti hiyo inapo toka, na kisha linatoa nuru yenye kuliwaza macho. Ni
kama linakupeleka kwenye dunia nyingine kabisa.
Nani msanii wa kazi hii ya Crystal Skull? Ni
Msanii wa zama zipi, alitumia vitu gani kutengeneza kifaa cha namna hiyo, na
vipi alijua kuwa palihitajika kiasi fulani cha nuru ya mwezi, tena ukiwa kwenye
kituo Fulani ndiyo ‘maajabu’ ya kazi yake yaonekane?
Wanasayansi wetu si kwamba tu hawajaweza
kugundua ni kwa namna gani hili, ‘Crystal Skull’ linafanya hayo maajabu yake,
lakini hata nadharia ya namna gani linafanya hicho linacho kifanya hawana, au
hatuna.
Siyo siri, Sanaa ya zama zilizo sahaulika, ni
zaidi ya chochote tulicho wahi kufikiri kwenye uwanda huo. Crystal Skull ni kilainisha
koo, chakula chenyewe bado hakijatenga mezani.
Altamira, Spain, Lascaux, France, Ribadasella na
Shara: michoro ya mapangoni yenye muundo na muonekano wa ubora wa hali ya juu,
utadhani ni kazi ya Sanaa ya zama zetu, lakini ikionekana nay a kisasa kwa zama
zozote utkayo iweka!
Kukubaliana na kusimama kwa ubora zama zozote utakazo
ziweka.
Mistari yake namna inavyo kizana sehemu moja na
kuowana sehemu nyingine, na muonekano zinayo toa, zinafanya kazi hizo zionekane
ni bora, nzuri na zenye mvuto kushinda zile za Egypt, Babylon, Greece au Crete
na kiwango ambacho hakikiweza kufikiwa mpaka kwenye kipindi cha Renaissance
kwenye karne ya kumi na tano!
Ajanta, karibu na Bombay, India, mchoro unao ng’ara
ndani ya pango! Mchoro huo unamuonesha mwanamke amebeba zawadi. Lakini taa
inapo zimwa picha hiyo hubadilika na kuonekana na muundo wa 3D, kama vile
imetengenezwa kwa marumaru. Ukiwasha taa, mchoro unaonekana ni wa kawaida wa
1D. Ubunifu wa kiwango hiki umepotea na haupo kabisa au ni ndoto ambayo bado
kuifikia kwenye zama zetu?
Havea, Brazil, mlima umechongwa na kutoa taswira
ya mwanaume mwenye ndevu, kwa upande mwingine wa mlima anaonekana amevaa
helmenti.
Peru kwenye uwanda wa Marcahuasi, kuna kazi ya sanaa
ambayo iko kwenye 4D (Four Dimension), kwa mtu wa kawaida ni rahisi kumuelezea
1D, 2D na 3D lakini siyo 4D na kuendelea, lakini hapa tunakutana na kazi
iliyoko kwenye 4D!
Mfano wa karibu wa kile tunacho ita 4D, ni mfano
wa picha maarufu tunazo ziona za mtu anayeitwa, ‘Yesu’ au ‘Mama Bikira Maria na
mfano wake, ambazo, ukizitazama picha hizo kutoka engo moja utaona muhusika,
kafumba macho, kutoka engo nyingine picha hiyohiyo utaona muhusika kafumbua
macho.
Lakini hapa hatuzungumzi kwenye karatasi, bali
juu ya bonde la aridhi imetengenezwa 4D! Kazi hiyo inayo sura kadhaa tofauti,
inahitaji mtazamaji kusogea nukta moja kwenda nyingine na ataona sura aliyo
iyona mwanzo kwenye picha hiyo hiyo, inabadilika na kuwa na sura nyingine, au
kutoweka kabisa, now you see, now you not!
Picha hizo kuna muda unaziona na kuna muda
hazionekani, nyingi zinaonekana wakati wa jua la utosi, au wakati wa jua la
magharibi, miale ya jua linalo zama ikigonga kwenye uwanda huo, basi michoro
hiyo ya ajabu huonekana, na pia kwenye nyakati zingine maalum na siyo muda
mwingine wowote, huwezi kuziona! Utadhani unasoma ngano za Alfu Lela U Lela! Lakini hapa ni Peru eneo lisilo isha maajabu kwa kazi za
maajabu kutoka kwa viumbe vya maajabu.
Kuna kazi nyingine ya sanaa, ambayo ni umbo la
mtu mzima au mzee haswa, ambalo limechongwa, lakini unapo lipiga picha,
linabadilika na kuwa na uso wa kijana rijali! Kama mazingaumbwe vile, ni vipi
sayansi yetu ya sanaa inaweza kuelezea kazi ya namna hii.
Hapo tena tunapata nukta ya mambo ya kamera,
sababu ni baada ya kupiga picha ndiyo unapata picha ya kijana, ingawa kinyago
ulicho kipiga picha ni cha mzee! Ni vipi msanii wa kazi hii angeweza
kutengeneza aina hii ya matokeo kama hakuwa na kamera? Lakini swali tata zaidi
ni katika zama zipi ilifanyika kazi hii? Ilifanywa na binadam wa Darwin au
binadam yupi au ni viumbe kutoka sayari ya mbali?
Uhodari wa kazi hii ni wa ajabu kama ilivyo kazi
yenyewe! Msanii wa kazi hii alitakiwa kuwa na ujuzi wa ajabu mno kuhusiana na
tabia ya mwanga na tabia ya jicho, kiasi kwamba atengeneze kazi hii kwenye
mwamba, ambayo itafanya umbo la kitu lionekane kutoka engo moja tena ikiwiana
na kiasi cha mwanga maalum cha jua eidha la mchana au jioni tu na si
vinginevyo!
Lakini kazi hiyo siyo ya mchoro mmoja au miwili,
bali ni mingi kiasi cha kuchukua eneo la mraba wa maili moja!
Kuna michoro ya binadam kutoka rangi kuu nne za
binadam, yaani mweusi, mwekundu, manjano na mweupe, michoro ya Wanyama kutoka
kona tofauti za dunia. Lakini michoro yote hiyo ni kwa wakati maalum ndiyo
unaweza kuiyona, na pia huwezi kuiyona yote kwa pamoja, lazima usogee kona moja
kwenda nyingine, na kuna wakati uwanda mzima ni kama hakuna chochote! Now you
see, now you not!
Unakumbuka Easter Island, kwenye mabandiko
yaliyo pita, tulipo zungumzia masanam makubwa, yaliyo chongwa na kupangwa kwa
mstari mmoja yakiwa yame valishwa kofia nyekundu?
Kuna zaidi kwenye masanamu hayo.
Unapo yatizama utaona msanii kama vile haja yawekea
kopi. Lakini jua kwenye mzunguko wake wa mwaka mzima kuna wakati mwanga wa jua
unapo yamulika masanamu hayo kutoka kwenye engo maalum, yanatoa taswira ya kope
na jicho lake. Ingawa ukilitazama kipindi kingine hutaona kope wala jicho!
Mto Onega, Urusi, kazi hii ni kama filamu kwenye
mwamba! Michoro takribani 600 imechongwa na kupangiliwa kwenye mwamba mgumu wa
granite, kama ule ambao michoro ya Nazca kule Peru inapo patikana.
Granite ni moja ya mwamba mgumu sana, ambao
ukisha fanya kazi kwenye mwamba huo, si jua, upepo wala mvua vitakavyo kuja
kusahihisha kazi hiyo, lakini kwenye aridhi hiyo ngumu tuliona michoro zaidi ya
300 kule Peru, ambayo tuliiyona baada ya kuanza kurusha ndege, kwenye mwamba
huu, hapa Urusi kuna michoro zaidi ya 600, lakini hadithi yake haijaishia hapo.
Msanii wa kazi hii ametumia athari ya maji
yanayo tembea ya mto, pamoja na miale ya mwanga wa jua linalo zama kutengeneza
athari ya picha ‘inayotembea’, yaani unapo tizama kazi hiyo ni kama filamu,
lakini hapo ni kwenye mwamba na hakuna projekta!
Jua linapokuwa linazama, mwamba unakuwa na athari ya wekundu weusi, na rangi
nyingine kwenye mchoro huo zinaonekana vizuri kutokana na athari ya miale ya
jua linalo zama. Vijiwe vingi vya crystal alivyo tumia msanii kwenye kazi hii
navyo vinaakisi mwanga huo kwa kiwango kikubwa zaidi na kutoa nuru kali. Kisha
maajabu yanaanza, picha inaanza ‘kutembea’ kulingana na miale ya jua. Kwanza Chura
anaanza kubadilika na kuwa mfano wa Swala,kisha muwindaji anaoneka anarusha shoka
kwa mkono wa kulia, halafu mkono wa kushoto unaanza kutokea ukimpatia ‘balance’
muwindaji asianguke, movie hii inachukua kama dakika 45 tangu kuanza mpaka
kumalizika jua linapo zama kabisa.
Crystal zilizo ambatanishwa kwenye kazi hii
zinaakisi mwanga na kutoa nuru, na wakati huo huo kuanza kufifia kadiri miale
inavyo hama kutoka sehem moja kwenda nyingine na ndivyo ‘filam’ yenye
inavyoaanza na kufifia mpaka jua linapotea, bila kusahau athari yam to huo
ambao maji yake yanatembea na hivyo kuifanya picha hiyo kama filam!
Sanaa, bado kuna mengi ya kuandika kwenye kazi
kama hizi na mfano wake, sababu zipo za kutosha, only time not in our side.
Kuna ishu ya afya, madawa, magonjwa, upasuaji wa
kimatibabu, na mengine mfano wake kwenye nyanja hii ya utabibu, niwaachie
wasomaji wangu kwa nafasi na muda wao watafiti vitu hivyo na watashangazwa na
kile watakacho pata.
Tumekuja kutoka mbali mpaka hapa tulipo fika.
Tulianza na udadisi wa kutaka kufahamu uwezekano
wa kuwepo kwa viumbe wengine, tukaja kwenye alama na viashiria kuwa palikuwepo
na viumbe au binadam walio fanya kazi za maajabu, tumezipitia ni nyingi mno nni
nyingi nimeziacha.
Lakini nadhani niliyo yataja yanakidhi kiu,
kwamba kuna zaidi ya kile tunacho kiona, zaidi ya kile tulicho fundishwa
darasani na zaidi ya kile tulicho aminishwa!
Sasa ni wakati wa kukutana na muhusika wa kazi hizi.
Upo tayari?
Upo tayari kubadili mtazamo wa historia uliyo
kuwa unaifahamu?
Unadhani ni nani anaweza kuwa ndiyo muandishi
wakazi hizi tulizo ziona kutoka episodi ya 1 mpaka hii ya 15 kwenye season hii
ya pili?
Kabla sijaanza season 3 na finale kwenye kazi
hii, ningependa kupata maoni ya wasomaji juu ya nani wana wadhania au kufikiria
ni ndiyo wafanyaji wa maajabu hayo tuliyo yaona, uwanja
wa maoni ni wenu ……..
Till next time stay blessed
Hawa waliyofanya haya ni majini,Kwa sababu kabla ya kuja wanaadamu hawa ndio waliokuwa ulimwenguni makarne mengi sana yaliyopita,ila baada ya kufanya ufisadi na uharibifu,Allah akaleta gharka na kuwaondosha,ila bado napata ukakasi na hili ulipo sema kuwa katika Uchina,kulikuwa na taaluma hii na mfalme wao alikuwa na engineer wake aliekuwa anafahamu elimu hiyo,lakini bado nina yakini kuwa haya yote ni ya majini,maana katika Nchi unazo zitaja bado athari ya mambo hayo yapo,India,China na Misri,lakini hata ukiwaskiliza wanao amini mambo ya majini wanasema kuwa bado wana utaalamu katika fani hizi za ulimwenguni na wanafanya kama sisi mambo ya Tiba,sayansi,teknolojia
ReplyDeleteVizuri sana mdau wangu.
DeleteIla mimi nina swali kwako, ikiwa ni majini ndiyi waliyo fanya hayo, na ikiwa waliyafanya kabla ya binadam kuja, ni vipi basi majini walifaham sura na umbile la binadam ambaye bado hakuwa amefika duniani, maana kazi nyingi ukizitazama utaona zina sura, umbile au athari fulani fulani za kibinadam. NI VIPI MAJINI YALIMFAHAM BINADAM KABLA YA KUJA KWAKE?
Nadhani unajua ya kuwa hawa Majini walikuwa na uwezo Mkubwa sana wa kutambu mambo na elimu kubwa kuliko ss,ijapo kuwa hili linakanushwa ktk kisa cha Nabii Sleiman alipokitaka koti cha Belqees Jini alisema atakileta kabla ya.... na Mwanaadamu mwenye elimu alisema atakileta kabla Nabii Sleyman hajatukusa ukope wa jicho,nini maana ya haya hata kabla ya kuletwa binaadamu ulimwenguni tayari habari za kiumbe huyu zilikuwa tayari,na hata huyu Ibilisi katika kuasi kwake sababu kubwa ni huyu binaadamu,na juu ya haya masuala unayo tuelezea nna hakika sana yana Mkono Mkubwa sana Wa Ibilisi, kwa hiyo majini waliweza kushirikiana na kaumu za zamani sana ambazo walishirikiana nao kufanya mambo kama hayo,mfano wa sanaaa iliyo kubwa na ambayo haihitaji ufafanuzi Mkubwa ni Baitul Muqaddis ya Phalestina hii ni kazi ya majini,nakshi ambazo zilizotumika humo mpka Leo bado sanaaa hii kuifika,mambo ya tires tangu kipindi cha nabii Sleyman zilikuwepo ndipo Belqees akadhani maji akawa anaruka akaambiwa kuwa ni marumaru,nadhani kwa hapa unapata picha kuwa Binaadamu waliwatumia majini katika fani zote hizo,waliwatumikisha katika ujenzi,Sanaa na mambo ya madini na machimbo,ktk ushirikiano huu ndo hao Watu wa jamii za siri ndio wakaamua kuficha elimu hii kwa kutaka kuhodhi mambo mbalimbali
DeleteYusuf Ally Yussuf niliekutumia Email kwa Edulinktz@gmail.com mm ni shabiki Mkubwa wa kazi zako Alhamdulillaah
DeleteShukran mdau, ila sidhani kama niliipata email yako ... may you try to send it again.
DeleteKaka nakufatilia tangu nipo shule ya msingi napnda sana Nazi zako kaka saana
DeleteSheikh Salim lete vitu bhana,tumechoka kuchungulia Blog kila time
ReplyDeleteUkweli nimepata kitu ambacho nitajivunia maisha yangu yote nitakayo kua hai kuhusu kazi hizi....nimepata kufaham kwanini Darwin alikuja na propoganda zake coz yeye kawa kivuli cha kuziba ukweli wa kazi hizi.Brother katika majina 99 ya Allah kuna jina ukilitaja kwa wingi Allah anakuonyesha siri ya yaliyo fichikana hapa ulimwenguni namini Allah kanifunguria kupitia wew.TENKS BROTHER ALLAH AKUONGOZE COZ KILA NAPO PITIA KAZI ZAKO HUWA NAPATA KUONGEZA KUTAMBUA UKUBWA WA ALLAH
ReplyDeletekaribu sana na wakaribishe wengine ...
Delete