Friar
Roger Bacon katika kazi zake aliacha
sentesi ya maajabu iliyosemeka hivi, “Vyombo vya kurukia angani kama hivi
vilikuwa ni vya zamani sana, na hata sasa katika zama zetu bado vinatengenezwa”.
Kauli kama hii kwenye maandishi ya karne ya 13 ni kitendawili kisicho na jibu.
Kwanza Bacon anathibitisha kwamba vyombo vinavyo ruka angani ni jambo
lililokuwepo katika zama zilizotangulia, lakini zaidi pia kwenye zama zake si
kitu kipya, huenda kama tunavyoona kwenye zama zetu kwamba ni kitu kipya,
lakini kwenye karne ya 13 hakikuwa kitu kipya.
Hermes au Mercury alivaa ndala na kofia zenye
mbawa ambao zilimsafirisha kwa kasi ya ajabu juu ya aridhi na juu ya bahari,
lakini hadithi kuhusu Mercury zimerikodiwa kama ngano za kale!
Lakini la kushangaza zaidi ni kuhusiana na mtawala wa China aliyefahamika kama Shun
(2258-2208 KK) ambaye si kwamba tu alitengeneza mashine ya kurukia lakini pia
alitengeneza parachute
Mfalme Cheng Tang (1766 KK) alimuamuru
Ki-Kung-Shi kumtengenezea chombo kinacho ruka angani. Injinia huyo akamaliza
mchoro wake na kutengeneza chombo hicho na kukifanyia majaribio na kusafiri
nacho mpaka kwenye eneo la Honan.
Mshairi wa Kichina, Chu Yuan (wa karne ya 3 KK)
aliiandika juu ya chombo chake cha angani ambacho kiliruka juu sana juu ya
jangwa la Gobi kuelekea kwenye vilele vya barafu vya mlima Kun Lun. Akaelezea
namna gani chombo chake kilivyo kuwa hakiwezi kuathiriwa na upepo na vumbi la
jangwa la Gobi na namna alivyo tumia chombo hicho kufanya, ‘aerial survey.’
Mwanzoni mwa karne ya nne, Ko-Hung aliandika kuhusiana
na Helkopta iliyopo China. Somo kuhusiana na usafiri wa angani lilikuwepo tangu
mwanzoni mwa historia kama tunavyo weza kuona neon la Sancrit ‘Vidya’
lenye maana ya kutengeneza na kuendesha vyombo vya angani. Mawazo ya msingi juu
ya usafiri wa anga yapo kwenye karne na zama ambazo mjomba Darwin anasema
binadam anaishi mapangoni na anawasha moto kwa kutumia vijiti vya mti.
Kitabu cha kale mno duniani kutoka India kinacho
kwenda kwa jina la Muhabharata, kinazungumzia kuhusu chombo kinacho ruka angani
kilicho tengenezwa kwa mbawa za chuma. Ndege?
Vimana inatajwa kuwa ni chombo ambacho kinayo
sehem mbili, juu na chini kwa ajili ya abiria, madirisha, muundo wa ‘dome’ na
mapanga yanayo zunguka. Zinaruka kwa kasi ya upepo na kutoa sauti murua. Kama
vile wanazungumzia ndege zetu za kisasa. Rubani lazima apitie mafunzo maalum
ndiyo akabidhiwe vimana.
Ndege hizo zilifanya maajabu pia ambayo tunayaona
yakifanywa na helkopta zetu leo. Kama vile kusimama angani bila kwenda mbele
wala kurudi nyuma. Vimana ziliruka juu sana mpaka kuyapita mawingu na bahari
kuonekana kama kabwawa kadogo! Rubani aliweza kuona pwani za bahari na mito
inayotiririka kuelekea baharini.
Vimana ziliwekwa kwenye ‘vimana griha’,
zilitumika kwa ajili ya vita, safari na michezo. ‘Aren’t we doing the same
thing with flight to day?’ Lakini ni kweli taarifa, maelezo na maelekezo haya
kutoka kwenye karne na zama zilizoitwa za kiza, kwamba zinaweza kuwa ‘ndoto za
mchana’ za muandishi? Au ngano za kale zilizo sahaulika au kweli zilikuwepo
ndege, kama jet, helkopta na bombadia zama hizo?
Kunayo aina mbili za vitabu vya kale vya
Sanscrit huko India, aina moja imegemea kwenye mambo ya kiroho, kidini na
maajabu, hii inafahamika kama ‘Daiva’ na aina ya pili ni ile inayo husiana na
taarifa za ‘kisayansi’,
inafahamika kama ‘Manusa.’ Kwenye ‘manusa’, kuna sura
ya ‘Samara Sutradhara’ inayohusiana na mambo ya ‘kisayansi’, kijitabu hicho
ndani ya ‘manusa’ kinaelezea namna miambili na thelathini za kutengeneza chombo
kinacho ruka angani, namna ya kukiendesha kwa maelfu ya kilometa, namna ya
kutua kwa njia ya kawaida, kwa lazima na kwa kulazimishwa, lakini pia uwezekano
wa chombo hicho kugongana na ndege wa kawaida huko angani! Kama taarifa hii ni
ngano ya kufikirika ya kale, basi hii itakuwa ni moja ya ngano bora kuandikwa
kuhisiana na elimu ya nga kutoka kwenye zama zilizo sahaulika.
Vita vya angani, kama tunavyo vifanya kwenye
zama zetu, si kitu kipya, kwenye zama za historia zilizo sahauliwa, zama ambazo
hazina kumbukumbu yoyote ya binadam zaidi ya ‘mnyama aliyekuwa anajaribu
kuyamudu mazingira yake’ kwenye zama hizo vita vya anga, vita vya nyuklia
vilipiganwa! Vilipiganwa na binadam yupi? Binadam wa Darwin au mwingine?
Kwenye kitabu hicho cha ‘manusa’ silaha za
maangamizi ikiwemo nyuklia vimerikodiwa?
Hiroshima haikuwa sehemu ya kwanza
kupigwa na bomu la Nyuklia na wala Marekani siyo taifa la kwanza kutumia bomu
la Nyuklia!
Nyaraka kutoka kwenye Pyramid zinaeleza kuwa
moja ya kazi za Pyramid ni njia ya kuelekea kwenye uwanda mwingine.
Techonolojia hii sijui kama ‘tumeshaigundua’ au bado tunaijaribu kwa siri kasha
baadae tuite uvumbuzi! Egypt, mungu Isis siku zote amekuwa akichorwa ni mungu
mwenye mbawa anaye ruka angani au anasafiri kwenye chombo maalum kinacho rukwa
angani.
Dhana ya binadam kuruka angani si mpya, ni ya zamani kama walivyo ndege
warukao angani ambao wamekuwa wakimshawishi binadam kufanya hivyo.
Mwanzoni kabisa mwa karne hizoo, binadam na hamu
ya kuruka angani havikutofautishwa kama akili na wazo. Binadam aliwaza na
alitengeneza ndege katika zama hizo zilizo sahaulika. Kutoka kwa binadam wa
kwanza aliyekuwa na wazo la kupaa mpaka zama za mwanafunzi wa ‘mystery Schools’
Leonardo wazo linaonekana kuwa ni moja, michoro, zana, muelekeo na malengo ni
mageni katika zama zao, lakini sawia katika zama tofauti na maeneo tofauti kama
vile muandishi wa mawazo hayo ni mmoja.
Wachache wanajua juu ya elimu ya kuruka
angani na kutengeneza vifaa hivyo, lakini wanajua pia kuwa elimu , vifaa na
zana zake zilikuwepo si tu kwenye zama zao lakini hata zama zilizopita, na
wengine wote tupo kizani tunadhani ni uvumbuzi katika ‘zama’ zetu!
Hamu ya binadam wa zama zilizo sahaulika haikuwa
kusafiri angani tu, bali kusafiri mpaka kwenye sayari na nyota za mbali!
Hamu
ambayo binadam wa leo bado anayo pia, au ameirithi kutoka kwa mababu zake.
Lakini binadam wa leo akijinadi kuwa yeye ndiye wa kwanza kupekeleka chombo
angani; kwenye Mars, kumpeleka binadam mwezini, kama kweli alienda mwezini,
lakini ukweli binadam wa leo siyo wa kwanza kupeleka chombo angani na kwenye
sayari zingine, na huenda akawa anatumia maarifa ya kale mno kutafuta njia ya
kufika kwenye Mars, kwa siri lakini, ili aweze kuwadanganya wenzake kwamba yeye
ndiye mvumbuzi.
Wahindi waliishi Marekani kwa milenia nyingi,
lakini walikuambia ni Columbus ndiye aliye vumbua bara hilo! Wachaga wameishi
chini ya mlima Kilimanjaro kwa muda mrefu kadiri tutakavyo weza kukumbuka,
lakini ni mzungu ndiye aliyegundua mlima huo, kweli? Kama wanaweza kudanganya
kwenye lililo mbele ya uso wako, vipi usiyo yafahamu?
Babilon kuna hadithi iliyo rikodiwa miaka 4,700
iliyopita, hadithi ya Etana inayohusiana na kusafiri angani.
‘Nitakupeleka kwenye kiti cha enzi cha Anu,’
anasema tai. Wakasafiri kwa muda wa lisaa limoja kasha tai akasema: ‘Tizama
chini, dunia imekuwaje?’ Etana akatazama chini akaona dunia imekuwa kama
kabonde na bahari kama kisima. Kisha wakasafiri tena kwa lisaa linguine limoja,
kwa mara nyingine tena Etana akatizama chini, na dunia ilikuwa kama jabali na
bahari kama chungu, baada ya saa jingine moja dunia ilikuwa kama tembe ya
mchanga na bahari haionekani tena!
Anu kwenye ngano za kale ni moja ya ‘wageni’
waliokuja kutoka sayari ya mbali na ‘kumtengeneza binadam’, zaidi pitia bandiko
la ‘NAMTAFUTA MUNGU’ kwenye blogi hii. Hadithi hii ya Etana kutoka Babiloni, ni
ngano au ni kweli Etana alisafiri juu ya mgongo wa tai, haijalishi sana zaidi
ya kuthibitisha kuwa zana ya kusafiri angani kwa binadam ni ya kale mno, lakini
maelezo ya namna ambvyo dunia na bahari zilivyo kuwa zikibadilika kila baada ya
umbali Fulani, inatilia mashaka kuita hadithi hii kuwa ni ngano, sababu ndicho
hasa tunacho kiona leo karne ya ishirini na moja tunapo kuwa safarini angani,
kama hawakusafiri angani ni vipi waliona tunacho kiona leo?
‘Hapa mahala hakuna hewa, utulivu na ukimya wake
haupimiki, na kweusi kama weusi wa usiku mkuu’. Maelezo ya namna hii utayapata
kwenye hadithi ya wananga wetu wa leo! Lakini huo ni mstari kutoka kwenye
kitabu cha kale cha watu wa Egypt kinacho kwenda kwa jina la Book of the Dead
cha zaidi ya miaka 3500 iliyopita.
Maandishi ya kimila ya kihistoria ya watu kutoka
China wame mtaja mtu aliyeitwa Hou-Yih au Chih-Chiang Tzu-Yu, injinia wa mfalme
Yao ambaye alikuwa mpenzi wa mambo ya angani. Mwaka 2309 KK aliamua kwenda
kwenye Mwezi kwa kutumia ndege wa chuma. Ndege huyu wa chuma pia alikuwa anajua
ni muda gani jua linazama na kuchomoza. Je ndege huyu wa chuma siyo kile
tunacho ita ‘space-ship?’
Hou Yih alisafiri kwenda angani na kufika mahala
ambapo Jua lilikuwa halizunguki/ halisafiri.
Kauli hiyo ni maalum sana kwenye
elimu ya anga, kwani huwezi kuona / kuhisi au kudhani Jua halisafiri mpaka
ukiwa angani, kwenye safari ya kwenye mwangu wa anga, mbali kabisa na uso wa
dunia.
Injinia huyu alisafiri na mke wake Chang Ngo, kwenye
safari hiyo ya kwenda mwezini, Chang Ngo anasema ‘Mwezi ni kama tufe lenye kung’aa,
linang’aa kama kioo kikubwa na kIsha ni la baridi sana, mwanga wa mwezi
unatokana na jua’, anasema Chang Ngo.
Ujumbe wa mwanamke huyu wa ki China kwenye
safari hii ya mwezini ndiyo inayo shangaza kwenye hadithi hii iliyorikodiwa
miaka 4,300 iliyo pita. Taarifa za Chang Ngo kutoka maelfu hayo ya miaka
yaliyopita, ndiyo taarifa ambazo leo kwenye karne ya ishirini na moja
tunazisimamia kuhusiana na mazingira ya mwezi. Kwamba aridhi au udongo wa
mwezini ni kama kioo, na kuna baridi mno kushinda vilele vya barafu za
Himalaya!
Je sisi ni wa kwanza kwenda mwezini?
Nani kasema? Taarifa
za zaidi ya miaka elfu nne iliyopita, zinatuambia kile ambacho, ‘tumekivumbua’
kwenye karne ya 21. Ni vipi miaka hiyo tunayo iita ya giza kulirikodiwa taarifa
zinazo thibitishwa ukweli wake na zama zetu zinazo itwa za teknolojia?Too buzy, but I will work this work to the end Inshallah .... see yaa ...
Maaaasha-allaah
ReplyDeleteAllah akujaze pale ulipopungukiwa
ReplyDeleteAllah akujaze pale ulipopungukiwa
ReplyDeleteAmeen
DeleteAllah akujaze pale ulipopungukiwa
ReplyDeleteallah akutie nguvu labda kupitia post zako watu wanaweza wa kaujua ukwel na wakaingia kwenye dini ya haki
ReplyDeletena tukaikimbia mikono ya wamagharibi
allhamdullah allah akutie nguvu kwa kaz yako labda watu wanaeza kujua na kuingia kwenye haki na kusalimika (Islam) na mikono ya wamagharibi.
ReplyDeleteTupo pa1
ReplyDeleteNashukuru sana kwa ujumbe wako ninapo usoma
ReplyDeletepamoja sana mdau
ReplyDelete