Mwaka 1938-39 Wilhelm Konig, mwana historia wa Kijerumani aliokota ‘betri’
zilizo tengenezwa kwa kopa na udongo na kuwa mfano kama wa jagi au kibuyu,
aliokota vifaa hivyo maeneo ya Baghdad, vifaa hivyo vilikariwa kuwa ni vya
zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Baada ya WWII, Willard Gray wa kampuni ya General Electric, aka-copy na ku-paste aina hiyo ya betri ya miaka 2000 iliyopita, na ilipojaribiwa ilifanya
kazi. Ushahidi kuwa Babiloni zama hizo walikuwa wanatumia betri!
Ikumbukwe kuwa utengenezaji wa betri katika zama zetu ulianza mwanzoni mwa
karne ya 19.
Uatikanaji wa Betri hizo za Baghdad ni uthibitisho kuwa, kwenye zama ambazo
tulidhani ni zama za kiza, kiuhakika zilikuwa zama za ‘mwanga’ sababu walitumia
vifaa vya umeme.
Denis Saurat, mwandishi na mtafiti wa Kifaransa alipata ushahidi wa kuwepo
vifaa vya kiumeme Egypt.
Lakini kwa upande mwingine kumekuwa na hadithi juu ya uwepo wa taa za kale
zinazo waka milele bila kuzimika. Imeshindwa ‘kufahamika’ ni aina gani ya
nishati hasa ambayo ilitumika kuziwasha taa hizo zisizo zimika.
Luciana, (120-180 BK) mwandishi maarufu wa zama hizo, anaandika katika
kusafiri kwake kwenye miji ya Hierapolis, Syria, kwenye hekalu lilikuwepo
sanamu ambalo liliwekwa kifaa ambacho giza linapoingia, kifaa hicho
kililiangaza hekalu lote kwa nuru iliyo itoa!
Hekalu jingine la Hadad au Jupiter lilikuwa na kifaa kama hicho ambacho
giza linapoingia basi hekalu zima linajazwa nuru na kifaa hicho.
Pausanias mwana jeografia wa kigiriki anaandika juu ya dhahabu iliyokuwa
ikiwaka kwa mwaka mzima kwenye hekalu la Minerva.
St. Augustine wa 354-430 BK, aliandika juu ya taa ya ajabu ambayo si mvua
wala upepo uliyo weza kuizima taa hiyo iliyo kuwepo Egypt kwenye hekalu la
mungu Isis. Aina hii ya taa ilipatikana Antioch wakati dola ya Bezantiya
ilipokuwa moja ya super power ya dunia, karne ya 6; juzi tu hapo. Taa hiyo ilikuwa
ikiwaka kwa zaidi ya miaka 500.
Hadithi za taa zinazo waka maelfu ya miaka utazikuta, katika miji ya kale
ambayo ustaarabu wao haujulikani ni wapi hasa ulitokea.
India pia zimepatikana aina hizo za taa, ambazo zinadaiwa zilikuwa ni taa
za waungu wao walio itwa nagas, waungu nyoka, na ziliwaka kwa mamia kama siyo
maelfu ya miaka.
Mahekalu yaliyo patikana kwenye miji ya Sumeria, Egypty, Babiloni, India,
Himalaya, Tibet, Peru, Mexico kutaja kwa uchache makuhani na makaburi ya
makuhani hao kume kutikana taa zilizo weza kuwaka kwa mamia kama siyo maelfu ya
miaka.
Taa hizo mahali pengine zinatajwa kama aina fulani ya mawe, katika miji
mingine ya kale na kwenye miji ya chini ya aridhi kumekuwa na maansidhi kwamba
kuna ‘mawe’ yanayo ning’inia hewani na yakitoa nuru wakati wa usiku kama mwezi!
Maswali ni mengi, si kwamba zama hizo zilizo sahaulika walikuwa wanatumia
umeme na betri, lakini walitumia umeme na betri bora kuliko ambazo tulizowahi
kutengeneza kwenye zam zetu.
Betri yenye zaidi ya miaka 2000 inajaribiwa kwenye karne ya 20 na inawaka!
Makaburi na mahekalu yamewekwa taa zinazo waka mamia na maelfu ya miaka!
Hatujawahi kuwa na betri au taa za namna hii, au kuwa na mawe yanayo waka kama
mwezi wakati usiku.
Ni teknolojia gani hii ilitumika, waliitolea wapi ina hii ya teknolojia, ikapotelea
wapi aina hiyo ya teknolojia.
Next post we are going to catch a plane back in time ... planes of ancient world and perhaps destination to the moon...
See yaaaa .... there!
Allahu akbar
ReplyDeleteAllah akufungulie mengi nasi 2pate faida
Tupo pa1
ReplyDeleteShegh 2pe vitu tupate faida koz nataman kujua huyo mjenzi wa haya yote
ReplyDeleteUPO KIMYA SANA MAALIM