Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?
Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.
Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.
Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!
Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%
Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...
Sunday, November 27, 2016
JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? S02, Ep1 (Ujio wa Wageni kutoka Sayari ya Mbali)
Bandiko la Queen Replaced, bado linaendelea, nadhani linaweza kuwa moja ya
bandiko refu kupata kubandiko kwenye blogi hii. Muandishi anaendelea kukusanya
ushahidi na taarifa zingine kuhusiana na kitimbi hichi cha Queen Replaced, na
kadiri taarifa zenye mashiko zitakapo patikana basi nitaendelea kuririka hapa
kwenye bandiko hilo, nadhani litaendelea na episode moja baada ya nyingine
mpaka Mfalme Trump atakapo ondoka au kuthibitisha vinginevyo.
Leo nataka tuizungumzie mada hiyo kwa kina zaidi ...
“Historia ni mtazamo wa zama zilizopita ambapo watu wamekubaliana juu ya
mtizamo huo”- Nepoleon Bonaparte
“Wanao tawala wakati wetu ulio kuwepo ndiyo wanao tawala wakati wetu
uliopita, (na wanao tawala historia yetu, ndiyo wanao tawala hatma yetu) ”- George Orwell
Historia ya dunia inatazamwa katika mitazamo mikuu miwili, historia ya
dunia kwa misingi ya kisekula, na historia ya dunia kwa misingi ya kidini.
Lakini hiyo siyo yote, kuna kundi jingile lenye mtazamo tofauti wa historia ya
dunia; tofauti na mtazamo wa kidini na kisekula ambayo mara zote inakinzana,
kushindana na kila moja ikitafuta upenyo wa kumuangusha mwenzake.
Historia ya siri ya dunia, umeona Mapiramid na alama ya jicho moja.
Mtazamo wa
kundi hili la tatu unajumuisha mitazamo yote miwili, ingawa inaifanyia marekebisho
mitazamo hiyo katika baadhi ya sehemu kabla ya kuikubali, lakini zaidi kundi
hili la tatu linaongezea na kingine zaidi kwenye mtazamo wao; wanaongeza kile
ambacho hakikubaliki au hakiwafikiani na mtazamo wa kidini au kisekula. Kundi
hili na la asasi za siri.
Mchoro wenye maana elfu moja kwenye asasi za siri.
Asasi za siri al-maarufu secret societies kabla ya mapinduzi ya mawasiliano
hasa kwa upande wa mitandao kilikuwa ni kitu kigeni masikioni pa wengi na bado
hata sasa bado ni kitu kigeni mno kwa watu wa kawaida ambao wanaamini kuwa
wanakwenda shule na wakifika huko watasoma na kujua kila kitu, lakini kinyume
chake ni tofauti kabisa.
Shuleni tunafundishwa kuwa wajinga na siyo waerevu.
Huwezi popote pale kwenye mtaala wa somo lolote, chuo chochote duniani ukakutana na somo linalo husiana na ‘secret societies’;
ispokuwa kwa wale ambao si kwamba tunaamini juu ya kuwepo kwa secret societies,
bali tunayo ushahidi wa kutosha kuthibitisha hilo.
Kitabu hichi kinaelezea historia ya asasi za siri.
Tunakubaliana kuwa mwenendo
wa dunia unayo iyona sasa, na dunia iliyo lala nyuma kwenye historia ya miaka
1,000 na Zaidi, na historia unayoisoma na utakayo endelea kuisoma, waandishi
wake walikuwa, nab ado wataendelea kuwa ni ‘secrete societies’.
Jim Marrs akionganisha doti kuthibitisha uwepo wa njama za kuitawala dunia kupitia asasi za siri.
Asasi hizi za siri nazo zinayo mtazamo tofauti juu ya historia ya dunia.
Ukitaka kupata dondoo za historia ya dunia kwa mujibu wa asasi za siri, tizama
kazi iliyo fanywa na mtu anayeitwa, Jonathan Black, kwenye kitabu kinacho
kwenda kwa jina la ‘The Secret History of the World.’ Halafu tazama kazi ya
mwanafalsafa na mwanamasonia wa daraja la juu, bwana Mainly P Hall, kwenye
kitabu chake alichokiita, ‘Secret Teaching of all Ages.
Kitabu hichi kinaelezea historia ya uumbwaji kwa mtazamo wa asasi za siri.
Historia ya dunia kwa upande wa kisekula haijawahi hata mara moja kukiri
juu ya uwepo wa viumbe wengine wenye ‘uhuru’ kama binadam, lakini kinyume chake
imekuwa ikikiri juu ya kuwepo kwa viumbe wa aina hiyo kupitia kazi mbalimbali
za filamu, muziki na vitabu, lakini kazi hizo zimekuwa zikichukuliwa au
kufahamika na watu wa kawaida kama ‘science fiction’.
Kiumbe kutoka sayari nyingine akiwa amejivikangozi ya binadam, kama inavyonekana kwenye series maarufu ya V.
Maelfu na maelfu ya kazi
zinazo zalishwa Hollywood na kwenye makampuni mengine ya filamu kote duniani,
yamekuwa yakitumia elimu ya sekula kuthibitisha juu ya uwepo wa aina hiyo ya
viumbe.
Kumekuwa na kazi nyingii za filamu na vitabu zikitahadharisha umma juu ya uwepo na ujio wa viumbe hao kwa mara nyingine tena. Picha hii ni mfano wa kazi hizo.
Kwa upande wa dini, kumekuwa na hadithi nyingi zinazo zungumzia juu ya
uwepo wa aina hiyo ya viumbe, hadithi kwa upande wa dini, mila na utamaduni wa
jamii mbalimbali kote duniani, zimekuwepo na zimekuwa zikizunguka na kurithishwa
kutoka vizazi hadi vizazi.
Wa-Egypty wa kale ni moja ya jamii ambazo zilijikita sana na hadithi hizi za wageni kutoka sayari ya mbali. Mchoro huu ukionesha mashirikiano hayo baina ya wageni na binadam.
Ingawa zimetofautiana kwa namna mbalimbali, lakini
dhana na maudhui ya hadithi hizo zimebaki kuwa moja; kwamba si binadam pekee
yake mwenye ‘uhuru’ wa kuamua, wapo wengine wenye uhuru kama yeye.
Moja ya filamu zinazo zungumzia dhana ya binadam kuumbwa na viumbe kutoka sayari ya mbali.
Katika mfululuzo wa mabandiko haya ya ‘Je Tupo Wenyewe; Season 2,
tutatizama kwa kina juu ya habari hizi, tutazitizama kote kwa upande wa dini,
kisekula, na kwa uapnde wa asasi za siri, mpaka tutakapo maliza mabandiko haya,
basi tutakuwa na majibu na msimamo sahihi juu dhana nzima ya kuwepo au
kutokuwepo kwa viumbe hao, na kama wapo ni nafasi gani waliyonayo kwenye
ulimwengu huu, je sote sisi na wao tunayo asili moja kwa maana ya Muumba Mmoja
au wao wanao wakao na sisi tunao wa kwetu?
Wgeni kutoka sayari ya mbali kama wanavyo onekana kwenye filamu za leo na majarida mbalimbali. Juu yao ni meli yao ya angani maarufu kama UFO.
Kwa upande wa asasi za siri taarifa na mafunzo yao juu ya chochote kile
siyo kitu unachoweza ukakibeba kama kilivyo, hii ni kutokana na kwamba, taarifa
moja kwao inaweza kuwa na maana alrfu moja kwa watu tofauti wa madaraja
tofauti.
Kichwa cha shetani na alama mbalimbali za asasi za siri ikiwemo freemason.
Mathalani kwenye freemason unapokuwa kwenye daraja la kwanza, au la
pili au la tatu, ambayo ni maarufu kama Blue Degree, mambo utakayo fundishwa
hapo ni tofauti nay ale utakayo fundishwa kwenye daraja la 28 na kuendelea
ikiwa utabahatika kufika huko. Asilimia 80 ya freemason wote duniani wapo
kwenye blue degree.
Piramidi likionesha daraja mbalimbali za freemason.
Wateule wa chache ndiyo wanao ruhusiwa kupanda na kufika
madaraja ya juu. Kwenye Blue Degree Freemason anaambiwa kuwa anaye abudiwa ni
Mungu Mmoja, lakini anapofika daraja la 28, anaambiwa kuwa yale yote aliyokuwa
akifundishwa ni uwongo, na kwamba kuanzia hapo sasa ndiyo atakapo anza
kufundishwa mambo ya kweli, na mojawapo ni kwamba freemason hawamuabudu Mungu
Mmoja, bali Shetani.
Wakubwa wa kifreemason, lakini hawa ni visible freemason na wapo
madaraja ya chini.
Kufika kwenye hizo daraja inaweza kumchukua mtu robo tatu
ya Maisha yake, lakini unapokaribia na kudhani umefika, unambiwa kuwa ndiyo
kwanza unaanza.
Hivyo tunapo itazama historia ya dunia kwa mujibu wa asasi za siri,
hatutaweza kubeba kila kile wanacho tuambia, uchambuzi yakinifu unahitajika
kuchambua almasi kwenye vipande vya vioo.
Shaq O’nel naye ni mfuasi wa Freemason.
Hivyo nitachukua machache kulingana
na mada yetu. Asasi nyingi za siri zinaamini juu ya uwepo wa viumbe wenye
nguvu, busara, elimu, maarifa na mapenzi makuu kushinda binadam. Viumbe hao
kwenye asasi za siri kuna wanao tambulika kama waungu au wenye kusahiki
kutawala na wengine wanao stahiki kutawaliwa.
Waunga wa kale wa Egypt, akiweno Osiris, alama ya jua ambayo ndiyo mungu
mkuu anayeabudiwa tangu enzi na enzi mpaka leo. Waungu hao ni zao la
mchanganyiko wa binadam na wageni kutoka sayari ya mbali.
Kwenye asasi za siri dunia na ulimwengu haujatokea kwa nasibu kama anavyo
dai Darwin, ambaye naye alikuwa ni mfuasi wa asasi ya siri iliyokwenda kwa jina
la . Wala kwenye asasi za siri hawatambui juu ya kuumbwa kwa dunia na ulimwengu
kama zinavyo tambua dini zenye Imani ya Mungu Mmoja; wao wanaamini kuwa nguvu
iliyo umba hii dunia na ulimwengu wote ni nguvu mahususi na maalum ambayo ipo
ndani ya kila mmoja wetu. Pia wanaamini kuwa binadam wa kwanza aliumbwa na
wageni kutoka sayari ya mbali, wageni ambao waliwapatia binadam maarifa na
ujuzi, wageni hao ndiyo walio muumba binadam wa kwanza wa kiume na mwanamke wa
kwanza.
Buzz alipokuwa ana hojiwa na Luccry
King kwenye CNN mnamo miaka ya 2000. Alisema kuwa walipkuwa huko mwezini waliona
dalili ya uwepo wa viumbe wengine. Ingawa tunafaham hawakwenda mwezini, na hilo
nimethibitisha hapa kwenye posti inayoitwa. HATUKWENDA MWEZINI.
Wageni hao walipokuwa hapa duniani walianzisha asasi ya siri iliyo kwenda
kwa jina la ‘Brotherhood of the Snake’ Haidithi hii imetajwa kwenye moja ya
vitabu vinavyo tegemewa sana na asasi za siri, kitabu kutoka kwa jamii ya kale
ya watu wa Sumeria. Hadithi ya nyoka nayo ni hadithi yenye maana elfu moja
kwenye asasi za siri kama tutakavyo ona huko mbele.
Waungu, DNA, kwa juu inaonekana
meli yao ya angani na kwa mbali ni nyota ya Draco wanaposema wametokea.
Wageni hao walikuwa na maumbile mfano wa nyoka au mijusi, nao walikuja
kwenye sayari hii kwa ajili ya kutafuta malighafi, au walikimbia vita kutoka
kwenye sayari yao, au walikuja kwa ridhaa yao kuwafundisha binadam maarifa
mbalimbali, ambayo wao wamesha yafikia kwenye sayari zao.
Vidio fupi ikielezea ikielezea ujio wa viumbe toka sayari ya mbali, kwanini walikuja na jinsi walivyo muumba binadam wa kwanza.
Dhana hii ya wageni
kutoka sayari ya mbali unaweza kuiyona kama ukitazama series ya ‘The Event’,
The V’ na nyinginezo pia filamu kama ‘Transformer 1, 2, na 3, They Lived, Men
in Black na nyinginezo. Kuna maelfu na maelfu ya kazi za namna hiyo zinazo
zungumzia ujio na uwepo wa aina hiyo ya viumbe.
Wageni wakimuumba binadam.
Binadam wa kwanza na kizazi chake walitengenezwa na wageni hao ili waweze
kuwafanyia kazi za kukusanya hizo malighafi. Hivyo walitengenezwa kama aina
Fulani ya watumwa. Baadae wakawaboresha Zaidi na kuwapa uwezo wa kuzaa. Kisha
wakawapatia na maarifa ya juu Zaidi kuhusiana na asili ya waungu na hao
binadam.
Kitabu cha wasumeri kikionesha waungu wanao itwa Annunaki, wakiamuumba binadam kwa kutumia DNA yao na kile kinacho fahamika kama tree of life na zoezi hilo likisimamiwa na mungu anayeitwa ANU, au baba wa mbinguni.
Hili likaleta mvutano baina ya wageni wao kwa wao. Kwani usalama wao
upo kadiri binadam anavyo baki kuwa mjinga wa kutokujua yeye ni nani na kwanini
yupo hapa. Hili likapelekea baadhi ya wageni hao kuungana na binadam dhidi ya
ndugu zao, ndipo asasi ya kwanza ya siri duniani ikatengeneza; The Brotherhood
of the Snake, lengo la asasi hii likiwa ni kuwafundisha binadam na kuwafumbua
macho juu ya asili yao, kwanini wapo hapa na mengine mfano wa hayo.
Asasi hiyo haikudumu sababu wageni waliokuwa kinyume na asasi hiyo
walijipenyeza na kuisambaratisha; baadae zikazaliwa asasi nyingine za siri kama
Freemasonry, the Rosicrucians, The Knight Templars, Ordo Templi Orientis,
Knights of Malta, The Order of the Illuminati na nyingine nyingi.
Asasi za siri si tu kwamba zinatambua juu ya uwepo wa viumbe ‘huru’ mbali
na binadam, lakini kwa milenia kadhaa kama tutakavyoona, asasi za sri zimekuwa
zikiaandaa mazingira mahususi ya ujio wa wageni hao kwa mara nyingine kwa ajili
ya kuwakomboa binadam na madhila wanayo pitia sasa.
Nembo hii maarufu sana kwenye ulimwengu wa afya na utabibu, lakini asili yake ni mbali zaidi ya hapo kama tutakavyoona.
Karatasi za kale za wasumeria zinaelezea kuwa Anunnaki waliokuja na vyombo
vieleavyo angani vyenye umbo kama ya ungo, walikuwa ni kabila la mijusi au
zaidi reptilia. Kwa wayahudi wametajwa kama ‘NEFILIM’ yaani watoto wa waungu au
‘AWWIM’ neno limaanishalo viumbe watambaao kwa tumbo , wafalme wa Egypt na
utawala mzima wa kifarao mara zote wamekuwa wakihusishwa na nyoka, reptilia.
Sina hakika juu ya pcha hii, lakini mengi yamesemwa juu ya uwepo wa binadam wenye maumbo makubwa
Mtafiti mmoja wa kimarekani, David Sielaff anasisitiza kwamba Nefilim siyo
watoto wa waungu bali ni kizazi cha baina ya Binaadam na viumbe wasio kuwa
binadam baada ya muingiliano wao.
Sisemi kuwa picha hizi ni za uwongo, lakini pia sisemi kuwa ni za kweli. Lakini katika dunia ambayo asasi za siri ndiyo watawala, ni vigumu kuwa na jibu la moja kwa moja kwenye mambo kama haya. Lakini ni nukta zinazo paswa kutizamwa kwa jicho la tatu.
Kwenye kitabu cha waumini wa dini ya kikristo, biblia agano la kale kwenye
kitabu cha Mwanzo wavamizi hao wametajwa kama waungu.
“Ikawa wanaadam walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wakike walizaliwa
kwao wana wa mungu waliwaona hao mabinti za wanaadam ya kuwa ni wazuri;
wakajitwalia wake wao wowote walio wachagua. ... tena, baada ya hayo wana wa
mungu walipoingia kwa binti za wanaadam, waka zaa nao wana, hao ndio waliokuwa
watu hodari zamani, watu wenye sifa”
Ni kweli? Sijui fanya uchunguzi wako binafsi.
Bibilia inawataja watu hawa kuwa walikuwa ni mijitu mikubwa mno. Katika
Quran tunajifunza kabila jingine lenye sifa kama hizi kabila la Iram. Quran 8
9: 7 - 8, ambalo nalo limetajwa kama kabila lilikuwa na watu wakubwa mno ambao
hawajapata kupatikana mfano wake katika uso wa dunia na ambalo lilijenga majumba
yao kwa kuchonga na kukata majabali. Sina hakika kuwa ndilo kabila la kizazi
cha wana wamungu kilichotajwa katika kitabu cha Mwanazo kwenye Bibilia ila
uchunguzi zaidi unahitajika.
Wachunguzi wengine wanasema neno hili Nefilim lina maana ya “wale waliodondoka
kutoka mbinguni” neno “watu wenye sifa” katika kitabu cha Mwanzo limefasiriwa
kutoka kwenye neno la Kisumeria “shem” ambalo Sitchin anasema lina maana ya
“gari la angani”. Anasema neno hilo linatokana na mzizi wa neno “shu-mu” ambalo
lina maanisha kile ambacho ni “MU” na MU linamaana ya chombo cha kurukia,
kwahiyo, anaendelea kusema “watu wenye sifa” iliyo tajwa katika kitabu cha
Mwanzo inamaanisha sifa yao hiyo waliokuwa nayo ya kusafiri angani . Kwa hiyo
hii ndiyo jamii iliyoingiliana na wanawake wa kibinaadam.
Bado tunao watu wenye maumbo makubwa katika zama zetu.
Wachunguzi wengi wa mambo kuhusiana na kabila hili la reptilia
wanakubaliana kuwa wametokea katika Nyota ya Draco, iliyopo baina ya Nyota saba
zing’arazo sana, ambazo kati ya majina mengi zijulikanazo kwayo moja wapo ni
Great Bear na ile ilyopo kushotoni mwa nyota hizo yani Little Bear au Northen
Star ijulikanayo kama Alfa. Majengo ya maelfu ya miaka nyuma kama mapiramid ya
Egypt, sanamu la Simba lenye kichwa cha binaadam, Sphinx, lilloko Gaza ambalo
nilazamani zaidi kuliko mapiramidi yenyewe, Angkor Wat lililoko Kambodia, na
mengine huko Japan yaliyojengwa kwa vipindi tofauti kwa kutumia ustadi mkubwa
wa elimu ya nyota, mahesabu, elimu ya maumbo na sayansi ya hali ya juu
yamejengwa moja kwa moja kufuata muelekeo wa Draco.
Wanatoka wapi watu hawa?
Hata hivyo wachunguzi wengine wa mambo wanadai kuwa kabila hilo la reptilia
liliishi katika mashimo na mapango na inawezekana ndipo walipo tokea.
Gazeti la
Horizona la 1909 mwezi wa nne liliandika
habari kuhusu machimbo ya madini yaliyopatikana karibu na eneo la Grand Canyon
lenye ukubwa wa kuchukua watu elfu hamsini pamoja na vitu vingine, vitu kadhaa
vilipatikana vinavyohusiana na kabila hilo la reptilia.
Mashimo mengine mengi
yamepatikana sehemu mbali mbali duniani yanayo elezea hadithi ile ile kwamba
yalikuwa ni nyumba na sehemu za uzalishaji za reptilia.
Sanamu maarufu kama Olmec, sanamu hizi zilipatikana Mexico. Ninani aliyachonga masanamu hayo makubwa hakuna anayefaham. Sura za masanamu hayo ni watu weusi, je mtu mweusi alifikaje Mexico kipindi hicho ambapo sanamu hizi zinasadikiwa kuwa ni za zamani hata kabla ya ustaarabu wa watu wa Mya, Inca na hata kabla ya Columbus kufika Amerika.
Wanakubaliana kuwa reptilia hawa moja wapo ya njia walizo zitumia kumtawala
binaadam katika kila njia ni kujivaa katika mwili wa binaadam kama nguo au
kifupi kama koti kubwa na kuanza kuutawala mwili huo au mtu huyo na pale muhusika
anapo kufa basi reptilia huyo anahamia kwenye mwili wa binaadam mwingine ajenda
ni kuichukua dunia na binaadam ndiyo gari la kufanikisha safari hiyo,
likizimika moja anahamia kwenye gari lingine.
Mchoro huu unamuonesha binadam wa Mexico akipambana na mijitu mikubwa. Ni wapi wa Mexico walizitolea habari hizi?
Kwa sasa wachunguzi huru na wachambuzi wa dini pamoja na wanahistoria
wanakubaliana kuwa kitabu cha Mwanzo kilichopo katika agano la kale
kimechukuliwa kutoka vitabu na kwenye rikodi za vitabu vya Wasumeri wa kale,
kama ambavyo Musa, Nuhu na Ibrahim walivyotajwa katika kumbukumbu hizo za
Wasumeri na kuonekana kuwa ni kweli katika biblia ndivyo ambavyo walivyotajwa
Anunnaki ambao nao kwa mtazamo wa rikodi za Wasumeri ni kweli walikuwepo na
ndivyo ilivyo katika kitabu cha Mwanzo katika agano la kale.
i hiLaurence ni mmoja wa wafuasi wa asasi za siri, na kazi zaki zimekuwa zikitia nuru kazi zilizokuwa zinafichwa na asasi za siri.
Mwandishi mmoja wa
vitabu bwana Laurence Gardner, freemason na anaye jinadi kuwa anayo damu
‘tukufu’ ya waungu, anasema,
“Kila maandishi yaliyopatikana kuthibitisha kuwa Wasumeri waliishi na
Anunnaki yamethibitisha kuwa jamii hiyo ya Anunnaki wakiwemo Enki, Enhil,
Nin-khursag na Inanna walifanya kazi mbalimbali za kijamii hapa duniani.
Walikuwa ni wasimamizi na viongozi, walimu na wanasheria, wataalam wa maarifa
mbalimbali, teknolojia na wafalme... Kukubali kuwepo kwa Anunnaki ni jambo
litakalo wachanganya wanahistoria, lugha yao itawakanganya wataalam wa lugha, na
teknolojia yao ya hali ya juu itawachanganya na kuwaacha vinywa wazi wataalam
na wanasayansi wetu, lakini endapo tutakataa kuwepo kwao huo utakuwa ni upuuzi.
Wasemeriani wenyewe wameshatuambia kuwa Anunnaki ni akina nani na wapi
walikuwepo na hakuna sayansi na au historia itakayo weza kutuambia vinginevyo.”
Rikodi za Wasumeria zimeelezea kwa mapana habari za Anunnaki pamoja na
jamii yao wakiwemo Enki, Enlil, Ninki, Inanna, Utu, Ningishzida, Marduk na
wengine wengi. Habari iliyotawala katika hadithi nzima ya watu hawa ni vita
baina ya vizazi hivi na hasa Enki na Enhili, hadithi ambazo pia tunaweza
kuzipata kutoka kwenye kitabu cha Mwanzo katika gano la kale.
i hiWaungu wa kale wa Babiloni. Tizama maumbo yao ni kama mjusi.
Lakini hata hivyo
jamii hiyo ilikuwa na zaidi ya vita baina yao, ilihusisha waungu wa kike na
waungu wa kiume katika mabaraza yao ambayo kila wakati yalikutana kupanga na
kutatua matatizo baina yao na pia kujadili hatma yao kwa wakati ujao na hatma
ya binaadam kiumbe ambaye ana nguvu sawa na wao, kiumbe ambaye ni huru kama
wao.
Inasemwa walipigana vita vya kinyuklia.
Miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia kuongezeka katika vyombo vya habari
kazi mbalimbali zenye maudhui kuhusu Reptilia katika sura ya Dragon, Dinosaur
na Reptilia wenyewe.
Soko la vyombo vya habari, sanaa, michezo na burudani
mbalimbali limetawaliwa kwa wingi na maudhi ya viumbe hawa na kulifanya soko
lake kuwa ni kubwa mno kutoka kwenye midoli na vikaragosi vya watoto mpaka
kwenye sinema zilizo pata mafanikio makubwa. Lakini kile ambacho wengi hawafamu
ni kuwa binaadam tunaandaliwa taratibu kukubalina na kuwepo viumbe vya aina hii
ifikie kiwango ambacho kila mtu anatamani kuwaona viumbe hao, hii itapunguza
upinzani pale wakati utakapo fika ambapo waungu hao watakaporudi katika uso wa
dunia na kuishi nasi kama awali.
Athari ya waungu hawa tunaipata zaidi katika umbile la nyoka. Katika jamii
nyingi za kale na hata za sasa nyoka anahusishwa na hekima, maarifa, matibabu
ambapo nembo nyingi za tiba duniani zinatumia alama ya nyoka, alama ambayo
unaweza kuiyona pia kwenye noti ya shilingi mia tano ya Tanzania.
Alama ya asasi ya siri ya Brotherhood of the snake.
lakini pia
alama ya pesa kwa dola ya Marekani ni herufi ‘S’ na ‘I’ ambapo kwa pamoja
zinatengeneza alama ya ‘$’ ambayo ni alama ya nyoka aliye jiviringisha kwenye
mti. Nyoka amehusishwa na maajabu pamoja na mazingambwe rejea hadithi ya mtume
Musa na wachawi wa Firauni, rejea hadithi za wahubiri waliobadilika na kuwa
nyoka mbele ya waumini wao. Kutoka Babylon, Mexico, Egypt na kwengineko duniani, hii ni alama
tukufu na ya maajabu katika mambo mbalimbali.
Mabudha mmoja wa mwanafalsafa wao anayeitwa Nagarjuna wa India huoneshwa
akiwa na miali ya mwanga inayowakilishwa na nyoka saba, ambayo hiyo ni alama ya
daraja la juu katika utawa wa kibudha. Alama ya nyoka saba ambao mara nyingi
huwa ni Kobra pia ni inapatikana kwa wamasonia mpaka kwa Mafarao wa Egypt.
Nagarjuna
Afrika Magharibi tunakutana na hadithi ya mungu aliyeitwa Nana-Buluku na
msaidizi wake ambaye ni mungu nyoka aliyeitwa Da. Hadithi kama hii utaikuta
Afrika ya Kusini kwa jamii ya Wazulu, utaikuta Scandanavia, Mexico na kwa
makabila mbalimbali hapa nyumbani Tanzania.
Medusa, mungu wa Babiloni ya kale.
Tuitizame India kidogo ambako hadithi kuhusu kile kinachoitwa mungu nyoka
kina nafasi kubwa katika jamii hizo. Kwa jamii mbalimbali za wahindi mungu
nyoka anajulikana kama Nagas. Waungu hawa wanaishi katika matabaka kadhaa
yaliyoko chini ya aridhi, matabaka hayo yako saba na hivyo dunia saba, Mexico,
Uturuki na England na baadhi ya sehemu zingine duniani pia wana hadithi hii ya
matabaka saba na au dunia saba zilizo chini ya aridhi. Katika dunia hizo za
chini ya aridhi waungu hao wanasadikiwa kuwa ndiyo walinzi wakubwa wa mali za dhahabu
na vito vingine vyenye thamani katika macho ya mwanaadam na hii ndiyo sababu
kuu ya makafara mbalimbali yafanywayo na wachimba madini katika sehemu
mbalimbali duniani ili kuwaridhisha waungu hawa wa aridhi saba na au dunia saba
waweze kutoa mali hizo.
mungu wa chini ya aridhi, au mungu wa kuzimu kwa watu wa Egypt ya kale.
Matabaka hayo saba kwa wahindi ni Atala, Vitala, Sutala, Talatala,
Mahatala, Rasatala na Patala. Katika Dunia hizo saba zilizopo chini ya aridhi
kutokana na mafundisho ya kihindi, Mexico na kwa Wagiriki wa kale kunapatikana
nyumba nzuri mno, bustani na vitu vingine vya burudani kwa wakazi wa nchi hizo.
Wakazi wengi wa nchi hizo za chini ya aridhi wanajulikana kama Daityas, Danavas na Nagasi ingawa sehemu
zingine duniani wanaweza kujulikana kwa majina tofauti, umewahi kusikia hadithi
ya mji ulioko chini ya Ziwa Victoria? Ni mfano wa hadithi za miji saba katika
matabaka saba chini ya aridhi katika jamii tofauti duniani.
Kumekuwepo na miradi mikubwa mikubwa ya kujenga makazi chini ya aridhi kama tutakavyoona kwenye mfululizo wa posti hizi.
Miji yao imejengwa na kurembwa kwa ustadi mkubwa na inahesabiwa kuwa na
kila kinacho patikana katika miji yetu ya uso wa dunia, ispokuwa jua, na hivyo
hawana mchana wala usiku ingawa miji hiyo imepambwa na mataa makubwa makubwa na
inang’ara kama jumba la Taj Mahal, hizi ni ngano kutoka kwa jamii mbalimbali za
kihindi, pia ni ngano unazoweza kuzipata katika jamii zingine tofauti duniani,
lakini nashindwa kuendelea kuziita ngano pale ambapo hadithi hizo
zinapothibitishwa na watu mbalimbali ambao wao binafsi wamepata kufika katika
nchi hizo, na au athari na ushahidi wa nyoka hao wenye maarifa zinapo patikana
katika uso wa dunia yetu na hata wakati mwingine kutembelewa na watu
waliozaliwa na kuishi huko kama tutakavyoona. Hupaswi kuamini unapaswa kuelewa.
Imekuwaje binaadam akatawaliwa na hayawani? Nini hasa kilitokea mpaka
binaadam akatawaliwa na mijusi? Kiumbe ambaye ni huru mwenye uhuru kamili
atawaliwe na kiumbe asiye na uhuru anayeishi kwa kufuata silka yake inawezekana
vipi? Binaadam alitawaliwa na bado anaendelea kutawaliwa na binaadam mwenzake
katika hali mbalimbali lakini hii ni kwa sababu wote ni binaadam, wanatabia
zinazo fanana, kibaiolojia, kikemia na kifizikia na juu ya yote hakuna kiumbe
aliyepatikana na uwezo mkubwa wa kiakili kukabiliana na mazingira yake kama
binaadam vipi atawaliwe na kilicho duni kishinda yeye?
Sayari ambayo viumbe hao wanadai wametokea kama ilivyoandikwa kwenye
karatasi za kale za Wasumeria yaani sayari ya Neburu inamashaka kuwepo kwake,
na pia katika sayari zingine ambazo waandishi na wachunguzi mbalimbali wanahisi
wametokea huko hakuna ushahidi unao onesha athari kuwa viumbe hao walipata
kuishi katika sayari hizo.
Viumbe hao ni akina nani? Je kweli walipta kuwepo au ni ngano za kale tu? Kwanini waliondoka, je watarudi tena? Maswali ni mengi lakini yatajibiwa hapa hapa. catch me here next time ....
Mm binafsi napenda kulijua ilo mm mama mm naona niurongo mana majini niwaongo.
ReplyDeletestay tune mdau elizabeth ...
Delete