Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Saturday, May 3, 2014

BAADA YA IMF na WB nini KINAFUATA ...



Benki ya Dunia (WB) inakopesha fedha kwenye nchi za dunia ya tatu kwa ajili ya kuratibu na kuendeleza miradi ambayo inahitajika kwa manufaa ya nchi ‘wahisani’ a.k.a nchi wadhamini.  WB inapowezesha kifedha miradi ambayo haina tija wala manufaa yeyote kwa wakazi wa eneo husika; utambue kuwa na uchumi wa eneo hilo unazoroteshwa.


International Monetary Fund (IMF) wanakuja kama mwokozi pale ambapo fedha zilizo tolewa na (WB) zinapofanya kile kilicho kusudiwa, ambacho ni kuuzorotesha uchumi wa nchi husika na wakati huohuo kuzifanya fedha hizo kuwa ni mzigo usio lipika.  (IMF) wanapoingia wanatoa mikopo zaidi na hivyo kuongeza deni lisilo lipika kuwa ni kubwa zaidi, lakini mikopo hiyo inakuja na masharti, kama vile ‘uongozi mzuri’, ‘utawala bora,’ ‘haki za mashoga,’ ‘kutoa aridhi na rasilimali nyingine kwa wawekezaji.’
Kuna kile kinacho fahamika kama ‘free trade’, ambacho kinahusisha makubaliano ya kimataifa kama vile GATT, NAFTA na APEC ambayo yanachukuliwa kama ni kitu kizuri na bora zaidi na mawakala wa Illuminanti, sababu ni mfano ‘mzuri’ wa mashirikiano ya kimataifa. Lakini wasicho kijua mabilioni ya watu ni kuwa ‘free trade’ inaigeuza dunia nzima kuwa tegemezi wa bidhaa kutoka kwenye mashirika ‘mahususi’ ya kimataifa.

Majina makubwa kwenye biashara kama vile NIKE, GAP, PEPSI, TN, LEVIS’S, REEBOK, CALVIN KLEIN, COCA COLA, ADIDAS, MC DONALD, na mengine na mengine. Haya ni mashirika ya kimataifa ambayo bidhaa zake zipo kwenye kila kona na uchochoro wa dunia hii, bidhaa zake ndiyo bidhaa unazozikuta kwenye maduka makubwa kama ‘Mall’ na vijiduka vidogo vya kina ‘Mangi’. Maana yake ni kuwa bidhaa za wazawa wa eneo husika hazitauzika, viwanda vyao na teknolojia yao itadumaa na wataishia kuzalisha malighafi zitakazo nunuliwa kwa bei ya chini na mashirika hayo, ambayo baadaye watarudi na bidhaa watakayo uza bei kubwa maradufu kushinda malighafi walizo chukua. 

Mbaya zaidi ‘free trade’ inaondoa zoezi la kutoza ushuru baina ya nchi washirika, bidhaa za ndani zinapoteza ulinzi dhidi ya bidhaa kutoka nje kwa kutotozwa ushuru. Hivyo vijinchi vyetu katu havitakaa vinyanyuke kiviwanda wala teknolojia, siku zote tutaendelea kuwa tegemezi kwenye bidhaa za mashirika ya kimataifa. Kwa vile hatutaweza kulipa deni la (WB) na (IMF) wameongeza mzigo wa deni hilo, aridhi yetu inakuwa ni mali yao, mali ya mashirika ya kimataifa kuitumia watakavyo. WAKO WAPI WASOMI WANAO SEMA AFRIKA TULIPEWA UHURU? MBONA ARIDHI ZINAKWENDA? MASHIMO YA MADINI NA VISIMA VYA MAFUTA VINAKWENDA?



Chakula nacho ni nukta ya muhimu kwenye hili. Sasa yananyanyuka mashirika ya kimataifa yenye sura kama NIKE au ADIDAS, lakini haya si kwenye viatu au nguo; Ila kwenye chakula. Hivi sasa nchi zetu za dunia ya tatu zimekumbwa na mafuriko ya kuangamiza mbegu zetu za asili na kutupatia mbegu za kisasa, tizama posti hii,  http://salimmsangi.blogspot.com/search/label/gmo
   Utazisikia serikali zetu, maajenti wao na maajenti wa Illuminanti wakilipigia sana jambo hili zumari, na kulipigia debe mno, kwamba hatma yetu suluhisho la njaa zetu, ni mbegu za kisasa. Loh! Tumekuwa ‘wajinga’ na ‘wapumbavu’ wa mwisho, tunapewa kichupa chenye rangi ya dhahabu na sisi tunatoa dhahabu halisi!!! Kwa utaratibu huu sasa, 90% ya chakula wanacho kula walimwengu kipo kwenye mikono ya mashirika ya kimataifa  machache yenye kuhesabika. Huu ni msiba juu ya msiba.

KAMA UNAZO MBEGU ZAKO ZA ASILI ZITUNZE NA ENDELEA KUZALISHA KWA MBEGU HIZO NA WARITHISHE WANAO, KAMA UNAVYO WARITHISHA MALI ZINGINE, SABABU SIKU ITAFIKA, DUNIA NZIMA HAKUTAKUWA NA HATA MBEGU MOJA YA ASILI ...


Katika mfumo wa uchumi tulio nao sasa, mashirika yote hayo ya kimataifa ni mali za wamiliki wa mabenki au punde yatakuwa hivyo kama bado. Ikiwa hivyo ndivyo basi utambue na aridhi ambazo mashirika hayo wanazipora kwa vijinchi hivi vinavyo endelea ni mali za mabenki hayo au punde zitakuwa kwenye mifuko yao.
Illuminanti wanaulinda mfumo huo kwa kila aina ya nyenzo waliyo nayo, sababu ndiyo mfumo pekee ulio fanikiwa kuitia kwenye mifuko yao kila serikali duniani na kila raia, hata yule ambaye bado hajazaliwa!!!


Mfumo huu, ukamilifu wake utakuwa pale ambapo ulimwengu mzima umeingizwa kwenye mfumo mpya utakao fahamika kama, ‘electronic money systeam.’

Kinacho hitajika ni kitu kimoja tu, anguko la kiuchumi ambalo ukubwa wake litaigusa kila kona ya dunia, na joto lake kila mtu atalihisi na hapo kelele zitapigwa za kutaka kitu kifanyike. Na mpango ulikuwa ukingojewa taratibu, kama hawataki vile, utaingizwa na kuanza kufanya kazi.

Kumbuka hazina ya nchi mbalimbali duniani leo haipo kwenye ‘DHAHABU’ kama ilivyo kuwa awali, hazina hiyo ipo kwenye sarafu ya DOLA au EURO. Kinachotakiwa ni kitu kimoja tu, kuiporomosha thamani ya DOLA, na kila ambaye hazina yake ipo kwenye dola, lazima atakaa chini kama si kuzimia kabisa.

Hakuna nchi ambayo itaweza kulipa deni lake, lakini mbaya zaidi, aridhi, mashimo ya dhahabu, na maeneo mengine yaliyo chukuliwa kama dhamana na mashirika ya kimataifa yanaingia kwenye mifuko ya mabenki.



Kwa maneno mengine dunia yote na rasilimali zote zinakuwa mali yao.

Mfumo huu wa fedha wa Illuminanti umejengwa kwenye misingi ya ‘kuondoa thamani halisi ya pesa.’ Kwenye mzunguko wa pesa zote duniani, na kuingiza pesa ambazo hazina thamani halisi ya pesa kwenye mzunguko huo. Pesa ambazo ziko kwenye mzunguko kote duniani, hazina thamani ya kuitwa pesa, ni makaratasi tu, hivyo ni jambo jepesi kwa Illuminanti kuyashusha thamani makaratasi hayo kwa namna watakavyo.

Wanapo shusha ‘thamani’ ya sarafu kwa nchi fulani, basi gharama za wafanyakazi, mali, samani, na huduma zinakuwa chini karibu na bure, na nchi husika haitakuwa na uwezo wa kulipa deni lake, samani zake zinachukuliwa kwa bei ya kutupwa na nchi wahisani a.k.a wamiliki wa mabenki.

Hatma yake ni kuwa, sehemu moja ya dunia kuna watu ambao daima wataishi raha mustarehe kwa gharama za wengine, yaani kwa gharama ya vijinchi vyetu ambavyo wafanyakazi wetu watafanya kazi kubwa, ngumu kwa bei ya kutupa kabisa, umasikini utaendelea kukua na rushwa haitokufa kamwe.



Tutadanganywa tutengeneze taasisi za kuzuia rushwa, lakini taasisi hiyohiyo itakuwa ni mtuhumiwa namba moja wa jinai ya rushwa, sababu haitakuwa na uwezo wa kupambana na mzizi wa fitina, bali kila uchao itapambana na matokeo au athari za rushwa, lakini palipo na mzizi wa tatizo katu patasogelewa.

Thamani ya sarafu kwa nchi husika inaposhushwa, IMF wanaingia na sera za ubinafsishaji wa Mashirika ya UMMA, Illuminanti ambao walikuwa nyuma ya mchezo wote huu wanawatuma mawakala wao kuja kununua visima vya mafuta na nishati nyinginezo, mashimo ya madini na mashamba n.k, lakini bei ambayo ipo chini sana kulingana na thamani halisi ya vitu hivyo.

Lakini Illuminati kama ulivyo mfumo wao wa kibeberu, hawaridhiki kwa kuishi kwa kuwanyonya wengine kwa kutumia mfumo wao wa fedha ulio mbaya na uovu kupita. Lakini zaidi hatua ya mwisho wa mpango huu ni kumfanya kila mmoja wetu katika uso wa dunia kuwa mtumwa!


Mfumo huo utapelekea kusimamishwa kwa dola ambayo kiongozi wake si mwingine bali ni Masihdajjal / Mpinga Kristo.

Kila Myahudi anafahamu ya kuwa na anaamini, juu ya ujio wa kiongozi wa kiroho, ambaye mlango wa historia ya dunia kwake yeye utafungwa, atakuwa ni mfalme na mtume, na makao makuu yake yatakuwa ni Jerusalem, jiji la wafalme kama wanavyo litambua Illuminanti, lakini Waislam tunalifahamu hilo ni jiji la Mitume wa Allah.

Wayahudi wanaamini juu ya Masiha ambaye atalikomboa taifa hilo na kusimamisha dola ya Kiyahudi kwenye aridhi takatifu ya Jerusalem, na kuwafanya Wayahudi kuwa ni watawala wa Dunia.
Baada ya yote kama vile Wayahudi wameshinda. Aridhi yao imekombolewa 1917, na ulimwengu umeshuhudia mamilioni ya Wayahudi wakirejea Jerusalem miaka 2000 baada ya kutimuliwa hapo.  Israel sasa imekuwa na inaelekea kuchukua nafasi ya U- Super Power wa Dunia. Punde tu inaonekana Israel itawanyang’anya Marekani kiti hicho. 

‘Elcetronic Money’ ndiyo itakayo wapatia Israel nafasi hiyo waliyoingojea kwa miaka 2000.



Utakumbuka April 1933 baada ya kile kilicho fahamika kama ‘great Depression’. Serikali ya Marekani ilipitisha sheria ambayo iliwakataza raia wa nchi hiyo kumiliki sarafu za dhahabu, dhahabu, minara ya dhahabu au cheti kinacho tambulisha kuwa unamiliki vitu hivyo. Kwa maneno mengine sarafu za dhahabu au dhahabu kwa namna yoyote ile, kisheria haikuwa tena ikihesabika kama ni pesa, ‘Legal Tender.’ Kama yeyote angekutwa na vitu hivyo baada ya tarehe fulani basi angepigwa faini ya dola 10,000 na au kifungo cha miezi 6 au vyote pamoja!


Wananchi walitakiwa kuzipeleka hizo sarafu za dhahabu, dhahabu, minara ya dhahabu au cheti kinacho thibitisha kuwa unamiliki vitu hivyo, walivipeleka kwa Federal Reserve Bank, ambayo ni taasisi ya fedha inayomilikiwa na watu binafsi, na siyo Serikali. Wanao miliki Federal Reserve Bank kwao kumiliki vitu hivyo hakukuwa na hatia ingawa nao walikuwa ni raia wa kawaida, na taasisi hiyo ilikuwa ni yao binafsi na wala siyo ya Serikali, na hata sasa bado inamilikiwa na watu binafsi.



Fedaral Reserve ilicho fanya baada ya kupokea dhahabu hizo halisi, iliwapatia wananchi wa Marekani makaratasi yaliyoandikwa tarakimu, na hapo tarakimu hizo ndizo zilikuwa thamani ya makaratasi hayo. Ukipewa karatasi lililoandikwa $ 20, hiyo inayo maana kwamba, unamiliki dola ishirini. Kwa kila wakia (ounce) mmoja wa dhahabu Federal Reserve walitoa karatasi lililoandikwa $ 20 likiwa na maandishi ‘Legal Tender.’


Kwasababu taarifa hii ilitolewa kiserikali, na walimwengu wanayo tabia ya kukikubali KILA KILE AMBACHO SERIKALI IMESEMA, basi Wamarekani wengi, walikimbilia kwenye Federal Reserve Bank na kubadilisha dhahabu zao halisi kwa makaratasi yaliyo andikwa Legal Tender. Wachache waliokuwa wakifahamu hatima ya mchezo huo nini, walizinunua dhahabu zile kwa sarafu za makaratasi na kuzihamishia kwenye benki za Uswis.
Kipindi hichohicho benki ya Uingereza ikafanya mchezo kama huo kwa raia zake.


Baada ya dhahabu zote za Marekani kuwa kwenye mikono ya Federal Reserve Bank, wahuni hao wakaanza ule mchezo wao, mchafu, wakashusha thamani ya yale makaratasi waliyo wapatia watu, a.k.a sarafu za makaratasi kwa 41%. Halafu Januari 1934 wakapitisha sheria ya kutengua sheria ya awali na hivyo kuwaruhusu Wamarekani kumiliki dhahabu tena, lakini sasa watanunua kwa $35 kwa wakia mmoja wa dhahabu. Kwa maneno mengine raia waliporwa 41% ya utajiri wao katika zoezi hilo. 


Unaweza kuona sarafu za makaratasi zinavyokuwa rahisi kuzipandisha na kuzishusha thamani. Lakini si hivyo tu utajiri wote ambao umethaminishwa kwa sarafu za makaratasi unashuka thamani pale makaratai hayo yanapo shushwa thamani. Hichi ndicho IMF anacho fanya kwenye vijinchi vyetu pale wanapo shusha thamani ya sarafu zetu, na kupora utajiri wetu kama ambavyo Federal Reserve walivyo wapora raia wa Marekani 1934.
Illuminanti hawakuishia hapo, wakaenda kutengeneza chombo, kitakacho bariki muundo wa wa ‘Sarafu za Karatasi’ kimataifa, mahala palipo fahamika kama Bretton Woods, mwaka 1944, wakaunda IMF.




IMF, AMBAYE KWA KUTUMIA MFUMO HUU WA FEDHA ZA MAKARATASI, SASA IMF NI MMILIKI HALALI WA ARIDHI KUBWA, MACHIMBO YA MADINI, MAFUTA NA MALIGHAFI NYINGI KATIKA NCHI ZINAZO ENDELEA, HATA KATIKA MIKUTANO YA KIMATAIFA INAYOHUSU MAMBO YA FEDHA NA UCHUMI IMF NDIYO MWAKILISHI WA NCHI HIZI!!!!!


Utawasikia watoto wa mjini wakisema ‘Nchi ishauzwa hii.’ Maneno yao hayapo mbali na ukweli.

IMF, ililetwa kazi moja tu, kubariki mfumo huu wa pesa kimataifa na kuwa ndiyo chombo pekee chenye mamlaka ya kushusha thamani ya sarafu yeyote ile duniani pale ambapo itaona inafaa kufanya hivyo.

Wakati Illuminanti wakizipatia nchi zilizo kuwa chini ya utawala wa kikoloni ‘uhuru’ wao, kwa upande mwingine walihakikisha nchi hizo zina fungamana na IMF katika masuala yao yote ya kiuchumi na fedha.

‘Katiba’ ya IMF ambayo inapaswa kusainiwa na nchi wanachama, imesema waziwazi kuwa, ‘NI MARUFUKU KWA DHAHABU KUTUMIKA KAMA PESA.
Mwongozo huo umefanya hivyo kwa kukata mahusiano yeyote yale kati ya ‘Dhahabu’ na ‘Pesa,’ kwa maneno mengine thamani ya ‘Dhahabu,’ itapimwa kwa karatasi na siyo vinginevyo. Lakini pia baada ya kuiondoa dhahabu kwenye kipimo cha utajiri na thamani ya kitu, wakaweka MBADALA.

UNAUJUA HUO MBADALA?

NILIDHANI HAUTA ULIZA!

MBADALA WENYEWE NI SARAFU YA DOLA au EURO.
HIVYO BASI NCHI WANACHAMA BADALA YA KULUNDIKA DHAHABU KWENYE HAZINA ZAO, WANALUNDIKA MAKARATASI YA DOLA NA EURO!!!!!!
LAKINI SI HIVYO TU, NA THAMANI NA UTAJIRI WA NCHI HUSIKA HAUPIMWI KWA MIGODI MINGAPI YA VITO, AU NISHATI, AU MALI ASILI, LAKINI KWA MAKARATASI KIASI GANI YA DOLA ua EURO, INAYO YAMILIKI.
HIVYO BASI VIONGOZI WA NCHI HIZI ZA DUNIA YA TATU WANAKIMBIZANA USIKU NA MCHANA, KUUZA RASILIMALI ZAO, KAMA MADINI YA ALAMASI, DHAHABU, TANZANITE, GESI MBALIMBALI, MAZAO NA HATA ARIDHI, KWA BEI YA KUTUPWA ILI WAWEZE KUYAPATA MAKARATASI HAYO YENYE NEMBO YA $ AU €.
UPO HAPO?
NI KUULIZE SWALI ..?
‘UNAFAHAMU MWANAUCHUMI AU KIONGOZI YOYOTE YULE WA NCHI YAKO ANAPOSEMA UCHUMI UMEKUWA KWA ASILIMIA 3.7, au 4.6, au 7.... UNAJUA ANAMAANISHA NINI?

NGOJA NILIPOTEZEE JIBU LAKE KWA SASA NISIJE KUIITWA MCHOCHEZI BURE!

Art. 4. Section 2(b) of the Articles of Agreement stated: “exchange arrangements may include (i) the maintenance by a member of a value for its currency in terms of the special drawing right or another denominator, other than gold, selected by the member, or (ii) cooperative arrangements by which members maintain the value of their currencies in relation to the value of the currency or currencies of other members, or (iii) other exchange arrangements of a member's choice.”
Umekiona kipengele hicho, si maneno yangu jamani.
Hivyo kama Tanzania inataka kununua bidhaa kutoka Kenya, hawawezi kutumia SARAFU YA SHILINGI, sababu hii kwenye mkataba wa IMF inafahamika kama ‘LOCAL CURRENCY,’ ambayo inakubalika kote ndani ya Tanzania kama ‘karatasi halali a.k.a fedha halali a.k.a legal tender.’ Lakini hii ni ndani ya Tanzani, inapovuka mpaka kwenda nchi nyingine hii si fedha halali kwa nchi ile, hivyo inabidi ipatikane sarafu ambayo nchi washirika katika biashara watakubaliana kuitumia kama ‘msulihishaji’ katika utaratibu wa ununuzi wa bidhaa, IMF sarafu yenye sifa hii inatambulika kama ‘International Currency a.k.a foreign Exchange a.k.a € a.k.a $.

Hivyo basi serikali ya Tanzani lazima iwe na Dola za kutosha ili kuweza kununua bidhaa na mahitaji yake ya kimataifa kutoka nje, hali kadhalika nchi nyingine yeyote ikitaka kufanya hivyo. Hivyo Tanzania haiwezo kwenda Kenya na mirundi ya dhahabu ili ipate bidhaa kutoka Kenya, dhahabu zimefanywa ni makarasi yasiyo na thamani, na makaratasi yakafanywa kinyume chake, na ikifanya hivyo itakuwa imekiuka mkataba wake na IMF, HIVYO ITAINGIA MATATANI.

Kwa kufanya hivyo IMF inazilazimisha nchi zote zilizo ingia mkataba na yeye ku-demand kila wakati kuwa na sarafu za Dola au Euro ili uchumi wao uweze ‘kukuwa.’ Federal Reserve anacho fanya ni KUPRINTI MAKARATASI HAYO NA KUTULETEA KWA GHARAMA YA UTAJIRI WETU HALISI!!!!!!!!!!!!! HALAFU WAO WANAUCHUKUA UTAJIRI HUO NA KUTUACHIA MAKARATASI YAO.
JAMANI KWANI NA SISI HATUWEZI KUPRINTI HAYO MAKARATASI?
NADHANI MOJ YA HAKI KUBWA AMBAYO BUNGE LA KATIKA LINAWEZA KUWATETENDEA WATANZANI, NI KULIGUSA HILI SUALA LA PESA AU KWA UWAZI ZAIDI BANK vs PEOPLE.
KATIKA KATIBA INAYO TUMIKA SASA, BUNGE HALINA MAMLAKA YEYOTE JUU YA SUALA LA FEDHA, KUANZIA UTENGENEZWAJI WAKE MPAKA KUINGIZWA KWENYE MZUNGUKO. HATA RAIS WA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA KWA MUJIBU WA KATIBA HIYO HANA MAMALAKA HAYO, SASA JIULIZE YAPO KWA NANI?
USISHANGAE UKIULIZWA HIVYO UKAAMBIWA KUWA JESHI LITACHUKUA NCHI. MH! JAMANI UKISTAAJABU YA MUSSA UTAONA YA FIR’AUN.


Mpango huu wa Kishetani malengo yake makuu ni kuzifanya Sarafu teule kama Dola, Euro, Pound, na za mawakala wengine wa Illuminanti, siku zote kuwa na thamani kubwa na yenye kuendelea kukua dhidi ya sarafu zingine zote duniani, ambazo siku zote zitakuwa kwenye kitanzi cha kuporomoka. Wanapo utaka utajiri wa nchi yeyote ile, cha kufanya ni kuishusha thamani ya sarafu yake, kinacho fuata ni deni halilipiki, na samani zako ulizoziweka kama hazina zinahamia kwenye mifuko ya Illuminanti kupitia mikono ya IMF. Watakuletea ‘policy’ kadha wa kadha kama vile, ‘restructure programme’, Structure Adjustment Programme, MKUKUTA na mengine na mengine, lakini tayari wameshakupora.


Nchi zilizo lengwa kuporomoshwa katika mfumo huu, ambazo sasa zinaitwa nchi za dunia ya tatu a.k.a nchi zinazo endelea katu hazitafanikiwa kuitwa nchi za dunia ya kwanza, wala nchi zilizo endelea, wala kutimiza malengo ya milenia wala Big Result Now, hakuna, na hakuna mwanauchumi yeyote yule atakaye weza kusimama mbele ya umma na kuwaambia wananchi wake kwamba tutaweza kuyafanikisha haya, labda awe ni mwongo, mwendawazimu au hajui anacho kisema.

Vijinchi vyetu hivi vitaendelea kunasa kwenye mitego mikubwa ya mabilioni ya dola na euro kama ‘mikopo’ ambayo daima tutapambana kuilipa kwa sarafu yetu ambayo kila wakati inaporomoka thamani yake, na kwa njia hiyo utajiri wetu halisi utaendelea kunyonywa mpaka siku moja watoto wetu wataamka kwenye nchi yao iliyo na sifa ya kuitwa ‘nchi ya maziwa na asali,’ ikiwa haina chochote zaidi ya vumbi tupu.



Ule wakati ukifika ambapo mwali mpya, ‘Israel’ anaingizwa kwenye kiti cha U-Super Power wa NWO, SARAFU YA Euro na Dola zitaporomoshwa thamani yake, sababu dunia nzima imeweka hazina yake kwenye makaratasi hayo, zitajikuta hazina chochote zaidi ya makaratasi, itakuwa balaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. Itakuwa vitaaaaaaaaaaaa, vuruguuuuuuuuuuuuu, mauwajiiiiiiiiiii, fujoooooooooo, kila kona na kila mahala kwenye dunia hiiiiiiiiiiiii. Israel watakuja na suluhisho, Electronic Money, hili nalo ni balaaaaa jingine, ukiona hivyo tambau sekunde yeyote kutoka hapo Dajjal / AntiChrist / Mpinga Kristo atatangazwa kwamba yupo kwenye dunia yetu ya 3D, NA NDIYO KIONGOZI WA DOLA HIYO MPYA YA ISRAEL, NA ULIMWENGU WOTE UNAPASWA KULA KIAPO CHA UTII JUU YAKE.................

JIBU LA SWALI LETU!

Wanapo sema kuwa Uchumi umekuwa kwa asilimia fulani, wanamaanisha kuwa, katika huo mwaka nchi imeweza kusafirisha kwa kiasi kikubwa bidhaa zake kama MAZAO, MADINI YALIYOSAFISHWA, MADINI KAMA MALI GHAFI, GESI na BIDHAA NYINGINE, kwenda nchi za watu na yenyewe KUPOKEA MAKARATASI MENGI SANA YENYE NEMBO ZA  €, £, na $.

Hivyo basi kwa nchi yako kubadilishana rasilimali zake kwa wingi na makaratasi hayo, na kuweza kuyahifadhi makaratasi hayo kwenye hazinia yake badala ya dhahabu, ndiyo tunaambiwa kuwa Uchumi umekuwa kwa asilimia kadhaaa .....
NDUGU, ENDELEA KUTAFAKARI, TILL NEXT TIME TCHAOOOOO ..........


1 comment:

  1. Kaka Salimu Mwenyezi Mungu akubariki kwa siri hii nzito isiyojulikana na wengi. Naomba kama kuna makala nyingine unitumie kwenye e-mail ya fokasimwakalinga@g-mail.com

    ReplyDelete