Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Thursday, October 31, 2013

BENKI JINAMIZI LA TAIFA (WEZI WALIO PEWA LESENI)

“Kama watu wa Marekani wataruhusu benki binafsi kusimamia suala nyeti la mzunguko wa fedha, kwa njia ya ‘inflation’ na ‘deflation’, benki hizo na mashirika yatakayo yazalishwa na nazo, yatawanyonya watu na kuwapora kila kitu mpaka siku moja watoto wao wataamka hawana nyumba kwenye bara ambalo baba zao walilipigania uhuru” – Thomas Jefferson



Watu wanaishi katika mataifa tajiri kuliko hapa duniani, lakini siku zote, eidha ni kwenye mataifa hayo au nchi masikini, utakuta kuna ukame au upungufu wa ‘fedha’. Leo hii wanawake nao wanaingia kwenye ajira, mamia kwa maelfu, wanaume zao wanatamani kupata kazi ya ziada au ongezo kwenye mshahara, watoto nao wameingia kwenye ajira, tena kwenye kazi mbovu za ajabu, deni la familia nalo linazidi kukuwa kila uchao, na watu wa saikolojia wanathibitisha kwenye tafiti zao kuwa moja ya sababu ya ndoa, familia kuvunjika na kuparaganyika ni juu ya kitu kinacho itwa ‘pesa.’


Lakini swali la kujiuliza ni ‘KWANINI FEDHA?’

NANI ANAYETENGENEZA FEDHA?

KWANINI KUNAKUWA NA UPUNGUFU WA FEDHA?

Katika ustaarabu wa dunia ya leo, bila pesa hakuna kinacho wezekana, tunaweza kujenga na kutengeneza kila kitu, lakini bila pesa viwanda vitatoweka na kuwa magofu. Mashamba yatakuwepo lakini kwa familia tu ipate chakula, chakula cha ziada kitaozea shambani, kazi hazitafanyika, usafirishaji wa bidhaa utasimama, wenye njaa watawamaliza wenzao ili wabakie hai, na kila serikali itatoweka isipokuwa ya familia tu.

UNADHANI NIMETIA CHUMVI MANENO HAYO?

Hapana, pesa leo ndiyo damu ya ustaarabu wetu, ndiyo njia ya biashara zetu zote. Ni kipimo ambacho kwacho bidhaa moja inanunuliwa na nyingine kuuzwa. Itoe pesa kwenye mzunguko au punguza kiasi cha pesa kinacho takiwa kwenye mzunguko na balaa lake kila binadamu wa eneo husika ataliona siku hiyo.
Unakumbuka miaka ya 1930 balaa lake? Historia ya fedha ya Marekani na duniani kwa ujumla haijakamilika bila kutaja balaa hilo. 

Unadhani nini kilitokea?

Ngoja nikupe darasa!

Kwenye miaka 1930 Marekani haikuwa na shida ya viwanda, haikuwa na shida ya aridhi yenye rutuba, wala haikuwa na shida ya wafanyakazi wenye ujuzi na maarifa.

 Marekani ilikuwa inayo usafiri bora na wa uhakika kutoka kwenye treni mpaka barabara, baharini na hata anga na kulikuwa na mtandao mzuri wa mwingiliano wa miundo mbinu hii. Mawasiliano baina ya miji mikubwa na ile midogo ndani ya Marekani ilikuwa ndiyo bora kipindi hicho katika uso huu wa dunia, kulikuwa na simu, radio, mfumo bora wa barua. Hakukuwa na vita wala uharibifu unao tokana na vita, hakukuwa na magonjwa yaliyamaliza nguvu kazi watu, wala hakukuwa na wakulima ambao wamegoma kulima. Isipokuwa mwaka 1930 taifa kubwa la Marekani lilikosa kitu kimoja tu.

MAREKANI YA MIAKA YA 1930 HAIKUWA NA KIASI CHA KUTOSHA CHA PESA KWENYE MZUNGUKO.

KWENYE MIAKA HIYO, AMBAPO CHANZO CHA PESA KILIKUWA (NA HATA SASA BADO NDIYO CHANZO PEKEE CHA PESA) BENKI NA MIKOPO, WENYE MABENKI KWA MAKUSUDI MAZIMA WALIKATAA KUTOA MIKOPO KWA VIWANDA, WAKULIMA NA WAFANYABISHARA.

Hata hivyo, ingawa jamaa hawa wa mabenki walisitisha kwa makusudi kutoa mikopo a.k.a fedha hewa, kwa wakati huo huo walidai marejesho ya mikopo yao ambayo tayari walishaitoa, na ghafla pesa ikatoweka kwenye mzunguko. Bidhaa bado zilikuwepo kwa ajili ya kununuliwa, kazi zilikuwepo zinazo subiri kufanywa, lakini kutoweka kwa pesa kwenye mzunguko kulilifanya taifa hilo kubwa duniani ‘kusimama tuli.’ Kwa mchezo mdogo tu kama huo, Marekani ikatumbukizwa kwenye kile kilicho fahamika kama ‘anguko la kiuchumi.’ Na watu walafi wamiliki wa mabenki wakawanyang’anya watu maelfu ya mashamba, nyumba, na mali zingine.

Watu wakaambiwa ‘tupo kwenye wakati mgumu’ na ‘pesa ni kidogo’. Hawakuwa kama ambavyo walivyo mabilioni wengine leo, hawafahamu mfumo wa benki unavyo fanya kazi, walipora mali zao kweupe pee.

Ilikuwa ni rahisi kama hivyo, hata leo BoT wakitoa amri mabenki ya sikopeshi, na wakati huohuo yaanze kudai marejesho ya mikopo yao, utaona balaa la mfumo huu wa uchumi tulio nao, hatma yetu ipo kwenye mikono ya watu wa benki.

Pesa yote unayo ona kwenye mzunguko ni kwa vile mabenki bado yanakopesha. Yanatupatia makaratasi yanayo itwa ‘pesa’ tunaweka rehani utajiri wa kweli kama nyumba, magari, mashamba na mengineyo, halafu wakisitisha kutoa mikopo, pesa ya kulipia mikopo inakosekana, kinacho fuata wanachukia utajiri halisi. Huo ndiyo ukweli wenyewe.

Jiulize kwa nini serikali haitengenezi pesa zake yenyewe mpaka zikakope kwenye mabenki, tena kwa riba?

Serikali kokote katika nchi husika, haichajiwi chochote kile, lakini inachajiwa riba inapokwenda kukopa kwenye mabenki. Ni nani anayemiliki benki kiasi aweze kuitoza serikali riba, ni nani mwenye nguvu ya ‘kuprinti’ fedha kiasi anaweza kuikopesha serikali kwa riba na serikali haiwezi ‘kuprinti’ fedha zake yenyewe?



Mwalimu wako wa uchumi anaweza kutusaidia kujibu swali hili?
Lakini kilicho kuwa cha ajabu zaidi WWII Ilipokuja na kile kilicho itwa ‘Great Depresion’ nacho kilikwisha! Watu walewale wanao miliki mabenki ambao mwanzoni mwa miaka ya 1930 hawakuwa na pesa kwa ajili ya viwanda, mashamba, nguo na vyakula, ghafla walikuwa na mabilioni yasiyo hesabika kwa ajili ya kukopesha nchi zinazo shiriki vita hivyo, kwa ajili ya kununulia silaha nzitonzito, kwa ajili ya kuviwezesha viwanda vya silaha, kwa ajili ya unifomu za kivita! Taifa ambalo mwaka 1934 halikuwa na uwezo wa kuzalisha mazoa ya biashara, ghafla tu iliweza kuzalisha mabomu ya bure kwenda Ujerumani na Japani.


Ongezeko la ghafla la pesa kwenye mzunguko, watu walianza kuajiriwa, mashamba yaliuza, mazao yao, viwanda vilianza kazi, machimbo yalifunguliwa na kile kilicho fahamika kama ‘Great Depresion’ kilitoweka!

Kama kawaida kunawana siasa walio laumiwa kwa hilo, na kuna ambao walipandishwa chati kwa hilo. Lakini ukweli wa msingi unabakia kuwa MABENKI YALIAMUA KUWEPO NA VITA VYA WWII, NA NJIA NYEPESI NI KUONDOA PESA KWENYE MZUNGUKO NA KUDAI MAREJESHO YAO, NA KILICHO FUATIA NI HISTORIA. UKWELI HUU HUWEZI KUUPATA KWA MWALIMU WA HISTORIA WALA WA UCHUMI, LAKINI ILIKUWA NI RAHISI KAMA HIVYO.

NANI ANAYE TENGENEZA/UMBA FEDHA?

Binafsi nimejaribu kupitia katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, hakuna hata mahala pamoja iliposema ni nani na jukumu la nani kutengeneza fedha, au kuchapisha fedha. 

Lakini cha ajabu mno ni kuwa katiba hii imejaa vifungu na vifungu vya namna gani fedha zitumiwe, namna gani matumizi na mahesabu yake yakaguliwe, lakini zinatoka wapi hizo fedha, hakuna jibu la swali hilo.

Kwa sababu fedha ni kitu muhimu na kina mguso kwa kila mwananchi, nilidhani basi moja ya shughuli za bunge ni kusimamia, na kuelekeza mchakato mzima wa kuhusiana na suala la kuchapisha hela/fedha/pesa/sarafu/noti, lakini hakuna isipokuwa kipo kifungu mahususi kinacho  LINYANG’ANYA BUNGE NGUVU ZA KISHERIA KUHUSU MAMBO YA FEDHA.


Utaratibu wa kutunga sharia kuhusu mambo ya fedha Sheria ya 1984 Na.15 ib.14
99.-(1) Bunge halitashughulikia jambo lolote kati ya mambo
yanayohusika na ibara hii isipokuwa kama Rais amependekeza
kwamba jambo hilo lishughulikiwe na Bunge na pendekezo hilo la
Rais liwe limewasilishwa kwenye Bunge na Waziri.

AJABU SANA, MOJA YA KAZI KUU NA MAHUSUSI ZA BUNGE NI KUTUNGA SHERIA, LAKINI HAPA KWENYE KIFUNGO HICHO HAPO JUU, KAZI HIYO KWENYE UPANDE WA MAMBO YOTE FEDHA BUNGE IMENYANG’ANYWA, NA NANI KAPEWA KAZI HII, KATIBA HAIJAMTAJA.

NI KWELI KITU MUHIMU KAMA HICHI KINAWEZA KIKAWA HAKINA SHERIA RASMI, NI KWELI BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HALINA NGUVU YOYOTE JUU YA KIASI GANI CHA FEDHA KIWEPO KWENYE MZUNGUKO? JUU YA THAMANI YA FEDHA NI IPI? SASA NI NANI HUYO MWENYE NGUVU HII, SI KUMBUKI KUIYONA KATIKA KAZI ZA RAIS...

MADHARA YA KULINYANGA’NYA BUNGE NGUVU ZA KISHERIA KUHUSIANA NA MBAO YA FEDHA NI YEPI?

TUITIZAME MAREKANI KWENYE HILI, NCHI AMBAYO KATIBA YAKE ILIELEZA WAZIWAZI JUU YA NGUVU HIZO ZA KISHERIA KUWEKWA KWENYE MIKONO YA BUNGE, MPAKA HAPO BAADAE MAJAMBAZI WA BENKI WALIPO PENYEZA RUPIA NA SHERIA HIYO KUPORWA BUNGE NA KUWEKWA KWENYE MIKONO YA WENYE MABENKI.

Serikali kama ya Marekani imetumia pesa zaidi ya zile ilizochukua kutoka kwa wananchi wake kwa njia ya kodi. Kwa sababu serikali haina pesa, na chombo chake mahususi cha kusimamia sheria inayo husiana na pesa kimeporwa nguvu hizo za kisheria, basi serikali huenda kwa wale wenye nguvu hizo za kutengeneza/kuumbwa fedha. Tuseme inahitaji dola bilioni 1, lakini ‘Federal Reserve’ , ambayo inamilikiwa na watu binafsi licha ya kutumia jina ‘federal’, haizitoi pesa hizo bure, ipo tayari kuipatia serikali ya Marekani fedha hizo zikiwa taslimu au kwa njia ya mkopo lakini kwa sharti kwamba serikali lazima izilipe fedha hizo tena na riba juu. Kisha baada ya hapo bunge linaruhusu kitengo cha HAZINA kuchapisha hati fungate (Treasury Bill) zenye thamani ya dola za Marekani Bilioni 1 ambazo Federal Reserve watakabidhiwa kama dhamana (YAANI HATA SERIKALI HAIAMINIWI!) Kisha watachukua makaratasi na kuyachorachora nambari na michoro ya ajabuajabu na kuziita karatasi hizo fedha, labda inaweza kuwagharimu dola elfu 1 kuchapisha makaratasi hayo na kuwapatia serikali kama ndiyo dola bilioni moja 
walizotaka.

JAMANI MUMEONA KILICHO TOKEA, NI KAMA MAZINGAMBWE VILE, SERIKALI INAWEKA DHAMANA YENYE THAMANI YA DOLA BILIONI MOJA KISHA INAPEWA MAKARATASI YENYE RANGIRANGI NA NAMBARI NA IKITAKIWA KUYALIPA MAKARATASI HAYO NA RIBA JUU, JINA LA MAKARATASI HAYO NI ‘FEDHA.’
JAMANI KWANI SERIKALI IMESHINDWA KUNUNUA HAYO MAKARATASI NA HIZO MASHINE ZA KUCHAPISHIA NA KUPRINTI HIZO NOTI NA KUZIPA THAMANI YA DOLA BILIONI MOJA?

SASA BASI SERIKALI IMEPATA MAKARATASI YAKE ‘YENYE THAMANI HEWA YA DOLA BILIONI MOJA’ WANACHI WAMESHAFANYWA WADENI WA FEDERAL RESERVE NA BADO WATATAKIWA KULIPA DENI HILO NA RIBA JUU.

MPAKA KWENYE MIAKA YA 1980 SERIKALI YA MAREKANI ILIKUWA INADAIWA NA FEDERAL RESERVE ZAIDI YA DOLA TRILIONI MOJA AMBAZO RIBA YAKE KILA MWAKA NI ZAIDI YA DOLA BILIONI 100, HIYO NI RIBA TU.

TURUDI HAPA KWETU TZ

KWANINI SERIKALI YETU INAPOPITISHA BAJETI YAKE YA MATUMIZI KWA MWAKA UNAO FUATA IANZE KUTEGEMEA VIKAPU NA NCHI WAHISANI KUTUNISHA BAJETI HIYO. KWANINI SERIKALI ISICHAPISHE KIASI HICHO CHA FEDHA, BILA RIBA NA KUKIINGIZA KWENYE MZUNGUKO KUKIDHI MAHITAJI YAKE YA MWAKA HUO???????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????

NADHANI NITAANDIKA HIZO ALAMA ZA KUULIZA MPAKA ‘KEYBORD’ ITOBOKE NA SITAPATA JIBU.


“Hatuna hata kidogo mfumo imara wa pesa ... pesa ni somo lililo la muhimu mno na ambalo mtu mwenye akili na maarifa makubwa, anaweza kulichambua na kuja na majibu. Ni muhimu sana kutambua kuwa ustaarabu ambao tunao sasa unaweza kuparaganyika kama suala linalo husiana na mfumo wa kibenki halitatafutiwa tiba.
Robert H. Hemphill, Credit Manager 
Federal Reserve Bank of Atlanta, Georgia (1935) 
In the foreword to a book by
 Irving Fisher, entitled 100% Money (1935)


“Kila siku ambayo benki inato mkopo kwenda kwa mteja, utambue kuwa – pesa mpya kabisa – salio jipya kabisa ambalo halikuwepo kwenye mzunguko hapo kabla limeingizwa na benki. (Pesa tulizo nazo 95 ni mikopo)”
Graham F. Towers, Director, Bank of Canada


“Mfumo wa kuitengeneza pesa na kuingiza kwenye mzunguko ni mwepesi, rahisi na kawaida sana kiasi kwamba akili inashindwa kuung’amua.”
Irving Fisher

Kwamba mzunguko wa pesa kwenye taifa letu (sasa ni dunia nzima) hatma yake ipo kwenye idadi na kiasi cha mikopo inayo tolewa na benki, ambazo zinakopesha, lakini hazikopeshi fedha, bali zinakopesha ahadi ya kumpatia mteja fedha ambazo hawana”
Hivyo ndivyo mfumo wetu wa fedha ulivyo. Kama kutakuwa hakuna MKOPO katika mzunguko wa hela, hakutakuwa na hata senti moja kwenye mzunguko”
Marriner S. Eccles, Chairman and Governor of the Federal Reserve Board


Kila mtu anajua kwenye akili yake kwamba benki hawakopeshi fedha walizo pokea kutoka kwa wateja wao. Unapo kwenda kutoa fedha kwenye akaunti yako, benki hawakukatalii kwa vile eti wameikopesha fedha yako.”
Mark Mansfield


Kama mikopo yote ya benki ikalipwa yote kwa wakati mmoja na ikamalizika, ujue hakuna hata mmoja ambaye atabakiwa na hata senti kwenye akaunti, na hakutakuwa na noti wala sarafu kwenye mzunguko. Unaweza ukashangazwa sana na hili. Wote sisi ni tegemezi kwenye mabenki ya biashara. Kila noti au sarafu unayo iona kwenye mzunguko, utambue kuwa kuna ambaye kakopa pesa hiyo. Kama benki watatoa ‘mikopo’, mambo yetu yanakuwa mazuri, kama la, tunahaha. Hatuna kabisa mfumo wa fedha wa uhakika. Kama ukiitazama picha hii na kuielewa, basi atatambua kwamba, balaa lisilo na matumaini linalo tungojea ni kubwa kabisa”

“Bado sijaweza kukutana na yeyote yule ambaye, kwa kutumia sababu na akili, anaweza kuhalalisha kwa serikali kukopa fedha kwa ajili ya matumizi yake ... naamini siku itafika ambapo watu watataka mabadiliko. Naamini siku itafika katika nchi hii ambapo watu watakulaumu wewe na mimi na kila yule ambaye anahusiana na bunge kwa kukaa kimya bila kufanya chochote na kuacha mfumo huo mbovu kuendelea”
Congressman Wright Patman

 “ Mfumo wa leo wa kibenki wa kutengeneza fedha kutoka hewani. Utaratibu huu kiuhakika ni moja ya kazi ya utapeli kuweza kubuniwa. Benki imeumbwa kwenye uovu na kuzaliwa kwenye dhambi. Wenye mabenki wanamiliki dunia. Wanyang’anye hii dunia, lakini waachie uwezo wa kutengeneza fedha hewa kwa mikopo, na kwa mkato wa kalamu wataweza kutengeneza fedha za kutosha kuweza kuinunua tena dunia yote ... kama unataka kuendelea kuwa mtumwa na kuendelea kulipa gharama za utumwa huo, basi waachie benki waendelee kutengeneza fedha hewa za mikopo.”
Sir Josiah Stamp, Mkurugenzi wa Bank of Endland 1928-1941

WANAHARAKATI,
WANASIASA,
WAZALENDO,
WASOMI WA LEO,
MNAOTAKA KUWA WABUNGE,
TAFADHALI NI JIBUNI SWALI LANGU ... KABLA SIJAKUTANA NA NYIE HAPA KWA POSTI NYINGINE .... PLZ ANY ONE WHO CAN HELP POST SOMRTHING HERE ....................

WHY, WHY, WHY, WHY, WHY.............


1 comment: