Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Wednesday, July 3, 2013

MAANA HALISI YA 666

Wapendwa!
Tarehe ambayo 666 Ilikuwa ubaoni ....

Sehemu hii ndogo kuhusiana na nambari 666 nimeitoa kwenye, sura moja ndani ya kitabu kinacho kwenda kwa jina la “FREEMASON; Dunia usiyo ifahamu”

kitabu hichi ni nimeandika mwenyewe, na soon Maulana akipenda mtakiona mtaani, hivyo sehemu hii kuitoa kwenye kitabu na kuwamegea ni zawadi kwenu wasomaji wangu, please ipokeeni ....

.... Kwa watafiti huru wa mambo ya UFO na New World Order ni kuwa serikali na ‘sayansi’ wanapigia debe taarifa hizo kwa lengo lilelile la New World Order ambayo kiongozi wake atakuwa na ‘damu takatifu’ na mwenye nguvu za maajabu.

Mmoja anaye tegemewa ni wazo ambalo liko kwenye imani ya dini mbalimbali duniani, ikiwemo kwenye Uyahudi, Uislamu na Ukristo na bila kusahau kwenye imani na dini za kishetani ukiwemo Freemasons.


Hiyo ni 666 katika lugha yake ya asili ...

Wote wanasubiri juu ya kuja kwa Messiah, ambaye atakaye kuja kuuokoa ulimwengu. Kutokana na mafunzo na falsafa za kimasonia ni kuwa Masiha wa kwanza, yaani Yesu alikuja kwa ajili ya kusimamisha ufalme wa mbinguni, lakini Masiha wa mara ya pili ambaye ni …? Atakuja kuisimamisha New World Order chini ya utawala wake.

Kuhusiana na Masiha huyo, Freemasons wa daraja la 33 Manly P. Hall, katika kitabu chake cha “The Secret Destiny of America ameandika hivi,

Jawabu la mpango huu wa siri ni World Order chini ya mfalme mwenye nguvu za kimaajabu. Mfalme huyu anatokana na ukoo wa wenye damu tukufu; hii ni kusema, anatokea kwenye asasi ya Illuminati na walio na hekima, anatokana na familia ya mashujaa ya binadamu walio wakamilifu”

Mtu aliyetajwa na Hall sote tunamjua ni nani, ametajwa vizuri kwenye vitabu vitakatifu, hasa kwenye mafundisho ya Kiislamu. Wasomi na watafiti huru  dini zote watakubaliana na mimi kwamba hakuna dini iliyo weza kuelezea vyema maisha yatakayo kuja na alama zake, maisha ya kaburi na maisha ya motoni na peponi kama Uislamu, na mtu huyu ametajwa vilivyo na alama zake mbalimbali katika mafunzo hayo ya Uislamu.

... .... vurugu za New Age, lakini kwa kiasi fulani vurugu hizi zinawiana na yule mmoja anaye ngojewa, tumchambue kidogo kwa mustakabali wa sura hii  (Sura hii kwenye kitabu hicho nimeipatia jina la: Wageni Wanarudi Tena ...) Tukianza na kitabu cha Ufunuo kwenye biblia tunakutana na habari maarufu sana ya ‘mnyama’ kama ifuatavyo.

“Anataka kila mmoja – mkubwa na mdogo, tajiri na maskini, mtumwa na aliye huru wapewe chapa kwenye mkono wa kulia au katika paji la uso. Hakuna atakaye nunua au kuuza chochote pasipokuwa na chapa, ambayo ni jina la mnyama au ile namba inayowakilisha jina lake. Inahitaji hekima kufahamu mambo haya. Yeye aliye na ufahamu na aihesabu namba ya mnyama huyo, kwa kuwa ni namba ya kibinadamu. Namba yake ni 666” .

Mbali na kuwa na tafsiri mbalimbali juu ya mnyama huyo ni nani na anawakilisha nini kwenye maelezo hayo hapo juu, watu wengi wame chukuliwa sana na maneno ya mwisho ya kipengele hicho, yaani 666. Lakini mbali na hilo dunia ya leo tunaona ni namna gani ilivyo mezwa na vitu mbalimbali kutoka, alama na nembo, mpaka majina na herufi za 666. Nami pia sitajikita katika kutaka kufahamu pembe au kichwa au kinywa cha mnyama huyo kinawakilisha kitu gani ila nitakwenda moja kwa moja kwenye jina lake nalo ni 666.

Wakati nilipo kuwa nasoma hadithi za Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) kuhusu Dajjal na vitimbi vyake nilikuwa nashangaa kwa nini Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) amekuwa akituonya mara kwa mara juu yake, wakati ameshatuambia muda mrefu kuhusu alama zake ambazo itakuwa ni rahisi kwetu sisi kumtambua na kumkana, Mpaka nilipokuja kufahamu Freemasons ni nani na wanafanya nini ndipo nikafahamu kuwa ni kweli Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) alikuwa na haja ya kutuonya sana juu ya mtu huyo. Wanao muandalia kiti chake cha Utawala wa Dunia tayari wameshatufunga kwenye minyororo yake hata kabla ya Dajjal mwenyewe hajafika itakuwaje ndugu yangu Dajjal mwenyewe atakapo kuja?

666 ---- Kwa Wagiriki wa zamani wakati kila namba ilikuwa ni sawa na herufi, namba 6=W, yaani namba sita inachukuliwa ni sawa na herufi W. www kwenye mtandao wa internet, ingeweza kuwa W, au WW lakini mtu fulani akachagua iwe WWW yaani 666! Hivyo ufunguo wa tovuti yoyote ni 666! Yaani badala ya kuanza na jina la Mola Wetu mtukufu kama inavyo paswa watu Fulani wanataka tuanze na jina la ‘mnyama’, 666.

Sarafu ya Ulaya Euro ina Nyota 6 upande wa chini, na Nyota 6 upande wa juu na mistari 6 inayounganisha nyota hizo, hivyo kutengeneza jina la mnyama, 666!

 Bar Code ya bidhaa zote za duniani ambazo zitauzwa nje ya mpaka wa nchi husika lazima ziwe na namba 666, iko hivi, mistari mingi, mingi unayoiona katika Bar Code hizo, mistari hiyo huwakilisha namba, nayo nambari sita (6) huwakilishwa na ‘bars’ au mistari miwili mirefu kushinda mingine, daima utaiona mistari hiyo mwanzo kabisa, katikati na mwisho mwa Bar Code, wakati mwingine utaona wame kuandikia nambari sita (6) chini ya ‘bars’ hizo mbili au wakati mwingine hawaandiki chochote, lakini lazima utaitambua tu, kwa vile yenyewe ni mirefu kupita mistari mingine, huenda hata kwenye kitabu hichi unacho soma ukaiona, au tizama bidhaa yoyote kutoka nje ya nchi yako, au inayo uzwa nje ya nchi yako na utaiona. Namba ya kwanza daima ni 6, namba ya katikati ni 6 na namba ya mwisho ni 6 vilevile, jina la ‘mnyama’ yaani 666.


Bar Code mpya ya Urusi kwa ajili ya kufuatilia watu wake ni 666,hii ni sawa na microchip (somo kuhusu mikrochip nitaliposti wakati mwingine).

Bunge la Ulaya lina viti 679, kila kiti kimoja ni kwa ajili ya mtunga sharia mmoja, mathalani kiti namba 663 ni kwa ajili ya Rep Souchet, 664 kwa ajili ya Thomas-Mauro, 665 kwa ajili ya  Zizzner na kiti namba 667 kwa ajili ya Rep Cappato. Wakati siti hizo zikiwa na majina ya wanachama wanao vikalia, kiti kimoja hakina jina la mwanachama anaye kikalia, na pia vilevile hakikaliwi na yoyote, kiti hicho ni namba 666.
Haswa kiti hicho ni kwa ajili ya mmoja anaye ngojewa, ambaye bado kufika, lakini nafasi yake ipo tayari inamsubiri. Ni kama muhuri wa Marekani ‘The Great Seal’ wenye nembo ya jicho moja na piramidi ambalo halijakamilika, muhuri huu nao unasemekana unamsubiri mmoja anaye ngojewa ambaye mpaka sasa tunamjua kama mnyama mwenye jina la 666!


Nembo ya Umoja wa Ulaya ni ngao ya mwanamke aliyepanda mnyama! Mwanamke huyu naye ametajwa kwenye kitabu cha ufunuo.


“Kisha, Roho akanikumba, akaniongoza mpaka jangwani. Huko nikamwona mwanamke ameketi juu ya mnyama mwekundu. Mnyama huyo alikuwa ameandikwa kila mahali majina ya makufuru; alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.”


Lakini tukiachana na Umoja wa Ulaya, sehemu nyingi duniani, makampuni, wasanii wafanya biashara, wanasiasa na hata viongozi wa kidini kwa namna mbalimbali wamekuwa wakiipeperusha alama na nembo hii ya 666 kwa kila mtu kuona, na mazingira hayakuonesha kama vitu hivyo vimefanywa kwa bahati mbaya tu, bali kwa makusudi mazima.


Lakini ni nini hasa maana ya jina hili 666? Je tunaweza kumjua mmoja anaye ngojewa kwa kutumia jina hilo?


  Wakristo wengi wanafahamu kuwa 666 ni alama ya Mpinga Kristo ambaye Waislam wanamuita Masih Dajjal. Katika moja ya hadithi za mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) inasema. Hata kama ataleta machafuko makubwa, neno Kafir litakuwa wazi limeandikwa katikati ya macho yake (ana macho mawili ila moja ni chongo halioni ndiyo maana mara nyingi anajulikana kama mwenye jicho moja), maelezo mengine yanasema neno hilo litaandikwa ‘Kaf’, ‘Fa’, ‘Ra’ kwa uwazi kabisa ili kila mtu aone.


“Hakuna nabii aliyetumwa isipokuwa aliwaonya watu wake kuhusiana na muongo mwenye jicho moja. Yeye ana jicho moja, lakini Mola wako si mwenye jicho moja, na baina ya macho yake pata andikwa ‘kaafir.


Kwenye Lugha ya Kiarabu herufi zilizo tajwa hapo ziko hivi;  ر ف ق Kama tutazigeuza herufi hizo chini juu tutapata kitu kinachofanana na 666. Lakini kutokana na mafunzo ya mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) herufi hizo zitaonekana kama zinavyo tamkwa kwenye lugha ya Kiarabu.

Wasomaji waelewe kwamba alama/namba 666 inatokana na tafsiri ya namba za Kigiriki kuja kwenye lugha ya kingereza nazo zinawakilisha jina la mtu ambaye wengi wanamuita Mpinga Kristo. Kwa hiyo tukiangalia kwa undani tunaona kuna majina mawili hapo, jina la Kristo na kuna jina la Mpinga Kristo.  Jina hili Kristo Kigiriki ni Christos ambapo katika maandishi ya Kigiriki lingeandikwa hivi Χ ξ ς, ambapo kwa Wagiriki namba zilitumika badala ya herufi, jina hilo lilisomeka hivi ,yaani (Chi, Xi na Sigma) kwa hiyo  (chi) = 600 nayo ni herufi ya kwanza ya jina lake.  (xi)= 60 inawakilisha nyoka na ni mfano wa herufi ‘E’ na  (sigma) = 6 herufi ya mwisho ya jina lake, na ambapo jumla yake tunapata ni 666 kama ilivyoelezewa kwenye ufunuo 13:18 Namba hizo za Kigiriki zilizotumika badala ya jina Kristo.

Ilikuwa ni miaka 60 ya baraza la Umoja wa Mataifa, lakini umeona wakuu walivyo idizaini hiyo sitni na kusoemka 666, si kwa bahati mbaya hiyo jooo!!!! Some one get paid and perfome his job so well

 Kama nilivyo elezea hapo juu ukizitamka namba hizo unapata sauti hii  Xes au Ches sawa na sauti ya “Jes” kwa Jesus. Herufi “J” ni herufi inayotokana na herufi “I” nayo ni ya mwisho kuingizwa kwenye herufi za lugha ya kingereza mnamo karne ya 16 na inatamkwa kama “Ye” na hii ndiyo maana jina Jesus linapoingizwa kwenye Kiswahili linatamkwa kama Yesu ambayo ni sawa na “Xes” Kigiriki na “Jes” kingereza. Wagiriki jina hili Christos (Kristo) wamelichukua kutoka kwenye lugha ya Kiaramaiki kwa Wayahudi wa kale ambapo lilikuwa na maudhui yaleyale ya Jesus (Yesu)/ Yeshua/ Messiah.

Nadhani jamaa unamjua, lakini umeona nyuma yake kuna kitu gani ...?!!!

Tunapo tizama moja ya maana ya majina hayo yaani Jesus/Yesu/Yeshua/Messiah/Kristo ni “Mpakwa Mafuta”. Kwa maneno mengine Kristo ni mtu mwenye upako, mtu aliye pakwa mafuta kama alama ya uteule wake. Leo duniani kuna wetu wengi wanao jinadi kuwa wanao upako, yaani wamepakwa mafuta, kwa maneno mengine watu hao ni Kristo na au Yesu, na au Yeshua na au Messiah. 

Unaiitaje tena hii? Mi sikumbuki labda geuza kompyuta yako chini juu, juu chini unaweza kuisoma .... lol

Watu hao pia wanafanya mambo ya maajabu, wanaponya watu maradhi mbalimbali, wanawapatia utajiri na kadhalika, yote haya hayana shida, kama mtu kapewa kipawa cha kuweza kufanya hayo si jambo la ajabu, lakini kuna wale wanao dai wanaweza kufufua watu, hili nina mashaka nalo, lakini jambo lililo na utata zaidi ni wao kujipamba na sifa isiyo yao, sifa ya Kristo, ni wazi watu hao wanajiita wao ni Yesu, hata hivyo kuja kwa watu hawa kumeshaelezewa katika vitabu vitakatifu ikiwemo Biblia na hapa si mahala pake na wale ambao wanahisi hili lina wagusa na warejelee vitabu vya dini zao kupata ukweli wa mambo.

Kerry yupo kazini, lakini mbele yake kuna 666

Hivyo namba/alama 666 inayo maana ya Kristo lakini kama tulivyoona mwanzo kuwa namba/ alama hiyo ni jina na ambapo tunapata majina mawili yaani jina la Kristo na Jina la Mpinga Kristo je Freemasons wanamaanisha jina lipi wanapo tumia 666?

Upo Hapo?????

Turudi kwenye lugha ya Kiarameiki ambapo neno Messiah lenye maana ya Kristo ndipo lilipotoka, neno hilo lina maana ya Msema kweli, Msema Uongo, mtu mwenye kasoro, mtu wa  kuzunguka dunia nzima, maana hizo chache zinatosha kutupatia jibu letu. Sifa ya kuwa na Kasoro ni sifa ya Masih Dajjal/ Mpinga Kristo kwani kati ya macho yake mawili moja ni chongo yaani halioni na hii inahusishwa na alama ya jicho moja kwenye nembo za Freemasons. Sifa ya kusema uwongo ni sifa ya Masih Dajjal/ Mpinga Kristo na hii pia ni sifa waliyonayo Freemasons. Sifa ya Kuzunguka dunia nzima nayo ni Sifa ya Masih Dajjal kutokana na mafundisho ya Kiislam ataizunguka dunia nzima kwa siku arobaini tu. 

Hivyo sifa moja inayobakia ya kusema Ukweli hii ni sifa ya Mtume wa Mungu Masihi Issa (Yesu) hivyo moja kwa moja tunapata picha kuwa Freemasons wanapotumia namba/alama 666 wanamaanisha jina gani, Masihi Dajjal/Mpinga Kristo. Jina hilo lipo kwenye shilingi mpya ya Euro, kwenye Bar Code ya bidhaa za Marekani , kwenye nembo za Microsoft  kutaja kwa uchache ila kiuhakika ziko kila kona na kwa njia moja ama nyingine tunazitumia kufanikisha mambo yetu ya kila siku bila kufahamu.

Wale wanao jinadi kuwa wa upako nao hawaunguki katika sifa za mtume wa Mungu Mmoja bali katika sifa za Mpinga Kristo, kama nilivyokwisha elezea kuna ambao wamepatikana wakijibadilisha na kuwa Nyoka, tuna waona wanavyozunguka dunia nzima leo kwa mahubiri yao, kuna wanao dai kuwa wanafufua watu, ni hii ni moja kati ya uwongo mkubwa atakao kuja nao Mpinga Kristo atadai ana fufua watu na atafanya hivyo lakini kiuhakika hatamfufua mtu bali mashetani anao shirikiana nao ndiyo watakao jibadilisha na kuwa katika umbile na sura ya mtu fulani aliyekufa na kudai yeye ndiye mtu huyo aliyefufuka.


Freemasons ni wasimamizi wa mlango, na punde tu au muda kidogo mwenye mlango atasimama mahala pake, naye si mwingine bali ni Dajjal / Mpinga Kristo ambaye  mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake) amemtaja kama hivi,

 “Nimewaeleza mengi kuhusu Dajjal kiasi kwamba nahofia mtakuwa hamjamuelewa, Dajjal ni mfupi, vidole vyake ni vipana na mwili wake umejaa nywele, ana jicho moja linaloona na jingine lisiloona ... kama utamuona fahamu kuwa Mungu wako si jicho moja.”


Inajulikana kuwa kabla ya kuja kwake kuna watu wataandaa njia na mazingira ya kuja kwake, mfumo wa kufanya mambo ya watu hao utabeba sifa zote za Dajjal, kwa maneno mengine waandaaji wa njia hiyo si wengine bali ni Freemasons. Jicho moja ni mojawapo ya njia ya kumtambua Dajjal na jicho moja ni moja alama za Freemasons, Dajjal ni muwaji na katili kwa wale watakao mpinga, atakuwa na nguvu ya kuwapa watu aridhi kubwa zaidi au kuiharibu itategemea na jinsi gani watu hao watamfuata, sawasawa na Freemasons wa magharibi kupitia World Bank wanazishikilia na kuzivunja vunja nchi za Dunia ya Tatu kiuchumi kama haziendi na kufanya kulingana na sera zao. IMF na mikopo yake ya ‘maendeleo’ imekuwa kama mitego juu ya nchi hizi inawawekea riba kubwa ambayo daima inazifanya nchi hizo kuinama juu ya kila kitakachosemwa na Freemasons hao ambacho si kingine ila ni sera zinazo za kuporomosha uchumi wao na kuziacha masikini daima watumwa wa kuomba omba.


Njia nyingine ambayo Dajjal ataitumia kuwalazimisha watu wamfuate ni kwa kusambaza maradhi. Atakuwa na uwezo wa kusambaza maradhi na kuyatibu kiusahihi na sawasawa. Kwa kutumia nguvu hiyo atawavuta wengi katika dini yake, dini ya Freemasons au kiuwazi zaidi ni ya kishetani. Tunawaona Freemasons pia wakicheza na maisha ya watu kwa njia kama hii, ushahidi mwingi unaonesha kuwa aina nyingi za virusi wa maradhi mbalimbali ukiwemo UKIMWI vimetengenezwa maabara na baadaye vikatumiwa kwa majaribio kwenye miili ya binaadam. 

Dajjal atawadanganya watu kwa kujitangaza mwenyewe na sifa za Mungu aliyetukuka. Freemasons nao wanatumia kila walilo nalo kuziondoa amri za Mungu kwa kuweka amri zao kama wao ndiyo Mungu na ndiyo wanao uwezo wakufanya lolote watakalo, wanatumia teknolojia mbayo hawataki watu wajue kuwa wanayo kuyatawala maisha ya watu na kila kitu chao, wanata kuona na kusukia kila unachofanya, wanatumia genetic kuharakisha maumbile na kuyabadilisha kutokana na wanavyo taka wao. Waharibifu hawa hawaoni mipaka na wala hawatambui sheria kwani vyote hivyo ni wao wameviweka.


Kama ilivyo kwenye filamu ya Independence Day, watatujengea mazingira ya kukubali serikali moja chini ya kiongozi mmoja wa kidunia kama njia ya pekee ya kupambana na ‘adui kutoka nje ya dunia’. Watatupatia kiongozi wao huyo kama nembo ya umoja dhidi ya wote wanao pingana na serikali hiyo wakiwemo hao ‘wageni’.


Lakini pia wanaweza kutumia teknolojia yao ya ‘Project Bluebeam’ ....

KAMA NILIVYO SEMA KAJIPANDE HAKA NIMEKITOA KWENYE MOJA YA SURA ZA KITABU CHANGU, HIVYO HAYO MAMBO YA PROJECTBEAM TUYAACHE TUTAKUTANA NAYO HUMO KITABU KIKIWA TAYARI INSHALLAH ...

28 comments:

  1. Dah,hali inatisha kwa jinsi hawa watu walivyo tawala dunia cha msing ni kuzidisha swala na kumcha mwenyezi mungu na kufuata maamlisho yake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. This comment has been removed by the author.

      Delete
  2. ummenikumbusha kitu kuna movie ya holliday ya mr. Bean inaanza kwa namba ya kushinda baati nasibu ya kwenda france ambapo utaiona namba hiyo 666

    ReplyDelete
  3. Binfasi sijaiyona movie hiyo, lakini hiyo inaweza kuwa ni moja kati ya movie nyingi wanazo tumia kuishawishi jamii kukubaliana na maono yao. Vizuri, inaonekana umeanza kuona sasa kile ambacho kinacho fichwa hadharani.

    ReplyDelete
  4. kwahiyo unamaanisha yesu ndiye mnyama 666 or?

    ReplyDelete
  5. Hapana, Yesu si mnyama anayekwenda kwa jina la 666. Yesu ni nabii wa kweli wa Mungu Mmoja, ispokuwa jina KRISTO, katika lugha yake ya asili ya Kiyahudi lilipoandikwa nambari lilisomeka 666.
    Na ndiyo maana Mnyama wa 666 Aanafahamika kama 'mpinga kristo' au 'ajifananishae na kristo' au 'kristo wa uwongo' kwa sababu Kristo ni jina, au 666 ni jina lakini nani ni nabii na nani ni mnyama kwenye jina hilo, hapo ndipo palipo na hekima. Yesu ni nabii na Dajjal ni mnyama.

    ReplyDelete
  6. Mmh kweli ianatisha sasa kitabu mpaka leo bado ujakitoa kiongozi

    ReplyDelete
  7. KWA KWELI KITABU KIMEKAMILIKA KABISA, TABU IPO KWENYE UHAKIKI NA USAHIHISHAJI, NILIYEMPATIA KAZI HIYO YUPO BIZE KWELIKWELI, LAKINI MUNGU AKIPENDA TUTAKIWEKA HADHARANI HIVYO HIVYO TIME IS NOT IN OUR SIDE, AND OUR ENEMY IS MOVE FAST THAN ANYTHING WE CAN IMAGINE

    ReplyDelete
  8. Run morre dan u thnk bg_up

    ReplyDelete
  9. I have read so many articles or reviews regarding the blogger lovers but this
    piece of writing is in fact a good post, keep it up.


    Review my homepage - clothing styles

    ReplyDelete
  10. 666 INAMHUSU KAISARI WA HIMAYA YA KIRUMI ALIYEJULIKANA KWA JINA LA nero. KIONGOZI HUYU NDIYE ALIYEWAUA MITUME PETRO NA PAUL MWAKA 67

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakushukuru kwa maoni yako. Nami ningependa uthibitishe ni namna gani 666 inamuhusu NERO ili wasomaji wangu wasitatizike kutokana na kile nilicho kileleza kuhusiana na 666.

      Delete
  11. Jitahidi kumfuatilia mhakiki ili tukipate hicho kitabu hongera

    ReplyDelete
  12. dah wadau MBNA dunia wameikomba inabidi tumrudie mungu mabaya yao tunayo yaona tujtaidi kuyakwepa lakn tusiyo yajua tunatubu kwa mungu

    ReplyDelete
  13. Mwandishi wa makala hii ametumia uwezo wa kusoma vitabu na kuperuzi mitandaoni tu,na kuegemea zaidi upande ambao haueleweki juu ya unabii wa mwisho.Matokeo yake ninini?
    1.Maana ya namba 666 kwa mjibu wa biblia siyo hiyo aliyoitoa,watu wengi ni wajinga wa kuelewa ndio maana onyo limetolewa mwenye akili aihesabu namba hiyo maana ni namba ya kibinadamu.
    2.Suala la chapa katika paji za uso watu wamezipokea kuanzia mwaka wa 321BK.na hawakuweza kuuza wala kununua mpaka wawe na chapa hizo.
    3.Wakristo milioni 50 waliuawa baada ya kukataa kupokea chapa hiyo.Kwa tafasiri ya leo ni kwamba wakristo wote wanao mwabudu MUNGU kinyume chake aliye juu yaani siku ya JUMAPILI NI MASALIA YA WALE WALIOPOKEA CHAPA YA MNYAMA.
    4.Waislamu wote ambao hawakuitunza sabato takatifu sawasawa na torati ni MASALIA YA WALE WALIO IPOKEA CHAPA YA MNYAMA.

    KATIKA BIBLIA Mnyama amenenwa ndiye msimamizi na wa makahaba amezini na watu wengi,kabila lugha na taifa.

    NDUGU ULIYE TOA MAKALA HII.
    Kumbuka kuwa hauwezi kutafsiri unabii wa YESU ukiwa hauna ROHO WA KRISTO.Neno limesema hivi ''Roho wa Kristo ndiyo royo ya unabii'' hivyo ni wazi kua mtu mwenye ROHO wa kristo hawezi kutoa maana ya unabii kama wewe ulivyotoa.Soma unabii wa Danieli kwanza:
    1.Majuma sabini
    2.Wanyama wanne aliowaona pia malaika ametoa na tafsiri yake wanyama ninini
    3.Rejea chanzo cha IBADA YA KIPAGANI KATIKA UKRISTO mwaka 321BK,Kazi iliyo fanywa na Majesuit wa Vatican kuanzisha UISLAMU''Freemasonry Order number570''.
    SASA WEWE UNAWEKA BAR CODE IKIWA NDIYO MFANO WA NAMBA 666 HAPANAA.HUO SIO UNABII.Bar code ni namba za electronic zinazotofautisha aina,mahali,hali na mtengenezaji wa bidhaa kuwa halisi au bandia.Bar code husomwa na kamera maalumu inayoitwa ''bar codeleader''.
    Kwa jiji la DAR ES SALAAM hata tiketi za UDART MWENDO KASI zinatumia mfumo huo.
    HIVYO HUWEZI KUFAFANUA Unabii aliofunuliwa Yohana mtakatifu kwa misingi hiyo.Anzia kwanza na ROHO WA KRISTO UNAYE AU HAUNA KISHA NJOO KWENYE Unabii wa Danieli ujue maana ya wanyama,maji mengi,mfalme wa kaskazini,mfalme wa kusini, WAFALME WANNE.

    Baada ya hapo njoo kwenye Kitabu cha UFUNUO WA YOHANA mwambiye ROHO wa Kristo''yale uliyo mfunulia Yohana yafunue kwangu''Kama Roho wa kristo unaye atakufunulia moja baada ya jingine ila kama hauna huyo ROHO basi.

    INTERNET ITAKUFUNULIA UONGO ILI UENDELEE KUPOTEA.
    Agenda ya kupunguza watu Duniani sio ya leo ilianza mwaka 538 BK hata huyo mtume Muhammad hajazaliwa.Kuanzia mwaka huo niliotaja kuna nchi ambazo mnyama aliamuru zifutwe Duniani na zilifutwa kabisaa yaani watu wake waliuliwa wote baada ya kuonekana kwamba nchi hizo zilimpinga Mnyama na hazikua tayari kupokea chapa yake.
    UFUNUO WA YOHANA Anaposema ''mnyama akapewa kufanya vita na watakatifu na akawashinda''Maana yake alipigana na watakatifu waliokua duniani akawaua wote na akasimamisha IBADA YAKE MWENYEWE KINYUME CHA ALIYE JUU.
    NAITARUDI BAADAYE...

    ReplyDelete
    Replies
    1. No research no right to speak
      Nashukuru umetaja baadhi ya vyanzo nilivyovitumia katika tafiti zangu, ingawa hujataja zote, nimesikitika kwa kuvipa mtazamo hasi vyanzo hivyo, wakati unafahamu kwenye ulimwengu wasasa ambao tunaita zama za mawasiliano na teknolojia, internet ndiyo nyenzo kuu kwenye hili. Maoni yako nimeyapata sababu yapo kwenye internet, hii inamaanisha na wewe unatumia net, biblia leo unaipata kwenye net, vitabu mbalimbali vipo kwenye net na tunavisoma na ikibidi tunaviprint, siyoni kuna kasoro gani kutumia internet na vitabu mbalimbali katika kwenye tafiti, ama vinginevyo hatutakuwa na tafiti bali tutakuwa na kile ambacho mtu binafsi anakiamini, kama unavo amini wewe juu ya chapa, mnyama na 666, lakini imani na tafiti ni vitu viwili tofauti, ninacho kifanya hapa ni kuchapisha tafiti zangu binafsi, na wewe utazipima kwa kutumia akili na vynazo mbalimbali kasha utakuja na tafiti yako inayoendana na hiyo au kipingana, lakini si kuja na kile unacho amini, hivyo umakini wa ziada unatakiwa pale tunapo yaendeya maswala haya.
      1. Maana niliyoitoa ya 666 unasema siyo hiyo kwa mujibu wa biblia, lakini na wewe hujasema maana ya 666 kwa mujibu wa biblia ni ipi. Mimi nimetafiti na kutizama kazi za watafiti mbalimbali, na nikaitazama si kwa mujibu tu wa biblia, lakini kwa Wayahudi nao wanasemaje, Waislam nao wanasemaje na wote watatu wanakuja kwenye hitimisho moja, kwamba 666 ni jina la BINADAMU ANAYEITWA MASIHDAJJAL (Kwa Waislam), MPINGA KRISTO (Kwa Wakristo), na MASIHI/MFALME ANAYENGOJEWA (Kwa Wayahudi)
      Ambapo 666 nikasema ni jina lake na lilitumika wakati ambapo Wagiriki na Wayahudi walitumia nambari badala ya herufi, na nambari hizo ikizileta kwenye herufi unapata majina niliyo yataja hapo juu. Ili kukuongezea faida ni kwamba kwa mujibu wa Waislamu mtu huyu atandikwa kwenye uso wake jina lenye herufi TATU, Herufi hizo zitaandikwa kwa lugha ya kiarabu na zitasomwa na kila muumini anayejua kusoma na asiyejua kusoma, herufi hizo zitasomeka KA-FI-R zikiwa kwenye lugha ya kiarabu herufi hizo zitaonekana hivi ق־ف־ر Kilicho cha ajabu ni kuwa herufi hizo ukizigeuza chini juu unakaribia kuipata the same numbers 666. Lete utafiti wako na wewe kasha tuupime kwenye mizani.

      Delete
    2. 1. Ushahidi wako ni upi kwamba mwaka huo watu walianza kupokea chapa za Uso na aliyezito ni nani? Ila mimi ninachofahamu ni kuwa mwaka huo 321BK lilitokea tukio moja muhimu kwenye dini ya Kikristo, tukio ambalo liliibadilisha ile SIKU YA SABATO AMBAYO NI JUMAMOSI na KUIHAMISHIA JUMAPILI, AMBAYO WAROMA NA DOLA YAKE WALIITUMIA SIKU HIYO KUMUABUDU MUNGU JUA KWENYE DINI YAO HIYO ILIYOJULIKANA KAMA MITHRA.
      Around 200 years after Christ, and beginning with the church in Rome, Christians began to participate with the pagan religions in their Sunday (Day of the Sun) celebrations while still continuing to observe the Sabbath. Since these Sunday celebrations were more enjoyable than the solemn ceremonies that they participated in on the seventh day of the week, they began to look with disfavor on the seventh day and began to worship on Sunday.
      In 321 A.D., the emperor Constantine signed a law decreeing that all people, not involved in agriculture, should worship on Sunday (the first day of the week). The English translation of the decree reads as follows:
      "All judges and city people and the craftsmen shall rest upon the venerable Day of the Sun. Country people, however, may freely attend to the cultivation of the fields, because it frequently happens that no other days are better adapted for planting the grain in the furrows or the vines in the trenches. So that the advantage given by heavenly providence may not for the occasion of a short time perish." Joseph Cullen Ayer, A Source Book for Ancient Church History (New York: Charles Scribner's Sons, 1913), div. 2, per. 1, ch. 1, sec. 59, g, pp. 284, 285.
      Tafiti za kuwa mwaka huo watu walipokea chapa ni zipi?

      Delete
    3. 1. Nadhani mimi na wewe tonatofautiana kwenye tafsiri. Ninapo itizama nukta yako hii ya (3) Napata jibu kwa nini nukta yako ya (2) umeita kitendo cha Sabato kuhamishiwa Jumapili ni kitendo cha kupokea chapa.
      Nashindwa kuelewa aina hii ya tafsi unaitolea wapi, sababu kimeelezwa wazi katika historia kwamba SABATO ilihamishwa kutoka JUMAMOSI kwenda JUMAPILI, Lakini kitendo cha kupokea chapa kama ulivyo ainisha ni ALAMA mahususi ambayo mtu anawekewa kwenye paji lake la uso, vitu viwili tofauti.
      Unacho kizungumzia kwenye nukta hii ya (3) ni ile tafsiri uliyo nayo kwamba wakreisto milioni 50 waliuwawa sababu walikataa kupokea chapa na wakristo wanaoendelea kuabudu SABATO ndani ya JUMAPILI hii leo ni sawa na wale waliopokea chapa. Lakini Hakuna kwenye historia kokote popote kwamba wakristo hao na hawa wa leo wanao abudu Sabato ndani ya Jumapili wanayo chapa au alama yeyote katika uso wao, na wewe ambaye unajihesabu kama huna chapa hiyo, unauza na kununua wala hubaguliwi na yeyote, je ni chapa hipi unayoizungumzia wewe, mbona unachnganya mambo.

      Idadi ya Wakristo walio uwawa kuanzia mwaka 313BK baada ya mfalme Constantine kupitisha azimio kwamba ‘Ukristo’ ndiyo dini ya dola ya Roma ni zaidi ya Milioni 50. Wakristo hawa waliuwawa kwa njia mbalimbali ikiwemo kuteswa, kuchomwa moto wakiwa hai, kuingizwa kwenye chungu kinacho chemka mafuta au maji, na mengine na mengine. Waliuwawa sababu dini ya ukristo ya dola la Roma iliyo tangazwa na mfalme ni dini mpya ambayo waungu wa kipagani wanaingizwa ndani ya hekalu na kuabudiwa. Hii ndiyo maana sabato ikahamishwa kutoka Jumamosi kwenda Jumapili ambayo jumapili hasa ndiyo siku ya mungu jua (SUN-DAY), Dini ya MITHRA ya kipagani ikafanywa ndiyo UKRISTO na DINI YA KIKRISTO KATIKA MISINGI YAKE ILIYOLETWA NA KUFUNDISHWA NA MTUME (ISSA) YESU. IKAFUTWA NA WAFUASI WAKE WA KWELI ZAIDI YA MILIONI 50 WALIUWAWA.
      Je kuikataa dini hii mpya ndiyo kukataa kupokea chapa? Utakuwa unachanganya mambo ukisema hivyo, sababu ishu ya Chapa na ishu ya Ukristo kubadilisha ni vitu viwili tofauti, ndiyo maana hata wewe unayejiita kuwa hujapokea chapa kwa kuendelea kuitumikia Sabato ya Jumamosi, unauza, unanunua na hubaguliwi na yeyote, wakati maandiko yanasema asiyekuwa na chapa hiyo hatoweza kununua wala kuuza. Hakuna popote kwenye historia wala katika zama zetu ambapo tunapata kuwa kuna watu, kizazi, au jamii ambayo imeshaanza kupokea au ilipokea chapa. Kama wapo, leta ushahidi wako.

      Delete
    4. 1. Nikija kwenye nukta yako ya (4) ni hivi, Misingi ya dini ya uislamu haibagui, mitume wala vitabu vya MUNGU MMOJA. Waislamu tumefundishwa na tunaamini kuwa Mtume Daud (DAVID) Alipewa kitabu kilicho itwa ZABURI, Mtume Musa (Mosses) alipewa kitabu kilicho itwa Taurati, Mtume Issa (JESUS/YESU) alipewa kitabu kilicho itwa Injili na mtume Muhammad (s) amepewa kitabu kinacho itwa Quran. Hawa watano kwa mujibu wa Uislamu ndiyo mitume wakubwa, lakini kwenye Quran wametajwa mitume 25, tangu binadam wa kwanza Adam mpaka mtume wa mwisho Muahammad Jumala ya mitume waliyo kuja ni 125,000. Mitume wote hao walikuja na amri mbalimbali za MUNGU MMOJA, kuna ambao walitimiliza amri zilizo tangulia kama alivyo fanya Yesu kwa Musa, mwenye akisema “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.” (Mathayo 5:17)
      Pia wapo waliokuja kuzitengua baadhi ya Sheria zilizo tangulia, nayo ni hii Quran,
      Quran 2:285 “Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako.”
      Muhhamad (s) ndiye kigizo chetu kwa kila kitu, ikiwa aliwahi kufanya ibada mahususi ya kuabudu katika siku ya Sabato hapana shaka tungekuwa na taarifa kwenye Sunna na kwenye Quran juu ya ibada hiyo na sisi tungeifanya bila kupinga, Muhammad (s) aliwakuta Mayahudi wanafunga siku ya Ashura, akawauliza kwanini wanafunga, wakasema ni kwasababu hiyo ndiyo siku ambayo Allah aliwaokoa kutokana na Firauni na kuwavukisha bahari huku akimuangamiza Firauni katika bahari hiyohiyo. Mtume Muhammad (s) akasema mtume Musa ni ndugu yake na hivyo yeye anayo haki zaidi ya kuifunga siku hiyo, na akaanza kuifunga lakini akitofautisha siku ya kufunga na ile ya Mayahudi, na mpaka leo waislamu wote duniani tunafuata hivyo hivyo, tunafunga hiyo siku ya Ashura. Hivyo na Sabato nayo tungetakiwa kufanya kupitia mtume wetu, tungeifanya.

      Nukta zilizo bakia tafadhali pitia posti za ‘NAMTAFUTA MUNGU’ ya kwanza hadi ya mwisho maswali yako yatajijibu na yakishindikana rudisha hapa tutayapatia ufumbuzi Inshallah.

      Utakaporudi kama ulivyo ahidi tafadhali, rudi na tafiti na siyo maneno matupu

      Delete
    5. This comment has been removed by the author.

      Delete
  14. Replies
    1. Chilu nadhani ulikuwa unasema umefurahishwa sana, endelea kufurahi na kuelimika pia.

      Delete
  15. Kama atakuwa hajakuelewa anaubishi wa jadi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nadhani ameelewa maana hajarudi tena kama alivyoa ahidi.

      Delete
  16. Mkuu nawezaje kupaya kitabu plzz nitumie namba zako

    ReplyDelete
  17. Mkuu nawezaje kupata kutabu naomba tiwasiliane plz

    ReplyDelete
  18. Atakua kaelewa mkuu haina haja ya kuumiza kichwa apo

    ReplyDelete