Kama ambavyo
tutakavyo ona Freemason na wenzao wanaabudu miungu wengi katika majina mengi
tofauti, katika kutekeleza ibada hizo au kuonesha utii kwa miungu hao, maadui
zetu wamechagua njia mbalimbali, alama mbalimbali zikiwemo hizi zinazo fanyizwa
kwa kutumia viungo vya mwili.
Freemason wote
wa YORK RITE, SCOTTISH RITE, SKULL & BONES, na katika kila asasi ya siri za
kishetani kwenye mstari huu wa Illuminanti, wanayo aina fulani ya kusalimiana
na aina fulani ya alama zinazo fanyizwa na mikono yao, alama hizo huwa na maana
mahususi kwa wanachama.
Kwenye buku
rejea la freemason (Masonic Encyclopedia) imeandikwa hivi,
“Mkono ni muhimu
sana kwa freemason ... kwani sababu na lengo la kupokea utambulisho hufanya kwa
mkono.”
MWANACHAMA KATIKA
ROYAL ARCH AU SEVENTH DEGREE, UNAWEZA KUIKUZA HII PICHA NA KUSOMA KILE KILICHO
ANDIKWA CHINI YAKE.
Alama hizi za
kimasonia, ni lugha ya kimataifa baina yao, huizungumza baina yao na huelewana
bila kujali utaifa wao. Manfred Adler, kwenye kitabu chake alicho kiita The Freemason and The Vatican, amesema kuwa
ni kweli kabisa freemason wanawasiliana kokote ulimwenguni bila kikwazo cha
mipaka baina ya nchi zao kwa kutumia alama mbalimbali. Amendika kwamba,
kutokana na tafiti zilizofanywa na ‘United States
Senate Committee’ ambayo ilikuwa
ikiwachunguza CIA, amendikwa kwamba,
“Asilimia tisini
ya taarifa za siri, zinatangazwa, zinapitishwa, zinatumwa kwa kupitia kwenye
vyombo vya habari, kama vile magazeti, kwa msaada wa maneno yaliyofungwa kama
code na picha”
Huyu jamaa
natuambia kuwa kutokana na utafiti huo ni kwamba maadui zetu taarifa zao,
hawazifichi kokote, wanazituma waziwazi kupitia kwenye vyombo vya habari,
kupitia kwenye taarifa ya habari tunayo tizama, magazeti tunayo soma, taarifa
tunazo soma, lakini hatuoni chochote, kwa vile lugha wanayo tumia, ni ngeni
kwetu. Msomaji wa habari au mgeni kwenye kipindi fulani cha Luninga, anaweza
kufanya kitu ambacho mtazamaji anaweza kudhani ni makosa, bahati mbaya au
kioja, lakini walio kusudiwa wakaupata ujumbe wao vyema.
Moja ya filamu za kimasonia waigizaji wake wapo mbele ya Washington monument, ambao ni mnara wa kimasonia, wenye maana pana sana na ambao utaukuta katika kila mji mkubwa duniani ulioshikiliwa na freemason.
ITAENDELEA ......
diamond je,?
ReplyDelete