Tunaendelea pale tulipo ishia ....
Alama ya
‘Entered Apprentice’ au daraja la kwanza au First Degree kwa Blue Lodge,au pia
inafahamika kama daraja la kwanza kwenye blue degree, inayo fanywa na
mwanachama wa daraja hilo, wakati anapoingizwa kwenye jumuiya, alama hiyo, kama
inavyo oneshwa na picha hapo chini, huelezea au kuelekeza wakati mwanachama
anapo chukua kiapo chake kwa mara ya kwanza ndani ya hekalu la kimasonia
kukubali kujiunga na jumuiya hiyo.
“Mkono wangu
wa kushoto unaishikilia Biblia na mkono wangu wa kulia upo juu ya Biblia”
Hivyo ni kwa
mwanachama ambaye imani yake ni ile ya
Kikristu, mwislam atafanya hivyo kwa Quran, na wengine kulingana na vitabu vyao
vya kidini.
Utaona hapa
mwanachama anaapa kwa kutumia kitabu cha dini yake, kwa vile katika Blue
degree, yaani daraja la i,ii, na iii, mwanachama haambiwi kama freemasoni ni
dini mpaka atakapo fika daraja la 18, lakini wengi wao hawavuki daraja la iii,
na hivyo utawakuta freemason wengi hawakubali wanapo ambiwa kuwa wapo kwenye
mtandao unao muabudu shetani, kama nilivyo sema kwenye posti zingine, hawa ni
MAUWA mazuri kwenye ukuta wa nyumba chafu ya dhambi.
Katika daraja
hilohilo, yaani daraja la kwanza, mwanachama huonesha alama nyingine kama
inavyo onekana kwenye picha hii hapo chini.
Alama hii ambayo
nayo hutambulishwa kwa mkono vilevile huwa na maana ifuatayo.
Alama hii
hufanyizwa kwa kupitisha kiganja cha mkono wa kulia, kwa haraka mno, kwenye
shingo.
(Ishara hii huwa tunaiona mtaani kwetu kila
mara ambapo inapotokea mtu anamtishia mwenzake kumchinja)
Alama hii
inaelezea adhabu ambayo mwanamasonia ataipata endapo atakwenda kinyume na
jumuiya aliyo jiunga nayo, jumuiya ya kimasonia.
Mwanamasonia
wakati wa kuchukua kiapo hicho kwa kutumia alama hiyo ya mkono huwa anasema, au
kumaanisha maneno haya.
“Koromeo langu
likatwe katikati, ulimi wangu uvutwe nje wote, na mwili wangu uzikwe kwenye
mchanga mbaya wa ufukweni mwa bahari, ambako mawimbi yanapiga mara mbili kwa
masaa ishirini na nne, ikiwa mimi nitakiuka miiko ya kuingia kwenye daraja hili
la kwanza”
Hicho ni kiapo
kwenye daraja la kwanza kabisa. Rais Kennedy aliuwawa kwa kukatwa koromeo lake
kwa risasi, wakati wa jua la utosi, alikiuka miiko ya kimasonia, ingawa hakuna
ushahidi kama alikuwa ni freemason, ispokuwa kunayo ushahidi kuwa aliwapinga.
Kifo cha Steven Kanumba hata kidogo, hakioneshi aina ya mauwaji yanayo fanywa
na freemason endapo utakiuka miiko yao, na kama nilivyo elezea, Kanumba hakuwa
Freemason na wala hakuna ushaihid wa kushikika kama alikuwa ni freemason, zaidi
ya maneno ya mtaani.
Bado tukiwa
kwenye daraja la kwanza, kuna kile kinacho fahamika kama, BOAZ,
Hapa ni pale
mwanachama mpya anapo anza kutambulishwa kwa wanachama wenzake, kunayo namna
fulani ya kushikana mikono na wanachama wenzake. Aina hii ya kushikana mikono
ataitumia hapo kama utambulisho, wa kutambulishwa, lakini pia katika maisha
yake ya kila siku kama freemason na hata atakapo panda madaraja mengine,
ataendelea pia kuitumia aina hii ya kushikana mikono na freemason wenzake, kama
njia ya kutambulishana baina yao na wenzake.
BOAZ ipo kama
inavyo onekana kwenye mchoro huo hapo.
Mwanachama atalibonyeza DOLE GUMBA lake, Kwenye NAKOSI ya kidole
cha shahada (Index finger), naye mwanachama mwenzake atafanya hivyohivyo.
Mwanachama mpya, atakapo kuwa anafanya hivyo, atasema meneno
yafuatayo kwa mwanachama mwenzake, ambaye ni ‘Worhipful Master’, hichi ni cheo cha juu sana ndani ya hekalu la kimasonia.
Mwanachama Mpya au yule anaye andaliwa kuwa mwanachama, akiwa
amepiga magoti kama ishara ya kuwa tayari kupokea digirii ya kwanza, ataambiwa
maneno haya na Worshipful Master ambaye atakuwa na msaidizi wake.
“Mimi sasa hivi ninaweka mkono wangu wa kulia kama ishara ya
urafiki, udugu na upendo, na nitafanya hivyo kwa kukushika mkono na kutamka
maneno. Maneno haya utatakiwa kuyatamka, kila unapo fanya ishara hii kama
ambavyo yatakavyo tamkwa mbele yako na msaidizi wangu.”
Kisha Worshipful Master atamgeukia msaidizi au mtu wa daraja la
chini yake, wakiwa mbele ya MWANAMASONIA MTARAJIWA, ambaye bado kapiga magoti
na wataanza kubadilishana maneno yafuatayo, kama somo kwa Mtarajiwa mwanachama
aliyopo mbele yao.
VIFUPISHO:
WM: Worshipful Master na SD: Senior Deacon (Msaidizi au
aliyechini ya WM)
WM: Ndugu unayenifuata kwa daraja.
SD: Worshipful Master.
WM: Natanga
SD: Nafanya siri
WM: Unachofanya siri ni nini?
SD: Siri zote za kimasonia, ambazo zinafichwa na alama hii ya
mkono. (Kisha hapo, mwanachama mtarajiwa, anaoneshwa ishara ya BOAZ)
WM: Hiki ni nini?
SD: Mshiko wa mkono.
WM: Wa nini?
SD: Wa - Enterered Apprentice (Daraja la kwanza)
WM: Je huo mshiko unajina?
SD: Unayo jina.
WM: Je utanipatia hilo jina?
SD: Mimi sikupokea, wala sitalitoa.
WM: Ni vipi sasa, utaliweka jina nilielewe.
SD: Taja herufi zake au ligawe kwa usawa.
WM: Taja herufi zake na anza.
SD: Anza wewe.
WM: Anza wewe.
SD: A
WM: B
SD: O
WM: Z
WM: (Akimuambia mwanamasonia mtarajiwa): “BOAZ, ndugu yangu,
ndilo jina la mshiko huu, na lazima litolewe kwa utaratibu wake, kwa kulitaja
kwa herufi au kwa kuligawa nusu kwa nusu. Unapo litaja kwa herufi daima anza na
herufi, ‘A’.
Blair na Papa, wanajua nini wanacho fanya, hiyo ni BOAZ
Papa John na kiongozi wa Israeli, tizama mahali ambapo Sharon ameweka kidole gumba chake, ni juu ya index finger ya Papa John. Wanajua wanfanya nini.
Unaona ni wapi kidole gumba cha huyu ambaye kamshika Bush mkono kilipo wekwa? Jinsi kiganja cha Bush kilivyo kaa, nacho kinatoa nafasi kwa kidole gumba chake, kufanya hivyo hivyo, B-O-A-Z.
Papa Paul VI, naye ndani ya mjengo, kwenye picha ndogo inaonekana vyema namna wote wawili, wanavyo vibonyeza vidole vya shahada vya kila mmoja wao, kwa kutumia vidole gumba vyao.
Kama kawaida ... BOAZ
Wakubwa wawili, kutoka kona tofauti za dunia, wenye mitazamo tofauti ya siasa, uchumi na dini, lakini hapa wanatambuana kwa alama ya siri ya kushikana mikono, jicho la kawaida haliwezi kuona hilo, inaitwa B-O-A-Z.
Unawaona tena hapa, nadhani mimi na wewe tunawafahamu watu hawa kama maadui, Blair na Ghadafi, lakini hapa vizuri kabisa wanasalimiana kwa kutumia, salam maalum, siyo ASALAMALYKUM, WALA TUMSIFU YESU KRISTO, NI B-O-A-Z.
Hii hapa haihitaji maelezo anayeonekana kwenye picha, aliwahi kuwa raisi wa Urusi, halafu akawa waziri mkuu, halafu tena amerudi kuwa Rais wa nchi hiyo ... nadhani unamfaham.
HATA KWENYE MIKUTANO YETU NA WAANDISHI WA HABARI, PALE TUNAPO PEANA MIKONO, KAMA ISHARA YA UPENDO NA UPATANISHI, BADO TUNATUMIA ALAMA YETU YA SIRI Y BOAZ.
Alama hii ya
BOAZ hunaswa na kamera au na jicho la anaye fahamu nini kinaendelea, au kinyume
chake, utaona ni mshiko wa mkono wa kawaida tu.
Itaendelea
....
MIMI SIYO MFUASI WA FRIMASON; LAKINI HAPO NI UONGO MTUPU.
ReplyDeletemmmgh kwa kweli ki\aza sama
Deletenataka kujua vipi free manson unaweza kumjua unapomuona kwa dalili zake
Delete