WAKATI UKIPITIA POSTI HII NA MFANO WA HIZI NAKUOMBA UTAFAKARI MANENO HAYO YA PLATO.
Guys!
Nasikitika mwendelezo wa posti ya ‘PICHA ZA UCHI NA
TATIZO LA NGUVU ZA KIUME’, utaendelea baada ya posti moja au mbili za KISANGA CHA
‘BOKO HARAM’,
Umma umekuwa katika kiza na lindi la ujinga kiasi ambacho
hatuwezi kutofautisha katika ya KIZA na NURU. Haidithi ya Boko Haram na zingine
mfano wake ni mfano hai juu ya maneno ya mtukufu wa daraja (SAW) aliposema zama
karibu na Kiyaam, watu watakuwa WAJINGA MNO. Muumba atuhifadhi na hali hiyo.
Najiuliza ni kipi wanacho fanya Boko Haraam kinaonekana
ni cha Kiislam kiasi waumin wa kiislam kusimamia kidedea jambo hilo na kuliunga
mkono kama ni la kwetu? Ni kama vile waislam tunacheza MUZIKI USIO WA KWETU na
huku tukijinasibu na kujisifia kana kwamba ni wa kwetu na unavionjo na ladha ya kiislam. Si
kweli. Lakini yapi maarifa yetu mpaka tunafika hapa na kuwashabikia Alshabaab
na akina Boko Haram?
YES! MADAM NA YEYE KAGUSWA!! UKISTAAJAB YA MUSA UTAONA YA FIRAUNI.
Maswali hayo ndiyo yaliyonisukuma kuandika posti.
Kikundi cha Kigaidi kilichopo Nigeria, kimekuwa
kikiongoza kwenye vichwa vya vyombo vya habari kote Ulimwenguni. Habari kuhusu
Syria zimezikwa, Iraq kimya, Afighanstan hakuna, sasa wimbo unaoshika chati na
kuuzika kwenye vyombo vyote vya habari ni BOKO HARAAM!
Zi wapi akili zetu, sisi tulioitwa kwenye Quran karim kuwa
WATU WENYE KUFIKIRI, WATU WENYE AKILI, na mfano wa hayo, mbona tunacheza muziki
usio kuwa wa kwetu?
MTIZAME NA SILAHA YAKE NZITO NA KICHWANI AMEWEKA ANUANI YAKE KUWA YEYE NI NANI. LAKINI NI KWELI HIYO ANUANI ALIYOIVAA KICHWANI NDIYO INAMUONGOZA KUFANYA HIVYO, AU NI AJENDA ZA WASHINGTON NDIZO ZINAZOMUONGOZA?
Wimbo huu wa Boko Haraam unatofautiana gani na wimbo wa
9/11, wimbo wa Iraq, Afighanstan, Alqaeedah na wengine?
Bila maarifa na mbinu zenye kufahamika za kivita, kikundi
kidogo cha Boko Haraam kimeweza kuteka watoto wa kike wapatao 300 kutoka shule
iliyopo Chibok, April 14 mwaka huu.
Muda ambao tukio hili limetokea, na muda ambao vyombo vya
habari vimekuja kuliripoti ni kama filamu za kuigiza kutoka Hollywood, karibu
mwezi mzima ndiyo dunia inajua kwamba Boko Haraam wameshafanya mambo! Jamani
hii ni kweli?
Dengu imezuka tu hapa kwetu, lakini sasa kila mtu anajua
kuna ‘dengu’ Tanzania, lakini watoto 300, mwezi unaisha ndiyo dunia inafahamu
jamani mi hainiingii akili hata kidogo.
Washington nadhani walikuwa bizzzzz sana kuzinyaka hizi
nyuzi, lakini siunajua kwamba Obama safari hii yupo Bize sana na Urussi kule
..., halafu kuna zoezi la kugawa na kusambaza silaha kwa vikundi vya kiislam
kote duniani kuendeleza vita vya kigaidi, halafu si unajua kuna ile ishi ya
ndege iliyopotea ... ha ha ha dunia leo inayo vioja kama siyo viroja, ishu ya
ndege nitakuja nayo soon tu, siamini kwamba kwenye uso huu wa dunia ndege
inaweza potea, ajabu sana, sana, sana ..... any way tuendelee na mtanange wetu
wa Boko Haraam.
KILEMBA KIKUBWA, MSWAKI WA MTI, NDEVU NYINGI, VYOTE HIVYO VINAKUAMBIA YEYE NI NANI, LAKINI NI KWELI YEYE NDIYO HUYO AU ANATUMIA MAVAZI YETU KUIPOTOSHA DINI YETU?
Lakini yote juu ya yote, FBI tayari wapo ndani ya nyumba
kututatulia jambo letu, maana askari wa kila nchi na majeshi yao hawajafanya
kazi yao ikakamilika kama FBI hawajaalikwa.
Lakini kama kweli FBI wanataka kutambua ukweli wa tukio
zima, nadhani wangeanzia Washington ambapo, kwa muda mrefu jina la Boko
Haram kwa sababu zisizo weza fahamika haraka hawakuingizwa kwenye orodha ya
kikundi cha kigaidi pamoja na yote waliyo kuwa wakiyafanya.
Halafu zikaja habari zingine kuwa zaidi ya wasichana 50 wamefanikiwa kutoroka kwenye mikono ya Boko
Haram na zaidi ya wasichana 200, bado wapo nao.
Bado sijapata data wasichana hao wametorokaje na nini
walicho shuhudia walipokuwa kwenye mikono ya Boko Haram, nadhani watakutanishwa
na FBI iliwaanze ‘kushoot’ vidio za namna walivyo toroka na urongo mwingine
halafu waturishie kupitia BBC na CNN.
Kama ilivyo tabia ya vikundi vingine vya kigaidi mfano wa
hivi, Boko Haram nao wapo kwa ajili ya kusimamisha dola ya Kiislam, a.k.a
Sharia Law na mipango yao ni Nigeria, Cameroon na Niger. Shughuli kubwa ni
kuuwa waumini wa Kikristo, kuwafanyia ugaidi, kulipua makanisa, majengo ya
serikali, kuteka watalii kutoka nchi za magharibi, na lingine kwenye orodha na
ingawa si la mwisho ni kuwashambulia waislam wenzao ambao wanao msimamo tofauti
na wao, na sasa naona wamejiingiza kwenye biashara ya kuteka watoto. Ofcourse BBC Swahili wanatuambia
wasichana wote walio tekwa sasa wamesilimu na walionekana wakisoma Quran na
kushikilia bango lenye maneno ya Kalima
tawhiid. Likini BBC wakapiga kimya kutuambia katika waliokamatwa wamo pia
Waislaam.
WALIO KAMATWA HAO, HAPO WANAOMBA 'DUA' PICHA HII INANITIA MASHAKA MENGI, MOJA WAPO NI NAMNA BINTI HAWA WALIVYO TULIA, YAANI WAMERIDHIIKA KABISA NA DUA WANAOMBA, MH! OOOOH BBC WALITUAMBIA KUWA WOTE WAMESILIMU, DUH!
Nigeria ni moja ya nchi tajiri mno barani Afrika, tajiri
wa mafuta, lakini kama yalivyo mataifa mengine barani humu nalo limegawanywa
kwenye misingi ya kidini, kikabila kwa malengo mahususi. Makampuni kama BP,
Shell, na Chevron wanavuna mafuta kama hawataki vile, na ili waendelee
kufaidika na hili lazima Nigeria ibaki kwenye migawanyiko na kila wakati pawepo
na lile la kuwa shughulisha, na leo ni Boko Haram.
Boko Haram haifanyi hayo kwa faida ya Uislam na Waislam,
bali kwa faida ya Illuminati na ajenda zao. Nigeria likidorora kiuchumi,
kisiasa, na kila wakati ikiwa bizz kushughulika na Alqaeeda na Boko Haram,
Illuminanti wanaendelea kuingiza majeshi yao kwa kisingizio hichohicho na
kuendelea kuitawala na kuinyonya.
Moja ya malengo makubwa ya US na NATO chini ya utawala wa
kibaraka mweusi anayeitwa Obama ni kuhakikisha kuwa Marekani na washirika wake
wanawekeza kijeshi katika bara hili kwa kuingiza majeshi yao hasa, kwenye hili
tumeona story ya Rwanda na Afrika ya kati, tizama posti hii http://salimmsangi.blogspot.com/2014/01/malighafi-za-afrika-na-damu-ya-waafrika.html
Mpango huu
ulianza tangu wakati wa utawala wa Bush, 2007.
Waweza pitia dokumenti hii kupata undani wa habari
yenyewe, http://www.africom.mil/downloadCenter.asp
Lengo la mpango huo ni upi basi?
Mchina hatakiwa Afrika, It all about Power and Enomics,
HAKUNA ISHU YA SHARIAH WALA UGAIDI,
ITS ALL ABOUT POWER. SI MUZIKI WETU HUU ...
Kwenye muswada huo Washington walikuwa na bado wanahofia
kwamba Mchina na yeye ataleta majeshi yake kwa ajili ya kulinda maslahi yake
Afrika, ilikuondoa uwezekano huo, lazima wao watengeneze mazingira ya wao kutia
mguu kwanza, Boko Haram, Alshabab, na vikundi vingine vya kigaidi ndani ya Afrika
vitarahisisha hilo.
BUSINESS HOUR AS USUAL
Nato na US wapo Libya, lakini sote tunajua wamefikaje hapo,
wapo pwani ya Somali, tunajua wamefikaje hapo, na sasa FBI wapo Nigeria,
hutasikia lini wanaondoka, lakini utasikia lini wanaongezwa wengine. FBI
watakuwepo na Boko wataendelea kurindima kama kawaida.
Lakini kuna anaye fahamu zaidi ya Washington kwamba
ukitaka kuingiza majeshi yako sehemu fulani ufanye nini? Washington wanajua
ukitangaza kuna gaidi kona fulani, hakuna atakaye kuuliza chochote endapo
utaamua kuweka kambi mahala hapo. Vikundi vya kigaidi Afrika vimekuwa kama
migawaha ya Mcdonald au kinywaji cha Coca Cola. Kila kona utazikuta bidhaa
hizi, lakini watengenezaji ni tofauti kutoka kona moja ya dunia kwenda nyingine,
isipokuwa LADHA YAKE NI ILEILE. Wenyewe wanaiata ‘FRANCHISE BUSINESS’.
Ugaidi nao umekuwa franchise,
mfano Boko Haram sasa ni jina la kibiashara, kama ilivyo kwa Alqaeedah, si
unajua Alqaeedah baada ya Afighanstan, wakawa na maajenti, Afrika, Marekani,
Ulaya, na nchi za Asia, yesss, its all
about business. Ndani ya Nigeria kwenyewe kuna zaidi ya Boko Haram 5, kumbuka
Franchised Business. Swali la
kujiuliza ni nani anayetoa mtaji?
Tutakuja huko.
Kitu kimoja ambacho uongozi wa Obama umefanikiwa kwa
kiasi kikubwa ni kugawa na kutawanya silaha kila pale zinapohitajika kupitia
mawakala wake mbalimbali. Eidha ni Mexico kwa wauza unga, Libya kwa
wanamapinduzi, Syria kwa ‘Free Army of Syria, Somalia kwa Alshabaab, Algeria na
Mali kwa Alqaeedah, hapana shaka imekuwa ni business
nzuri kwa Washington na mashirika ya silaha duniani.
KILA MTU ATASHIKA BANGO HILI, SUBIRI TU, SOON UTAWAONA VIONGOZI WA KITAIFA NAO WAKIANZA KUSHIKA BANGO HILO. LENGO NI KUKUSHIKA KIAKILI NA HIZO PROPAGANDA NA KUSAHAU KUWA ADUI NA HUYO ANAYESHIKA BANGO WOTE LAO NI MOJA.
Wakati NATO walipokuwa Libya, kulikuwa na watu
waliofahamika kama Libyan Islamic Fighting Group ambao nao wakajiunga na tawi
la Alqaeedah lilipo hapo Libya, na makundi yote mawili chemchem yake ni miaka
ya 80 ambapo Washington walikuwa wakimuondoa Mrusi kwenye U-Super Power. Sasa Washington
wameuza leseni ya ugaidi kwa Boko Haram katika mtindo ule ule wa Franchise business.
Wakati wa mahojiano na kiongozi wa Alqaeedah kwenye tawi
la Libya, Abu Mousab Abdel Wadoud, kiongozi wa kundi hilo, alisema kuwa kundi
lake hilo linatoa mchango wa silaha kwa Boko Haram ililiwaze kuwalinda waislam
wa Nigeria. Utakumbuka kipindi fulani nyuma Alshaabab nao walisema wameungana
na Alqaeedah kwa madhumuni hayohayo. Lakini mimi sina shaka na madhumuni yao,
shaka yangu na kwa Washington ambao ndiyo wanao viunda vikundi hivi na
kuhakikisha kuwa vinaendelea kuwepo.
Washington wanafahamu kuwa hawawezi kuimba ALQAEEDAH,
ALQAEEDAH, miaka nenda rudi, wataonekana ni wendawazimu kwamba hawezi
kuwashinda jamaa hao, sasa wafanyaje, tufanye Franchise kwenye business ya
ugaidi, ndiyo sasa ukawaona kina Boko Haram, Alshabab, Free Syria Army, n.k.
Unapo watizama mawakala hao wa Washington waliopewa
leseni ya kufanya ugaidi utaona kazi zao kubwa ni kuzorotesha nchi husika
kiuchumi, kiulinzi, kisiasa na kijamii na kujenga migawanyiko na matabaka baina
ya wananchi husika kiasi nchi haiwezi kukalika tena mpaka Washington na washirika
wake watakapo ingia na ‘kuiweka’ nchi sawa.
Kwa uchache mawakala hao wenye leseni za kufanya hivyo
kutoka Washington ni:-
-
Boko Haram leseni yao inawaruhusu kufanya
kazi yao Nigeria, Niger, na Mali.
-
Alshaabab leseni yao ni Somalia na Kenya.
-
Al Qaeedah in Islamic Magreb (AQIM) hawa ni
Algeria na Mali.
-
Musilim Brotherhood hawa ni Egypt.
-
Libyan Islami Fighting Group hawa ni Libya.
-
Al Qaeedah hawa leseni yao ni dunia nzima.
-
Majina hayo kwa uchache lakini yapo mengi
mno.
Waweza pitia mitandao ifuatayo kwa
undani wa habari hii.
http://www.theguardian.com/world/feedarticle/11322064
WikiLeaks revealed that they are part of the US Central Inteligence Agency:
http://imnig.org/boko-haram-cia-covert-operation-%E2%80%93-wikileaks
http://www.washingtontimes.com/news/2013/nov/13/us-designates-boko-haram-terrorist-organization/?page=all WikiLeaks revealed that they are part of the US Central Inteligence Agency:
http://imnig.org/boko-haram-cia-covert-operation-%E2%80%93-wikileaks
UMEELEWA KIKARAGOSI HICHO. ? TAFAKARI TILL NEXT TIME
No comments:
Post a Comment