Clinton alisimama kama muwakilishi wa wapenda vita, wauwaji, waporaji na
kila kila baya unaloweza kulirikodi kwenye historia ya dunia.
Trump alisimama kama malaika, mpingaji wa yote Clinton anayo yawakilisha,
anaye taka kubadilisha njia ambayo umma umeupita kila uchao.
Vyombo vya habari kote duniani, wasomi, watu maarufu kwa kiasi kikubwa
waliona nguvu iliyo nyuma ya Clinton, na hakuna anayetaka kucheza kamari na
akashindwa, hivyo mahala pa kuweka pesa yako na ushinde ulikuwa ni upande wa
Clinton.
Lakini imekuja tofauti!
Je wananchi wameshinda?
Trump tangu mwanzo wa safari hii alikuja tofauti sana, sizungumzii kipindi
cha kampeni, lakini nyuma kabisa kwenye miaka ya 80 alipokuwa ananyanyuka
kibiashara, alipoulizwa swali juu ya sera za Marekani na nini anaweza kufanya
kuibadilisha, alionekana yupo tofauti kabisa, na amekuja hivyo mpaka amekuwa
rais mteule.
Amekuwa kinyume na chama chake, na sera zake ni kinyume na sera za mambo ya
nje za Marekani kama ulivyoona kwenye hiyo vidio hapo juu.
Lakini mfumo wa utawala na siasa za Marekani wenye nguvu si wanasiasa.
Hillary alipokea pesa nyingi kwa maana ya michango kutoka kwa mashirika na
taasisi ambazo zimekuwa zikifanya hivyo zama zote za uchaguzi, na kila mgombea
aliye shinda aliwasikiliza kwanza mabwana wakubwa waliyo muwezesha kufika hapo,
mabwana wakubwa ambao inasemekana wana mtazamo na malengo na mipango tofauti
dhidi ya walimwengu wote. Kama ulivyo muona Trump na kumsikia kwenye hiyo vidio hapo juu akithibitisha hilo la wanasiasa kununuliwa.
Trump naye alipokea vijisenti hivyo kupitia chama chake, au kwake moja kwa
moja, ingawa havikuwa vinono kama vya Clinton. Je ni kusema atasimama dhidi ya
‘mfumo’?
Swali hili linaonesha ni namna gani jamii imesukwa na mfumo kiasi haiwezi
kuona njia tofauti na hiyo ya mfumo. Tuliona kuwa Hillary ndiye atakaye shinda
sababu tumesukwa kuona hakuna jema litakalo kuja ile ubaya, kiasi cha kutamani
ubaya, na ikawa ni maajabu Trump aliposhinda dhidi ya Hillary, hakuna aliyeona
hilo linakuja.
Ispokuwa wale wale ambao tuludhani wanataka Hillary ashinde ndiyo waliona kuwa Trump atashinda, au ndiyo waliotaka Trump ashinde, tizama hiyo katuni ya simpsoni hapo juu. Ilitolewa nadhani ni mapema mwaka 2016 kama siyo nyuma kidogo.
Kwa taarifa tu ni kuwa simposoni na katuni nyingine na pia filamu nyigni za Hollywood zimekuwa zikitumika sana kuwaambia walimwengu mambao yatakayo kuja miaka kadhaa baadae, na hii ikithibitisha kuwa matukio mengi ya kihistoria na makubwa duniani yalisha pangwa kitambo.
Ispokuwa wale wale ambao tuludhani wanataka Hillary ashinde ndiyo waliona kuwa Trump atashinda, au ndiyo waliotaka Trump ashinde, tizama hiyo katuni ya simpsoni hapo juu. Ilitolewa nadhani ni mapema mwaka 2016 kama siyo nyuma kidogo.
NI SHIDDAH!!
Kwa taarifa tu ni kuwa simposoni na katuni nyingine na pia filamu nyigni za Hollywood zimekuwa zikitumika sana kuwaambia walimwengu mambao yatakayo kuja miaka kadhaa baadae, na hii ikithibitisha kuwa matukio mengi ya kihistoria na makubwa duniani yalisha pangwa kitambo.
Je ni saikolojia hiyo hiyo inayo tuongoza kuona kuwa Trump hawezi kufanya
chochote sababu ‘mfumo’ unazo nguvu mara milioni kushinda yeye?
Ukitizama historia ya ‘mfumo’, kwa wale ambao tunaamini juu ya kuwepo kwa
mfumo, kutokana na kuwepo kwa viashiria na doti za kutosha zinazo chora picha
ya ‘mfumo’ kwenye maisha na matukio ya kila siku kutoka ya kijamii, kiasiasa,
kiuchumi na kidini.
Mfumo huu ni wa muda mrefu kuliko kama ilivyo historia ya binadam mwenyewe
kwenye sayari hii. Iwe unaitazama historia yake, kidini, au kiuchumi, au
kijamii na hata kiasiasa, kote huko pana onekana uwepo wa mikono ya siri inayo
amualia matakwa na muelekeo wa sayari hii na mustakbali wa vilivyomo.
Lakini lengo kuu la mfumo kutokana na nukta tulizo weza kuzi onganisha kwa
wale ambao tunao amini juu ya kuwepo kwa mfumo huo ni kusimamisha (1) Serikali
moja ya dunia nzima, (2) Mtawala mmoja wa dunia nzima (3) Dini moja kwa binadam wote (4) Sarafu moja kwa dunia
nzima. Zaidi kuhusu malengo na mipango hiyo tizama posti hii_ http://salimmsangi.blogspot.com/2013/05/tunaendelea-na-safari-lakini-leo.html
Utaona kuwa ‘mfumo’ huo si kwamba tu ni mpango wa zaidi ya milenia kadhaa
wa kadha, lakini pia umegharimu mamilioni ya roho za watu, matrilioni ya dola
za Marekani, maelfu ya mipango na mikakati, sera na sheria, vita na majadiliano
mpaka umefika hapa. Kilicho nyuma ya historia ya ‘mfumo’ hata kidogo huwezi
kukilinganisha na Trump. Mfumo na Trump ni kama Nyangumi vs Kambare.
Kivitendo demokrasia imeshindwa.
Demokrasia imeshindwa kuwapatia wanachi mtu sahihi atakayesimama kama
kiongozi wao. Demokrasia imeshindwa kuleta majibu sahihi na mikakati dhidi ya
matatizo yanayo wakabili wanachi kote duniani.
Matatizo mengi tuliyo nayo sasa ni kutokana na mfumo unao tumika kutatua
matatizo hayo. Hii si kwa Marekani tu, lakini kote duniani. Ukitazama katika nchi zetu zinazo endelea
ndiyo imekuwa balaa zaidi.
Ni mjadala mwingine mpana kuzungumza ni vipi demokrasia imeshindwa. Lakini
ikiwa vyama viwili vinavyo shiriki kutoa mgombea na hatimaye raisi wa nchi;
vipo juu ya wananchi; yaani wananchi hawana lolote kwenye vyama hivyo zaidi ya
kadi ya uanachama, unafikiri ni vipi vyama au wagombea wao wataweza
kuwasikiliza wananchi?
Unapo ichambua siasa ya Marekani utaona wanachi wanatakiwa kuwapigia kura
wagombea ambao ni vyama ndiyo vimewapa baraka ya kushika bendera ya kugombea
uraisi; siyo wananchi.
Lakini vyama hivyo wawezeshaji wao wakubwa ni walewale maadui wa wananchi.
Au ni watu wachache wenye matakwa yao binafsi ambayo wanatumai yatatimizwa na
wagombea pindi watakapo ingia madarakani, hivyo wana wahonga wagombea kabla ya
uchaguzi kwa kutoa michango mbalimbali kusaidia kampeni zao. Mahitaji ya hao wachache
ndiyo yanayo tengeneza sera na sheria za nchi.
Sasa Trump naye ameingia madarakani kwa mfumo huo huo, ni vigumu
kunishawishi kwamba atakata tawi la mti alilokalia.
Mfumo ulioshindwa, demokrasia, ndiyo uliyomuingiza madarakani, je tunaweza
kutatua tatizo kwa akili ile ile iliyotumika kutengeneza tatizo? HAPANA.
Pamoja na ushahidi wa kihistoria ambao una msimamisha Trump kama mtu
tofauti na mfumo ulivyo, mtu ambaye kwa muda mrefu sana amekuwa akizikosea sera
za nje na za ndani za Marekani, na ambaye aliitamani nafasi hiyo ili aweze
kufanya mabadiliko, ni vigumu kusema this time people won?
PLAY HII VIDIO, NA WEWE UWE HAKIMU
To be continued Inshallah ...



















No comments:
Post a Comment