Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Friday, December 13, 2013

FREEMASON WA KIKOLONI HAWAKUIACHA AFRIKA HURU ...

Umewahi kuitizama filamu iliyokwenda kwa jina la ‘Sugar Hill’, ni filamu ya siku nyingi, na naweza kusema moja ya filamu za mwanzo kuchezwa na Wesley Snipes, nimeitaja filamu hii kwa vile maudhui yake kwa namna fulani yanataka kuwiana na posti yetu ya leo.

Katika filamu hii familia ya ‘Skuggs’ ambayo ndiyo familia anayo toka Wesley Snipes, imeathirika na dawa za kulevyea, kutoka Baba, Mama na baadaye watoto na hasa kaka yake na Snipes.
Snipes na ndugu yake walishuhudia mama yao akifa mbele ya macho yao baada ya kuzidisha dozi ya dawa za kulevyea, badaye baba yake alipata ulemavu kutoka kwa wauza baada ya kushindwa kulipa fedha alizokuwa akidaiwa, ulemavu huo ambao nusura uondoke na maisha yake, lakini hata hivyo bado ni dawa za kulevyea ndizo zilizo kuja kumua baba yao.


Ingawa familia hii ya Skugg haikuwaandaa watoto wao wasiingie kwenye njia iliyo wazamisha wao, lakini yalikuwa ni maombi, matumaini na tamaa yao kuona watoto hao watasimama kwenye njia tofauti na ile waliyopita wazazi wao.

Lakini hadithi ilikuwa ni tofauti kabisa...

Familia hii ya Skugg, kwenye filamu hii ya Sugar Hilll, haina tofauti sana na hadithi ya wapigania uhuru wa Afrika na wale walio zirithi nchi hizi baada ya uhuru.

Katika Sugar Hill wazee wake na Snipes hawakuwaachia wanawe mwongozo wasiingie kwenye dawa za kulevyea ingawa ilikuwa ni HAMU yao kuona HAWAINGII huko. Wakati Babu zetu wanatukabidhi nchi zetu baada ya uhuru, ilikuwa ni HAMU yao kuona kuwa watoto tulio zapokea nchi hizo KAMWE HATUTO ZIRUDISHA KWENYE MIKONO YA WAKOLONI.’
Lakini kama ilivyokuwa kwenye Sugar Hill, hadithi ya bara hili nayo ikawa ni tofauti kabisa ...

Wakati Snipes amekuwa mtu mzima na anajitambua, alimkumbuka mama yake siku moja, na akasema maneno haya akiwa kwenye kaburi la mama yake ...

Dear mother, seems like eternity since you have bee gone. So much has happened. So many dreams turn into nightmares. You always wanted the best for me. But I guess it wasn’t meant to be that way. The Sugar Hill where you always wanted us to live, is now a memory, a burned out jungle, a ghost of a better days, like my father- lost out of reach. And the Boy you loved has become the man you feared, getting rich of the same poison that killed you and destroyed my father. Partner with the same men that stripped away our family dignity. Uneasy partners, tied together by time, fear, and greed ...

Maneno hayo,

Maneno hayo, yatizame tena, nadhani ni maneno ambayo tunaposimama kuwakumbuka wale ambao walipoteza mali, familia na uhai kupigania uhuru wa mataifa yetu, kama basi hatutaweza kuyatamka maneno hayo kwa haya tulizo nazo, basi tuyakiri mioyoni mwetu, kwamba tumewasaliti.

Kwamba zile ndoto za uhuru zimegeuka na kuwa jinamizi, kwamba tumegeuka na kuwa watu ambao wao waliwaogopa, tunajitajirisha kwa kile ambacho kilicho wauwa wao na kuzichana familia zetu, tunashirikiana na watu ambao walizivua heshima nchi zetu, katika ushirika mgumu unao lindwa na muda, hofu na tamaa ...
Hivyo ndivyo Afrika yetu ilivyo leo, hatukukabidhiwa uhuru, kwa maana ya uhuru uliopiganiwa na wazee wetu ...

Kwenye hili nataka tuitizame Afrika ya kati halafu ni kuache na maswali ya nini hatma ya Afrika Mashariki.

Utakuwa umelala usingizi wa pono kama bado unaamini au unafikiri kuwa kile kilicho tokea Rwanda ni kwa sababu ya ‘Ukabila’ kati ya Wahutu na Watusi, kama ambavyo vyombo vya habari vya kimagharibi na vile vya kwetu vya ku-copy n paste vilivyo ripoti.

Ingawa kweli kuliwa na chuki za kibaguzi baina ya Wahutu na Watusi, tena chuki ambazo zilitengeneza makusudi na wakoloni katika kipindi cha ukoloni, lakini hiyo haikuwa sababu kuu iliyopelekea ndani ya siku 100, watu takribani 1000000 wapoteza uhai, na dunia nzima ikitizama kama vile wanao uana si binadamu.

Mikono na sura ambazo zilikuwa hazionekani, lakini zilizo kuwa zikishughulika kwa kiasi kikubwa kufanikisha mauaji hayo ni IMF na World Bank.

Vyombo vya magharibi katika kuelezea mauaji haya vilitumia misamiati kama vile “countries in transition,” “A painful stage in their evolution from one party state towards democracy and the free market”

Wakati vikisema hayo ‘havikukumbuka’ kuuambia ulimwengu kuwa ni mpango na sera mpya za kilimo chini ya IMF na World Bank ambazo ziliwapelekea wakazi wa maeneo hayo kupotelea kwenye kiza cha umasikini.


Kuharibika kwa hali ya uchumi ambako, nako kulipelekea kuanguka kwa soko la kimataifa la kahawa, na kile kilicho fahamika kama ‘macro-economic reforms’ kutoka kwa Bretton Woods, kiliongeza msuguano baina wa kitabaka.

Utaratibu ulio wekwa na ‘International Coffee Agreement’ (ICA) kufahamika kama ‘quotas’ ulianza kuparanganyika. Wanunuzi wa kahawa ya Burundi, ambao waliinunua kwa bei ‘maalum’ waliyo taka wao hawakuwa wakilipa fedha zao kwa wakati, halafu soko la kahawa kimataifa likaporomoka kabisa na bei yake kushuka.

JINAMIZI LA UKOLONI

Kwanza ikumbukwe kabisa kuwa, chuki za baina ya Watusi na Wahutu ni matokeo ya mbegu ya mgawanyiko iliyo pandwa na wakoloni kwa faida na maslahi yao.

Utawala wa wa Belgiam wakati wameikalia nchi hiyo, ndiyo hasa ulio zaa chuki hiyo ya kikabila. Machifu walio teuliwa na wakoloni hao, walipewa mamlaka ya kuwalazimisha wananchi wao kufanya kazi za mkoloni kwa lazima, walipewa mamlaka ya kuwapiga na kuwanyanyasa wale ambao waligoma, kwa vile machifu walikuwa wakitoka kwenye kabila moja, hii ilitengeneza mazingira ya kuonewa kwa kabila jingine. Lakini hicho ndicho mkoloni alikitaka ili aweze kuvunja ule umoja wao wa kitaifa walio kuwa nao hapo kabla.



Mpaka hapo mkoloni hakuonekana kama ndiye adui wa Wanyarwanda, bali Mnyarwanda alimuona mwenzae ni adui kwa misingi ya kikabila. Katika kipindi hichi, Watusi ambao walikuwa ni wachache, ndiyo walio pewa mamlaka dhidi ya Wahutu walio wengi.

Mkoloni huyo akatengeneza vitambulisho, ambapo vilikuwa vikimtambulisha ‘HUYU NI MTUSI’ na ‘HUYU NI MHUTU’ Lakini zaidi ya hapo vitambulisho hivyo vikisema kuwa ‘Mtusi ni mfugaji’ na ‘Mhutu ni Mkulima.’ Katika kuongeza mgawanyiko huo, mkoloni alijenga shule ambazo walisomeshwa watoto wa machifu tu.

Utaratibu huu wa kikoloni wa kuwasomesha watoto wa machifu, au watoto wa tabaka aua kabila fulani, ulikuwa ni kote kwa sehemu zote wakoloni hawa walipokuwepo. Na hao watoto wa machifu walio someshwa, kama vile zilivyo kuwa, shughuli mbalimbali za mkoloni, kuwa ni kwa faida yao na nchi zao, na hata watoto hawa wa machifu walikuwa wakipatiwa elimu mahususi kwa ajili ya shughuli mbalimbali kwa manufaa ya wakoloni hapo baadaye.


Lakini kubwa zaidi, WAKOLONI WALIKUWA WAKIWATENGENEZA WATU WATAKAO WAACHIA NCHI WAO WATAKAPO ONDOKA, WATU HAO AMBAO WATAONEKANA NI WAAFRIKA WENZETU, LAKINI FIKRA NA MITAZAMO YAO ITAKUWA NI ILE YA KIKOLONI.
HII NDIYO MAANA NASEMA KUWA ‘AFRIKA HAIJAPATA UHURU WAKE BADO KUTOKA KWA MKOLONI.’ SABABU NI WATOTO WA MACHIFU WALIOANDALIWA NA MKOLONI NDIYO WALIOPEWA NCHI.

PIA UTAONA WAPIGANIA UHURU WENGI HAWAKUTOKA KWENYE LILE TABAKA AMBALO LILIKUWA NI ‘TABAKA’ TEULE LA MKOLONI, MFANO MZURI NI HISTORIA YA KUPIGANI UHURU WA TANZANIA ILIYO POTOSHWA.

WATOTO HAWA WA MACHIFU BAADA Y KUIPOKEA NCHI KUTOKA KWA WAKOLONI, WAKAIENDESHA KWA KUFUATA NJIA, NA MIPANGO NA MIKAKATI ILEILE YA MKOLONI, NA HATA HALI ILIZIDI KUWA MBAYA KATIKA KIPINDI HICHI CHA MKOLONI ‘MWEUSI.’
WALE AMBAO WALIKUWA WABISHI NA WALIKATAA MAONO HAYO YA WAKOLONI, BASI WALIONJA JOTO YA JIWE, TUNAMKUMBUKA, SAMORA MACHELE, PATRICE LIMUMBA, STEPHEN BIKO, ANWAR SADAT,WALTER RODNEY na wengine wachache ambao sijawataja...

HAWA NDIYO WALIO KUWA WATOTO WA AFRIKA.
WENGINE WENGI WALIOBAKIA NA WENGINE AMBAO BADO WAPO MADARAKANI MPAKA HIVI SASA, WANACHEZA NA KUIMBA WIMBO MMOJA NA WALE WALIO ITWA WAKOLONI, KAMA ALIVYO SEMA SNIPES KWENYE ‘SUGAR HILL’ ... Partner with the same men that stripped away our family dignity. Uneasy partners, tied together by time, fear, and greed ...’

WAKABADILISHA HISTORIA ZA NCHI ZAO ILIWAONEKANE KUWA WAO NDIYO WATOTO WA AFRIKA, LAKINI lies never stand the taste of time au kama wanavyo sema waswahili ... penye ukweli uwongo hujitenga ... LEO TUNAWAONA KWA SURA ZAO ZA HALISI, LEO TUNAJUA KUWA WAMETUFIKISHA HAPA TULIPO KWA VILE WAO NA WALE WAKOLONI LAO LILIKUWA NI MOJA.
KAMA TUNAZUNGUMZA KWA KUTUMIA MISEMO, BASI NI KWELI KABISA TANZANIA NI NCHI YA MAZIWA NA ASALI ... LAKINI LEO IKO WAPI, MIAKA 52 YA UHURU NA NCHI INAZAMA KILA UCHAO KATIKA KILA AINA YA SHIDA, CHUKI,MATATIZO NA DHIKI. YUKO WAPI YULE ALIYO ITWA ‘BABA WA TAIFA?’ MIAKA 25 BAADA YA KUMTUMIKIA MKOLONI NA KUHARIBU HATA VILE VILIVYO ACHWA NA MKOLONI MWENYEWE AKAAMUA ‘KUNG’ATUKA.’ LAKINI HISTORIA IMEBADILISHWA NA YEYE ANAONEKANA KAMA NDIYE MPIGANIA UHURU NAMBA MOJA WA NCHI HII, WAKATI SOTE WENYE AKILI TUNAFAHAMU, WAKATI YEYE ANAZALIWA WATU WALISHAANZA KUPIGANIA UHURU, MBONA HAWATAJWI HAO MASHUJAA WENGINE WA KWELI?
MBONA HAPAULIZWI NI VIPI MWALIMU ALIFIKA PALE ALIPOFIKA, LAKINI SWALI LA MSINGI KULIKO YOTE KWANINI ALIISALITI TANZANIA? ...

ANY WAY TURUDI RWANDA ....
Tangu nchi hiyo ilipo pata uhuru wake mwaka 1962, mahusiano yake na wale walioitwa wakoloni na ‘donors’ yakawa ya ajabu zaidi. Wakati wa ukoloni walio pewa nafasi kubwa kimamlaka walikuwa ni Watusi, lakini ‘walipoondoka’ wakoloni, madaraka wakayaacha kwa Wahutu, hii ilikuwa ni muhimu ilikuchochea moto unao waka! Wahutu wanapewa nafasi ya kulipiza machungu yao wakati wa Ukoloni.
WAPO PAMOJA NA MABWANA WAKUBWA ....

Pamoja na kuwa nchi ya Rwanda ilibaki kwa Wanyarwanda wenyewe, lakini mbegu ya chuki ya kikabila iliyo pandikizwa na mkoloni ilishamea vizuri. Sasa chuki hiyo ilianza kuonekana kwenye sekta za serikali kama vile kwenye jeshi, kwenye mambo ya kiuchumi na kwenye mambo ya kijamii pia.

Mwaka 1990, mbegu ya chuki ya kikoloni ikaanza kutoa matunda yake, machafuko ya ndani ya kazuka, baina ya Watusi dhidi ya Serikali ya Wahutu. Kama kawaida ‘Donors’ na aliyekuwa mkoloni wakaingilia kati mzozo huo, wakataka mapigano yamalizwe na watu warudi mezani wazungumze. Donors wakaweka masharti yao wanayo taka yafuatwe ili waweze kutoa chochote ‘kuijenga’ nchi na uchumi wake.

Walicho kitaka ‘Donors’ kwa Rwanda ili waweze kuwapatia hiyo ‘misaada’ ni kile walichokiita ‘Democratization.’  Walitaka kile wanacho kiita ‘mfumo wa vyama vingi.’

Lakini walifahamu hilo halitoweza kuwezekana kwa nchi ambayo tayari imeshagawanywa kwenye misingi ya kikabila, kwa nchi ambayo tangu kuanguka kwa bei ya kahawa kwenye soko la kimataifa, imefanywa kuwa ni tegemezi kwenye mifuko ya Donors chini ya IMF NA WB.

Nchi hiyo ili iweze kuendelea kupokea ‘misaada’ kutoka Marekani, ilikuwa ni lazima ibadilishe sera zake za kiutawala na uchumi pamoja na kuonesha ukuaji wa ‘demokrasia.’

Maisha magumu na mazingira magumu ya kiuchumi kwa Wanyarwanda, yaliyosababishwa na vita pamoja na sera za IMF, vilikuwa ni vikwazo vigumu kabisa vya kuelekea kwenye hiyo demokrasia ambayo mataifa wahisani walikuwa wakiitaka Rwanda ieleke huko. Wahisani hao wakaja na msamiati mwingine, ‘Good Governance,’ msamiati huu ulitilia mkazo kwenye ‘democratization’ ambayo ilipandikiza mfumo wa vyama vingi kwa gharama za nchi wahisani!

UCHUMI BAADA YA UHURU

Zao kuu la biashara ni kahawa, ambapo Rwanda ilivuna 80% ya pato lake la kigeni huko. Kama zilivyo nchi nyingine za Afrika, mazao yake ya biashara ni yale ambayo mkoloni aliyateua, na yaliendelea kulimwa baada ya yeye kuondoka, na yaliendelea kuuzwa kwa wanunuzi walewale, ambao walinunua kwa bei waliyo taka wao kama ilivyo kuwa katika ukoloni.

Uchumi uliachwa kwenye bidhaa moja tu, Kahawa, bei ya bidhaa hiyo ilipo anguka kwenye soko la dunia, uchumi wa Rwanda ulibaki matatani, lakini zaidi hata hicho kidogo kilicho kusanywa kilirudishwa kwa nchi wahisani kulipa madeni yao.

IMF mmoja kati ya wale walio iletea nchi hiyo matatizo, akaja na ‘suluhisho,’ la tatizo walilosababisha. Kwenye ‘suluhisho’ jipya 50% ya sarafu ya Rwanda ilishushwa thamani yake Novemba 1990, wiki sita tu baada ya jeshi la waasi wa Rwanda kutoka Uganda kuivamia Uganda, jeshi hilo ni  Rwandan Patriotic Front (RPF) chini ya Paul Kagame.

Kushushwa kwa thamani sarafu ya Rwanda, IMF walisema kungewezesha usafirishaji wa Kahawa kwa wingi nje na hivyo kuingizia Rwanda pato kubwa zaidi, na kuondoa vita. Lakini kinyume chake ndicho kilicho tokea, vita vya wenyewe kwa wenyewe vikapamba moto, kipato cha wananchi mmojammoja kikapungua kutokana na kuanguka kwa thamani ya sarafu. Lakini wiki chache tu baada ya sarafu hiyo kushushwa thamani, bei ya mafuta na bidhaa nyingine muhimu ikapanda juu. Deni la nchi hiyo ambapo mwaka 1985 lilikua kwa mara mbili zaidi, na baada ya sarafu kushushwa thamani yake, DENI HILO  likaongezeka kwa 34% kati ya mwaka 1989 na 1992.



 Serikali haikuwa na pesa za kuendesha mambo yake, shughuli za kijamii ziliporomoka. Wananchi wenye hasira wakaanza kuing’oa miche ya mikahawa, takribani miti 300,000 ya kahawa  iling’olewa. Wananchi hawakuwa tayari kurudi kulima chakula.

IMF hawakuridhika, mwaka 1992 wakatoa amri tena kwamba sarafu hiyo ya Rwanda lazima ishushwe tena thamani kwa mara nyingine. Hili likaongeza gharama kwenye bidhaa muhimu na mafuta. Pesa iliota mbawa kwenye mifuko ya Wanyarwanda.

Septemba 1990, wakati nchi ipo kwenye hali mbaya na inaelekea kwenye machafuko, yaani wiki chache tu kabla ya uvamizi wa waasi kutoka Uganda, kulikuwa na kikao kizito ndani ya Washington DC, kati ya IMF na waziri wa mambo ya uchumi wa Rwanda, ambapo IMF walishabariki kutoa kiasi kikubwa cha fedha kwenda Rwanda.


Oktoba mosi, wakati mamilioni hayo ya dola yanaingizwa kwenye benki kuu ya Rwanda, ni siku hiyohiyo waasi kutoka Uganda wanavuka boda kuingia Rwanda na kuanza machafuko. Ni kama waasi waliambiwa subirini kwanza fedha ziingie ... Fedha hizo za ‘msaada’ kutoka kwa nchi wahisani zilitolewa kwa madhumuni ya ‘kuingiza bidhaa kutoka nje,’ bidhaa za kijamii ilikupunguza makali ya kiuchumi. Hata hivyo kiasi kikubwa cha mkopo huu wa harakaharaka, kilitumiwa na serikali kwa mahitaji tofauti na yale yaliyo lengwa. 



Zilitumika kununulia zana na vifaa vya kijeshi kutoka South Africa, Egypt, na Ulaya Mashariki. Kuanzi Oktoba mosi jeshi la Rwanda lilipanuka ghafla kutoka askari 5000 mpaka askari 40,0000, vijana wasiokuwa na ajira kutokana na kuanguka kwa uchumi ndiyo walioandaliwa na hatimaye kuingizwa jeshini.

 Wakati nchi ikiwa imechanika chanika kutokana na hali mbaya ya uchumi, kiasi cha dola za Marekani Milioni 260, zilimwaga kwenye benki kuu, kutoka nchi wahisani ambao ni Ufaransa, Ujerumani, Ubelgiji, European Community, na Marekani. Fedha hizi hazikwenda kurekebisha hali ya uchumi iliyo kuwepo, bali kusaidia kulipa deni la Rwanda lililo tangulia pamoja na kununua zana za kivita. Hivyo ndivyo nchi wahisani walivyo taka pesa zao zitumike.
Pia ikumbukwe kwamba IMF kupitia kwa mshirika wake Interanational Development Association (IDA) ilitoa amri kwa serikali ya Rwanda kubinafsisha shirika la umeme na maji, Electrogaz. Sababu ya kubinafsishwa ni ili liweze kutumika kulipia deni la nchi hiyo. Haikuwa ajabu baada ya shirika hili kubinafsishwa bei ya umeme ilipandishwa maradufu, wananchi walizidi kukamuliwa ili deni liweze kulipika.


Septemba 1993, mwaka mmoja kabla ya mauaji ya kimbari shirika la mawasiliano na simu nalo likabinafsishwa, mwongozo mwingine kutoka IMF na WB.

Kama nchi wahisani wakishirikiana na WB na IMF, ni WABAKAJI, na nchi ya Rwanda ni MWANAMKE anayetaka kubakwa, basi mpaka hapo MWANAMKE HUYO ALIKUWA KISHA VULIWA NGUO ZOTE NA WABAKAJI WALIKUWA WAMESHAPANGA MSTARI KUIANZA DHAMBI YAO ....






TUKUTANE TENA HAPO, KUTIZAMA NAMNA DHAMBI HIYO ILIVYO TENDEKA ...

1 comment: