Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Friday, October 4, 2013

SIRI YA PESA NA ILLUMINANTI



“Kama kutakuwa na makundi mawili, badala ya kuwa benki na jamii, iwe mwana jamii mmoja na mwingine, wasingeweza kuendesha mfumo wa ukopeshaji kwa kanuni nyepesi tu, kwamba, mkopeshaji hawezi kukopesha kile asicho kuwa nacho, kama sinavyo fanya benki. Ni benki za biashara tu na taasisi zingine za fedha ndizo zinazo weza kukopesha pesa hewa wanazo zatengeneza kwa kukopesha.”
Profesa Irving Fisher, mwanauchumi kwenye kitabu chake 100% Money

“Nipe nguvu ya kutawala sarafu ya nchi na sitajali ni nani anaye tunga  sheria”
Amschel Rothschild


“Somo linalo husiana na mambo ya fedha, kwenye nyanja zote za masomo ya uchumi, ndilo somo ambalo ugumu utatiwa au kutumiwa kwa makusudi ili kuficha au kupoteza ukweli (kuhusiana na suala zima la fedha)”
 John Kenneth Galbraith, Mwanauchumi na Mwandishi.

“Suala ambalo limefanyiza ubaya kwa karne, na ambalo itabidi lipiganiwe ili liondolewe, punde tu au baadaye kidogo, ni wananchi dhidi ya taasisi za fedha (benki)”
Lord Acton (1834-1902, Mwanahistoria wa England

Pesa inatoka wapi?
Hili linaweza kuwa swali la mwaka.
Na hakuna wa kulijibu, siyo mwanauchumi wala mfanyabiashara, wala huwezi kulipata jibu lake kwenye machapisho na majarida ya kiuchumi, wala siyo la kiserikali, wala kwenye vipindi maalum vya kiuchumi kwenye luninga yako, mbadala wa wapi lipo jibu la swali hilo lazima upatikane, na ashakum siyo matusi.

Katika moja ya vitu ambavyo vimetawala au kuendesha maisha yetu ya kila siku ni; Pesa. 

Pesa ni nini, au inatoka wapi, ni swali jepesi, lenye majibu mepesi ambayo kwa namna moja ama nyingine, huwa hakuna anayejitolea kuyajibu, ni kama vile pesa yenyewe kupitia utaratibu wa kuitumia au inavyo tumika inatoa jibu la maswali hayo, inajijibu yenyewe, tunaona kwenye luninga, kwenye matangazo ya biashara, kwenye vitabu vikubwa vilivyo vunja rekodi za mauzo na filamu, maswali haya huwa yanajijibu yenyewe huko. Kutokana na majibu hayo ni kuwa, watu wengi unaondoka na majibu ya kuamini kuwa pesa zinatengenezwa na serikali.


 Kwamba serikali ndiyo inayo printi noti za fedha na sarafu zake. Kwamba serikali ndiyo inayo printi sarafu na noti ni kweli kabisa, ila huo siyo ukweli wote.

Ukweli wote ni upi?

Benki, huo ndiyo ukweli wote.

Tuashumu kuwa benki inakopesha fedha ilizo pewa kama amana na wateja wake, ingawa huo siyo ukweli, tunaashumu tu. Unapo kwenda benki kuchukua mkopo, benki inakupa mkopo huo baada ya kusaini mkataba ambao utakutaka wewe kulipa fedha hizo na riba juu. 

Dhamana ya ahadi hiyo, ambayo ni maarufu kama, ‘dhamana ya mkopo’ huwa ni mali zisizo hamishika au zinazo hamishika ambazo zinamilikiwa kihalali na mkopaji au na mdhamini wa mkopaji. Kisha kama wanavyo fanya wana mazingaombwe, benki wanageuza mkataba huo baina yao na mkopaji kuwa ndiyo fedha anazo pewa mkopaji. Ndiyo kama mazingaombwe vile, huwezi kuja kwangu, tukaandikishana mkataba wa kukopeshana, nami nikaugeuza mkataba huo kuwa ni fedha unazo taka, ila benki inafanya maajabu hayo kila siku, ila macho yetu hayaoni. 

Huwezi kuamini, ila huu ndiyo ukweli kuhusu namna benki zinavyo fanya kazi.
Vitu hueleweka zaidi kwa mifano, ngoja ni kupe kahadithi kidogo kama mfano wa namna ambavyo benki wanavyo fanya hayo mazingaombwe.


Hapo zamani za kale, kila kitu kilitumika kama fedha, ili mradi kiwe kinabebeka na watu wawe na imani kuwa kinaweza kubadilishwa na kingine chenye thamani kama yake. Hivyo mazao, mifugo, na bidhaa nyinginezo zilitumika kama pesa. Vitu vya thamani kama vile dhahabu na fedha vilivutia zaidi kwenye hili, navyo vilitumika katika biashara hii, iliitwa Barter Trade.


Mtu mmoja ambaye hapa tutamuita Sonara, kutokana na kazi yake ya kuyeyusha hivi vito vya thamani na kuviweka katika maumbo mbalimbali, yeye alikuja na wazo, kutokana na kwamba biashara yetu ya kubadilishana vitu inakumbana na kikwazo cha ‘thamani’ na inakuwa ni vigumu wakati mwingine haki kufanyika katika aina hii ya biashara ni vigumu kwa sababu hakuna kipimo maalum cha ‘thamani’ kwa bidhaa zote, Sonara akapendekeza jamii imruhusu atumie kipaji chake atengeneze sarafu za fedha na dhahabu ambazo zitatumika kama kipimo cha thamani kwa bidhaa mbalimbali.

 Bidhaa ambazo upatikanaji wake ulihitaji nguvu na shughuli nzito basi thamani ya bidhaa hiyo itakuwa kubwa kuliko ile ambayo uzalishaji wake haukuhitaji nguvu na akili nyingi. Sonara akapewa mikoba na kuanza kutengeneza sarafu za fedha na dhahabu.
Sonara akatengeneza chumba maalum chenye mlango mkubwa na mzito, na huko akazimimina sarafu zake za fedha na dhahabu na akaweka walinzi juu kuhakikisha hakuna anaye cheza na ‘mayai’ yake. Watu nao wakalipenda wazo la Sonara, wakaleta fedha na dhahabu zao kwa wingi zihifadhiwe na Sonara, naye akiwachaji malipo kidogo kwa huduma hiyo.

Sonara akapata wasiwasi, endapo watu wote watakuja kuchukua dhahabu na fedha zao, yeye atabaki na kitu gani?
Sonara akatengeneza risiti, kwa wale wanao leta dhahabu na fedha kwake, risiti hizo zilibeba thamani ya dhahabu au fedha zilizo hifadhiwa na muhusika. Risiti hizo zikawa zinaweza kutumika mbadala wa fedha na dhahabu, yaani ukiwa na risiti hizo ni sawa na kumiliki kiasi cha dhahabu au fedha kilicho andikwa kwenye risiti hizo. Na kama ukipenda unaweza ukarudi kwa Sonara na risiti hizo na Sonara akakupa dhahabu au fedha halisi, hii itategemea na thamani iliyo andikwa kwenye risiti hiyo.


Nyuma ya mapazia Sonara alikuwa akifanya biashara nyingine, alizikopesha fedha na dhahabu zake kwa wafanyabiashara mbalimbali, lakini kwa riba. Lakini Sonara hili nalo lilimpa wazo kubwa zaidi, kwa sababu ni watu wachache tu ndiyo waliyo amua kuzichukua dhahabu na fedha halisi, akaona ni bora kwa kila dhahabu moja na fedha anayo miliki kuiandikia risiti, na kwamba badala ya kukopesha fedha halisi na dhahabu atakopesha risiti hizo. Ilimradi risiti hizo zitalipwa baadaye kama dhahabu halisi au fedha halisi kama riba, Sonara ataendelea kufurahia ugunduzi wake huo.

Lakini mara maneno yakaanza, ikasemekana Sonara anakopesha fedha ambazo siyo zake kwa riba, fedha alizo pewa kama amana, Sonara hakuwa na shida, kwa vile alicho kikopesha siyo dhahabu wala fedha halisi, bali ni risiti zenye thamani ya kile anacho kimiliki jumlisha kile alicho pewa kama amana, akaenda kuwaonesha lango lake, akalifungua na wananchi walipo tizama ndani waliona dhahabu na fedha zao zipo salama, watu wakamuacha Sonara akaendelea na biashara yake.

Lakini wananchi wakarudi tena, wakamuambia Sonara, kwa vile yeye anatumia dhahabu na fedha zao kuwakopesha watu kwa riba, na wao walio weka dhahabu na fedha halisi wakahitaji wawe na mgawo kwenye faida hiyo ya Sonara, wapewe kiasi fulani cha faida kama riba, na hapo kitu kipya kikazaliwa, mfumo wa benki.
Hitajio la mkopo likazidi kuwa kubwa kutokana na upanukaji wa biashara kwenye miji mbalimbali, naye Sonara wetu hawezi kukopesha zaidi ya kile alicho nacho, risiti alizo zitaoa zimebeba thamani ya kile ambacho kilichopo kwenye volti yake. Lakini akapata wazo zaidi, wazo zuri zaidi; kwa vile hakuna yoyote isipokuwa yeye anayefahamu ni kiasi gani hasa cha dhahabu na fedha halisi kilichomo kwenye volti yake, anaweza kuprinti risiti nyingi zaidi kadiri awezavyo na kuzikopesha kwa wafanya biashara, na kuzipa risiti hizo thamani yeyote ile na hakuna atakaye shuku, kwa vile hakuna atakaye rudi muda huo, huo kwa Sonara na kuhitaji dhahabu au fedha halisi ni nani atakaye fahamu kuwa Sonara anakopesha risiti hewa? Hakuna, ila yeye tu mwenyewe Sonara, Bingo!


Sonara akawa tajiri, naye akawamegea siri hiyo Sonara wenzake wa nchi zingine, duara lao likawa kubwa na lenye nguvu na wakaja na taasisi waliyo ita benki, wakaendelea kukusanya utajiri mkubwa kwa riba inayo patikana kwenye mikopo ya risiti hewa. 

Lakini mambo yakaanza tena, wananchi wakataka dhahabu na fedha halisi, kwa vile zile zilikuwa ni risiti hewa, masonara hawakuwa na chochote cha kuwapa; sasa tutafanyaje? Kimbia, kimbia, kimbia, kimbiaaaaaaa kadiri utakavyo weza, ndivyo walivyo fanya masonara, mlango wa nyuma wakachukua dhahabu na fedha zilizobakia zikiwemo zile walizo pewa kama amana na kutokomea. 

Mara nyingi wanapo fanya hivyo huwa hatusemi kuwa wamekimbia na fedha zetu au dhahabu zetu au mali zetu, bali wanauchumi wetu wamekipatia kitendo hicho jina maalum, wanaita anguko la kiuchumi.

Utajiri halisi ukabaki kwenye makaratasi, vurugu zilifuata kama kawaida, serikali ikaingilia kati, mfumo wa Sonara ukapitiwa, serikali ikaweka vifungu vyake na kisha ikaubariki mfumo huo. Benki zikapewa kipimo cha mwisho cha kukopesha kutokana na fedha inazo kuwa nazo, kipimo hicho kinaitwa Friction Reserve. Lakini bado kiwango hicho ni kikubwa ukilinganisha na kiwango cha fedha ambazo benki inazo kwenye vitabu vyake. 

Au kama ilivyo kuwa awali kiwango hicho ni kikubwa kushinda dhahabu na fedha halisi iliyo kuwa kwenye milki ya benki.

Benki za kitaifa zikapatikana, ambazo kazi yake ni kusimamia taratibu za kibenki kwa vijibenki vingine ambavyo siyo ‘Central Bank’ taratibu ambazo ziliwaruhusu vijibenki vidogo dogo kukopesha zaidi ya kile walicho nacho, vijibenki hivyo vilitakiwa kuwa na kiwango maalum au uwiano baina ya kile walicho nacho na kile wanacho kikopesha, Loan to deposit Ration.
Mfumo wa benki ukabadilika, suala la fedha na dhahabu kama kipimo cha thamani ya bidhaa na huduma kikatoweka, na nafasi yake ikachukuliwa na jinamizi jingine kubwa, Deni

Mathalani kama unaweza kuzipata fedha za zamani kidogo karne mbili, tatu nyuma, utaona thamani yake ilikuwa ni sawa na kiasi fulani cha dhahabu na au fedha halisi. Lakini sasa hivi thamani ya sarafu au noti ni sawa na sarafu au noti nyingine, yaani bati kwa bati au karatasi kwa karatasi. Katika kipindi hicho benki binafsi ziliweza kutengeneza risiti badala ya fedha na dhahabu halisi, lakini watu walikuwa na uhuru wa kuzikubali au kuzikataa, kama ilivyo leo ambavyo mtu yupo huru kuikubali au kuikataa hundi anayo pewa na mtu mwingine.. Lakini leo mabenki yaliyo pewa leseni na serikali yanaweza kuzitoa sarafu na noti ambazo zimetiwa baraka na serikali na benki kuu kama fedha halali kwa kiasi fulani cha malipo.

Ni kiasi gani cha fedha ambacho serikali na benki kuu wanacho weza kukitengeneza na kukipa thamani na kukiweka katika mzunguko?

Ni vipi aina hii ya mfumo ulivyo mzigo kwa umma?

Ni vipi mfumo huu unavyo wanufaisha wachache, hususan Illuminnati?

Je unamjua Sonara katika hadithi hii?

Uchumi wa nchi unaweza kutengemaa kwa kutegemea aina hii ya mfumo?

Hey, njoo hapa tena wakati ujao kwa majibu ya maswali hayo na mengine mengi.

No comments:

Post a Comment