Baada
ya raisi Kennedy kuuwawa mwaka 1969, Scottish Rite Freemasonry, walisimamisha
mnara, ‘obelisk’ Dealey Plaza na juu yake wakaweka ‘moto wa kimasonia’ (mwenge).
Lakini kama hilo halitoshi kwenye kaburi lake wamewasha moto ambao unawaka
mpaka hivi leo, ‘eternal flame’.
Juu ya
Pont de L’Alma, mahala ambapo Malkia Diana aliuwawa baada ya gari yake
kugongezwa kwenye nguzo ya 13, Illuminanti wamesimamisha hapo ‘moto wa dhahabu
wa kimasonia’, (mwenge). Mwenge huo umesimamishwa juu ya nyota yenye ncha tano.
Kwenye
kaburi lake Diana nako wameweka mwenge. Kwenye eneo ambalo ilikuwepo minara
miwili ya WTC, mara baada ya minara ile kwenda chini nako waliweka mfano wa
mwenge kama walivyoweka kwenye kaburi la Diana.
Kwenye
New York Harbor utaona sanamu la Statue of Liberty, ambalo nalo limesimama na
limeshikilia ‘mwenge’ au moto wa kimasonia.
Dhana
ya kutumia ‘mwenge’ kwa freemason, ni kuwa mwanga unatoa nuru, yaani wao
wanaitikadi juu ya nuru hiyo kuwa na elimu iliyo porwa kutoka kwa waungu na
kupewa binadamu wachache kutoka kwenye kiazi maalum.
Alama
nyingine zinazotumiwa na Freemason ni Moto ambao kwa wao ina maana ya elimu
mara nyingi sanamu la Libert lililoko New York linawakilisha alama hiyo,
walipomua Kennedy na Malkia Diana wakaweka alama hiyo kwenye makaburi yao.
“Lucifer, anaye beba nuru! Inashangaza na
ni ajabu jina hili kupewa Roho ya Kiza! Lucifer, nyota ya alfajiri! Ni yeye
ndiye abebaye nuru, na kwa miali yake mikali yenye kupenya, na kutia upofu
macho ...”
Mwanamasonia katika hatua yake ya mwanzo,
katika daraja la kwanza, anahimizwa ;kuitafuta nuru!’ Mason wa kawaida ambaye
yupo kwenye daraja la blue au aliye juu ya hapo lakini ni visible freemason,
daima huwa anaitafuta nuru, na atatumia uhai wake kama mmasonia kuitafuta au
kuifuata nuru.
Wale ambao hawafahamu watadhani nuru ni mafundisho matakatifu ya
MUNGU MMOJA, lakini tumemsikia invisible freemason, na mwanamasonia anaye
abudiwa katika zama zote Albert Pike, akisema kuwa nuru ni Lucifer. Lakini pia
Pike anasema mwanamasonia wa daraja la 18, anafundishwa kuwa Mungu ndiye mwenye
kubeba nuru, lakini haambiwi kuwa Mungu ni nani mpaka atakapo fika kwenye
daraja la 19, ndipo anapo ambiwa kuwa Lucifer ndiye anaye beba nuru.
Hivyo moto kama alama ambayo freemason huitumia na kuiweka katika maeneo na sehemu mbalimbali, na pia kuifanya kama nembo kwenye mashirika na makapuni pamoja na taasisi binfsi na zile za kiserikali, huwakilisha 'ELIMU MAALUM KWA WATU MAALUM, ELIMU AU MAARIFA AMBAYO MBEBA NURU ALIWALETEA KIZAZI TEULE KUTOKA KWA WAUNGU, MBEBA NURU HUYO SI MWINGINE BALI NI LUCIFER MWENYEWE.
No comments:
Post a Comment