Haki za
wanawake, za watoto na zile za mashoga ni moja ya mfano mzuri wa namna ambayo
Illuminanti wanatumia kuishika jamii yetu.
Kwa
miaka michache hivyo, tkribani miaka 40 tangu kampeni hizi zilipoanza, wanawake
wengi wamepoteza njia yao ya asili na lengo lao mahususi na muhimu katika
jamii. Matokeo yake ni kwa familia kusambaratika, ngono holela kuongezeka, kuwa
na idadi kubwa ya watoto wa zinaa na idadi ya watu kiujumla kupungua.
Kwa
mwanamke yeyote mapenzi, huruma na kujitoa ni moja ya sifa za kipekee na adhimu
katika maumbile ya mwanamke. Anajitoa kwa mume wake na watoto wako kwa mapenzi
makuu na huruma na hamu yake kubwa ni kuona mafanikio ya familia yake. Kazi
yake adhimu isiyo na mbadala ni kumleta duniani mwanafamilia, kumlea, kumkuza
na kumfundisha mengi ikiwemo upendo na huruma. Kazi hii haina mbadala, hakuna
anyeweza kuifanya kazi hii kwa ubora wake kumshinda mama mwenyewe, hakuna.
Haijalishi
Daycare imepambwa kwa namna gani, inatoa huduma bora kiasi gani, kwa gharama
gani, katu haiwezi kuvaa viatu vya mama. Wakati mama anamlea na kumkuza
mwanafamilia, daycare inalea na kumkuza mwanajamii.
Mwanafamilia
msingi wake mkuu ni MAPENZI mwanajamii msingi wake mkuu ni MASLAHI. Wakati
mwanafamilia anaandaliwa kujitoa na kutumikia wengine kwa kutanguliza UTU,
Mwanajamii anafanya hivyo kwa kutanguliza MASLAHI.
Mwanafamilia
hawezi kumpeleka Mama yake mahakamani lakini mwanajamii anaweza kufanya hivyo.
Anakuambia “What is it for me”
Hivyo
mwanamke kama nguzo muhimu kwenye familia, anapofanya hayo yote, kwa upande
mwingine, mwanamume naye silka yake inamuongoza moja kwa moja katika kumsaidia
huyu mwanamke kwa kumuhakikishia ulinzi, ulinzi wa kiuchumi, ulinzi wa
kimaamuzi na ulinzi wa kimazingira. Hapo ndipo tunapo pata maana halisi ya
ndoa, ambapo sasa muhiri wa muungano huo ni tendo takatifu la ndoa linalo
waunganisha wawili hawa na kila mmoja na majukumu yake na sehemu yake katika
ndoa hiyo kuelekea kwenye kusimamisha serikali yao ndogo ya familia, yenye
kiongozi ambaye ni baba na msaidizi ambaye ni mama, na watumishi ambao ni
watoto, na anaye hudumiwa hapa kwenye serikali hii si mwingine, si chochote,
bali ni malengo makuu ya kuletwa hapa duniani, MUNGU MMOJA, KUMUABUDU YEYE PAKE
YAKE BILA KUMSHIRIKISHA NA YEYOTE.
Haki za
wanawake zimewapika na zinaendelea kuwapika wanawake kulikataa jukumu hilo
makhususi kwao, halikadhalika, haki za mashoga zikiwapika wanaume kulikimbia
jukumu lao na haki za watoto zikimuandaa mtoto kuwa mwanajamii badala ya
mwanafamilia. Harakati zote hizo zinaonekana kusimamia mambo ya msingi kwenye
makundi hayo, lakini kinyume chake ndiyo
sahihi, na kundi la mashoga likiwa ni sumu mbaya sana kwenye familia.
Mwandishi
mmoja wa Uingereza alipata kuwarekodi wanawake wawili wakisema hivi,
“Wanaume
wote siku hizi ni bure kabisa,” alisema mmoja. “Ndiyoo,” akasema mwingine.
“Shida ni kuwa hawajalelewa kupambana na changamoto za wanawake. Hawafahamu
kuwa tunawahitaji wao kuonesha uanaume wao zaidi, lakini badala yake wamekimbia
majukumu yao.”
Wanaume
hawapo hapa kupambana au kushindana na wanawake, halikadhalika wanawake
hivyohivyo, bali kusaidiana katika jukumu muhimu la kujenga familia. Ikiwa
mwanamke analelewa kupambana au kushindana na mwanaume, kama wanavyo dai
kinadada hao, na hayo ni maoni utakayo yapata kwenye majarida ya wanawake kama
vile Jarida la TRUE LOVE, COSMOPOLITIAN na mengine mengi, matokeo yake ni kuwa
mwanaume ataikimbia ndoa, sababu kwa nini mwanamume alale kitanda kimoja na mtu
ambaye anayo mtizamo wa kumfanya yeye mwanamume awe kama yeye, yaani awe na
mtizamo wa kike? Lazima ndoa itakuwa ngumu sababu badala ya kusaidiana,
tunashindana.
Sababu
thamani ya ndoa kwenye jamii imeondolewa na harakati za kinamama, wanawake sasa
hawana cha kubadilishana kwa MAPENZI zaidi ya NGONO. Utakubaliana na mimi kuwa
pamoja na yote mwanamke wa leo kafanywa ni chombo cha starehe, mwanamume
hamtizami mwanamke kama mshirika wake, bali adui yake ambaye inabidi amtege,
amlaghai, amdanganye, ili afanye naye NGONO na kisha kumuacha kwenye mataa, NOW
RELATIONSHIP ITS A GAME, AND EVERYDAY PEOPLE A CHANGE COACHER LIKE A FOOTBAL
TEAM.
Mtayarishaji
wa filamu anayekwenda kwa jina la Aaron Russo, anathibitisha haya ninayo
yasema,
Wakati
maadui zetu walipokuwa wakimuandaa Russo iliwamuingize kwenye asasi ya siri
inayo kwenda kwa jina la CFR, Nicholas Rockefeller alimuambia Russo kwamba,
Rockefeller Foundation imetengeneza ‘HARAKATI ZA WANAWAKE’ kwa kutumia vyombo
vya habari kama mpango wa muda mrefu wa kuutawala umma. Nenda ka Google,
“Rockefeller Foundation” + “Women Studies” na utapata majibu yako.
Haki za
akina mama zinafanya kazi ileile, kuivunja familia, kupunguza idadi ya watu,
kumtoa mwanaume kwenye nafasi yake.
Mtazamo
wa watu lazima ubadilishwe kutengeneza kile ambacho freemason na Illuminanti
wanacho kihitaji. Rockefeller ni familia na ni moja wawachezaji hodari na
mahiri kwenye New World Order, Rockefeller wanashikilia vyombo vingi vya habari
vyenye kuaminika kwa jamii. Kwa kutumia nguvu hiyo ya vyombo vya habari
wanaurubuni umma ili waweze kuutawala. Moja ya matukio ya kutengeneza wanayo
tumia kuurubuni umma ni vita dhidi ya ugaidi na tukio la 9/11.
Rockefeller
alimuambia Russo kuhusiana na mpango kamambe wa 9/11 mwaka mmoja kabla ya tukio
lenyewe kutokea.
Illuminanti
wanacho hitaji ni dhana au falsafa itakayo wapa kibali cha kuwatia walimwengu
wote kwenye minyororo yao. Hivi sasa kila nchi duniani imeingia kwenye
minyororo ya madeni kutoka kwenye mabenki ambayo yapo kwenye mikono yao, karibu
kila mmoja wetu sasa analo deni katika benki fulani, kila kampuni au shirika,
lipo kwenye mfuko wa suruali za wanao miliki mabenki.
Maadui
wetu hawana dhana nyingine waliyo ona inayofaa ispokuwa dhana ya ushetani,
wanautawala ulimwengu kwa kushirikiana na asasi zingine za kishetani kama vile,
freemasonry, Ukomunisti, Demokrasia kutaja kwa uchache sana.
Utamaduni
wa kimagharibi umeegemea kwenye dhana ya Ushetani, freemason inafundisha kuwa
ni mtu na siyo mungu mwenye sauti juu ya dunia hii. Wanapindua dhana ya kiroho
na imani ilikusimamisha dhana yao ya ushetani. Kupitia vyombo vyao vya habari,
wanaharakati wao na propaganda, suala la kishetani la ushoga linafanywa kuwa ni
suala la kijamii, la kiserikali, nchi lazima zikubali kuwatambua watu hawa.
Kwa
ajili ya kuivunja serikali ya familia, Illuminanti na vyombo vyao vya habari
vinawaambia kina mama lazima wasimame wenyewe wajitegee na wasimtegemee
mwanaume, yaani wasitegemee mkataba wa ndoa kuwaokoa, ndoa haina maana,
mahusiano baina ya mwanaume na mwanamke kama wanandoa ni suala la kupotezana muda.
Wanaharakati
wa haki hizi za wanawake kwa kutumia vyombo vya habari, hichi ndicho wanacho
waambia Mama, na Dada zetu kama njia ya ‘kuwapatia uhuru’ wao ambao kwa karne
kadhaa umekuwa ukishikiliwa na wanaume visivyo halali.
i.
Wanaume
hawaaminiki, wanaume ni mwaumbwa, walaghai, wezi, wanyonyaji, wakati mwanamke
ndiye anaye fanya yote kwa mwanaume kuitwa mwanaume.
ii.
Wanawake ni
wahanga wa jinsia zao, lazima waamke sasa wapambane na wachukue kilicho chao.
iii. Wanawake lazima wawe ni wabinafsi sasa, muda waliokuwa wanautoa
kwa waume zao, watoto hakuna tena muda huo, bora kutumia muda huo na ‘girl
friend’ wako (lesbian au ushoga kwa wanawake) lakini bila kuwa na mume au
mtoto.
iv. Ngono si kwa ajili ya ndoa na mapenzi. Majarida kama Glamour na
Cosmopolitan yanawaambia dada zetu wanapo toka ‘out’ na wanaume wawe wazi
kuhusu ngono, na wawaoneshe umahiri wao kitandani hata kama ndiyo siku ya
kwanza wamekutana. Hakuna kuzungumzia ambao ya ndoa au familia.
v.
Mafanikio ya
kweli yapo kwenye kupata kazi nzuri na siyo kwenye kuolewa na kuwa na familia.
Kwa aina hizi za kampeni na harakati, hivi sasa wanawake wengi
wapo njia panda baina ya kufuata silka yao na kufuata propaganda za
wanaharakati wa haki za kinamama.
Wakati balaa hilo likiwakumba dada zetu na mama zetu, Majarida
kama PlayBoy, mitandao ya porn na wenzake wanatengeneza ujumbe kama huohuo kwa ajili
ya kina baba na kina kaka, kwamba huhitaji kuowa ili uweze kupata ngono, Ndoa
na watoto ni pasua kichwa ... kwa kuna Girl Next Door changamka. Nakumbuka
kwenye miaka ya 90 wakati nipo darasa la 4 kama siyo la 5, walitufundisha jinsi
ya kuvalisha kondomu kwenye uume, sijui leo hii watoto wetu wanafundishwa nini
huko mashuleni ...
Vyombo
vya habari na harakati za haki za wanawake zimemgeuza mwanamke kuwa chombo cha
jamii na kiburudisho cha ngono kwa yeyote anaye taka kwa bei inayofaa.
Freemason wa daraja la chini huwa hawalioni hili kwa vile wao wanastahiki
kudanganywa, lakini kuanzia daraja la 28 na kuendelea wanafahamu malengo ya
harakati hizo dhidi ya umma, wamiliki wa vyombo vya habari pia wanalifahamu
hilo vizuri sana, kwamba malengo yao ni kuharibu na siyo kujenga.
THIS IS THE WAR, AND STILL YOU AND YOUR FAMILY ARE NUMBER ONE TARGET.
No comments:
Post a Comment