TUENDELEE NA SEHEMU YA TATU ....
Katika
daraja la pili, maarufu kama FELLOW CRAFT DEGREE
(Second Degree in the Blue Lodge)
DUEGARD OF THE FELLOW
CRAFT
Mwanachama wa
kimasinia anapo ingizwa au kupandishwa katika daraja hili, hufanya au husimama
katika hali ambayo tunaiyona hapo juu katika picha.
“Mkono wangu
wa kulia upo kwenye biblia takatifu, bikari na kompasi, mkono wangu wa kushoto
unatengeneza engo
Alama inayo fanyizwa kama kiapo, mfuasi
anapo ingia daraja la pili la umasonia. Alama hiyo hufanyizwa kwa kuupitisha mkono
wa kulia juu ya kifua, upande wa titi la kushoto,mkono huo unapitishwa haraka
na kishwa muhusika hurejesha mkono wake kama askari aliyesimama sawa kwenye
gwaride.
Maana ya lama hiyo ni nini basi?
“Kifua changu kipasuliwe, upande wa
kushoto, moyo wangu uchomolewe, na upewe kwa wanyama na ndege wa porini”
Hii ni kama mwanachama atakwenda kinyume na miiko ya
kuingia kwenye daraja hilo.
Katika daraja hilo ipo namna ya kusalimiana na
kushikana mikono iliyo tofauti kidogo na ile ya daraja lililo tangulia. Hii
inaitwa SHIBBOLETH
Kwa haraka kuitizama alama hii ya kushikana mkono
utaona haina tofauti sana na ile ya BOAZ, LAKINI HAPA WANACHAMA HUSHIKANA MKONO
KAMA KAWAIDA WANAVYO SHIKANA WATU
WENGINE, KISHA KILA MMOJA HUWEKA DOLE GUMBA LAKE BAINA YA NAFASI ILIYOPO KWENYE
NAKOZI MBILI, NAKOZI YA KIDOLE CHA SHAHADA NA NAKOZI YA KIDOLE KINACHOFUATA.
Kisha baada ya hapo mwanachama huoneshwa aina hiyo ya mshiko na WM, kama alivyo oneshwa katika hatua ya awali kwenye BOAZ, na jina la mshiko huo hutamkwa kwa namna kama ile iliyo tumika kutamka BOAZ, ispokuwa hapa jina hugawanywa mara tatu, yaani
SD: Shib
WM: bo
SD: leth
WM: bo
SD: leth
Mwanachama ataambiwa kuwa hivyo ndivyo anavyo paswa kulitamka jina la mshiko huo endapo itampasa kulitamka, lazima ligawanywe mara tatu.
SHIBBOLETH IKIFANYIWA KAZI NA VIONGOZI WETU
... ITAENDELEA ...
No comments:
Post a Comment