WAPENDWA MTANANGE WETU BADO UNAENDELEA, MTANIWIA RADHI NINAPOSHINDWA KUPOST KWA WAKATI, HII NI KUTOKANA NA MAJUKUMU MENGINE YANAYO NI BANA, LAKINI TWENDE PAMOJA...... TUNAENDELEA TULIPOISHIA JANA ...
Leo hii,
N.M Rothschild & Sons ni benki ya kuu ya uwekezaji ambayo ipo nje ya
London. Ni moja kati ya 10 bora benki za uwezeshaji duniani. Mwaka 2007 benki
hii iliweza kutengeneza faida ya kiasi cha dola bilioni 566. Hicho ni kile
kinacho fahamika kama ‘taarifa rasmi’ lakini wanazo benki duniani kote, ambazo
zinawawezesha kuwa na maamuzi ya kiuchumi kote duniani.
Rockefellers
wanamiizizi mirefu ndani ya Marekani, walianza kwenye karne ya 19, kwa msaada wa
fedha toka kwa JP Morgan ambaye naye aliukwaa utajiri huo kupitia kwa ushawishi
wa Rothschild. John D. Rockefeller alipewa fedha hizo kwa ajili ya kazi ya
kusimamia na kuendeleza malighafi zihusianazo na mafuta.
Rockefeller
fedha zao nyingi zinafichwa kwenye taasisi mbalimbali za kijamii walizo anzisha
na ambazo zina majina na maaudhui ya kusaidia jamii, kama vile The Rockeffeller
Foundation.
Mwaka 1913
The Rockefeller Foundation ikawa moja wa wadhamini wakubwa kwenye tafiti za
utabibu. Iliwachagua wanasayansi na madaktari ambao walionekana wanafaa kudhaminiwa
kwenye tafiti hizo. Msisitizo ulikuwa ni kwenye madawa namna gani madawa
yanafanya kazi mwilini na namna gani mwili unapata athari kutokana na madawa
hayo. Tafiti hizo zikarudishwa vyuoni, hasa vyuo vya udaktari na kuwapatia
madaktari matokeo ya tafiti hizo, yaani aina ya dawa zilizo patikana, nazo ziwe
kwa ajili ya kutibu watu, LAKINI KILA MWENYE AKILI HAAMBIWI TIZAMA, LEO NI DAWA
NDIYO ZINAZO UWA WATU. Mpaka leo tafiti hizo bado zinaendelea. Aina hii ya
hadithi tuipata katika kila Nyanja au sekta ambazo ‘aina hizi’ za mashirika
zimeweka fedha zao.
Kwenye
mambo ya kibenki Rockefeller nao ni wazima, walikuwa wanamiliki Chase Bank
tangu 1930, halafu wakaja wakaigawanya, Rockefeller akapatiwa Equitable Trust
Company ya New York pamoja na Chase National Bank. Kutoka mwaka 1970 mpaka 1980
Chase Manhattan ilisimamiwa na kuendeshwa na David Rockefeller.
“…Kuna
ambao wanaamini kwamba sisi (familia ya Rockefeller) ni sehemu ya mtandao wa
siri unao fanya kazi zake dhidi ya Marekani, kinyume cha matakwa ya Marekani,
wanaitangaza familia yangu na mimi mwenyewe kama ‘internationalists’ na wenye
njama tukishirikiana na wengine kote duniani kuunda aina ya mfumo wenye
maingiliano ya kisiasa na kiuchumi – dunia moja (serikali moja ya dunia). Kama
haya ndiyo mashtaka yangu, basi ni kweli ninakiri kuwa na hatia hiyo (nakubali
mashtaka), na nina jivunia kuwa na hatia hiyo.”(David Rockeffelee, Memoirs,
2002)
“Tunawashukuru
sana Washington Post, The New York Times, Time Magazine na wachapaji wengine
wakubwa wa habari ambao wakurugenzi wao wamehudhuria vikao vyetu na wakatimiza
ahadi zao za kutokuandika chochote kuhusiana na vikao hivyo kwa karibu miaka
arobaini. Ingelikuwa vigumu sana kwa sisi kuendeleza mpango wetu wa kuitawala
dunia kama tungekuwa tunamulikwa na kuandikwa na vyombo hivyo. Lakini sasa
dunia imeshaiva na iko tayari kuelekea kwenye New World Order…” (David
Rockeffeler, alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa asasi ya siri inayo kwenda
kwa jina la Bilderberg Group, mkutano huo ulifanyikia Baden, Ujerumani)
J.P Moragan
alikuwa kama wakala au ‘mpambe’ wa karibu wa Rothschild. Anayo historia nzuri
ya kutajirika kutokana na majanga, yaani wengine wanapo kuwa kwenye maangamizi
na maporomoko, eyey ndiye anapo tokea hapo, walisema waswahili, “Kufa kufaana..”,
hivi sasa familia hiyo imejiweka vizuri au imo ndani au ndiyo wamiliki wa Chase
Bank na CitiGroup. Bank hizi mbili zinatajwa vizuri kama ndiyo vinara wa anguko
la uchumi la mwaka 2008, na wao walifaaidika vizuri sababu raisi waliyo muweka
madarakani, Bush alikuja na ‘Bail Out’ ambayo ni kutoka kwenye kodi ya
wananchi, benki zikalipwa iliziendelee na kazi nzuri ya kupora fedha za
wananchi, na wakati huohuo walipa kodi wakipoteza nyumba zao, peshseni zao,
kazi zao, na hilo halikuwa kwa bahati mbaya, historia ni kama inajirudia rudia,
kila mara, kwa mikono ya watu wale wale, sura zile zile, mbinu zile zile,
lakini wengi wetu tumelala fofofo …. Zzzzzzzzzzzzzz!
“Watu
hamsini wameiendesha Marekani, na idadi hiyo ni kubwa mno” (Joseph Kennedy,
baba wa JFK, KWENYE The New York Times, July 26, 1936)
“… Pale
ambapo mapambano yataonekana kuhama na moja kwa moja kuonekana yanaelekea
kwenye mfumo mpya wa kiutawala wa kidunia, bado kutakuwa na vikwazo vikubwa na
ucheleweshwaji wa kufikia hatua hiyo, na kabla mfumo huo haujawa imara na wenye
manufaa kwa walimwengu na ulimwengu. Watu wasio na idadi … wataichukia New
World Order … na watakuawa tayari kufa kuipinga. Tunapo zichambua faida za New
World Order, tuwe tunakumbuka kuwa na madhara gani yatawapata watu au kwa maneno
mengine kundi la wapingaji wa mfumo huo, ambao wengi wao ni watu makini, wenye
roho za kizalendo na ujasiri.” (H. G
Wells, kwenye kitabu alicho kiita The New World Order)
“Hii ni hatua
nyingine katika maendeleo ya binaadam katika kipindi cha katika ya miaka 20 na
30 tutakuwa na serikali ya dunia hili ni jambo isilo weza kuzuilika”
Mwanamasonia mwingine wa daraja ya juu kabisa na
mwanastratejia wa New World Order, bwana Zbigniew Brzezinski naye katika maka
1970 aliweka hili hadharani;
“Sina wasiwasi
kuwa serikali ya dunia itatokea katika zama zetu .... hatuwezi tukaihamisha
dunia yetu katika hatua moja na ya haraka ... hatua za muhimu kwa ajili ya kulifikia
lengo hilo ni kuendelea kuanganisha mabara kwa njia hii tunaelekea katika kitu
kimoja kikubwa chenye nguvu na chenye ushirikiano”
Maneno hayo ya Zbigniew Brzezinski hayatofautiani na
maneno ya Freemasons mwenzake bwana Stalin aliposema;
“Baadaye maeneo
tofauti (mabara) yataungana na kutengeneza dunia moja yenye utawala mmoja wa
kidikteta”
Masonia mwingine anayejulikana sana
bwana James Paul Warburg alisema kwenye baraza la Seneti la Marekani la mwaka Februari
17 mwaka 1950 kuwa;
“Lazima tutakuwa
na Serikali ya Dunia, ikiwa tunataka au hatutaki lazima tuwe nayo. Swali kuu ni
moja tu ikiwa serikali ya dunia itapatikana kwa nguvu au kwa mashauriano lakini
lazima iwepo”.
No comments:
Post a Comment