Wednesday, May 15, 2013

FREEMASONRY WANAFANYA NINI NA MALENGO YAO NI YEPI? Part II


Hadithi ya Illuminanti ya kutawala ulimwengu wote ni ya kale mno kama ilivyo historia ya binadam mwenyewe, ni kwenye historia hiyo na njama hizo kuliko pelekea kuwepo na kile kinacho fahamika kama ‘BENKI KUU’ katika kila kona ya dunia- ambapo ni watu wachache Fulani wasiyo fahamika kwenye macho na masiko ya wanajamii wengine, ndiyo wanao tengeneza ‘FEDHA HEWA’ kwa kuwakopesha watu kwa riba, kwenyenye mfumo huu wa benki ndipo ulipo uti wa mgongo wa BABILON BROTHERHOOD, AMBAPO BENKI ZINAKOPESHA FEDHA AMBAZO HAINA NA KUCHAJI RIBA KWENYE GEDHA HIZO.


Dirisha la kwanza kufungulia kwenye aina hii ya uchumi na benki ni ile Bank of Amsterdam, ambayo iliundwa mwaka 1609, kisha ikaja Bank of England mwaka 1694. Na hapo mlango ulikuwa unawazuia Illuminanti kutekeleza ajenda yao ukawa UMEVUNJWA, mfumo huo ukaingia katika kila aina ya benki hapa duniani, na ndiyo mfumo unaotumiwa na benki zote duniani nan chi zote hivi leo.
Nyuma ya mabenki haya utazikuta familia na watu wachache tu kama vile Rothscilds, Rockefrllers, Moragan na wanachama wa asasi za siri kama vile Trilateral Commission, Royal Institute of Internationa Affair, Skull and Bones, Committee of 300, Committee of 33, Council of 9, CIA na nyinginezo, zote hizo ni vidole vya mkono mmoja vinavyo fanya kazi moja.
“Serikali za sasa siyo tu kwamba zinapambana na serikali zingine, wafalme, mawaziri, lakini pia na asasi za siri ambazo ziko kila mahala na mawakala wao hatari, na ambao aktika nukta ya mwisho kabisa wanaweza kuugeuza mpango wa serikali kichwa chini miguu juu,” (aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, Benjamin Disraeli, 1876)

Kuwa na sauti, nguvu na uwezo wa kumiliki na kutoa sarafu ndiyo nguzo kuu ya Illuminanti ambayo imewawezesha kutufikisha hapa tulipo sasa. Mtandao huu kutoka Babilon ndiyo ulio wafadhili akina Hitler na Mussolin, ndiyo walio panga WWI na WWII na kudhamini pande zote mbili za vita. Kwa zaidi ya karnbe sasa lengo lao limekuwa ni kutengeneza serikali moja kuu ya dunia. Walijaribu kutengeneza League of Nations baada ya WWI, shirika hilo nalo lilidhaminiwa na watu wale, wale, Rockefellers na Rothschilds, mpango wao huu ulianguka, waliufanya ushindwe ili watengeneze chombo chenye nguvu zaidi cha kuweza kuishika dunia, wakaja na United Nations baada ya WWII, makao yake makuu yakawa New York kwenye aridhi iliyo tolewa zawadi na Rockefellers.

Tizama walivyo ifanya UN kubwa, znito na yenye sauti ya ushawishi kisiasa na kiuchumi kote duniani, maarufu kama kiranja wa  ‘kutuliza amani duniania’, Amani ambayo tangu shirika hilo liundwe dunia haijaiyona zaidi ya kinyume chake. UN ndiyo msimamizi kwa sasa wa hiyo serikali ya dunia kabla hajatangaza rasmi na inashirikiana kwa karibu na NATO, ambayo nayo inasimama kama jeshi la dunia, na WORLD BANK, kama kitengo cha usimamizi wa uchumi wa kidunia, Mashirika makubwa makubwa mengine yanayo fuata chini ya vivuli ya hayo mashirika mama, kama vile The World Trade Organization, World Health Organization, na mengine utakuta yametengenezwa au kuwepo kwao kunayo dhamana kubwa ya Rockefellers, Rothschilds, au Morgans.

John D. Rockefeller, III, Kulia akiwakilisha hundi ya dola 8,500,000 kwa Trygave Lie, Katibu mkuu wa kwanza wa United Nations. Pesa hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kununulia aridhi Manhattan ambapo jengo la UN litajengwa

Ni vipi mfumo wa kibenki tuliyo nao sasa, ulianzishwa, na mapaka sasa umeingi kwenye mfuko wa suruali ya kila mmoja wetu ni moja ya somo tamu sana la kihistoria mbalo hutokaa ukafundishwa na mwalimu wako awe wa historia yenyewe au wa uchumi, lakini Mungu akipenda hapa siku moja kuna siku tutaligusa.
Rothschilds ni moja ya familia kongwe, tajiri, yenyenguvu kubwa ndani ya Ulaya kushinda serikali zenyewe, na moja ya familia kongwe za kibenki ambayo mfuko wao unaoyo senti ya kila mvuja jasho duniani kote. Nguvu yao kwenye mambo ya fedha ilianza kuinuka pale ambapo mtu aliyeitwa Mayer Amschel Rothschild, aliyeishi Franfurt, Ujerumani, kama ‘sonara’ alipoanzisha nyumba ambayo watu walikuwa wakija kubadilishia ‘sarafu’ ama dhahabu zao au kuzitunza kwa mtu huyo.

ROUND TABLE


Watoto wake wa tano aliwasambaza Ulaya yote kwenye miaka ya mwishoni mwa 1700 na mapaema mwaka 1800, walikuwa wameisha ishika Frankfurt, Vienna, London, Naples na Parisi na kutengeneza mtandao wa kifamilia ya kibenki. June 1815 Nathan Rothschild, alitumia watu wake wa siri kuvujisha taarifa kuwa ushindi ambao Uingereza umeupata dhidi ya majeshi ya Kifaransa ya Napoleon si wa kweli bali majeshi ya Ufaransa ndiyo yaliyo shinda dhidi ya Uingereza, na kama kawaida, Rothschilds walikuwa wamezamini pande zote mbili za vitu, kwenye soko la hisa Hati fungati ya serikali za Uibgereza zikaanza kushuka thamani, mali na vitu vingi vya Ungereza viliporomoka thamani, watu waliuuza vitu vyao kwa bei ya chini mno, taratibu Nathan kupitia mawakala wa familia wakaanza kuvinunua vitu hivyo na hati fungati hizo kwa bei ya kutupwa, na muda ulipofika, na taarifa rasmi zilipokuja kwamba ni Uingereza ndiyo waliyo shinda vita, Rothschild katika mikono yao tayari walikuwa wanamiliki utajiri wote wa Uingereza. Ilipofika katikati ya miaka ya 1800 walikuwa wanamiliki benki zote za Ulaya, wakatumia fedha hizo kuwadhamini watu kama akina Morgans, Vanderbilts, Carnegies, na Cecil Rhodes kufanya au kutafiti kazi zenye maudhui yale yale ya New World Order.


Rothschild akishirikiana na Morgan, Paul Warburg, mshirika wa Kuhn, Loeb & Co pamoja na wamiliki wengine wa kibenki za binafsi walikutana kwa siri na kutengenezwa muswada ambao ulikuja kupitishwa 1913, muswada huo ukaiwezesha benki kuweza kutengeneza asilimia 90 ya fedha zote ambazo zipo kwenye mzunguko kwa njia ya mikopo hewa, muswada huo umezipa benki nguvu na uwezo wa kusimamimia uchumi wa nchi. Utajiri wao unakadiriw kufikia dola trilioni 100. (The Feferal Reserve Cartel: Part III By Dean Henderson)


WAPENDWA TUKUTANE TENA WAKATI MWINGINE KUUENDELEZA MTANANGE WETU HUU, MUTA NIWIA RADHI KWA SABABU NAKUWA NA MUDA MCHACHE SANA WA KUWALETEA HAYA ..... LAKINI MSIJALI KARIBUNI HIVI MTAPATA KITU KIMOJA CHENYE KILA KITU ..... KITABU ..... KINAKUJA ......


No comments:

Post a Comment