Hata
hivyo kulikuwa na madhehebu mengine ya watu walio fahamika kama Essenes, hawa
nao walikuwa ni Wayahudi, mafunzo yao hawa nayo yanakuja kuwa ni sehemu muhimu
ya mafunzo na muongozo kwa Illuminati na freemasonry katika historia yao yote.
Essenes katika picha hii wana uzito wa kipekee, kwa vile ni kutoka kwao ndiyo
freemasonry wanajivunia walivyo navyo. Ingawa Essene walipatikana Palestina
zaidi lakini mafunzo yao yalienea mpaka Egypt. Essene hawa walikuwa ni moja
kati ya madhehebu makubwa matatu ya Kiyahudi katika dini hizi za kipagani,
wengine walikuwa ni Pharisees na Sudducees. Essene walitambulika kama warithi
wa mafundisho ya Chaldea, elimu ya nyota ya wa Misri, na elimu ya tiba ya wa
Persia wa kale, wali fananishwa na makuhani wa Magi kutoka Persia.
Kwa msaada wa mitume waliofuata hekalu lilijengwa upya, lakini
likaja kubomolewa tena kwa mara nyingine na Wayahudi kubakizwa kwenye dini za
kipagani za watu wa Roma.
Hivyo
mafunzo haya ya kipagani yaliwatoa kabisa Wayahudi katika imani ya Mungu Mmoja
na kuwaingiza katika imani za kishirikina ambazo ndani yake shetani aliabudiwa
waziwazi.
Quran
nayo ikalitaja hili kuhusiana na Wayahudi na athari waliyo ipata baada ya
kutekwa na kupelekwa Babyloni.
“Na wakafuata yale waliyo zua
mashet'ani kuuzulia ufalme wa Suleiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali
mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa
kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika mji wa Baabil (Babiloni). Wala hao
hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru.
Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi
kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala
hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye fuata haya hatakuwa na fungu
lolote katika Akhera (maisha baada ya kifo). Na hakika ni kiovu mno walicho
jiuzia nafsi zao laiti wangelijua.”( Quran2: 102)
Kutoka
kwa mungu Mithra aliyeingizwa Ugiriki na Wayahudi kutoka Babyloni mpaka kuundwa
kwa madhehebu ya Mithra ambayo yatabakia kama dira ya Illuminati katika zama
zitakazo fuata, kote huko familia za Illuminati zilikuwa ni sehemu ya ukuaji
huo. Ukoo wa nyumba ya Commagene iliungana na ile ya Herod Great, pamoja na
familia za watu wa Siria wakiwemo
makuhani na wachungaji wa mungu Baal pamoja na familia ya Julius Caesar.
Waliyafuata yale madhehebu ya Mithra wakaichanganya na mafunzo ya maajabu
kutoka kwenye Kabbala na kutengeneza kitu kipya chenye mchanganyiko wa maajabu
ya kichawi na elimu za nyota. Dini hiyo ikafuata ile mila ya dini ya Kibabiloni
ambapo wafalme waliabudiwa kama mfano wa mungu jua, mungu Mithra katika haya
madhehebu yaliyo toholewa akawa kwenye umbo la binadamu naye akaabudiwa kama
Alexander the Great ambaye pia alimuwakilisha mungu Jua.
Mafunzo
haya yalishika mizizi ndani ya mashariki ya kati vilivyo, hata Uislamu
ulipobisha hodi kwa mara nyingine Mashariki ya kati na kuanza kuimeza miji
mmoja baada ya mwingine, haikusalimika na mafunzo haya ya kipagani.
baadhi
ya wafasiri hasa wa zile kazi za Magi, Mithra, Essene waliacha dini yao ya Kiislam
na wengine walichanganya mafunzo ya Uislamu na yale ya Upagani na hapo ukawa
mwanzo wa kuundwa dini mpya ndani ya dini ya Uislamu, dini ya kisufi, walijiita
kuwa ni Waislam lakini hawakuwa na
chochote cha kufanania na Uislamu zaidi ya mavazi yao. Mafunzo haya yalikwenda
yakaingizwa katika dini nyingine ya Kishia ambayo nao pia walishatoka kwenye
Uislamu kutokana na mhimili wa mafunzo
yao, lakini kama walivyo Sufi nao
wanajiita kuwa ni Waislam, kupitia kwa Ismailia dhehebu jingine la dini
ya Shia kazi hizi au mafunzo haya
zikawafikia Knights Templar ambao wakazipeleka Ulaya na kutengeneza Scottish Rite Freemasons. Wakati Knights
Templar wanazichukua kazi hizi tayari zilikuwa kwenye maudhui sawa na ya
Freemasons tunao waona leo. Egypt kulikuwa na mahekalu ya kimasoni hata kabla
ya Ulaya, kulikuwa na madaraja 3 mpaka 10. Hivyo Freemasons na asasi nyingine
za siri zilizokwenda kwa majina tofauti zilikuwa zimeshaota mizizi Mashariki ya
kati kwa karne nyingi kabla aina hii ya maarifa haijapiga hodi katika nchi za
Ulaya. Preure de Sion na Knights Templar walipotengeneza Scottish Rite Freemasons wakaipatia madaraja 33. Lakini waliita ‘Ancient and Accepted Rite’ akiwa na maana kuwa walicho kiongezea juu ya kile cha mababu wa
Freemasons wa Egypt kimekubalika. Ile ya Egypt ilikuwa ikifahamika kama, ‘Ancient and Primitive Rite’, hii ndiyo
baba na babu wa Freemasons zote tunazo ziona leo duniani.
Nembo na muhiri wa Knights Templar.
Knights
Templar nayo hadithi yao ilikuwa ikivutia mno, wao walijinadi kuwa kazi yao ni
ulinzi kwa mahujaji wa Kikristo walio kuwa wakifika hapo kwa ajili ya ibada
hiyo, lakini iliwachukua miaka 20 baada ya vita vya msalaba wao kuchukua dhima
hiyo, na kwa muda wa miaka 10 walikuwa wapo tisa (9), unaikumbuka nambari hii
niliitaja huko nyuma wakati mfalme Agrippa alipokutana na wenzake kuasisi
Mysterious Force?
Alama kuu ya Knights Templar, ambayo inatumika mpaka hivi leo,
utaiona kwenye vazi la Papa, na pia utaiona kwenye bendera ya Uingereza.
Jamaa hawa tisa walikuwa bize kuchakura
chakura na kutafuta kitu fulani au masalio ya namna fulani katika kaburi
alilozikwa mfalme Agrippa na katika hekalu la mara ya pili la Wayahudi ambalo
lilibomolewa na Titus mnamo mwaka 70 AD.
ASKARI WA KNIGHTS TEMPLAR
Kwa
muda wote huo walikuwa wakichimba chimba katika maeneo ya masalio ya hekalu
hilo, kwa miaka yote hiyo kulikuwa na kitu ambacho walikuwa wakikitafuta. Mpaka
leo hakuna anayefahamu kinagaubaga kuwa
nini hasa Templar walichokipata katika hekalu hilo, ila hakuna maswali
wala shaka kuwa kuna ambacho walikipata, kitu chenye thamani kubwa, kitu
kilicho ibadilisha historia ya Templar tangu hapo. Inasemekana waliipata hazina
ya mfalme Suleiman ambayo si Nebuchadnezzar II wala Waroma waliofanikiwa
kuipata. Inasemekana kuwa hazina iliyo kuwepo kwenye hekalu hilo ni tani 65 za
fedha (Silver) na tani 26 za dhahabu. Mengine ambayo yanadhaniwa yalichukuliwa
na Knights Templar kutoka kwenye hilo hekalu ni nyaraka na maandishi mengine
muhimu kuhusu Yesu na familia yake
KIKARAGOSI KINACHO ONESHA PICHA YA JACOB DE MOLAY
Baada
ya hapo Templar walirudi Ulaya.
Baada
tu ya kupata baraka za Papa, utajiri waliokuwa nao, pamoja na aridhi na mamia
wakijiunga kutoka katika familia za kifalme na watu kutoka katika familia
tajiri na huku wakitoa mali zao kwa
Templers ikawa ni sababu ya wao kuweza kumiliki aridhi sehemu mbalimbali za
Ulaya kama Uingereza, Portugal, Spain, Germany, Italy, Austria Ufaransa na
kwengineko. Baada ya kipindi kifupi tu Templers wakawa karibu kabisa na kanisa
la Romani kiushawishi na kiutajiri pia. Mwaka 1139 Papa Innocent II aliifanya
jumuiya hii ya Templar huru juu ya wafalme wote, na kwa wazee wa baraza za
kifalme, aliyeruhusiwa kuwaingilia shughuli zao ni Papa peke yake na ndiye
msimamizi wa shughuli zao mpaka hivi leo
Mtandao
huu wa Tampler ukazidi kupata nguvu, walifanya walivyotaka, walikuwa ni
wataalam wa tiba na madawa ya miti shamba, ndiyo waasisi wa benki na ndiyo watu
wa kwanza kutumia hundi, na watozaji wa riba kubwa katika biashara zao, katika
sehemu kubwa ya Ulaya wakawa ni watu wenye ujuzi mkubwa wa mambo ya benki,
walifanya kazi ya kusafirisha fedha za wafanyabiashara kupitia kwa watu wao
waliko Ulaya, wafalme wa nchi nyingi waliwakopesha Templer kiasi kikubwa cha
fedha, yote haya ilikuwa ni mbegu ya kuzaliwa kile tunachokiita ubepari na
mifumo ya benki. Templar hawakutakiwa kulipa kodi, walijihusisha pia na mambo
ya ujenzi na wakaruhusiwa kujenga makanisa yao wenyewe, ambayo yalikuwa ni ya
maajabu kwa utaalam wa mahesabu na elimu ya hali ya juu ya maumbo iliyotumika
ambayo watu wengine hawakuwa na maarifa nayo
Mnamo
mwaka 1296 wazo lilitolewa kuwa Jumuiya ya Knights Templar na ile ya St. John
ziungane, kiongozi wa Templar, Jacques de Molay alilipinga wazo hilo. Aliyekuwa
mfalme wa Ufaransa Philip IV na ambaye alikuwa amewakopesha Templar kiasi
kikubwa cha fedha na alitaka kuwa mwanachama wa jumuiya hii yenye nguvu na
ushawishi mkubwa lakini akakataliwa na hivyo akafikiria namna ya kuivunja vunja
jumuiya hii, ikumbukwe si Papa wala mfalme Philip IV aliyekuwa na sauti juu ya
Tampler.
Mfalme
akaweka majasusi kufuatilia ajenda za jumuiya hii na haikuchukua muda akatambua
kuwa Templar waliojiita watumishi masikini wa hekalu la Mfalme Suleiman, na
wanajeshi masikini wa dini ya Kikristo na wanao tumia nembo ya wapanda farasi
wawili juu ya mgongo wa farasi mmoja kuonesha umasikini na undugu wao; kumbe
wao ni watu matajiri, wenye nguvu kubwa za kijeshi na kiuchumi na wanao tishia
ufalme wake, wao ni wafuasi wa dini ya mashetani, wanashirikiana na wachawi,
wanavitumia vitabu vichafu vya kimila kutoka Babyloni, Kabbala na Talmudi
kufanya mambo ya nguvu za giza, wanawafundisha wanawake kutoa mimba, wanatoa
kafara za watoto wachanga na wanafanya ngono kinyume cha maumbile. Tarehe 22
Septemba 1307 mfalme akatoa amri ya kukamatwa kwa Templar wote, amri hiyo
ilitolewa katika mfumo wa barua iliyofungwa ikapigwa muhuri juu na amri ya kuwa
barua hiyo isifunguliwe mpaka jioni ya tarehe 13 Oktoba 1307, barua hiyo
wakapewa viongozi wote wa kiserikali waliyo chini ya utawala wa Philip IV, na
pia viongozi wa kifalme wa nchi zingine walipewa barua hiyo.
Ijumaa
ya tarehe 13 Oktoba 1307 ilikuwa ni siku mbaya kwa Templar, bado tarehe 13 Oktoba
inaadhimishwa na Freemasonry kama siku mbaya kuliko. Kati ya Templar 3200 ni
620 tu ndiyo waliokamatwa wengine walifanikiwa kutoroka.
JACOB DE MOLAY ANACHOMWA MOTO AKIWA HAI, Mpaka leo freemasonry wanalipiza kisasi juu ya kifo cha kiongozi wao huyo kwa njia mbalimbali.
Knights
Tampler walikimbilia Scotland, walipokelewa na mfalme Robert the Bruce ambaye
alikana kuitekeleza amri ya mfalme, hii ni kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa ni
mfuasi wa Tampler. Kutokea hapo Scotland Tampler wakazizika shughuli zao, chini
kwa chini kama mto wa chini ya aridhi uelekeao baharini, Templer walianza
kuikamata Ulaya na koo mbalimbali za kifalme huku wakisubiri fursa nzuri
kujitokeza upya, lakini wakiwa na jina jingine tofauti na lile la awali.
Unakumbuka
hadithi ya Black Death, walikuwepo watu waliyo itwa masoni, baada ya zahama la
Black Death, masoni walianza kuwapa uanachama wale wasiyo kuwa masoni, yaani wasiyo
kuwa na taaluma ya ujenzi kuwa wanachama katika jumuiya hii, watu mbalimbali
walijipenyeza ndani ya masoni kwa sababu mbalimbali, lakini pia kwenye kona
fulani yenye kiza totoro, watu fulani walio funika nyuso zao, ambao walikuwa
wakifahamika kama Tampler, wakaona fursa waliyo kuwa wakiisubiri kwa muda
mrefu, hatimaye imefika, Tampler wakajipenyeza ndani ya Masoni.
Ajenda
ya Knights Templar ilikuwa kuichukua jumuiya ya kimasoni ambayo kipindi hicho
ilikuwa ikihusika na mambo ya ujenzi kwa kutumia elimu ya siri iliyo fahamika
kwa wajenzi wa jumuiya pekee. Kwa sababu kipindi hicho jumuiya hiyo ilikuwa na
hali ngumu kiuchumi ilitumia fursa ambayo Knights Templar waliona faida yake
kwao, kwani hawakuhitaji uwe mjuzi katika ujenzi bali ulipe ada tu ya uanachama.
Walikuwa na hamu kubwa ya kufahamu nini kilicho nyuma ya kazi za ujenzi za
jamaa hawa, na kwa vile masoni walikuwa wamejijenga mpaka nje ya England,
ingewapatia fursa Knights Templar kujitanua chini ya kivuli cha wamasonia na
wakati huo, huo wakisubiri wakati muafaka wa kuitumia masoni kama pazia la
kufichia ajenda yao kuu. (kutoka kwenye kitabu ambacho Salim Msangi anakiandaa)
Walio
ingia ndani ya Masoni, walikuwepo Francis Bacon, halafu akaja mwana mahesabu na
mwana kemia Robert Moray
Msomi
mwingine mkubwa katika nyanja ya Alchemy, nyota na uchawi Elias Ashmole
akajiunga ndani ya hekalu la kimasoni, halafu akaingia mwana Kabbala Robert
Boyle ambaye naye alikuwa na taaluma ya kemia na fizikia, na pia kipindi fulani
nyuma alikuwa ni grand master wa asasi ya siri cha Prieure de Sion 1654 mpaka
1691, kikundi hicho ndiyo baba wa Knights Templar ambao nao kwa sasa walikuwa wanajipenyeza
ndani ya masonia, baba na mwana. Halafu Sir Christopher Wren mjenzi na mjuzi wa
taaluma ya nyota, jamaa huyu ndiye aliye fanisi hekalu la St.Paul na pia
alichora ramani ya kulijenga upya jiji la London baada yakuharibiwa na moto
mkubwa mnamo mwaka 1666. Isaac Newton akawa mwana jumuiya mnamo mwaka 1672,
kama alivyokuwa Boyle, Newton naye alikuwa ni grand master wa Prieure de Sion
kutoka 1691 mpaka 1727
Bwana
wakubwa hawa katika ulimwengu wa kisayansi, wakiwa ndani ya hekalu la kimasoni
wakaanza kuigeuza sayansi kichwa chini miguu juu kwa faida za kisiasa na kwa
malengo ya jumuiya za siri walizo toka, wakatengeneza nadharia ya inayo
julikana kama Materialist, maarufu kwa lugha yetu kama sayansi ya Darwin na
sasa inakwenda kwa jina la Humanist, sayansi na nadharia hii, ina kataa kuwepo
kwa roho, nadharia hii inasimamiwa vilivyo na vikundi vinavyoitwa wasimamizi wa
haki za binaadam, chini kabisa ya nadharia hii ni kukataa kuwepo kwa Mungu,
wanadai kuwa ulimwengu umejitengeneza wenyewe na kifo hakihusiani kabisa na
kuwepo kwa Mungu.
Mwaka
1717 Templers wakajitokeza tena Ulaya, idadi yao imekuwa kubwa mno na nguvu yao
imeongezeka na wako tayari kutengeneza kitambulisho kipya. Kitambulisho
kitakacho waacha huru na matendo yao ya karne zilizotangulia na wakipewa nguvu
na watwana pamoja na masultani wa England. Na jina walilolichagua litajulikana
na wengi lakini litafahamika na wachache.... hili jina jipya..... ni.......
FREEMASONRY.......
Mkuu endela kutumwagia vituzzz
ReplyDeleteKaka nasubiri ishu uliyo tuahidi ya kina Kanumba, Diamond na mastaa wengineee
ReplyDeleteKuhusiana na hilo la wasanii wabongo kuhusishwa na zahama hili, ningependa munipe muda kidogo, na ndani ya wiki ijayo nadhani nitaweka post juu ya hili, lakini kutokukuweka njia panda ni kwamba hakuna kati yao aliye freemasonry, na vipi nimefikia kwenye hitimisho hilo, tukutane kwenye blog hii hii nitakupatia 'details'
ReplyDeletekaka jinc ya kujiunga na hawa mashetan inakujaje
ReplyDeletekaka jinc ya kujiunga na hawa mashetan inakujaje
ReplyDelete