Kuna vyanzo
vingi vinavyo elezea kuwepo kwa freemasonry Kabbala ya 1717, vyanzo hivyo ni
vingi, vinahitaji muda na uyakinifu ilikuweza kutofautisha baina ya almasi na
vipande vya vioo. Kuna vilivyo andikwa kwa nia nzuri tu, kuna vilivyo andikwa
kwa ajili ya kupotosha, na kuna vilivyo andikwa na wale wasio fahamu wanacho
andika, lakini wote wakijaribu kuthibitisha au kukanusha kuwepo kwa freemasonry
kabla ya 1717.
Katika mtandao
wa Bible Beliver, wameweka hadithi moja nzuri sana ya namna ambavyo freemasonry
walivyo kuwepo kabla ya 1717, napo hapo nitaiangalia kwa uchache sana, kwa
urefu hadithi hii unaweza kuitizama mwenye hapa. http://www.biblebelievers.org.au/masonry2.htm
Hadithi yenyewe
inazungumzia habari ya mwaka 43, kipindu kifupi sana baada ya Yesu/Kristo (Issa
Mwana wa Mariam Rehma ya Mungu iwe juu yao wote) alipo paishwa kwenda mbinguni.
Ulitokea mtafaruku baina ya waumini wa dini za kipagani na dini aliyoiacha
Yesu. Jamii ilikuwa imechanika chanika mno. Baba anamakana mwana, mwana anamkana
baba, mama na baba hawaelewani, dada na kaka na ndugu wengine halikadhalika.
Uadui mkubwa umeletwa na kile kilicho onekana kama ‘dini mpya’.
Waliyo zikataa
‘dini mpya’ alikuwemo mtu aliyeitwa Mfalme Herod Agrippa II, anatajwa kama
alikuwa ni kibaraka wa dola ya Roma, na Wayahudi walinyanyasika vibaya kwenye
mikono yake, hasa pale walipo itikadi kuwa Yesu ni mtume wa Mungu Mmoja na wao
wanayafuata mafundisho yake.
Mfalme Herod
Agrippa II
Mfalme Herod alisimama mbele ya baraza la
Jerusalem na kulihutubia juu ya zahama au kisu kilicho ichana jamii yao, juu ya
mafundisho ya ‘dini mpya’ na namna gani watasimama dhidi ya dini hiyo, na
wafuasi wake na mafundisho yao, ili nyumba za Jerusalem zisalimike na ‘balaa’
lake.
Katika baraza
hilo mfalme alikutana na watu tisa tu (9), hii namba itizame na ikumbeke
vizuri, tutakutana nayo huko mbele na kasha nitakueleza maana yake hasa nini.
Waheshimiwa tisa walio kuwepo kwenye baraza hilo ni Herod Agrippa II, Moab Levy, Adoniram, Johanan, Jacob Abdon, Antipas, Solomon
Aberon, Ashadi Abia,
na Hiram Abiud.
Mfalme
Agrippa akawambia kwanza hakubaliani na Yesu kwamba ndiye Kristo,
kwa vile yeye na wenzake na mababu zao kunayo Kristo mwingine waliyekuwa
wanamngojea, ambaye ndiye atakuwa KING/Mfalme wa Jerusalem, na sasa hivi kiti
chake kipo kinamngojea, kama tunavyo jua harakati hizi za kuwa na kiongozi
mmoja duniani kote, serikali ya kiongozi huyo itakuwa ni Jerusalem na hapo
tumemuona Agrippa miaka hiyo akizungumzia kitu hicho, hicho, na leo hii
tunawaona freemasonry wakiandaa makazi ya mfalme huyo, na kumbuka kwenye
hadithi ya Mtume Muhammad (s.a.w) kuwa Dajjali, Mpinga Kristo, au huyo Kristo
ambaye Mfalme Agrippa anayemtaja, atauwawa katika eneo linaloitwa ‘Baab Lud’
leo panajulikana kama Tel Aviv, hapo ndipo Dajjali atakapo uwawa, kwa vile ni
ndani ya Jerusalem ndipo atakapo taka kusimamishia dola yake na ukitizama
matukio ya kiulimwengu leo ndicho hasa Illuminati wanacho kiandaa, kitu cha
mfalme mwenye jicho moja.
Kazi ya Nikolai Bodarevsky, 1875, ikimuonesha mtume Paulo akihukumiwa mbele
Mfalme Agrippa.
Agrippa
akaendelea kuliambia baraza lake kuwa na hicho alicho kuja nacho Yesu mababu
zake walishapambana nacho kabla yao na wao akina Agrippa wataendelea kupambana
na hicho mpaka mwisho. Alicho kuja nacho Yesu si kingine bali dini ya Mungu
Mmoja. Hivyo basi Agrippa kwa ushawishi wa Hiram Abiud wakaanzisha kile walicho
kiita ‘Mysterious Force’ kama anavyo elezea mwenyewe.
“Tutawafanya
waamini kuwa jumuiya yetu ni ya kale kwa kutumia alama za zana za ujenzi zilizo
tumiwa na ndugu yetu Hiram Abiff kulijenga hekalu la Suleimani (Solomon) kama
vile nyundo, bikari, kampasi n.k vyote vya mbao kama alivyo kuwa navyo Abiff.
Katika jumuiya yetu tutaweka madaraja (degree) madaraja hayo yatakuwa
thelathini na tatu kama ulivyo umri wa Muongo, mzushi aliyejiita Massehia. Kila
daraja tutalipa jina na tutatengeneza nembo zingine. Yote haya ni mawazo yangu
pamoja na mawazo ya ndugu zetu Hiram na Moab. Maana ya ndani ya nembo hizi
haitafichuliwa itabakia kuwa ni siri kati yetu sisi watu tisa tulioanzisha
jumuiya hii. Kwa watu wengine watakao jiunga nasi katika jumuiya yetu hii,
inatosha kwa wao kujua kuwa hivi ni
vifaa vya ujenzi vya enzi na enzi, hivyo wataamini kuwa jumuiya yetu
imeanzishwa tangu wakati wa Suleiman.”
“Mimi
kutokana na nguvu zangu kama kiongozi nawa zawadia kila mmoja heshima ya kuwa
katika daraja la 33 (33 degrees) daraja la juu kabisa katika jumuiya yetu....
na kwa sababu ndugu yetu Hiram Abif ni yatima wa Baba, tangu utotoni mwake
hakuna aliyemjua ila mama yake mjane na pendekeza pia jumuiya yetu kuitwa “Mjane” (The Widow) kutoka sasa na
kuendelea sisi waasisi tutaitwa watoto wa mjane (The Sons of the Widow), na
kila mshirika atajiita mtoto wa mjane mpaka mwisho wa dunia kwani tunaamini
kuwa jumuiya yetu itaishi mpaka mwisho wa dunia.”
Maneno
hayo yalitamkwa muda mchache baada ya Yesu kupaishwa kwenda mbinguni, na maneno
hayo yameweza kusimama dhidi ya muda, dhidi ya kila janga lililoikumba dunia
yetu tangu, na leo tunawaona watu au jumuiya ambayo inawiana 100% na maneno
hayo, tunawaona freemasonry.
Lakini
kama alivyo sema mfalme Agrippa, kuwa hiyo ‘dini mpya’ mababu zao
walishapambana nayo, hivyo akimaanisha kuwa kabla ya Yesu kuna wengine walikuja
na ujumbe sawa na huo, yaani mitume wengine kama Daud, Musa na wengineo (Amani
ya Mungu iwe juu yao) na walipingwa na mababu wa akina Agrippa na wenzake, kwa
maana mababu hao tayari walikuwa na dini au mfumo wao wa kuishi tofauti na huo
ulioletwa na mitume wa Mungu Mmoja, hivyo basi utaona kuwa Freemasonry
haikuanzia kwa Agrippa, bali kwa mababu kabla yake.
Hadithi
yenyewe iko hivi,
Utakumbukwa
kwamba, katika wafuasi wa dini ya Mungu Mmoja, ambao walipata shida sana
kutokana na jeuri yao na kiburi ni Wayahudi, kuna wakati waliadhibiwa na mfalme
katili mpaka nyumba yao ya ibada ikateketezwa na wakachukuliwa kwenda utumwani Babyloni. Walipokuwa huko mawasiliano ya kiroho
yalikatwa, na kwa kipindi kirefu sana watu hawa wakawa chini ya ibada
mbalimbali za kimila na kishetani.
Wayahudi
waliotokea utumwani Babyloni na dini ya kimila iliyobeba mafunzo ya Kabbala
walikuwa wakidhaniwa kuwa ni wafuasi wa dini ya Chaldea Magi. Watu wa Persia
walikuwa ni wafuasi wa dini ya Zoroastrian ambayo Magi walikuwa ni wachungaji
wa dini hiyo, hivyo Wagiriki walidhani kuwa hawa Wayahudi ni wachungaji wa
Magi. Dini hii ya Magi asili yake inasemwa kuwa ilikuwa ni dini ya Mungu Mmoja
lakini baadaye ikachanganya na mafundisho ya kibabiloni na kuharibiwa. Dini hii
ikawa imejikita zaidi katika sanaa na elimu ya mambo ya nyota, inasemwa
makuhani wao ndiyo wa mwanzo katika karne ya 6 BC kuifanikisha elimu hii ya
mambo ya angani, misingi yake ikawa ni kuabudu nyota. Elimu hii nyota ikaenda
sambamba na ile hadithi ya kufa na kufufuka kwa mungu
Mchoro huu unaonesha uharibifu kwenye hekalu la kwanza la Wayahudi,
ambapo baada ya hapo walikamatwa kama watumwa na kupelekwa Babyloni.
Mungu
wa watu wa Persia alifahamika kama Mithra ambaye alikuwa sawa na Baal wa Babyloni,
mungu huyu wa Persia alitukuzwa kwa nguvu na sifa zote za kichawi. Dola hii ya Persia
ilivyo zidi kupanuka , mafundisho ya Magi nayo yakatapakaa kila ambapo dola
hiyo iliingiza mguu au ilikuwa na mahusiano na watu husika. Wagiriki
walizipokea tamaduni hizi na zingine mfano wa hizi na kuzitafsiri kwenye lugha
zao. Wagiriki wanatajwa kuwa wao ndiyo wa mwanzo kuiweka Kabbala kwenye
maandishi wakati kabla ilikuwa ni aina ya fasihi simulizi. Baadaye mafundisho
haya yalichukuliwa na Waislam walioacha mafunzo sahihi ya dini ya mdomo mnamo
karne ya saba na kuanza kuzitafsiri kazi hizi katika lugha ya Kiarabu na kisha
kupelekea kuundwa kwa dini mpya ya Usufi ambayo mafunzo yake yalikuwa sawa na
yale ya Kabbala na Zoroastrian zaidi, nao walijiita Waislam lakini imani yao,
matendo na mafundisho yao hayakufanana chochote na Waislam. Kama tutakavyo kuja
kuona Wasufi ndiyo walio wapatia Knights Templar mafunzo haya nao wakayapeleka
Ulaya ambapo matokeo yake tukawapata Scottish
Rite Freemasons
Baada ya nyumba ya ibada kubomolewa kabisa na Nebuchadnezzar ,
Wayahudi walikamatwa kama watumwa na kupelekwa Babyloni. Mchoro huo unaelezea
safari hiyo ya kuelekea Babyloni.
Hivyo
Kabbala asili yake ni Babyloni lakini si huko ilipo anzwa kuwekwa kwenye
makaratasi, bali ni Ugiriki na watu wanao tajwa kufanya zoezi hilo ni
Pythagoras na baadaye Plato ambaye kwa muda mrefu tena kimakosa alikuwa
akitajwa kuwa ndiye muasisi na mtunzi wa Kabbala, lakini la Hasha, Kabbala ni
kubwa kushinda Plato mwenyewe, na hata leo inasemwa kuwa asili ya kitabu hichi
ni Babyloni lakini hajulikani mtunzi wake ni nani ndani ya hiyo Babyloni ila
hakuna shaka kuwa mafunzo haya haikuwa kazi ya binaadam bali Mashetani wenyewe.
Usikose sehemu inayofuata kwenye mtiririko huu, ...
maoni, maswali, michango vyote vinakaribishwa ..
I like it brother Salim
ReplyDeleteGood history !
ReplyDelete