Tuesday, May 8, 2018

JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? Season Finale, Ep 4 (The Face of the Giants..)



Kote duniani, jamii mbalimbali wamekuwa na hadithi juu ya binadam wenye maumbo makubwa kupata kuishi kwenye jamii zao kwenye zama zilizo tangulia. Kwamba binadam hao walikuwa na maumbo makubwa na kimo kikubwa na urefu pia, na walikuwa ni majitu yenye nguvu.


Watu wa Kotoko, Chad hapa kwetu Afrika wanasema mababu zao walikuwa ni majitu makubwa kiasi mtu kwao ulikuwa ni kitu kidogo sana.

China nako wanazo habari kama hizo na wanasema watu hao walifutika kwenye uso wa dunia baada ya kuongeza uharibifu.
Canada wanasema Mungu alikuwa na hasira na ‘majitu’ hivyo akawaletea gharika.

ULAYA
Ngano za watu wa Scandinavia zinasema watu wa mwanzo kuumbwa walikuwa wakubwa kama milima. Nordic wanasema watu wa mwanzo ambao wao waliwaita ‘Jotunn’ walikuwa ni majitu makubwa. Ujerumani ngano za kale kwenye makabila mengi zina zungumzia juu majitu makubwa yaliyoishi kabla ya binadam wa leo. 



Ireland wanazo hadithi za majitu yaliyo itwa ‘Fomoria’. Ugiriki majitu makubwa yaliitwa ‘Titans.’ British majitu makubwa yaliitwa ‘Gog na Magog’. Maeneo mengine Ulaya kwenye hadithi ya majitu makubwa ni Goths, na Sicily kutaja kwa uchache.


AFRIKA
Kama nilivyo taja hapo juu, kabila la watu wa Kotoko nchini Chad wanasema mababu zao walikuwa ni majitu makubwa.

ASIA
Kabila la watu waliofahamika kama ‘Izdubar’ walikuwa ni majitu makubwa kwenye nchi ya Chaldea.

BABILONI
Kwenye maandiko ya Talmudi, moja ya maandishi ya kale mno ambayo wayahudi walitoka nayo Babiloni inataja juu ya ‘majitu’ makubwa ambayo yalikuwa na vidole sita na ‘line’ mbili mbili za meno juu na chini.
Kwenye kitabu cha Enoch imeandikwa kuwa ‘majitu’ makubwa yalitawala dunia kabla ya kuja kwa gharika.

CHINA;
Kama tulivyo sema hapo juu China nao wanazo hadithi za majitu makubwa ambayo yaliangamizwa kwa kutofuata sharia za Mungu.

TIBET
Kwenye hadithi na ngano za watu wa Tibet, majitu makubwa na yenye nguvu ni kama kiunganishi kwenye hadithi zao. Rikodi zao zinaonesha kuwa wanaume wao walikuwa na urefu wa futi 15 na wanawake urefu wa futi 12.

AUSTRALIA
Kabila la watu wa Aborigines asili yake ni majitu makubwa weupe wenye nywele nyekundu. Aina ya watu kama zeruzeru. Kwenye kabila hilo nako kunazo hadithi nyingi juu ya majitu makubwa.

AMERIKANA (AMERIKA)


Kunazo hadithi kuwa Mungu alikasirishwa na majitu makubwa yaliyo ishi hapo na hivyo kuyapelekea mafuriko na kuyaangamiza.
Mexico panasemwa kabla ya gharika aridhi hiyo ilikuwa inakaliwa na majitu makubwa yaliyo itwa, ‘Tzocullixeco.’

MAYA, GUATEMALA; INCAS, PERU:


Panasemwa watu wa mwanzo kuumbwa, walikuwa ni majitu makubwa kabla ya gharika kufika. Moja kati ya makabila ya majitu makubwa ni Atian na Theitan.

Majina hayo mawili ukiyatazama yanagusa kitu Fulani, je Theitan ndiyo Ugiriki na Ulaya waliwaita Titan? Je Atian ndiyo Atlas, ambayo tunapata jina la mlima Atlas? Vipi mlima uhusiane na jina la kabila … punde tutaona.
Kingine kwenye hili, mara zote makabila haya yanatajwa mawili au kwa majina mawili, unakumbuka Gog na Magog, au Hajuja wa Mahajuja.

PERU
Kuna watu walifahamika kama Chavin, ambao ustaarabu wao ulitanuka kutoka bahari ya Pasifiki mpaka kwenye vyanzo vya mto Amazoni, watu hawa pia wanatajwa kuwa walikuwa ni majitu makubwa.


Nimetaja kwa uchache, lakini katika kila ngano zilizo wataja majitu zimewataja pia wakiwa ni watu wenye nguvu, akili, maarifa, ubunifu na kila sifa aliyo nayo binadam wa leo, lakini kwenye kilele cha ubora wake.


Pia ngano hizo zina wataja kuwa ndiyo wajenzi wakazi mbalimbali ambazo wao wamezikuta kama Pyramid, mahekalu na mfano wa hayo.
Lakini pia ngano hizo zinahitimisha kwa kauli moja, iwe ni Kanada, Marekani, India, Chad, Peru, Babiloni na kwengineko, zote zinahitimisha kuwa majitu yaliadhibiwa na kuondolewa kwenye uso wa dunia kwa gharika. 


Je hili ndiyo lile gharika la mtume Nuhu, tutaona punde tu.
Baada yah apo kizazi cha majitu kikaanza kupungua kwa idadi, maumbile na mengineyo, na ngano nyingi zikaanza kutaja kizazi cha mwisho cha majitu ambacho kinahusisha watu wenye urefu wa futi 15 mpaka 12.


Utakumbuka binadam wa kwanza kama tulivyoona huko nyuma alikuwa na kimo cha futi 90! Hivyo futi 15 mpaka 12 ni kama walikuwa ni watoto au vichenga vya majitu, hata ujana hawajaufikia, vipi kuhusu futi 6 mpaka 4 ambayo ndiyo wengi tuliyo sasa, nadhani tungekuwa ndiyo ujauzito wa majitu, bado kufikia ukubwa wa kuzaliwa! (Tena inawezekana kichanga akizaliwa njiti ndiyo kimo hicho)


Umri wao wa kuishi kwa uchache ni kama miaka 800 mpaka 900, na ukienda mbali zaidi unagusa kwenye elfu na kitu. Ndiyo maana nasema tumepungua kila kitu kwa zaidi ya asilimi 90. Nchi ‘zilizo endelea’ au nchi zenye mazingira mazuri ya Maisha umri wa mtu unakadiriwa kufikia 70 mpaka 80, wachache sana tena kesi maalum ndiyo wanafika 100 na kidogo!


Hivyo kizazi cha mwanzo kabla ya Gharika ni kama waliishi miaka 5000 – 6000 ndiyo gharika, kwa upande wa biblia ni zaidi ya hapo kama miaka 10,000, hii utategemea na wapi utamuweka mtume Nuhu (as) ambaye ndiye aliyekuwa dira wakati wa gharika.

Vyovyote viwavyo kizazi hichi cha majitu wenye kimo cha futi 60 mpaka 90 kwa makadirio waliishi kipindi kirefu sana kabla ya gharika. Ni kama milenia 6 au zaidi kabla ya gharika!


Ukichukua kipindi hicho ukajumlisha na maarifa waliyo kuwa nayo, nguvu na mengineyo mfano wa hayo jibu lake halina shaka ni Mistari ya Nazca, Pyramid za Egypt na kwengineko na kila kile ambacho kina tutazama kwenye uso wa dunia leo ambavyo hatuna majibu yake ya moja kwa moja na kuhusisha na aliens (viumbe kutoka sayari ngine) ambao kulingana na mfulilizo wa Makala haya, viumbe hao hawapo, au hakuna kitu cha namna hiyo.


Kumbuka baada ya gharika majitu yaliendelea kuishi na huenda ilichukua mamia kama siyo maelfu ya milenia kwa kizazi hicho cha majitu kufutika kabisa kwenye dunia. Hivyo bado kuna kazi zingine zisizo lingana na kizazi cha mwanzo cha majitu, lakini kikalingana na kizazi cha cha kati au cha mwisho.


Mathalani utaona majitu wanayo tajwa kwenye vitabu vitakatifu kama kwenye Quran na Biblia ni kama kizazi cha mwisho cha majitu, hasa unapo linganisha time line ya (kipindi hadithi yao inatajwa au kuwa hai).


Mfano wake ni Hajuja wa Maajuja, au Gog wa Magog, Goliathi na Daudi, wajitu yaliyo ishi kwenye nchi ya ahadi ambayo wana wa Israeli waliahidiwa, watu wa Adi na Thamudi, utaona kwenye zama hizo za hao wahusika si mbali sana na zama zetu, hivyo kama walikuwa ni majitu basi walikuwa ni vizazi vya mwisho vya majitu na siyo majitu kwenye kimo kile cha binadam wa kwanza. 

(NA MUNGU MMOJA NDIYE MJUZI ZAIDI)



Ukibwa huo haukuwa kwa binadam tu lakini hata kwa viumbe wengine kama ndege, mijusi, farasi, mamba na wengineo, wote walikuwa na maumba makubwa na hata uwoto wa asili kama miti, majani na mfano wake. Kwa maelezo ya kina pitia kitabu cha Lost World of Giants kilicho andikwa na Jonathan Gray.


MASALIA
AMERIKANA KASKAZINI
Panapo visiwa vya Aleutian, wakati wa WWII, watu walio kuwa wakijenga njia ya kurushia ndege, walikumbana na visiki au bonde, baada ya kuvifukua kwa kina kwenda chini walikuta masalia ya binadam kama sehemu ya fuvu la kichwa na mifupa ya miguu mirefu. 

Urefu wa fuvu la kichwa kutoka utosini mpaka kwenye kitako chake ni nchi 22-24 tofauti kabisa na fuvu la binadam wa leo ambalo ni nchi 8 tu. Hii ikidhihirisha kuwa ni binadam mwenye umbo kubwa. Wenye mamlaka waliliingilia hilo kati na kukusanya hayo masalio … kisha … kimya mpaka leo. (David Hatcher Childress, World Explorers Club)



Wenye mamalaka hawawezi katu kuukubali Ushahidi huu, sababu ni kuiandika upya sit u historia ya binadam, lakini historia ya ulimwengu, kitu kitakacho maanisha anguko la kila kilicho simama sasa ambavyo vyote vimekopa na kuegemea nadharia ya Darwin, ni nani anataka hilo?

Mto Tennessee, Marekani.
Nyaraka kutoka chapisho la ‘American Antiquities’, kuna taarifa kuhusu unyayo wa binadam ambao unayo urefu wan chi 16.
Alama hiyo ya unyayo inayo vidole sita!



Western Missour
Kume kutikana mabaki ya binadam yenye fuvu la kichwa lenye ukubwa usio wa kawaida na taya la chini lenye ukubwa mara mbili sawa na taya la binadam wa sasa! Mfupa wa paja unayo ukubwa wa farasi (Arnold T. Wilkins, Mysteries of Ancient South America, pp.
33,195)

Crittendon, Arizona
Kaburi, kwenye mwamba ndani yake jeneza lenye mwili wa binadamu mwenye urefu zaidi ya futi 12, na vidole sita kwenye kila mguu. (Frank Edwards, Stranger Than Science, p.78)



 Winslow, Arizona.
Fuvu kubwa la kichwa cha binadam ambalo katika meno lipo jino la dhahabu, ukubwa wa fuvu hilo ni uthibitisho wa binadam wakubwa kimaumbo waliopata kuishi. (Brad Steiger
Worlds Before Our Own, p.52)



Bear Creek, Montana
Magego mawili makubwa ya haja, yenye ukubwa mara 3 zaidi ukilinganisha na gego la binadam wa leo. (Peter Kolosimo, Not of This World, p.134; Frank Edwards, Stranger Than
Science, p.77)

Masalio yoye yaliyo kuwa yakipatikana eidha serikali iliingilia na kuzuia watafiti kuendelea na tafiti zao, au kuyachukua hayo masalio na kisha katika hali ya kutatanisha masalio yanatoweka na makaburi yanafukiwa na hadithi inaishia hapo.

EL Boquin, Nicaragua
Mifupa ya binadamu ambaye mbavu zake zina urefu wa yadi moja na upana wa nchi 4 na mfupa wa mguu mzito hauwezwi kubebwa na mtu mmoja. (Brad Steiger, Worlds Before Our Own, p.55)
Fuvu lenye urefu wa futi 22 limepatikana Valenceia Spain mwaka 1705. (Brad Steiger, Worlds Before Our Own, p.51)

Scotland mifupa ya mtu anaye kadiriwa kuwa na urefu wa futi 14, ilikuwa inahifadhiwa kama kumbukumbu ya majitu yaliyo pata kuishi uso wa dunia.
Mfupa wa paja wa binadamu uliyo chimbuliwa huko Mexico, mfupa huo unayo urefu wa futi 8 na nchi 4. Hata urefu wa Hasheem Thabeet haujafikia kimo hicho! Huo ni mfupa wa paja tu, vipi ulikuwa urefu wa mtu huyo?



Mafuvu ya binadam yaliyo fukuliwa huko Palermo, Sicily mwaka 1548 na 1550, ilipimwa na kufikia kimo cha futi 30, futi 33 na futi 30.
Athens, Ugiriki, mafuvu mawili yalipatikana kwenye karne za karibuni yakiwa na urefu wa futi 34 na linguine futi 36.

Guys naweza kuendelea kutiririka na kutiririka na Ushahidi wa kutosha juu ya fuvu la kichwa, kidole, gego, mbavu, unyayo wa mguu na mengine mfano wake kwenye kila bara, lakini naona kwa dondoo hizo nimesha gusa msingi wa kuthibitisha juu ya kupata kuwepo kwa binadam wenye maumbo makubwa kushinda binadam wa leo.
Kumbuka hichi nilicho andika ni kama ukurasa mmoja wa kitabu cha kurasa 1000! Hivyo ni juu yako msomaji uliyo vutika na unaye taka kufaham zaidi kufanya utafiti wako binafsi, natumai utakuja na mengi zaidi ya haya.



PETRIFICATION
Kwenye sayansi ya historia na miamba kuna kitu kinaitwa ‘petrification’. Kwenye lugha nyepesi ‘petrification’ ni hatua ambazo zinapitiwa kiumbe chochote au mmea wowote, kutoka kwenye hali yake ya asili na kugeuka kuwa udongo au mwamba baada ya kufa.
Masalio mengi ya historia yanayo fukuliwa aridhini au baharini, kutokana na muda ambao yamekaa eneo hilo unakuta tayari yalisha badilika na kuwa udongo au mwamba. 



Hivyo mengi ya masalio si mifupa kama wengi wanavyo dhani, bali ilisha badilika nakuwa udongo au mwamba. Hicho ndiyo tunaita ‘PETRIFICATION’.

Kote duniani sehemu mbalimbali, kumekuwa na 'miamba' au 'miinuko' ambayo inayo umbo la ajabu ajabu, lakini umbo hilo linawiana au kufanana ni kiumbe hai fulani.

Mh! (Ngoja ni gune kwanza)

Guna vizuri maana baada ya hapa kila utakacho kitazama kwenye mazingara yako utakuwa unaguna.

Lakini kwasababu, tukimchukua mtaalam yoyote wa miamba atanza kutuhadithia na kutupatia hadithi za nadharia za 'mmomonyoko' wa udongo na 'mabadiliko ya tabia nchi.' Basi tunaishia hapo, hatuhoji, sababu mara nyingi, 'muulizaji na muulizwaji' wote hawajui ...


Unaona nini hapo?

Hapa tutatizama kwa uchache aina hizo za maumbo na kuhitimisha mtanange huu kwa heshima!



Unaona nini hapo?
Ni mnyama gani huyo, ni mwamba na 'erosion' gani inayo weza kufanya kazi ya namna hii?

Unaona nini hapa, Je umeliona jicho, sikio, mkonge? Au unaona mwamba tu? we call it petrification na siyo erosion!

Ukitazama mazingira, lazima ujiulize ni vipi erosion imalize miamba yote na kubakiza huo wenye umbo la Tembo? Petrification.

Unamuona hapo tena?

Unaona, hii ni ile picha ya kwanza, hapa imepigwa kutoka mbali kidogo. Watakuambia ni mwamba uliofanyiwa erosion na maji. Lakini maelezo yao yanaacha maswali mengi tu. Kwanini mkonge, jicho, sikio vikae mahali pake sawia, kweli ni maji au kuna cha zaidi?

Should I say more? The picture says it all!
UnaonaWataalam wetu kuhusiana na miamba hii yenye ummbo la viumbe hai wanasema ni erosion iliyosababishwa na maji, upepo, hali ya hewa na tabia za miamba, lakini kwa vile akili zetu zinaona kile tunacho taka kuona, basi zinatuonesha kuwa hao ni viumbe fulani, lakini ni 'erosion' tu hakuna kitu hapo. Iweje basi akili na macho ya kila anaye tizama miamba hiyo aone kitu hicho hicho, kama akili inaona kile inachotaka, je akili za watu na maono yao wote ni sawa ?

Unaona nini hapo! Mi nimeona kanyoka na bichwa la jinyoka!

Unaona nini?

Unaona nini, (wanakuambia hiyo ni rock formation) lakini watu wote wanaita ni 'snake rock'


Tizama tena vizuri hapa, tunaita petrification!

Kwa karibu zaidi, umeyaona macho mawili, umeona mabaka ya kichwa cha jinyoka?

Ni nyoka ni mjusi sijui, lakini usiniambie hiyo ni kazi ya 'rock formation'. Hakuna Rock formation ya namna hiyo, hicho ni kiumbe katika zama za Ma-giants.

Zama hizo huyo ndiyo chura unayemuona, kimo chake ni futi 8 (Duniani kwa sasa kuna binadam wawili tu wanao fikia kimo hicho kwa tarehe ya leo ya post hii) urefu wake ni futi 13. Huyo ndiyo chura, binadam alikuwaje?

Ni mnyama gani huyu?

Hiyo ni New Zealand, anafahamika kama 'Lion Rock' ingawa kichwa hakipo, lakini umbo linaonekana vyema.

Unaona nini?

Dragon? 

Picha hajitoshelezi mpaka niseme?

Unajenga kisiwa kwenye mgongo wa Dolfin! ni aina gani hii ya 'erosion'?


Umemuona kobe?

Unaona nini?

Unaona ni mwamba, lakini unapo tizama vizuri, ni zaidi ya mwamba, unaona uso, wenyewe wanaita 'rock face'

Unaona nini? Angalia tena.

Unamuona huyo?

Wanaita sleeping beauty, je wewe umemuona au unasubiri geologist aje akuoneshe?

Unauwona huo uso?

Nakiona kile jicho langu linacho taka kuona au naona Patrification.

Yes open your eyes, did you see her sleep? Look again, did you see her? If not look the next picture.


Picha ya chini ni (kikaragosi)kama kopi ya huo mwamba, sasa tizama tena huo mwamba umeona nini, je umemuona mrembo aliye lala hapo?

Does the erosion knows the structure of human skull?

Serous we need to revise our all books! 

Is that Rock formation or patrification?


Umeyaona mafuvu?

Siyo photoshop hizi, maeneo ilipo miamba hiyo pametajwa.

Je unamuhitaji jiolojisti au Darwin kwenye hili? Nadhani unaihitaji akili yako tu.

Unaona nini hapo?

Golgotha?
Wataalam wetu watakuambia huu ni mwamba, na nadharia kede kede za namna gani ulitokea, lakini maswali utakayo uliza hayoto jibika, sababu asili yake haukuwa mwamba, ulikuwa mti. Tizama tena, tizama vizuri.

Siyo mlima au bonde, ni masalio ya mti uliokatwa.

Hii hapa tena, mti uliogeuka kuwa mwamba baada ya petrification.

Hapa tumelijenga kanisa, ni mti huo.

Unaona Mti huo, mapande au magome baada ya petrification.

Mchoro huu unaonesha maumbile ya mti au gogo unapo likata, linganisha mchoro huu na picha za hapo juu.

Kulia ni mti katika zama zetu, kushoto ni mwamba au mlima ambao nadharia ya erosion haitoshi kutuambia mwamba huo umetengenezwaje hapo, lakini petrification ya mti inajitosheleza.

Tizama vizuri picha ya chini, ni mwamba ndiyo, lakini mwanzo hakuwa mwamba, mwanzo ulikuwa ni mtu uliokatwa.

Tizama na hii.

Na hii je?

Unaona nini?



Petrification ikiwa kazini.
Duh!
Safari ilikuwa ni ndefu na hapa naifikisha tamati. Ushahidi lukuki nilio utiririsha hapa wengi wenu najua ni vitu vipya. Lazima viwe vipya sababu kuvifaham hivi ni kuhatarisha mfumo wa dunia uliopo sasa.

Mfumo wa dunia yote umejengwa kwenye nadharia ya Darwin na kumkataa Muumba. Kote duniani, serikali zote zimesimamia kwenye mifumo hiyo, hivyo unapokuja tofauti ni kama unataka kuzidondosha serikali zote za dunia.

Lakini mwishowe zitaanguka, ....haikuwa batili ila imefunga manishwa na kushindwa ... hiyo ndiyo sheria ya maumbile na hivyo ndivyo ilivyo ... They will all falls ... "They plan and Allah is the best of planner ..."

end
Wapendwa tukutane hapa tena kumalizia viporo kabla ya kuliamsha dude na mada nyingine tata zaidi ...

Tchaoooo ...





10 comments:

  1. Nimeongeza 1% katika ubongo wangu, ahsante bro, tupo pamoja.

    ReplyDelete
  2. Aseeeee
    Wewe ni PROFESSIONAL PROFESSOR
    ALLAH akupe maono marefu katika maisha yako

    ReplyDelete
  3. Mungu akupe kila la kheri
    Na akuondoshee na akuepushie na kila lililo LA Shari likuhame.

    Allahumma ameen

    ReplyDelete
  4. Kaka shusha mada nyingine motoooooo

    ReplyDelete
  5. Powerful article with vivid examples and proofs...we have to share so that the knowledge reaches outside...asante

    ReplyDelete
  6. Enter your comment...njoo brother tunakusubiri

    ReplyDelete
  7. Kwa ninavyofahamu binadamu tunakuwa na ufahamu tofauti i.e ktk nyanja tofaut kuna wanasheria,wanasayans,wanamahesabu,wanahistoria,wanauchumi,wanasiasa n.k hata katika din kuna fiq,tareeh,qur'an na sunna,lugha. inanipa dought kidogo japo unaushahid wa kutosha juu ya unachokielezea vp umeweza kumaster aspects zote kwa wakati mmoja.......!! Hila big up na Allah awe pamoja nac kufahamishana tusiyoyafahamu

    ReplyDelete
  8. Allah akuzidishie ndugu, ila umekua kimya asee

    ReplyDelete
  9. kaka umekuwa kimya mno miezi kibao tunakungojea utumalizie episodes za mwisho . tunaomba kama kuna lolote utujuze kaka .....tired of waiting ....

    ReplyDelete
  10. Pls come back.....!!!!

    ReplyDelete