Wednesday, March 18, 2015

VITA 'FAKE' DHIDI YA ISLAMIC STATE ...



Tangu Agosti 2914, Jeshi la Anga la Marekani na washirika wake, nchi 19 kwa pamoja bila kuchoka wamekuwa wakifanya mashambulizi ya nguvu dhidi ya Syria na Iraq, kwa dhana kwamba wana walenga Islamic State, wanamgambo wenye ‘msimamo wa kati’ ambao nguvu na silaha zake wamezipokea kutoka kwa Marekani na kwa nchi washirika.



Kutokana na mashambulizi hayo, mashambulizi ya anga yapatayo 16,000 yamefanywa kwa kipindi cha Agosti 2015 mpaka katikati ya Januari 2015 (Defense News)
Asilimia sitini (60%) ya mashambulizi hayo, yalifanywa na Jeshi la anga la Marekani kwa kutumia ndege za kisasa za kivita. Vyombo vya habari za magharibi vimekuwa vikiripoti kuwa vita hivyo ni dhidi ya wanamgambo wa ‘Islamic State’. Lakini kinyume chake ndiyo sahihi vita hivyo vimekuwa dhidi ya viwanda, miundo mbinu, makazi ya watu, hospitali na kila aina ya uharibifu kwa rai wa nchi hizo kuliko ‘Islamic Satate.’

Lakini pamoja na yote hayo, bado serikali ya Marekani inafikiria uwezekano wa kufanya mashambulizi makubwa zaidi, yenye nguvu zaidi, sababu ‘islami state’ ni kitisho dhidi ya utawala wa magharibi na ustaarabu wake.

Mpaka sasa ndege ambazo zimetumiwa kwenye kampeni hii za kuwapiga watu wa Syria na Iraq ni F-16 Fighting Falcon, F-15 Strike Eagle, The a-10 Warthog, na F-22 Raptor.

SWALI LA MSINGI LA KUJIULIZA?
Kwanini Jeshi la Marekani na washirika wa nchi 19 wameshindwa kuwafuta wanamgambo wa ‘ISALMIC STATE’ ambao, kwanza ni wanamgambo, pili silaha walizo kuwa nazo mwanzo zilikuwa ni silaha ndogondogo.

Tangu yalipoanza mashambulizi, ni wazi kabisa walengwa hawakuwa ISLAMIC STATE, lakini kinyume chake kabisa mashambulizi hayo yalilenga miundo mbinu ya Iraq na Syria.

Tizama hii picha hapa chini na utafakari! Picha hii inaonesha siku ambayo kundi la Islamic State lilisafiri KM 200, mchana kweupe, kwenye jangwa pana linalo gawa nchi mbili, kutoka Syria mpaka Iraq. Salama salmini wanamgambo hao wakiwa na msururu mrefu wa magari aina ya ‘Toyota Pickup’ waliingia Iraq Juni 2014.

Nini kilicho kosekana kwa ndege hizo za kivita za Marekani na nchi 19 washiriki kuufutilia mbali msafara huo kwenye janga jeupe lisilo na kichaka?

Kama kweli vita hivyo ni dhidi ya ISIS, basi kwenye jangwa hilo, na kwa silaha walizo nazo Marekani na washirika wake, hilo lingekuwa ni kaburi la ISIS, lakini wapi walimaliza km 200 wakiwa na msafara mrefu wa magari meusi, kwenye jangwa jeupe na kuingia Iraq, lakini ni wakati huohuo, ndege zisizo na rubani ‘drone’ zilikuwa zikiendelea mashambulizi ya nguvu Pakistani.

Yes! walikuwa bize Pakistani wakiwatwanga raia wasiyo na hatia, huku ISIS wakivuka jangwa salama salmini.

Ajabu nyingine ni kuwa hakuna chombo chochote cha habari kilicho ripoti msafara huo. Msafara hewa wa Boko Haram kupotelea msituni na binti zaidi ya 270, iliripotiwa na kila chombo cha habari, ingawa hakuna hata gari moja la Boko Haram lililonaswa na kamera ilikuwa na mabinti hao.

Lakini ISIS na msafara mrefu wa magari kutoka Syria mpaka Iraq kuvuka jangwa jeupe, hakuna chombo  hata kimoja kilicho ripoti.

F15, f22 Raptor, F16 zilitosha kabisa kuwazika ISIS ndani ya saa moja. Lakini kinyume chake ni vita vinavyo kwenda mwezi wa 9 sasa na ISIS inazidi kupata nguvu na kutanua mipaka yake. Ikilinganisha na NATO, 1999 iliwachukua miezi mitatu tu na YOGOSLAVIA ikawa nchi nyingine kabisa.

Lakini vyombo vya habari vinatuaminisha kuwa ISIS hawawezwi kumalizwa na jeshi kubwa la anga la Marekani na la nchi 19 washiriki!
Hivyo basi utaona vita hivi walengwa si ISIS, bali Syria na Iraq. ISIS wanatoa sababu maalum na mahususi kwa Mrekani na washirika kuzichanachana nchi hizo. Hivyo ISIS wanafanya kile ambacho Marekani na washirika wake wanacho taka, hivyo ISIS na Marekani na washirika wao lao ni moja. Lakini pia situmeona vile ISIS walivyo patiwa silaha kupitia kwa Seneta McCain mwenyewe, na fedha kuoka kuwait na nchi zingine za kiarabu.


Hivyo basi ISIS ni adui nambari moja wa WAISLAM na UISLAM, ISIS HAWAPIGANI DHIDI YA MAREKANI, LAKINI SAFU MOJA NA MAREKANI DHIDI YA UMMA WAKIISLAM, AMKA WEWE KIJANA UNYEOTA NDOTO ZA KUSIMAMISHa khilafa kwambinu za kina isis, alshabab, boko haram n.k, huo ni mtego na fitna kubwa kwa umma.

No comments:

Post a Comment