Benki ya Dunia (WB) inakopesha fedha kwenye nchi za dunia
ya tatu kwa ajili ya kuratibu na kuendeleza miradi ambayo inahitajika kwa
manufaa ya nchi ‘wahisani’ a.k.a nchi wadhamini. WB inapowezesha kifedha miradi ambayo haina
tija wala manufaa yeyote kwa wakazi wa eneo husika; utambue kuwa na uchumi wa
eneo hilo unazoroteshwa.
International Monetary Fund (IMF) wanakuja kama mwokozi
pale ambapo fedha zilizo tolewa na (WB) zinapofanya kile kilicho kusudiwa,
ambacho ni kuuzorotesha uchumi wa nchi husika na wakati huohuo kuzifanya fedha
hizo kuwa ni mzigo usio lipika. (IMF)
wanapoingia wanatoa mikopo zaidi na hivyo kuongeza deni lisilo lipika kuwa ni
kubwa zaidi, lakini mikopo hiyo inakuja na masharti, kama vile ‘uongozi mzuri’,
‘utawala bora,’ ‘haki za mashoga,’ ‘kutoa aridhi na rasilimali nyingine kwa
wawekezaji.’
Kuna kile kinacho fahamika kama ‘free trade’, ambacho
kinahusisha makubaliano ya kimataifa kama vile GATT, NAFTA na APEC ambayo
yanachukuliwa kama ni kitu kizuri na bora zaidi na mawakala wa Illuminanti,
sababu ni mfano ‘mzuri’ wa mashirikiano ya kimataifa. Lakini wasicho kijua
mabilioni ya watu ni kuwa ‘free trade’ inaigeuza dunia nzima kuwa tegemezi wa
bidhaa kutoka kwenye mashirika ‘mahususi’ ya kimataifa.
Majina makubwa kwenye biashara kama vile NIKE, GAP,
PEPSI, TN, LEVIS’S, REEBOK, CALVIN KLEIN, COCA COLA, ADIDAS, MC DONALD, na
mengine na mengine. Haya ni mashirika ya kimataifa ambayo bidhaa zake zipo
kwenye kila kona na uchochoro wa dunia hii, bidhaa zake ndiyo bidhaa unazozikuta
kwenye maduka makubwa kama ‘Mall’ na vijiduka vidogo vya kina ‘Mangi’. Maana
yake ni kuwa bidhaa za wazawa wa eneo husika hazitauzika, viwanda vyao na
teknolojia yao itadumaa na wataishia kuzalisha malighafi zitakazo nunuliwa kwa
bei ya chini na mashirika hayo, ambayo baadaye watarudi na bidhaa watakayo uza
bei kubwa maradufu kushinda malighafi walizo chukua.
Mbaya zaidi ‘free trade’
inaondoa zoezi la kutoza ushuru baina ya nchi washirika, bidhaa za ndani
zinapoteza ulinzi dhidi ya bidhaa kutoka nje kwa kutotozwa ushuru. Hivyo
vijinchi vyetu katu havitakaa vinyanyuke kiviwanda wala teknolojia, siku zote
tutaendelea kuwa tegemezi kwenye bidhaa za mashirika ya kimataifa. Kwa vile
hatutaweza kulipa deni la (WB) na (IMF) wameongeza mzigo wa deni hilo, aridhi
yetu inakuwa ni mali yao, mali ya mashirika ya kimataifa kuitumia watakavyo.
WAKO WAPI WASOMI WANAO SEMA AFRIKA TULIPEWA UHURU? MBONA ARIDHI ZINAKWENDA?
MASHIMO YA MADINI NA VISIMA VYA MAFUTA VINAKWENDA?
Chakula nacho ni nukta ya muhimu kwenye hili. Sasa
yananyanyuka mashirika ya kimataifa yenye sura kama NIKE au ADIDAS, lakini haya
si kwenye viatu au nguo; Ila kwenye chakula. Hivi sasa nchi zetu za dunia ya
tatu zimekumbwa na mafuriko ya kuangamiza mbegu zetu za asili na kutupatia
mbegu za kisasa, tizama posti hii, http://salimmsangi.blogspot.com/search/label/gmo
Utazisikia serikali zetu, maajenti wao na maajenti wa Illuminanti
wakilipigia sana jambo hili zumari, na kulipigia debe mno, kwamba hatma yetu
suluhisho la njaa zetu, ni mbegu za kisasa. Loh! Tumekuwa ‘wajinga’ na
‘wapumbavu’ wa mwisho, tunapewa kichupa chenye rangi ya dhahabu na sisi tunatoa
dhahabu halisi!!! Kwa utaratibu huu sasa, 90% ya chakula wanacho kula walimwengu
kipo kwenye mikono ya mashirika ya kimataifa
machache yenye kuhesabika. Huu ni msiba juu ya msiba.
KAMA UNAZO MBEGU ZAKO ZA ASILI ZITUNZE NA ENDELEA
KUZALISHA KWA MBEGU HIZO NA WARITHISHE WANAO, KAMA UNAVYO WARITHISHA MALI
ZINGINE, SABABU SIKU ITAFIKA, DUNIA NZIMA HAKUTAKUWA NA HATA MBEGU MOJA YA
ASILI ...
Katika mfumo wa uchumi tulio nao sasa, mashirika yote
hayo ya kimataifa ni mali za wamiliki wa mabenki au punde yatakuwa hivyo kama
bado. Ikiwa hivyo ndivyo basi utambue na aridhi ambazo mashirika hayo
wanazipora kwa vijinchi hivi vinavyo endelea ni mali za mabenki hayo au punde
zitakuwa kwenye mifuko yao.
Illuminanti wanaulinda mfumo huo kwa kila aina ya nyenzo
waliyo nayo, sababu ndiyo mfumo pekee ulio fanikiwa kuitia kwenye mifuko yao
kila serikali duniani na kila raia, hata yule ambaye bado hajazaliwa!!!
Mfumo huu, ukamilifu wake utakuwa pale ambapo ulimwengu
mzima umeingizwa kwenye mfumo mpya utakao fahamika kama, ‘electronic money
systeam.’
Kinacho hitajika ni kitu kimoja tu, anguko la kiuchumi
ambalo ukubwa wake litaigusa kila kona ya dunia, na joto lake kila mtu
atalihisi na hapo kelele zitapigwa za kutaka kitu kifanyike. Na mpango ulikuwa
ukingojewa taratibu, kama hawataki vile, utaingizwa na kuanza kufanya kazi.
Kumbuka hazina ya nchi mbalimbali duniani leo haipo
kwenye ‘DHAHABU’ kama ilivyo kuwa awali, hazina hiyo ipo kwenye sarafu ya DOLA
au EURO. Kinachotakiwa ni kitu kimoja tu, kuiporomosha thamani ya DOLA, na kila
ambaye hazina yake ipo kwenye dola, lazima atakaa chini kama si kuzimia kabisa.
Hakuna nchi ambayo itaweza kulipa deni lake, lakini mbaya
zaidi, aridhi, mashimo ya dhahabu, na maeneo mengine yaliyo chukuliwa kama
dhamana na mashirika ya kimataifa yanaingia kwenye mifuko ya mabenki.
Kwa maneno mengine dunia yote na rasilimali zote zinakuwa
mali yao.
Mfumo huu wa fedha wa Illuminanti umejengwa kwenye
misingi ya ‘kuondoa thamani halisi ya pesa.’ Kwenye mzunguko wa pesa zote
duniani, na kuingiza pesa ambazo hazina thamani halisi ya pesa kwenye mzunguko
huo. Pesa ambazo ziko kwenye mzunguko kote duniani, hazina thamani ya kuitwa
pesa, ni makaratasi tu, hivyo ni jambo jepesi kwa Illuminanti kuyashusha
thamani makaratasi hayo kwa namna watakavyo.
Wanapo shusha ‘thamani’ ya sarafu kwa nchi fulani, basi
gharama za wafanyakazi, mali, samani, na huduma zinakuwa chini karibu na bure,
na nchi husika haitakuwa na uwezo wa kulipa deni lake, samani zake
zinachukuliwa kwa bei ya kutupwa na nchi wahisani a.k.a wamiliki wa mabenki.
Hatma yake ni kuwa, sehemu moja ya dunia kuna watu ambao
daima wataishi raha mustarehe kwa gharama za wengine, yaani kwa gharama ya
vijinchi vyetu ambavyo wafanyakazi wetu watafanya kazi kubwa, ngumu kwa bei ya
kutupa kabisa, umasikini utaendelea kukua na rushwa haitokufa kamwe.
Tutadanganywa tutengeneze taasisi za kuzuia rushwa,
lakini taasisi hiyohiyo itakuwa ni mtuhumiwa namba moja wa jinai ya rushwa,
sababu haitakuwa na uwezo wa kupambana na mzizi wa fitina, bali kila uchao
itapambana na matokeo au athari za rushwa, lakini palipo na mzizi wa tatizo
katu patasogelewa.
Thamani ya sarafu kwa nchi husika inaposhushwa, IMF
wanaingia na sera za ubinafsishaji wa Mashirika ya UMMA, Illuminanti ambao
walikuwa nyuma ya mchezo wote huu wanawatuma mawakala wao kuja kununua visima
vya mafuta na nishati nyinginezo, mashimo ya madini na mashamba n.k, lakini bei
ambayo ipo chini sana kulingana na thamani halisi ya vitu hivyo.
Lakini Illuminati kama ulivyo mfumo wao wa kibeberu,
hawaridhiki kwa kuishi kwa kuwanyonya wengine kwa kutumia mfumo wao wa fedha
ulio mbaya na uovu kupita. Lakini zaidi hatua ya mwisho wa mpango huu ni
kumfanya kila mmoja wetu katika uso wa dunia kuwa mtumwa!
Mfumo huo utapelekea kusimamishwa kwa dola ambayo
kiongozi wake si mwingine bali ni Masihdajjal / Mpinga Kristo.
Kila Myahudi anafahamu ya kuwa na anaamini, juu ya ujio
wa kiongozi wa kiroho, ambaye mlango wa historia ya dunia kwake yeye utafungwa,
atakuwa ni mfalme na mtume, na makao makuu yake yatakuwa ni Jerusalem, jiji la
wafalme kama wanavyo litambua Illuminanti, lakini Waislam tunalifahamu hilo ni
jiji la Mitume wa Allah.
Wayahudi wanaamini juu ya Masiha ambaye atalikomboa taifa
hilo na kusimamisha dola ya Kiyahudi kwenye aridhi takatifu ya Jerusalem, na
kuwafanya Wayahudi kuwa ni watawala wa Dunia.
Baada ya yote kama vile Wayahudi wameshinda. Aridhi yao
imekombolewa 1917, na ulimwengu umeshuhudia mamilioni ya Wayahudi wakirejea
Jerusalem miaka 2000 baada ya kutimuliwa hapo.
Israel sasa imekuwa na inaelekea kuchukua nafasi ya U- Super Power wa
Dunia. Punde tu inaonekana Israel itawanyang’anya Marekani kiti hicho.
‘Elcetronic Money’ ndiyo itakayo wapatia Israel nafasi hiyo waliyoingojea kwa
miaka 2000.
Utakumbuka April 1933 baada ya kile kilicho fahamika kama
‘great Depression’. Serikali ya Marekani ilipitisha sheria ambayo iliwakataza
raia wa nchi hiyo kumiliki sarafu za dhahabu, dhahabu, minara ya dhahabu au
cheti kinacho tambulisha kuwa unamiliki vitu hivyo. Kwa maneno mengine sarafu
za dhahabu au dhahabu kwa namna yoyote ile, kisheria haikuwa tena ikihesabika
kama ni pesa, ‘Legal Tender.’ Kama yeyote angekutwa na vitu hivyo baada ya
tarehe fulani basi angepigwa faini ya dola 10,000 na au kifungo cha miezi 6 au
vyote pamoja!
Wananchi walitakiwa kuzipeleka hizo sarafu za dhahabu,
dhahabu, minara ya dhahabu au cheti kinacho thibitisha kuwa unamiliki vitu
hivyo, walivipeleka kwa Federal Reserve Bank, ambayo ni taasisi ya fedha
inayomilikiwa na watu binafsi, na siyo Serikali. Wanao miliki Federal Reserve
Bank kwao kumiliki vitu hivyo hakukuwa na hatia ingawa nao walikuwa ni raia wa
kawaida, na taasisi hiyo ilikuwa ni yao binafsi na wala siyo ya Serikali, na
hata sasa bado inamilikiwa na watu binafsi.
Fedaral Reserve ilicho fanya baada ya kupokea dhahabu
hizo halisi, iliwapatia wananchi wa Marekani makaratasi yaliyoandikwa tarakimu,
na hapo tarakimu hizo ndizo zilikuwa thamani ya makaratasi hayo. Ukipewa
karatasi lililoandikwa $ 20, hiyo inayo maana kwamba, unamiliki dola ishirini.
Kwa kila wakia (ounce) mmoja wa dhahabu Federal Reserve walitoa karatasi
lililoandikwa $ 20 likiwa na maandishi ‘Legal Tender.’
Kwasababu taarifa hii ilitolewa kiserikali, na walimwengu
wanayo tabia ya kukikubali KILA KILE AMBACHO SERIKALI IMESEMA, basi Wamarekani
wengi, walikimbilia kwenye Federal Reserve Bank na kubadilisha dhahabu zao
halisi kwa makaratasi yaliyo andikwa Legal Tender. Wachache waliokuwa
wakifahamu hatima ya mchezo huo nini, walizinunua dhahabu zile kwa sarafu za
makaratasi na kuzihamishia kwenye benki za Uswis.
Kipindi hichohicho benki ya Uingereza ikafanya mchezo
kama huo kwa raia zake.
Baada ya dhahabu zote za Marekani kuwa kwenye mikono ya
Federal Reserve Bank, wahuni hao wakaanza ule mchezo wao, mchafu, wakashusha
thamani ya yale makaratasi waliyo wapatia watu, a.k.a sarafu za makaratasi kwa
41%. Halafu Januari 1934 wakapitisha sheria ya kutengua sheria ya awali na
hivyo kuwaruhusu Wamarekani kumiliki dhahabu tena, lakini sasa watanunua kwa
$35 kwa wakia mmoja wa dhahabu. Kwa maneno mengine raia waliporwa 41% ya
utajiri wao katika zoezi hilo.
Unaweza kuona sarafu za makaratasi zinavyokuwa
rahisi kuzipandisha na kuzishusha thamani. Lakini si hivyo tu utajiri wote
ambao umethaminishwa kwa sarafu za makaratasi unashuka thamani pale makaratai
hayo yanapo shushwa thamani. Hichi ndicho IMF anacho fanya kwenye vijinchi
vyetu pale wanapo shusha thamani ya sarafu zetu, na kupora utajiri wetu kama
ambavyo Federal Reserve walivyo wapora raia wa Marekani 1934.
Illuminanti hawakuishia hapo, wakaenda kutengeneza
chombo, kitakacho bariki muundo wa wa ‘Sarafu za Karatasi’ kimataifa, mahala
palipo fahamika kama Bretton Woods, mwaka 1944, wakaunda IMF.
IMF, AMBAYE KWA KUTUMIA MFUMO HUU WA FEDHA ZA MAKARATASI,
SASA IMF NI MMILIKI HALALI WA ARIDHI KUBWA, MACHIMBO YA MADINI, MAFUTA NA
MALIGHAFI NYINGI KATIKA NCHI ZINAZO ENDELEA, HATA KATIKA MIKUTANO YA KIMATAIFA
INAYOHUSU MAMBO YA FEDHA NA UCHUMI IMF NDIYO MWAKILISHI WA NCHI HIZI!!!!!
Utawasikia watoto wa mjini wakisema ‘Nchi ishauzwa hii.’ Maneno
yao hayapo mbali na ukweli.
IMF, ililetwa kazi moja tu, kubariki mfumo huu wa pesa
kimataifa na kuwa ndiyo chombo pekee chenye mamlaka ya kushusha thamani ya
sarafu yeyote ile duniani pale ambapo itaona inafaa kufanya hivyo.
Wakati Illuminanti wakizipatia nchi zilizo kuwa chini ya
utawala wa kikoloni ‘uhuru’ wao, kwa upande mwingine walihakikisha nchi hizo
zina fungamana na IMF katika masuala yao yote ya kiuchumi na fedha.
‘Katiba’ ya IMF ambayo inapaswa kusainiwa na nchi
wanachama, imesema waziwazi kuwa, ‘NI MARUFUKU KWA DHAHABU KUTUMIKA KAMA PESA.’
Mwongozo huo umefanya hivyo kwa kukata mahusiano yeyote
yale kati ya ‘Dhahabu’ na ‘Pesa,’ kwa maneno mengine thamani ya ‘Dhahabu,’
itapimwa kwa karatasi na siyo vinginevyo. Lakini pia baada ya kuiondoa dhahabu
kwenye kipimo cha utajiri na thamani ya kitu, wakaweka MBADALA.
UNAUJUA HUO MBADALA?
NILIDHANI HAUTA ULIZA!
MBADALA WENYEWE NI SARAFU YA DOLA au EURO.
HIVYO BASI NCHI WANACHAMA BADALA YA KULUNDIKA DHAHABU
KWENYE HAZINA ZAO, WANALUNDIKA MAKARATASI YA DOLA NA EURO!!!!!!
LAKINI SI HIVYO TU, NA THAMANI NA UTAJIRI WA NCHI HUSIKA
HAUPIMWI KWA MIGODI MINGAPI YA VITO, AU NISHATI, AU MALI ASILI, LAKINI KWA
MAKARATASI KIASI GANI YA DOLA ua EURO, INAYO YAMILIKI.
HIVYO BASI VIONGOZI WA NCHI HIZI ZA DUNIA YA TATU
WANAKIMBIZANA USIKU NA MCHANA, KUUZA RASILIMALI ZAO, KAMA MADINI YA ALAMASI,
DHAHABU, TANZANITE, GESI MBALIMBALI, MAZAO NA HATA ARIDHI, KWA BEI YA KUTUPWA
ILI WAWEZE KUYAPATA MAKARATASI HAYO YENYE NEMBO YA $ AU €.
UPO HAPO?
NI KUULIZE SWALI ..?
‘UNAFAHAMU MWANAUCHUMI AU KIONGOZI YOYOTE YULE WA NCHI
YAKO ANAPOSEMA UCHUMI UMEKUWA KWA ASILIMIA 3.7, au 4.6, au 7.... UNAJUA
ANAMAANISHA NINI?
NGOJA NILIPOTEZEE JIBU LAKE KWA SASA NISIJE KUIITWA
MCHOCHEZI BURE!
Art.
4. Section 2(b) of the Articles of Agreement stated: “exchange arrangements may
include (i) the maintenance by a member of a value for its currency in terms of
the special drawing right or another denominator, other than gold, selected by
the member, or (ii) cooperative arrangements by which members maintain the
value of their currencies in relation to the value of the currency or
currencies of other members, or (iii) other exchange arrangements of a member's
choice.”
Umekiona kipengele hicho, si maneno yangu jamani.
Hivyo kama Tanzania inataka kununua bidhaa kutoka Kenya,
hawawezi kutumia SARAFU YA SHILINGI, sababu hii kwenye mkataba wa IMF
inafahamika kama ‘LOCAL CURRENCY,’ ambayo inakubalika kote ndani ya Tanzania
kama ‘karatasi halali a.k.a fedha halali a.k.a legal tender.’ Lakini hii ni
ndani ya Tanzani, inapovuka mpaka kwenda nchi nyingine hii si fedha halali kwa
nchi ile, hivyo inabidi ipatikane sarafu ambayo nchi washirika katika biashara
watakubaliana kuitumia kama ‘msulihishaji’ katika utaratibu wa ununuzi wa
bidhaa, IMF sarafu yenye sifa hii inatambulika kama ‘International Currency
a.k.a foreign Exchange a.k.a € a.k.a $.
Hivyo basi serikali ya Tanzani lazima iwe na Dola za
kutosha ili kuweza kununua bidhaa na mahitaji yake ya kimataifa kutoka nje,
hali kadhalika nchi nyingine yeyote ikitaka kufanya hivyo. Hivyo Tanzania
haiwezo kwenda Kenya na mirundi ya dhahabu ili ipate bidhaa kutoka Kenya,
dhahabu zimefanywa ni makarasi yasiyo na thamani, na makaratasi yakafanywa
kinyume chake, na ikifanya hivyo itakuwa imekiuka mkataba wake na IMF, HIVYO
ITAINGIA MATATANI.
Kwa kufanya hivyo IMF inazilazimisha nchi zote zilizo
ingia mkataba na yeye ku-demand kila wakati kuwa na sarafu za Dola au Euro ili
uchumi wao uweze ‘kukuwa.’ Federal Reserve anacho fanya ni KUPRINTI MAKARATASI
HAYO NA KUTULETEA KWA GHARAMA YA UTAJIRI WETU HALISI!!!!!!!!!!!!! HALAFU WAO
WANAUCHUKUA UTAJIRI HUO NA KUTUACHIA MAKARATASI YAO.
JAMANI KWANI NA SISI HATUWEZI KUPRINTI HAYO MAKARATASI?
NADHANI MOJ YA HAKI KUBWA AMBAYO BUNGE LA KATIKA LINAWEZA
KUWATETENDEA WATANZANI, NI KULIGUSA HILI SUALA LA PESA AU KWA UWAZI ZAIDI BANK
vs PEOPLE.
KATIKA KATIBA INAYO TUMIKA SASA, BUNGE HALINA MAMLAKA
YEYOTE JUU YA SUALA LA FEDHA, KUANZIA UTENGENEZWAJI WAKE MPAKA KUINGIZWA KWENYE
MZUNGUKO. HATA RAIS WA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA KWA MUJIBU WA KATIBA
HIYO HANA MAMALAKA HAYO, SASA JIULIZE YAPO KWA NANI?
USISHANGAE UKIULIZWA HIVYO UKAAMBIWA KUWA JESHI
LITACHUKUA NCHI. MH! JAMANI UKISTAAJABU YA MUSSA UTAONA YA FIR’AUN.
Mpango huu wa Kishetani malengo yake makuu ni kuzifanya
Sarafu teule kama Dola, Euro, Pound, na za mawakala wengine wa Illuminanti,
siku zote kuwa na thamani kubwa na yenye kuendelea kukua dhidi ya sarafu
zingine zote duniani, ambazo siku zote zitakuwa kwenye kitanzi cha kuporomoka.
Wanapo utaka utajiri wa nchi yeyote ile, cha kufanya ni kuishusha thamani ya
sarafu yake, kinacho fuata ni deni halilipiki, na samani zako ulizoziweka kama
hazina zinahamia kwenye mifuko ya Illuminanti kupitia mikono ya IMF.
Watakuletea ‘policy’ kadha wa kadha kama vile, ‘restructure programme’, Structure Adjustment Programme, MKUKUTA na
mengine na mengine, lakini tayari wameshakupora.
Nchi zilizo lengwa kuporomoshwa katika mfumo huu, ambazo
sasa zinaitwa nchi za dunia ya tatu a.k.a nchi zinazo endelea katu
hazitafanikiwa kuitwa nchi za dunia ya kwanza, wala nchi zilizo endelea, wala
kutimiza malengo ya milenia wala Big Result Now, hakuna, na hakuna mwanauchumi
yeyote yule atakaye weza kusimama mbele ya umma na kuwaambia wananchi wake
kwamba tutaweza kuyafanikisha haya, labda awe ni mwongo, mwendawazimu au hajui anacho kisema.
Vijinchi vyetu hivi vitaendelea kunasa kwenye mitego
mikubwa ya mabilioni ya dola na euro kama ‘mikopo’ ambayo daima tutapambana
kuilipa kwa sarafu yetu ambayo kila wakati inaporomoka thamani yake, na kwa
njia hiyo utajiri wetu halisi utaendelea kunyonywa mpaka siku moja watoto wetu
wataamka kwenye nchi yao iliyo na sifa ya kuitwa ‘nchi ya maziwa na asali,’
ikiwa haina chochote zaidi ya vumbi tupu.
Ule wakati ukifika ambapo mwali mpya, ‘Israel’ anaingizwa
kwenye kiti cha U-Super Power wa NWO, SARAFU YA Euro na Dola zitaporomoshwa
thamani yake, sababu dunia nzima imeweka hazina yake kwenye makaratasi hayo,
zitajikuta hazina chochote zaidi ya makaratasi, itakuwa
balaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. Itakuwa vitaaaaaaaaaaaa, vuruguuuuuuuuuuuuu,
mauwajiiiiiiiiiii, fujoooooooooo, kila kona na kila mahala kwenye dunia hiiiiiiiiiiiii.
Israel watakuja na suluhisho, Electronic Money, hili nalo ni balaaaaa jingine,
ukiona hivyo tambau sekunde yeyote kutoka hapo Dajjal / AntiChrist / Mpinga
Kristo atatangazwa kwamba yupo kwenye dunia yetu ya 3D, NA NDIYO KIONGOZI WA
DOLA HIYO MPYA YA ISRAEL, NA ULIMWENGU WOTE UNAPASWA KULA KIAPO CHA UTII JUU
YAKE.................
JIBU LA SWALI LETU!
Wanapo sema kuwa Uchumi umekuwa kwa asilimia fulani,
wanamaanisha kuwa, katika huo mwaka nchi imeweza kusafirisha kwa kiasi kikubwa
bidhaa zake kama MAZAO, MADINI YALIYOSAFISHWA, MADINI KAMA MALI GHAFI, GESI na
BIDHAA NYINGINE, kwenda nchi za watu na yenyewe KUPOKEA MAKARATASI MENGI SANA
YENYE NEMBO ZA €, £, na $.
Hivyo basi kwa nchi yako kubadilishana rasilimali zake
kwa wingi na makaratasi hayo, na kuweza kuyahifadhi makaratasi hayo kwenye
hazinia yake badala ya dhahabu, ndiyo tunaambiwa kuwa Uchumi umekuwa kwa
asilimia kadhaaa .....
NDUGU, ENDELEA KUTAFAKARI, TILL NEXT TIME TCHAOOOOO
..........
Kaka Salimu Mwenyezi Mungu akubariki kwa siri hii nzito isiyojulikana na wengi. Naomba kama kuna makala nyingine unitumie kwenye e-mail ya fokasimwakalinga@g-mail.com
ReplyDelete