“Kama
watu wa Marekani wataruhusu benki binafsi kusimamia suala nyeti la mzunguko wa
fedha, kwa njia ya ‘inflation’ na ‘deflation’, benki hizo na mashirika yatakayo
yazalishwa na nazo, yatawanyonya watu na kuwapora kila kitu mpaka siku moja
watoto wao wataamka hawana nyumba kwenye bara ambalo baba zao walilipigania
uhuru” – Thomas Jefferson
Watu
wanaishi katika mataifa tajiri kuliko hapa duniani, lakini siku zote, eidha ni
kwenye mataifa hayo au nchi masikini, utakuta kuna ukame au upungufu wa ‘fedha’.
Leo hii wanawake nao wanaingia kwenye ajira, mamia kwa maelfu, wanaume zao
wanatamani kupata kazi ya ziada au ongezo kwenye mshahara, watoto nao wameingia
kwenye ajira, tena kwenye kazi mbovu za ajabu, deni la familia nalo linazidi
kukuwa kila uchao, na watu wa saikolojia wanathibitisha kwenye tafiti zao kuwa
moja ya sababu ya ndoa, familia kuvunjika na kuparaganyika ni juu ya kitu
kinacho itwa ‘pesa.’
Lakini
swali la kujiuliza ni ‘KWANINI FEDHA?’
NANI
ANAYETENGENEZA FEDHA?
KWANINI
KUNAKUWA NA UPUNGUFU WA FEDHA?
Katika
ustaarabu wa dunia ya leo, bila pesa hakuna kinacho wezekana, tunaweza kujenga
na kutengeneza kila kitu, lakini bila pesa viwanda vitatoweka na kuwa magofu.
Mashamba yatakuwepo lakini kwa familia tu ipate chakula, chakula cha ziada
kitaozea shambani, kazi hazitafanyika, usafirishaji wa bidhaa utasimama, wenye
njaa watawamaliza wenzao ili wabakie hai, na kila serikali itatoweka isipokuwa
ya familia tu.
UNADHANI
NIMETIA CHUMVI MANENO HAYO?
Hapana,
pesa leo ndiyo damu ya ustaarabu wetu, ndiyo njia ya biashara zetu zote. Ni
kipimo ambacho kwacho bidhaa moja inanunuliwa na nyingine kuuzwa. Itoe pesa
kwenye mzunguko au punguza kiasi cha pesa kinacho takiwa kwenye mzunguko na
balaa lake kila binadamu wa eneo husika ataliona siku hiyo.
Unakumbuka
miaka ya 1930 balaa lake? Historia ya fedha ya Marekani na duniani kwa ujumla
haijakamilika bila kutaja balaa hilo.
Unadhani nini kilitokea?
Ngoja
nikupe darasa!
Kwenye
miaka 1930 Marekani haikuwa na shida ya viwanda, haikuwa na shida ya aridhi
yenye rutuba, wala haikuwa na shida ya wafanyakazi wenye ujuzi na maarifa.
Marekani ilikuwa inayo usafiri bora na wa uhakika kutoka kwenye treni mpaka
barabara, baharini na hata anga na kulikuwa na mtandao mzuri wa mwingiliano wa
miundo mbinu hii. Mawasiliano baina ya miji mikubwa na ile midogo ndani ya
Marekani ilikuwa ndiyo bora kipindi hicho katika uso huu wa dunia, kulikuwa na
simu, radio, mfumo bora wa barua. Hakukuwa na vita wala uharibifu unao tokana
na vita, hakukuwa na magonjwa yaliyamaliza nguvu kazi watu, wala hakukuwa na
wakulima ambao wamegoma kulima. Isipokuwa mwaka 1930 taifa kubwa la Marekani
lilikosa kitu kimoja tu.
MAREKANI
YA MIAKA YA 1930 HAIKUWA NA KIASI CHA KUTOSHA CHA PESA KWENYE MZUNGUKO.
KWENYE
MIAKA HIYO, AMBAPO CHANZO CHA PESA KILIKUWA (NA HATA SASA BADO NDIYO CHANZO
PEKEE CHA PESA) BENKI NA MIKOPO, WENYE MABENKI KWA MAKUSUDI MAZIMA WALIKATAA
KUTOA MIKOPO KWA VIWANDA, WAKULIMA NA WAFANYABISHARA.
Hata
hivyo, ingawa jamaa hawa wa mabenki walisitisha kwa makusudi kutoa mikopo a.k.a
fedha hewa, kwa wakati huo huo walidai marejesho ya mikopo yao ambayo tayari
walishaitoa, na ghafla pesa ikatoweka kwenye mzunguko. Bidhaa bado zilikuwepo
kwa ajili ya kununuliwa, kazi zilikuwepo zinazo subiri kufanywa, lakini
kutoweka kwa pesa kwenye mzunguko kulilifanya taifa hilo kubwa duniani
‘kusimama tuli.’ Kwa mchezo mdogo tu kama huo, Marekani ikatumbukizwa kwenye
kile kilicho fahamika kama ‘anguko la kiuchumi.’ Na watu walafi wamiliki wa
mabenki wakawanyang’anya watu maelfu ya mashamba, nyumba, na mali zingine.
Watu
wakaambiwa ‘tupo kwenye wakati mgumu’ na ‘pesa ni kidogo’. Hawakuwa kama
ambavyo walivyo mabilioni wengine leo, hawafahamu mfumo wa benki unavyo fanya
kazi, walipora mali zao kweupe pee.
Ilikuwa
ni rahisi kama hivyo, hata leo BoT wakitoa amri mabenki ya sikopeshi, na wakati
huohuo yaanze kudai marejesho ya mikopo yao, utaona balaa la mfumo huu wa
uchumi tulio nao, hatma yetu ipo kwenye mikono ya watu wa benki.
Pesa
yote unayo ona kwenye mzunguko ni kwa vile mabenki bado yanakopesha.
Yanatupatia makaratasi yanayo itwa ‘pesa’ tunaweka rehani utajiri wa kweli kama
nyumba, magari, mashamba na mengineyo, halafu wakisitisha kutoa mikopo, pesa ya
kulipia mikopo inakosekana, kinacho fuata wanachukia utajiri halisi. Huo ndiyo
ukweli wenyewe.
Jiulize
kwa nini serikali haitengenezi pesa zake yenyewe mpaka zikakope kwenye mabenki,
tena kwa riba?
Serikali
kokote katika nchi husika, haichajiwi chochote kile, lakini inachajiwa riba
inapokwenda kukopa kwenye mabenki. Ni nani anayemiliki benki kiasi aweze
kuitoza serikali riba, ni nani mwenye nguvu ya ‘kuprinti’ fedha kiasi anaweza
kuikopesha serikali kwa riba na serikali haiwezi ‘kuprinti’ fedha zake yenyewe?
Mwalimu
wako wa uchumi anaweza kutusaidia kujibu swali hili?
Lakini
kilicho kuwa cha ajabu zaidi WWII Ilipokuja na kile kilicho itwa ‘Great
Depresion’ nacho kilikwisha! Watu walewale wanao miliki mabenki ambao mwanzoni
mwa miaka ya 1930 hawakuwa na pesa kwa ajili ya viwanda, mashamba, nguo na
vyakula, ghafla walikuwa na mabilioni yasiyo hesabika kwa ajili ya kukopesha
nchi zinazo shiriki vita hivyo, kwa ajili ya kununulia silaha nzitonzito, kwa
ajili ya kuviwezesha viwanda vya silaha, kwa ajili ya unifomu za kivita! Taifa
ambalo mwaka 1934 halikuwa na uwezo wa kuzalisha mazoa ya biashara, ghafla tu
iliweza kuzalisha mabomu ya bure kwenda Ujerumani na Japani.
Ongezeko
la ghafla la pesa kwenye mzunguko, watu walianza kuajiriwa, mashamba yaliuza,
mazao yao, viwanda vilianza kazi, machimbo yalifunguliwa na kile kilicho
fahamika kama ‘Great Depresion’ kilitoweka!
Kama
kawaida kunawana siasa walio laumiwa kwa hilo, na kuna ambao walipandishwa
chati kwa hilo. Lakini ukweli wa msingi unabakia kuwa MABENKI YALIAMUA KUWEPO
NA VITA VYA WWII, NA NJIA NYEPESI NI KUONDOA PESA KWENYE MZUNGUKO NA KUDAI
MAREJESHO YAO, NA KILICHO FUATIA NI HISTORIA. UKWELI HUU HUWEZI KUUPATA KWA
MWALIMU WA HISTORIA WALA WA UCHUMI, LAKINI ILIKUWA NI RAHISI KAMA HIVYO.
NANI
ANAYE TENGENEZA/UMBA FEDHA?
Binafsi
nimejaribu kupitia katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, hakuna hata mahala pamoja
iliposema ni nani na jukumu la nani kutengeneza fedha, au kuchapisha fedha.
Lakini cha ajabu mno ni kuwa katiba hii imejaa vifungu na vifungu vya namna
gani fedha zitumiwe, namna gani matumizi na mahesabu yake yakaguliwe, lakini
zinatoka wapi hizo fedha, hakuna jibu la swali hilo.
Kwa sababu
fedha ni kitu muhimu na kina mguso kwa kila mwananchi, nilidhani basi moja ya
shughuli za bunge ni kusimamia, na kuelekeza mchakato mzima wa kuhusiana na
suala la kuchapisha hela/fedha/pesa/sarafu/noti, lakini hakuna isipokuwa kipo
kifungu mahususi kinacho LINYANG’ANYA
BUNGE NGUVU ZA KISHERIA KUHUSU MAMBO YA FEDHA.
Utaratibu wa kutunga sharia kuhusu mambo ya fedha Sheria ya 1984 Na.15 ib.14
99.-(1) Bunge halitashughulikia jambo lolote kati ya
mambo
yanayohusika
na ibara hii isipokuwa kama Rais amependekeza
kwamba jambo
hilo lishughulikiwe na Bunge na pendekezo hilo la
Rais
liwe limewasilishwa kwenye Bunge na Waziri.
AJABU
SANA, MOJA YA KAZI KUU NA MAHUSUSI ZA BUNGE NI KUTUNGA SHERIA, LAKINI HAPA
KWENYE KIFUNGO HICHO HAPO JUU, KAZI HIYO KWENYE UPANDE WA MAMBO YOTE FEDHA
BUNGE IMENYANG’ANYWA, NA NANI KAPEWA KAZI HII, KATIBA HAIJAMTAJA.
NI
KWELI KITU MUHIMU KAMA HICHI KINAWEZA KIKAWA HAKINA SHERIA RASMI, NI KWELI
BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HALINA NGUVU YOYOTE JUU YA KIASI GANI
CHA FEDHA KIWEPO KWENYE MZUNGUKO? JUU YA THAMANI YA FEDHA NI IPI? SASA NI NANI
HUYO MWENYE NGUVU HII, SI KUMBUKI KUIYONA KATIKA KAZI ZA RAIS...
MADHARA
YA KULINYANGA’NYA BUNGE NGUVU ZA KISHERIA KUHUSIANA NA MBAO YA FEDHA NI YEPI?
TUITIZAME
MAREKANI KWENYE HILI, NCHI AMBAYO KATIBA YAKE ILIELEZA WAZIWAZI JUU YA NGUVU
HIZO ZA KISHERIA KUWEKWA KWENYE MIKONO YA BUNGE, MPAKA HAPO BAADAE MAJAMBAZI WA
BENKI WALIPO PENYEZA RUPIA NA SHERIA HIYO KUPORWA BUNGE NA KUWEKWA KWENYE
MIKONO YA WENYE MABENKI.
Serikali
kama ya Marekani imetumia pesa zaidi ya zile ilizochukua kutoka kwa wananchi
wake kwa njia ya kodi. Kwa sababu serikali haina pesa, na chombo chake mahususi
cha kusimamia sheria inayo husiana na pesa kimeporwa nguvu hizo za kisheria,
basi serikali huenda kwa wale wenye nguvu hizo za kutengeneza/kuumbwa fedha.
Tuseme inahitaji dola bilioni 1, lakini ‘Federal Reserve’ , ambayo inamilikiwa
na watu binafsi licha ya kutumia jina ‘federal’, haizitoi pesa hizo bure, ipo
tayari kuipatia serikali ya Marekani fedha hizo zikiwa taslimu au kwa njia ya
mkopo lakini kwa sharti kwamba serikali lazima izilipe fedha hizo tena na riba
juu. Kisha baada ya hapo bunge linaruhusu kitengo cha HAZINA kuchapisha hati
fungate (Treasury Bill) zenye thamani ya dola za Marekani Bilioni 1 ambazo
Federal Reserve watakabidhiwa kama dhamana (YAANI HATA SERIKALI HAIAMINIWI!)
Kisha watachukua makaratasi na kuyachorachora nambari na michoro ya ajabuajabu
na kuziita karatasi hizo fedha, labda inaweza kuwagharimu dola elfu 1
kuchapisha makaratasi hayo na kuwapatia serikali kama ndiyo dola bilioni moja
walizotaka.
JAMANI
MUMEONA KILICHO TOKEA, NI KAMA MAZINGAMBWE VILE, SERIKALI INAWEKA DHAMANA YENYE
THAMANI YA DOLA BILIONI MOJA KISHA INAPEWA MAKARATASI YENYE RANGIRANGI NA
NAMBARI NA IKITAKIWA KUYALIPA MAKARATASI HAYO NA RIBA JUU, JINA LA MAKARATASI
HAYO NI ‘FEDHA.’
JAMANI
KWANI SERIKALI IMESHINDWA KUNUNUA HAYO MAKARATASI NA HIZO MASHINE ZA
KUCHAPISHIA NA KUPRINTI HIZO NOTI NA KUZIPA THAMANI YA DOLA BILIONI MOJA?
SASA
BASI SERIKALI IMEPATA MAKARATASI YAKE ‘YENYE THAMANI HEWA YA DOLA BILIONI MOJA’
WANACHI WAMESHAFANYWA WADENI WA FEDERAL RESERVE NA BADO WATATAKIWA KULIPA DENI
HILO NA RIBA JUU.
MPAKA
KWENYE MIAKA YA 1980 SERIKALI YA MAREKANI ILIKUWA INADAIWA NA FEDERAL RESERVE
ZAIDI YA DOLA TRILIONI MOJA AMBAZO RIBA YAKE KILA MWAKA NI ZAIDI YA DOLA
BILIONI 100, HIYO NI RIBA TU.
TURUDI
HAPA KWETU TZ
KWANINI
SERIKALI YETU INAPOPITISHA BAJETI YAKE YA MATUMIZI KWA MWAKA UNAO FUATA IANZE
KUTEGEMEA VIKAPU NA NCHI WAHISANI KUTUNISHA BAJETI HIYO. KWANINI SERIKALI
ISICHAPISHE KIASI HICHO CHA FEDHA, BILA RIBA NA KUKIINGIZA KWENYE MZUNGUKO
KUKIDHI MAHITAJI YAKE YA MWAKA HUO???????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????
NADHANI
NITAANDIKA HIZO ALAMA ZA KUULIZA MPAKA ‘KEYBORD’ ITOBOKE NA SITAPATA JIBU.
“Hatuna
hata kidogo mfumo imara wa pesa ... pesa ni somo lililo la muhimu mno na ambalo
mtu mwenye akili na maarifa makubwa, anaweza kulichambua na kuja na majibu. Ni
muhimu sana kutambua kuwa ustaarabu ambao tunao sasa unaweza kuparaganyika kama
suala linalo husiana na mfumo wa kibenki halitatafutiwa tiba.
Robert
H. Hemphill, Credit Manager
Federal Reserve Bank of Atlanta, Georgia (1935)
In the foreword to a book by Irving Fisher, entitled 100% Money (1935)
“Kila
siku ambayo benki inato mkopo kwenda kwa mteja, utambue kuwa – pesa mpya kabisa
– salio jipya kabisa ambalo halikuwepo kwenye mzunguko hapo kabla limeingizwa
na benki. (Pesa tulizo nazo 95 ni mikopo)”
Graham F.
Towers, Director, Bank of Canada
“Mfumo
wa kuitengeneza pesa na kuingiza kwenye mzunguko ni mwepesi, rahisi na kawaida
sana kiasi kwamba akili inashindwa kuung’amua.”
Irving
Fisher
Kwamba
mzunguko wa pesa kwenye taifa letu (sasa ni dunia nzima) hatma yake ipo kwenye idadi
na kiasi cha mikopo inayo tolewa na benki, ambazo zinakopesha, lakini
hazikopeshi fedha, bali zinakopesha ahadi ya kumpatia mteja fedha ambazo
hawana”
Hivyo
ndivyo mfumo wetu wa fedha ulivyo. Kama kutakuwa hakuna MKOPO katika mzunguko
wa hela, hakutakuwa na hata senti moja kwenye mzunguko”
Marriner S. Eccles, Chairman and
Governor of the Federal Reserve Board
Kila
mtu anajua kwenye akili yake kwamba benki hawakopeshi fedha walizo pokea kutoka
kwa wateja wao. Unapo kwenda kutoa fedha kwenye akaunti yako, benki
hawakukatalii kwa vile eti wameikopesha fedha yako.”
Mark Mansfield
Kama mikopo
yote ya benki ikalipwa yote kwa wakati mmoja na ikamalizika, ujue hakuna hata
mmoja ambaye atabakiwa na hata senti kwenye akaunti, na hakutakuwa na noti wala
sarafu kwenye mzunguko. Unaweza ukashangazwa sana na hili. Wote sisi ni tegemezi
kwenye mabenki ya biashara. Kila noti au sarafu unayo iona kwenye mzunguko,
utambue kuwa kuna ambaye kakopa pesa hiyo. Kama benki watatoa ‘mikopo’, mambo
yetu yanakuwa mazuri, kama la, tunahaha. Hatuna kabisa mfumo wa fedha wa
uhakika. Kama ukiitazama picha hii na kuielewa, basi atatambua kwamba, balaa
lisilo na matumaini linalo tungojea ni kubwa kabisa”
“Bado
sijaweza kukutana na yeyote yule ambaye, kwa kutumia sababu na akili, anaweza
kuhalalisha kwa serikali kukopa fedha kwa ajili ya matumizi yake ... naamini
siku itafika ambapo watu watataka mabadiliko. Naamini siku itafika katika nchi
hii ambapo watu watakulaumu wewe na mimi na kila yule ambaye anahusiana na
bunge kwa kukaa kimya bila kufanya chochote na kuacha mfumo huo mbovu
kuendelea”
Congressman Wright Patman
“ Mfumo wa leo wa kibenki wa kutengeneza fedha
kutoka hewani. Utaratibu huu kiuhakika ni moja ya kazi ya utapeli kuweza
kubuniwa. Benki imeumbwa kwenye uovu na kuzaliwa kwenye dhambi. Wenye mabenki
wanamiliki dunia. Wanyang’anye hii dunia, lakini waachie uwezo wa kutengeneza
fedha hewa kwa mikopo, na kwa mkato wa kalamu wataweza kutengeneza fedha za
kutosha kuweza kuinunua tena dunia yote ... kama unataka kuendelea kuwa mtumwa
na kuendelea kulipa gharama za utumwa huo, basi waachie benki waendelee
kutengeneza fedha hewa za mikopo.”
Sir Josiah
Stamp, Mkurugenzi wa Bank of Endland 1928-1941
WANAHARAKATI,
WANASIASA,
WAZALENDO,
WASOMI
WA LEO,
MNAOTAKA
KUWA WABUNGE,
TAFADHALI
NI JIBUNI SWALI LANGU ... KABLA SIJAKUTANA NA NYIE HAPA KWA POSTI NYINGINE ....
PLZ ANY ONE WHO CAN HELP POST SOMRTHING HERE ....................
WHY,
WHY, WHY, WHY, WHY.............
Kweli huo ni mswiba katika dunia hii
ReplyDelete