Saturday, August 17, 2013

NAMBARI ZA MAAFA ZA KIMASONIA 13 na 33

Unapo wapekua freemasons, marais wa Marekani, mfumo wao wa utawala, kila mara utakutana na nambari hizi, 13 na 33. Wale wanao itwa waanzilishi wa taifa ka Marekani ni Freemason na karibu wote wa maraisi wa taifa hilo ni freemason isipokuwa wachache.



Nambari 3,7,9,11,13,33,39 na jawabu ya kule kinacho patikana kwa kuzidisha nambari hizo kwa nyingine, zote hizo zinayo maana mahususi kwa Illuminanti. Tizama asasi ya siri ya Bilderberg Group inayo wanachama wakuu 39 ambao wamegawanywa kwenye makundi 3 yenye wanachama 13 kwa kila kundi. Wanachama wakuu 39 wapo chini ya Policy Committee yenye wajumbe 13. Wajumbe 13 wa Policy Committee wapo chini ya Round Table of Nine (9). Unafahamu kwamba idadi ya asili kwa majimbo ya Marekani ni 13. Katiba ya Marekani imegawanywa katika vifungu 7 na ilisainiwa na wajumbe 39 wa baraza la katiba” Secret Societies / New World Order" by Milton William Cooper



Watu wa mazingaombwe wanaamini kuwa, pale nembo au alama juu ya kitu fulani inapotengenezwa, basi inakuwa na nguvu sawa na kile inachokiwakilisha, hii ni elimu ya mazingaombwe. Alama hiyo inakuwa na nguvu zaidi inapokuwa ni mahususi inakinzana na sheria za maumbile zinazofahamika au inapokwenda kinyume na kanuni za Mungu Mmoja.



o   Kwenye mkono wa kushoto wa Tai kuna majani 13 ya Mzaituni.
o   Mistari 13 kwenye ngao.
o   Mishale 13 mkono wa kulia.
o   Nyota 13 juu ya kichwa cha tai.
o   Ribbon iliyopo mdomoni mwa Tai inayo herufi 13. “E Pluribus
o   Fritz Springmeir  kwenye kitabu chake The 13 Bloodlines anasema kuwa mistari 13 ya tofali kwenye piramidi inawakilisha familia13 za kishetani.

Picha ya Piramid inayo patikana kwenye Dollar Bill ya Marekani na maandishi yaliyo izunguka picha hiyo, unapo unganisha herufi kwenye nukta maalum kwenye picha hiyo, unapata neno ‘MASON’








Namba za Kiroma zinazo patikana kwenye kitako cha Piramid: MDCCLXXVI, Nambari hizi zinawakilisha Jina la Mnyama, au Jina la Mpinga Kristo au Kristo wa Uwongo au Masih Dajjal.

"MDCCLXXVI".
Unapo zisoma tarakimu hizo kuja kwenye nambari za kingereza, unapata 1
776 yaani siku ambayo makoloni 13 ya Uingereza, ambayo yalikuwa Amerika ya Kaskazini yamepata uhuru, ambapo ni sawa kabisa, lakini hapa hatutizami umbo la nje la kitu, bali kile ambacho kinawakilishwa na umbo hilo. Je unajua MDCCLXXVI inawakilisha nini kwenye habari hii? Inasimama badala ya jina la mnyama.
Kama tukichukua nambari hizo za Kiroma na kuzijumlisha pamoja, unajua tunapata nini?

Waroma walikuwa wakitumia herufi katika mfumo wao wa nambari, hivyo tukiichukua DCLXVI inakuwa D= 500, C=100, X=10, V=5 na I=1. Herufi ‘M’ haikuwa ikitumiwa na Waroma kama nambari mpaka baadaye sana.
Hivyo, 5+0+0+1+0+0+1+0+5+1= 13




Kunazo nyota 13 kwenye bikari ya Kimasonia inayo onekana kwenye muhiri wa Hazina.




E.W. Bullinger anaandika kuwa:
Tunapo zungumzia umuhimu wa nambari kumi na tatu (13) wote wanafahamu kwamba nambari hii, imeshushwa kwetu sisi kama nambari yenye kubashiria mambo mabaya, nambari ya balaa…”
“Bahati mbaya, wale wanao rudi nyuma kutafuta sababu mara chache sana wanarudi nyuma kiasi kinacho takiwa. Maelezo maarufu siyo, hata hivyo kama tunavyo fahamu, nambari hii inarudi nyuma sana hata kabla ya viongozi (wetu). Lakini ni lazima turudi nyuma mahala ambapo nambari kumi na tatu ilitokeza mwanzo, ili kuweza kugundua maana yake halisi. Ilitokea mwanzo kwenye kitabu cha Mwanzo 14 :4 ambapo kinasema, “Miaka kumi na miwili walimtumikia Kedorlaoma, hata mwaka wa kumi na tatu WAKAASI.”
Hivyo basi kila inapoonekana nambari 13 na kila ile yenye kuzidishwa kwayo, inamaasnisha kile ambacho inacho kisimamia ni UASI, UPAGANI, UHARIBIFU, UFISADI, UVUNJIFU, MAPINDUZI, NA YENYE KUFANANA NA HAYO.” (Bullinger, E.W. Number in Scripture, Kregel Publications, (c)1967, Uk. 205).

Je, kupatikana kwa taifa la Marekani hakukuwa ni UASI kwa Uingereza? 
Hazina ya Marekani iliyo chini ya Federal Reserve sindiyo inayo endesha mfumo wa kibenki unao wafunga walimwengu wote kwenye madeni?

Nambari 13 na 33 ni nambari za Kimasonia.

Tarehe 6, 1945, saa 8:15 a.m. United State B-29 Bomber Enola Gay, kwenye misheni nambari 13, ilidondosha bomu la nyuklia lililoitwa ‘Little Boy’, Hiroshima, Japan.
Hii ilikuwa ni ‘Day One’ ya zama mpya, zama za nuklia. Kuweza kuelewa mabadiliko haya, tugeuke tana na kuitizama nambari 13, kutoka kwenye kuundwa kwa taifa la Marekani mpaka kwenye milipuko wa Bomu la Nuklia ndani ya Hiroshima.

Mwaka 1935, Paul Foster Case aliandika:
Tangu tarehe, 1776, iweke chini kwenye tako la uvungu wa msingi wa Piramidi na kuwekwa kwenye muhuri mkuu, na tangu nambari hapo nambari 13 imekuwa ni nambari muhimu mno kwenye historia ya Marekani na kwenye nembo ya muhuri, siyo uwendawazimu kufikiri kwamba, mistari 13 ya Piramidi inaweza kuwa inawakilisha nyakati kumi na tatu, “kipindi cha tofauti ya miaka kumi na tatu kila kimoja." 13x13 ni sawa na miaka169.  Kutoka Julai 4,1776  mpaka Julai July 4, 1945  ni sawa na miaka 169. Kutoka Julai 4, 1945 mpaka Agosti 6, 1945 siku ambayo Hiroshima ilipigwa ni siku 33. Bomu hilo lilidondoshwa karibu kabisa na nyuzi 33 za latitude.



No comments:

Post a Comment