Waandishi
wawili wa habari waliokuwa wakifuatilia sakata ya hichi tunacho kizungumzia
hivi sasa au maarufu kama Blue Beam wote wawili walikutikana wamekufa kwa ‘ugonjwa
wa moyo’ ingawa kwenye historia yao hawakupata kuwa na magojwa ya moyo. Vifo
vyao vilitofautiana kwa wiki kila mmoja.
Sege
Monast alikuwa ni mwandishi wa Internationa Free Press Canada, huyu ni mmoja
kati ya waandishi wawili walio kutwa wamekufa kwa ‘ugonjwa wa moyo’.
Moja ya
wadau wanao isimamia Project Blue Beam ni NASA, na mradi huu umegawanywa katika
sehemu nne ambazo zitafanikisha kuisimamisha New World Order na Masih Dajjal/Kristo
wa Uwongo akiwa ndiye kiongozi wa serikali hiyo.
HATUA
YA KWANZA
Hatua
ya kwanza kabisa ya NASA Project Blue Beam inahusiana na uharibifu wa elimu sahihi ya historia na
ushahidi wake. Kimsingi hatua hii itakuwa inashughulikia kuonesha au
kuthibitisha kuwa maneno, hadithi na utabiri wa vitabu vya dini ni makosa ya
kufasiriwa vitabu hivyo au pia ni uwongo kwamba vitabu hivyo havina dira sahihi
kwa mwanaadamu.
Hatua
hii itahusisha ‘matetemeko ya aridhi’ ya kutengeneza, ‘ugunduzi mpya’ ambao
utakuja na taarifa tofauti na zile zinazo patikana katika vitabu vya dini
mbalimbali. ‘Ugunduzi’ huo utakuwa ukiwaambia watu kuwa vitabu hivyo havina
usahihi wala umakini wowote, kwa maneno mengine ulimwengu uachane kabisakabisa
na vitabu hivyo pamoja na imani ya kuwa kuna Mungu Mmoja kwa vile vitabu hivyo
kwenye ‘ugunduzi’ mpya vinaonekana siyo kitu bali urongo mtupu.
Mathalani
eneo fulani kutokana na vitabu vya dini fulani waumini wake wanaamini kulitokea
tukio fulani, au kutatokea tukio fulani, Project Blue Beam kazi yake ni
kuonesha mambo tofauti na vitabu hivyo, na mambo hayo yataitwa ‘ugunduzi wa
kisayansi’ na hivyo dini ambazo wakati mwingine zinaonekana kimakosa kuwa
zinakwenda kinyume na sayansi zitakuwa zinasambaratishwa hatua kwa hatua na
waumini wake kukosa imani na dini zao.
Hiyo
ndiyo hatua ya mwanzo kwenye Project Blue Beam kwa vile kile ambacho wao
wanataka kukiondoa si kingine bali ni imani za dini zote ulimwenguni na
kuwapatia imani ya dini mpya, New Age Religion’ ambayo itakuwa si nyingine bali
ni dini ya ‘Ushetani.’
Kwa
sasa Illuminanti wanamiliki teknolojia ya kutengeneza ‘Mitetemeko ya Aridhi,’
na pia teknolojia ya kubadilisha hali ya hewa, wanayo na wamepiga kimya kwa
vile hiyo ni silaha na mara kwa mara wamekuwa wakizitumia au kuzijaribu maeneo
mbalimbali duniani, wanataka wao wawe ndiye mungu kabla ya kumsimamisha mungu
wao ambaye ni Masih Dajjal/ Kristo wa uwongo.
Hatua
hii inahusisha vita vya kisaikolojia ambavyo vitakuwa vikiandaa akili za watu
kukubalina na hatua tatu za mwisho zitakazo fuata.
Kuna
kile kinacho fahamika kama HAARP, KIFUPI MTAMBO HUU UMETENGENEZWA KUFANYA KAZI
UKIWA NA NGUVU MFANO WA ZILE ZA JUA. NAKUACHIA HOMEWORK, NENDA KATAFUTE
KUHUSIANA NA HAARP, NAMNA IANVYO FANYA KAZI NA MADHARA YAKE.
HATUA
YA PILI.
SPACE
SHOW
Anga
litakuwa ni mfano wa kioo kikubwa cha luninga, kama umepta kutizama ‘series
inayo kwenda kwa jina la V’ Series hii
ni moja ya kazi zao dhidi yetu sisi, maadhui yake tutayazungumzia huko mbele isipokuwa
hapa nataka nikukumbushe tukio moja kwenye series hiyo ambapo ‘wageni’ wale
kutoka sayari ya mbali walipofika, kwanza kabisa walizungumza na walimwengu kwa
kutumia chombo chao ambacho kiligeuka na kuwa mfano wa luninga kubwa iliyopo
angani, na luninga hiyo iliweza kuonekana kupitia vyombo vyao vingine vilivyo
kuwa katika miji mingine duniani. Watu waliwaona ‘wageni’ na kusikia sauti zao.
SPACE
SHOW ya Project Blue Beam nayo itakuwa hivyohivyo, ispokuwa yenyewe itakuwa
bora zaidi kwa vile hakutakuwa na chombo cha wageni na maumbile ya wahusika
wataonekana kwenye maumbo ya 3D na sauti zao zitasikika vyema.
Sehemu
tofauti za dunia wataona maumbo tofauti kulingana na imani za watu husika la
lugha zao. Kuna ambao wataletewa umbile la Yesu, wengine Mahdi, wengine
Krishina, wengine Budha na wengine Muhammad, na ‘watu’ hawa yatazungumza kwa
lugha mbalimbali kulingana na jamii husika.
Silaha
itakayo tumika kufanya kazi hiyo si nyingine bali ni HAARP. Itatengeneza kile
kinacho fahamika kama HOLOGRAM angani.
‘Wateule’
hao watakuwa na ujumbe wa aina moja ingawa katika lugha na tafsiri tofauti
kuwalika watu kwenye New World Order, walimwengu wataambiwa wale ambao mlio
kuwa mnawangojea kwa ajili ya kuwaokoa wameshafika, wapokeeni, Mashia
watapelekewa Mahd wao ambaye wanasema yupo pangoni anasubiri tu muda ili aje, Waislamu
wa madhehebu mengine watapelekewa, Mahd ambaye tunaitikadia atakuja, Wakristo
na Wayahudi watapelekewa Yesu. Anga ndilo litakalo tumika kama kioo cha sinema
hizo.
Kama
tulivyo ona leo kuna watu wanasikia sauti zikiwaongoza na wanaamini kuwa wao ni
‘wateule’ au wao ni watu maalum, kuna ambao wanakuambia wameshamuona Yesu (Rehma
ziwe juu yake) kwa macho yao na wanazungumza naye, kuna wanao kuambia wao kila
siku wanaonana na Muhammadi (Rehma na Amani ziwe Juu Yake) na anawapa miongozo
mbalimbali, lakini tutafikia mahala matukio hayo yatakuwa ni ya kiulimwengu
zaidi, kila mtu ataona kama tunavyo liona jua, na atasikilizishwa kwa lugha
yake kama tunavyo sikiliza redio juu ya ujio wa mwokozi wetu, ambaye hatakuwa
mwingine bali ni Dajjali / Mpinga Kristo/Kristo wa Uwongo.
Kama
kawaida tutakuwepo wale tutakao pinga, wale ambao tutasema hilo silo ni uwongo
mtupu, lakini taarifa zetu hazitopewa maana yoyote ile kwenye chombo chochote
cha habari na tutaonekana kama wavunjaji sharia, au magaidi. Pia watakuwepo
‘waumini’ bandia, ambao wao watatumia vitabu hivyohivyo vitakatifu kukubaliana
na hali hiyo ya kutengenezwa, hawa taarifa zao zitapewa kipao mbele kwenye
vyombo vyote vya habari, huo utachukuliwa kama ukweli wa msingi.
aina hii ya
mfumo wa habari si ngeni hasa kwa wanaharakati, hapa kwetu tume uona na bado
tunaendelea kuona ukifanywa dhidi ya jamii fulani kwa ajili tu ya kuendelea
‘kuwachinjia baharini’.
Mwaka
1974 mtafiti G.F Shapits alisema,
“… katika
utafiti huu itaonekana kuwa ile sauti ambayo mlengwa anaisikia ni kuwa inaweza
kuwekwa katika hali ya kiumeme na kutumwa moja kwa moja kwenye subconscious
level ya ubongo bila kutumia kifaa chochote cha kimakanika kwa ajili ya kupokea
na kutafsiri ujumbe huo kwenye ubongo na bila ya muhusika kuweza kuzizuia
taarifa hizo zilizotumwa kwenye ubongo wake bila yeye kufahamu…”
Blue Beam
Project pia itatumika kupandikiza mawazo ya uwongo na mawasiliano yasiyo sahihi
kwa kutumia mawimbi ya mawasiliano yatakayo tumwa kupitia ELF, VLF, na LF
yatawafikia kila mtu na kwenda moja kwa moja kugonga kwenye ubongo kana kwamba
hicho anacho kiona au kukisikia muhusika ni kweli, na taarifa hizo zitamfanya
ahisi kuwa anaongea eidha na Muhammad, Yesu, Buddha, Jah na hata Mungu
mwenyewe, teknolojia hii ipo na siyo hadithi za kufikirika za kisayansi. Sehemu
mbalimbali duniani zipo kompyuta kubwa ambazo zimebeba taarifa za kila raia
duniani na mpaka lugha zao, kompyuta hizi hufanya kazi kwa kutumia satelaiti ni
kwa kutumia kompyuta hizo ndipo aina hizi za taarifa hutumwa kwa walengwa.
Sizungumzii
mambo yatakayo kuja kufanyika siku zijazo, ila mambo yanayo fanyika sasa.
Binafsi nimeshakutana na watu wawili ambao wanapokea aina hizi za taarifa, na
ninakueleza ni vigumu kumshawishi mtu huyo vinginevyo, ni vigumu kumuambia kuwa
anacho kisikia ni kazi ya watu fulani mahala fulani, ni ngumu. Si wote wanao
sikia sauti kwenye akili zao ni mawasiliano ya ELF, VLF na LF, hapana wengine
ni kweli akili zao tayari zina matatizo na wengine ni ushawishi wa majini ambao
wao wanadhani ni neema. Hivyo inahitaji uangalizi wa kina kabla ya kufahamu athari
iliyo tengenezwa kwa mtu kupitia Illuminati na teknolojia yao na athari iliyo
tengenezwa na mashetani.
Kibaya
zaidi na cha kutisha zaidi kwenye aina hii ya teknolojia, hasa inapo tumika
dhidi ya binadamu, na rafiki yangu nakuambia hajatengenezewa mwingine ila
binadamu ni kuwa inanyakua thamani yako wewe kuitwa binadamu. Inanyakua uhuru
wako. Uhuru wako ndiyo mstari mnene na mweusi tii, unao kutofautisha wewe na
viumbe wengine, ukiwaacha majini ambao nao wana sifa hiyo. Kama kuna kitu
ambacho thamani yake ni kubwa kuliko vyote ulivyo navyo ni; Uhuru, yote uliyo
pewa na majukumu yako yote ni kwa sababu wewe u-huru. Bila ya uhuru tofauti
yako wewe na kiumbe chengine chochote ukitoa majini, haipo.
Teknolojia hii
itakuja kuuchukua uhuru wako, utadhani mawazo na maneno unayo toa ni yako, utadhani
nguo unazo vaa ni chaguo lako nakadhalika, lakini hayo ni maamuzi ya watu
Fulani walio kwisha amulia maisha yako na wanakuongoza vile watakavyo. Hautakua
huru kuamua unacho taka kama binadamu bali utaongozwa punde tu kama kundi la
kondoo nyuma ya mchungaji wao, wakati huo wachungaji ni Babyloni Brotherhood.
Walimwengu
haiwaingii akilini kama kuna aina hii ya teknolojia achilia mbali kuamini, na
mimi sitaki uamini bali uelewe na akili yako huru. Watu wanapo dhani aina hii
ya teknolojia haiwezekani kwa sababu yoyote ile, watu hawa wanawarahisishia
kazi maadui zetu, kwani pale silaha hizo zitakapo anza kutumika kwa ajili ya
kuwafunga walimwengu wote kwa ujumla wake, watu hawa watakuwa upande wa Babyloni
Brotherhood, watu hawa wataamini kile wanacho kiona na kukisikia, watawapokea Masihi
na mitume wa uwongo na watachana na imani zao kwa ‘kufikiri’ mafundisho yake
yalisha kosewa tangu zamani.
HATUA
YA TATU
ALIEN
INVASION
Kwa
kutumia Blue Beam Project maadui zetu watatengeneza kile ambacho dunia wataona
ni uvamizi kutoka ‘nje’ ya sayari yetu, ‘uvamizi’ wa viumbe wasio julikana.
‘Uvamizi’ huo wa kutengeneza utasababisha mataifa yote yenye silaha za nyuklia
kutumia silaha zao dhidi ya ‘uvamizi’ huo na ambapo maafa makubwa yatakuwa
dhidi ya binadamu kwani kiuhakika kabisa hakuna uvamizi wowote. Mahakama ya
Umoja wa Mataifa itazitaka nchi ambazo zimetumia silaha zao za kinuklia dhidi
ya ‘uvamizi’ huo feki, kuziharibu silaha hizo mara moja. Hii itakuwa ni hatua
muhimu sana nchi mbalimbali duniani zina nyang’anywa silaha zao, hii ni kwa
ajili ya kuondoa kitisho chochote kile dhidi ya serikali mpya ambayo punde tuu
itawekwa hadharani.
Sharia hii haitazigusa nchi peke yake bali mpaka wananchi
wake, watu wote duniani hawatatakiwa kumiliki silaha, lengo ni lile, lile
kuondoa aina yoyote ile ya vikwazo kwa serikali inayo ngojewa.
Kwa Wakristo
kuna kitu kinaitwa ‘unyakuo’ kwamba Yesu atakapo rudi atawanyakua wale wateule
na kuwapeleka mbinguni kuwaepusha na mabalaa yatakayo fuata kwani hizo ni siku
za mwisho na mabalaa yake ni mengi. Wakati Illuminati wakitengeneza ‘uvamizi’
feki pia watatengeneza na ‘unyakuo’ wao, ambapo baadhi ya watu watanyakuliwa na
kutiwa kwenye vyombo ambavyo wao wataona ni UFO nakadhalika, kwani Masiha wao
amekuja kuwaokoa kutokana na kitisho cha ‘wavamizi’ kutoka nje ya dunia. Lengo
la unyakuo huu wa Illuminati ni kuivunja kabisa imani ya Kikristo kwani baadaye
unyakuo huo utaonekana ni feki na mafundisho ya Kikristo yata chukuliwa eidha
yalidanganya au yalitafsiriwa vile ambavyo sivyo.
Wakati
hayo yanatokea, ‘viumbe’ hao ambao wataitwa ‘wavamizi’ toka sayari ya mbali
wataonekana katika kila kona ya uso wa dunia, lakini hawatakuwa viumbe asili
bali ni maumbo ya holographic ya viumbe hao na mapicha yao kupitia Blue Beam
Project, kupitia vyombo na vifaa vingine vya mawasiliano kama nyaya, simu na
Luninga vitu hivyo ulimwengu mzima utaonekana kama umepagawa, watu watakuwa
wendawazimu, wahubiri wasio jua wanacho kihubiri au kwa makusudi na wasemaji wa
dini nyingine wataibuka na kusema huu ndiyo mwisho wa dunia, ni kama wanamwagia
mafuta kwenye moto unao waka, watu watajiua, wengine watauwana na kuua wenzao,
wengine kisaikolojia watamalizika kabisa na madhila mbali, mbali yatatokea na
wakati huo wengine wakishuhudia ‘unyakuo’ wa Illuminati.
Baada
ya zahama hili dunia nzima itakuwa tayari kumpokea Masih mpya kwa ajili ya
kuwaongoza, kwa ajili ya kuwatoa kwenye zahama hili, hatokuwa mwingine ile
‘mnyama’ ambaye jina lake ni K-F-R au 666 au Masih Dajjal au Mpinga Kristo.
HATUA
YA NNE
ANGUKO
LA KIUCHUMI LA KIDUNIA.
Kama
kawaida zahama hili litaanzia kwenye uchumi, fedha! Kutakuwa na anguko la
kiuchumi, nalo la kutengeneza, kama walivyo zoea kuyatengeneza mengine. Nalo
hili litapiga dunia nzima, benki zote za kwao, au zinafanya kazi kwa kufuata
sharia zao, anguko hili litatengeneza njia kwa ajili ya aina mpya ya sarafu
mpya. Lakini kinyume na sarafu tulizo zoea, sarafu hii mpya itakuwa
‘ki-elktronik’. Hutaiona pesa hiyo, wala hutaishika lakini itakuwepo. Baada ya
anguko hili watu watazitoa fedha zao kokote zilipo na kununua vile ambavyo
wataweza kuvinunua kabla pesa zao hazijapoteza thamani kabisa.
Watu watatumia
fedha zote kununua vitu ambavyo wanadhani baadaye wataviuza na kurejesha pesa
zao. Lengo ni kuhakikisha hakuna yoyote anaye bakiwa na hata sumuni ili watu
wasije kuzichanga fedha zao na kudhamini watu watakao pambana na serikali mpya.
Kila kikwazo kinaondolewa kwa umakini kabisa. Kiasi kwamba kusibakiwe na hata
mtu mmoja mwenye uwezo wa kujilisha mwenyewe, pesa haina thamani tena, kila mtu
atakuwa anategemea aina fulani ya uongozi ambao utapatiwa mamlaka na nguvu ya
kutoa mahitaji ya muhimu kwa watu.
Kuhakikisha
kuwa kila mtu atakuwa ameuweka uhai wake chini ya serikali mpya ya Masih Dajjal,
Illuminati wamesha tengeneza mpaka Microchip ambazo zitawekwa kwa wanyama pori,
ndege na samaki kiasi kwamba ukijifanya wewe huhitaji uwepo wao kuishi na
kwamba utakwenda kuwinda au kuvua, na hii inamaanisha kuwa wewe utakuwa
umekataa kuwekewa chip, basi punde tu unapo mshika mnyama huyo au samaki au
ndege baada ya kumuua kwa kutumia chip ambayo imewekwa kwa viumbe hao
watakunasa, sababu itawajulisha wewe ni nani na muhimu kabisa upo eneo gani
kwenye uso wa dunia, utakamatwa kwa kuitwa ‘gaidi’ utafungwa au utauwawa.
Hizi ni
baadhi ya filamu zinazo elezea ujio wa ‘wageni’ au ni baadhi ya silaha zinazo
tumika kwako na kwa familia yako na kwa nchi yako kisaikolojia kukubaliana na
ujio huo na kujiandaa kupambana nao, au kujiandaa kuutoa uhuru wako kwa
Illuminati na uwe mtumwa wao.
Baadhi tu ya filamu zao ni hizi, The Day the
Earth Stood Still ya mwaka 1951, War of
the Worlds ya mwaka 1953, Close Encounters of the Third Kind ya mwaka 1977, Star Wars ya mwaka 1977, Invasion of the Body
Snatchers ya mwaka 1978, E.T. ya mwaka 1982, Cocoon ya mwaka 1985, Independence
Day ya mwaka 1996, Dark City ya mwaka 1998,
Dreamcatcher ya mwaka 2003, District
9 ya mwaka 2009, Avatar ya mwaka 2009, Cowboys
and Aliens ya Julai 29, 2011, Monsters ya Oktoba, 2010, Megamind ya Novemba 5, 2010, Battle: Los Angeles ya Novemba 12, 2010, Battleship ya Mei 25, 2012, Paul ya Machi 18, 2011, Alien 5 ya mwaka 2012, Super
8 ya mwaka 2011, Area 51 ya mwaka
2010-2011, The Darkest Hour ya Aug 5, 2011, Skyline ya mwaka 2010
Hollywood
na makampuni yote ya filamu yapo chini ya Illuminati. Idadi hii kubwa ya filamu
na tamthilia kuhusiana na viumbe hawa wa kufikirika, ingawa sasa ulimwengu
unaamini kuwa wapo ni kuonesha jinsi gani maadui zetu walivyo jiandaa katika
kututengeneza kukubaliana na uwongo wao, kuwa kuna viumbe wengine nje ya sayari
yetu ambao muda wowote wanaweza kutuvamia na viumbe hawa ni hatari na mwokozi
wetu ni umoja wetu chini ya serikali moja ya dunia.
Lengo
si kukufanya uamini haya, narudia tena, lengo si kukufanya uamini haya niliyo
yaandika, kuna mabuku rejea ipomitandao ya internet,
chukua muda wako, kafanye utafiti wako binafsi na huenda ukaja na suluhisho
bora juu ya tatizo linalo ikabili dunia, kuliko kupinga na kubisha kibubusa.
Nakubaliana na unachokisema 99%,kwani nimechunguza,na hadithi zimeshafika kila kona ya dunia
ReplyDeleteNa nakuomba kushare nakala zako kwenye mitandao ya kijamii,mfano Facebook.